KUJAMBIA UKENI KWA WANAWAKE .
(Vagina flactulence).
Utangulizi.
Tatizo la kujambia ukeni kwa wanawake limekuwa kubwa na kuwakosesha amani wanawake wengi na kuwafanya wajisikie aibu pindi wanapotokewa na hali hiyo.
Kujambia ukeni kitalaamu hujulikana kama,
Vagina flatulence,Vagina gas,qeefing , vart au farts.
Kujambia ukeni ni hali inayomkuta mwanamke ya kutokwa na upepo kupitia uke, hutokea hasa kupindi cha kujamiana na mwenza wake au shughuli zingine za kimapenzi pamoja na ufanyaji mazoezi.
Sauti ya mjambo inayotoka ukeni hutaka kufanana na ile inayotoka nyuma (mkunduni) lakini sauti hii inayotoka ukeni haihusiani au haihusishi kutoka hewa chafu kama ile ya kutoka nyuma na haina harufu mbaya inayoambatana nayo.
Upepo unaotoka ukeni wenye kuambatana na harufu ya kujamba kwa nyuma au kinyesi ni ishara ya tatizo la fistula, tatizo linahusisha kuachia au kuchanika kwa eneo la uke na haja kubwa na kutengeneza tundu, hali hiyo huweza kutokea kutokana na athari za upasuaji, kujifungua au magonjwa kama Crohn disease tatizo la kuvimba kwa njia ya haja kubwa pamoja na sababu zingine zenye kuambatana na hizo.
Tatizo hili la kujambia ukeni linaweza kumpelekea mwanamke kupatwa na U.T.I pamoja na matatizo mengine ukeni.
Kutokwa na upepo ukeni inaweza pia kuwa ni dalili ya viungo au via vya uzazi kukaa vibaya kutoka kwenye mkao wake wa kawaida, kitaalamu hujulikana kama female genital prolapsed, hali hii maranyingi zaidi hutokea baada ya kujifungua kwa mwanamke.
SABABU ZA KUJAMBIA UKENI.
Kunasababu nyingi zinazompelekea mwanamke kutokwa na upepo ukeni, miongoni mwa sababu hizo zinahitaji uchunguzi na tiba kitabibu.
Shughuli za kingono au kujamiana.
Hii ni sababu kubwa zaidi inayochangia mwanamke kujambia ukeni au kutokwa na upepo ukeni, kitendo cha uume kuingia na kutoka ukeni hupelekea au hurahisisha hewa kuingia na kutoka, pindi misuli ya uke inapokuwa inabana kutokana na hisia au nyege au uume unapokuwa unatoka au kuchomoka hapo huruhusu hewa kutoka nje,utokaji wake unaweza kuambatana na sauti kama mbanano au mpishano wa hewa, kitendo hiko ndicho mtaani tunasema mwanamke amejambia ukeni.
Ngono ya mdomo au denda huweza kuchangia mwanamke kujambia ukeni pia, baadhi ya wenza wanangonozisizotulivu yani wanaandana kwa pupa “rough sex” kitendo hiko huweza kupelekea pia tatizo au hali nyingine inayojulikana kama “spontaneous pneumoperitoneum” ni hali ya kuingia na kujikusanya kwa hewa isiyo ya kawaida kwenye uwazi au sehemu ya chini mapafu, mwanamke anaweza kusikia maumivu ya kifua au sehemu ya juu ya tumbo.
Uwekaji wa vifaa au kitu chochote kwenye uke kwenye uchunguzi au nje ya uchunguzi huchangia mwanamke kujambia ukeni., vifaa kama vya toys za kujiridhisha kwa mwanamke, tampon,vidole na speculum kwaajili ya uchunguzi.
Ufanyaji mazoezi, kufanya mazoezi kwa mwanamke hupelekea misuli ya uke kubana na kuachia na kuruhusu hewa kuingia na kutoka, hivyo huwa kumfanya ajambie ukeni.
Ujauzito na ukomo wa hedhi , mwanamke mjamzito huweza kukutwa na hali hii kutokana na mgandamizo unaotokana na ukuaji wa mtoto unaopelekea kusukuma na kukandamiza baadhi ya viungo vinavyobana uke au kibofu hatimaye hewa hutoka kupitia ukeni, hivyo hivyo kwa mwanamke anayefikia ukomo wa hedhi, hali hiyo hutokana na ulegevu wa misuli ya uke.
Kujifungua au kuzaa , Mwanamke aliyetoka kujifungua maranyingi pia hukutana na hali hii,kutokana na misuli ya kiuno kulegea au kuwa dhaifu mara tu baada ya kujifungua, au kukaa vibaya kwa viungo vya uzazi baada ya kujifungua, kitalaamu hali hiyo hujulikana kama “pelvic floor dysfunction”.
Mbali na sababu hizo lakini ipo sababu nyingine ya kitabibu zaidi inayoweza kumpelekea mwanamke kuwa na hali hiyo ambayo hulikana kama FISTULA.
NJIA ZA KUZIA KUJAMBIA UKENI,
Kwa kawaida hakuna mbinu au njia maalumu ya kuzia hali hiyo japo wakati mwingine haina haja ya kuzuia kwani ni hali ya kutokwa tu na upepo na sauti ukeni ambayo haina maumivu, ni vyema zaidi kuchunguza hali hiyo kama haitokani na sababu za kawaida kama nilivyoeleza huko juu.
Endapo kujambia ukeni hakujaondoka kwenyewe basi wakati unakojoa jaribu kukojoa kwa mfumo kama unataka kuchuchumama
“ squatting down” husaidia kutoa hewa ukeni na kuondoka zake, kama kujambia ukeni kunatokana na kubana kwa misuli ya uke, jaribu kutulia na kuvuta hewa kwa nguvu ndani “deep breathing” inaweza kusaidia.
Kama kujambia ukeni kunatokana zaidi na kufanya tendo la ndoa au mazoezi unaweza kujizuia kufanya hivyo kwa muda, lakini pia kuacha kutumia vitu vya kusaifishia ukeni.
MAZOEZI YA KEGELI HUSAIDIA ZAIDI KUMALIZA TATIZO HILI. HIVYO NI VYEMA KUWEZA KUYAFANYA KILA SIKU. Ni kubana na kuachia mismisuli ya uke, kama unavyobana mkojo vilevile.
WAKATI GANI UNAPASWA KUONANA NA DAKTARI?
Ni mara chache sana kutokwa na upepo ukeni kunaweza kuwa ni dalili hatarishi ya afya au tatizo Fulani, Fistula maranyingi huwa ni tatizo lenye kutpelekea mwanamke kutokwa na upepo au kujambia ukeni, Lakini endapo mwanamke atatokwa na upepo au kujambia ukeni unaombatana na hali hizi chini, basi ni vyema kwenda kuonana na daktari kwaajili ya uchunguzi wa tatizo na kupata tiba sahihi ya tatizo husika,
Mimi Pia hili tatiz lilishawahi kumtokea mpenzi wangu Lakini sasa yeye lilikuwa likimtokea pindi tu ninapoitumia ile staili ya "Chuma matembele" ,Ambapo pindi tu nilipokuwa nikitaka kuchomoa hewa ilikuwa ikitoka na kusababisha yeye kujamba ,,,,Ambapo pindi ilipokuwa ikitokeA hivo alikuwa akiniambia kuwa Anaumia.....So sikuwah kujua ni nin cha kufanya....!!!!Ushauri plz naomba
ReplyDeleteUshauri mzuri n umenisaidia sana
ReplyDeleteGud
ReplyDeleteAise dictar naitaj ushaur maana nina aunt anasumbuliw sana natatizo hilo ila so wakat wakujamiiana ispokua huwa inatokea mda wowote basi kwakua nimda mlef huwa inatoka wakat akifany kaz yakutumia nguvu mfano kumnyanyua mtt au ndoo yamaj nk. tayali inatoka kwasaut kiasi hata ukiwa pemben unaiskia basi jana raha kabisa na hosptor hajaenda
ReplyDelete