JINSI MWANAMKE ANAVYOWEZA KUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME ZA MWANAUME WAKE - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

Sunday, March 24, 2019

JINSI MWANAMKE ANAVYOWEZA KUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME ZA MWANAUME WAKE

20190326_124716

IMG-20190324-WA0031

Habari, masuala ya nguvu za kiume yamejadiliwa sana huku mitandaoni, na yawezekana umeshasikia mengi kuhusiana na vyanzo vya tatizo hili kubwa.

Acha leo tutazamie kwa upande mwengine mpya, ambao mara nyingi hufumbiwa macho.

Mwanamke anawezaje kupunguza nguvu za kiume za mwanaume wake? Ni swali gumu, lakini jepesi fuatana nami sasa. Sababu ni hizi...

MAZOEA

Wapenzi wengi siku hizi hasa jinsia ya kike, wamekuwa wakiwazoea wapenzi wao kupitiliza, si vibaya kumzoea mwenza wako! lakini kumzoea kiasi cha kukaa ukiwa mtupu muda wote ukiwa nae chumbani hatakama hamfanyi mapenzi, husababisha mwanaume akuzoee na kuanza kukuona wakawaida tu, na hii hupelekea hata wanaume kukosa hisia kabisa na wapenzi wao, na huleta hali ya kufanya mapenzi kwa mazoea tu, lakini si kwasababu ya mvuto na msisimko wa mahaba. Kama tunavyojua wanaume huongozwa kwa tamaa hasa ya macho, sasa akishakizoea sana alichokitamani mwanzo, na huwa ndio mwanzo wakukosa hamu na mwenzi wake na hata akifanya mapenzi hatofanya kwa mahaba yote, atafanya kwasababu tu anataka kwa muda ule, na hapo ndipo huja suala la kushindwa kurudia tendo, na kuonekana dhaifu kwa mwanaume.

KEJELI

Ni wazi kuwa si kila mwanaume hukutana na mwanamke bikira, muda mwengine wanaume hukutana na wanawake waliokutana kimwili na wanaume zaidi ya watatu, na kila mwanaume ana size tofauti ya maumbile (Uume), wanawake wasio na busara huwakejeli, huwadhihaki wanaume wao wanapoona tofauti ndogondogo za kimapenzi kulinganisha na mahusiano yao yaliopita, hasa wakati wa ugonvi baina yao, maneno kama, "kwanza huniridhishi kitandani, una kibamia, tangu niwe na wewe hujawahi nifikisha kileleni" na kauli nyengine zinazo fanana na hizo, huaribu kabisa saikolojia ya mwanaume, na kujiona hawezi na kumsababishia mfadhaiko, na hata ule uwezo wake aliokuwanao kwenye kufanya tendo huzidi kupungua.

KUSHINDWA KUTUNZA SIRI ZA FARAGHA

Wadada wa mjini, wamekuwa na tabia za kushindwa kuficha/kutunza siri za wao na wenza wao wakiwa faragha, huyaanika madhaifu ya wanaume zao hadharani, hatakama matatizo yapo upande wao. Suala hili husababisha baadhi ya wanaume kusemwa vibaya kunyooshewa vidole, na hata wengine taarifa kuwafikia, na huo ndo huwa mwanzo wa msongo wa mawazo kwa wanaume, kujiona hawafai na mwisho kuathirika kisaikolojia na kupoteza hata ule uwezo aliwahi kuwanao hapo awali.

UCHAFU

Usafi wa mwili kabla ya tendo ni muhimu sana, wanaume wengi hushindwa kufurahia tendo kutokana na uchafu wa mwanamke, kutokunyoa, kuoga, harufu mbaya inayosababishwa na joto na kutokufuliwa kwa nguo za ndani, sio siri ni mambo yanayowatoa kabisa mchezoni wanaume na kusababisha wawe na haraka ya kumaliza mzunguko wa kwanza kisha kugeukia ukutani.

Yote kwa yote kufanya mapenzi ni kama kuzungumza, hutegemea utayari wa wote wawili, maelewano na juu ya yote Upendo.

Mwanamke anamchango mkubwa sana katika kuliboresha tendo, na kuliharibu pia, kupitia sababu hizo juu, tujifunze na tubadike.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad