Mwanamke ambaye hujaolewa: Mkimbie mwanamme anayemchukia mama yake mzazi. (asije kuzalisha vitoto vyenye kukuchukia) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

Sunday, March 24, 2019

Mwanamke ambaye hujaolewa: Mkimbie mwanamme anayemchukia mama yake mzazi. (asije kuzalisha vitoto vyenye kukuchukia)

20190326_124716

FB_IMG_1553292467935
Hamjambo wadau,
Kichwa cha Mada kinajieleza, katika jamii zetu kumekuwapo na baadhi ya wanaume wenzangu ambao hawawapendi mama zao wazazi hata baba zao pia, tena hawataki kabisa hata kuona nyuso zao, wengine hata matumizi ya kujikimu hawawapi mama/baba zao ilhali wanajua kabisa ni wazee/tegemezi wanaotegemea kutunzwa na wao.
Hebu jiulize japo kidogo, iweje mwanamme ashindwe kumpenda mama yake mzazi aliyehangaika naye sana tangu akiwa tumboni hadi kuja kuzaliwa na kumlea hadi kuwa mtu mzima halafu akupende wewe mliyekutana tu ukubwani?. Wakati mwingine mnaweza kuoana na kuishi hadi uzeeni bila kuachana ila sasa watoto mtakaozaa lazima tu ataibuka au wote watakuja kuwa na roho na vinasaba vya kuwachukia na kuwatelekeza bila kuwajali haijalishi mmewasomesha hadi chuo gani.
Hatahivyo, mwanamme wa hivyo akikuoa amini kuwa atakuzalisha vitoto vyenye roho ya chuki na vinasaba vya kuchukia mama/baba yake ambaye utakuwa ni wewe.
Tafuta kuolewa na mwanamme mwenye baraka za wazazi, mwanamme anayependa wazazi wake, mwanamme anayependa watu, mwanamme atakayekuzalisha watoto wenye vinasaba vyema tangu wakiwa tumboni mwako.
Maneno yangu siyo sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad