MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 09
TULIPOISHIA: Nilijitambua tukatoka hapo mbio, Patrick bila kujuwa hili wala lile kwasababu ya muziki kuwa mnene kwenye headfone aliendelea kuinjoi bila kujuwa kuwa wenzie wamekimbia Amebaki mwenyewe na kizaa zaa kipo nyuma yake.
SONGA NAYO!
Latina kwa nyuma alikuwa anamsomea lamani Patrick.
Patrick alipoangalia mbele hakuweza kuona mtu yeyote ndipo akajisemea moyoni: wameenda wapi?
Latina nyuma alinyoosha mkono ili kushusha kucha zake shingoni mwa Patrick.
Patrick bila kujielewa Akachomoa headfone mziki ukaendelea kulia kupitia simu, ajabu nyuma yake akaskia mchakacho unazidi akaanza kujiuliza nini kipo kinachezesha majani Chini taratibu akageuka kuangalia aisee nusu kuzimia uso kwa uso na Latina akiwa hatambuliki tena kama ni mrembo, kilichomshangaza zaidi Latina alikuwa anacheza lumba ile iliokuwa inapigwa kwenye simu ya Yule mkongo Chilunga ambayo kwa muda Huo Patrick ndo Alikuwa nayo.
Patrick baada ya kuona vile hakutaka kupoteza muda aliachia simu ikadondoka Chini kisha akakimbia nduki.
Upande wetu wasichana wote walikuwa wanalia, wanaume nao walikuwa wanalaani sana, kiukweli lawama zile walizielekeza kwangu, moyo uliniuma nikatamani kuwaeleza kuwa sio mimi ila ikashindikana.
Tukiwa tupo hapo kwa mbali tulimsikia Patrick akiwa anapiga kelele, fasta Dominic akamfuata, dakika kadhaa akaja nae, hakili za Patrick ziliruka dakika mbili kila akiulizwa hili anajibu tofauti ndipo Rodrigo akasema: mpeni muda kwanza.
Tulikaa chini kila mmoja hakutaka kumuongelesha mwenzie kwa muda huo.
Baada ya masaa kadhaa tulinyanyuka na safari ikaanza.
Joyce akiwa yupo na mpenzi wake Rodrigo alimuuliza: Najma si atageuka chizi pindi jambo hili likizidi?
Rodrigo: mimi na wewe ndo tulimshawishi umeona madhara yake!
Joyce: najilaumu sana.
Patrick kwa nyuma akawaambia wenzie ambao ni Zakayo na Abdul: Latina alicheza muziki muda ule.
Sote tuligeuka kumuangalia maana muda wote alikuwa hajazungumza chochote kuhusu alichokiona, haraka tukarudi nyuma na kumsogelea ili atuambie vizuri.
Patrick alituadithia kile alichokiona ndipo Chilunga akasema: labda hio mizimu inapenda sana muziki wa kwao.
Joyce akamuuliza Patrick: alicheza kabisa?
Patrick: nimemuacha anacheza mpaka sasa hivi.
Tulijiuliza nini tufanye ila hatukupata majibu.
Baada ya siku mbili kupita tuliendelea na safari ila kwa bahati nzuri hatukuweza kumuona Latina tena.
Tukiwa tupo sehemu tumejipumzisha, waangalia lamani walikuwa bize kuangalia tumebaki na safari ya kiasi gani.
Nikiwa nipo bize naangalia ndege wanavyoruka Derick alisogea nilipo na kusema: usihofu lazma Latina atapatikana.
Nikamjibu: amekuwa kitu cha ajabu mno halafu nakumbuka alisema ataua mmoja baada ya mwingine.
Derick: tusiliamini sana jambo hilo, sipendi kukuona ukiwa kwenye hali hio ukweli mimi nakupenda.
Nikamjibu: tatizo wewe haupo siriazi.
Derick: kwanini?
Muda huo tuliambiwa safari iendelee, ndipo tulikata maongezi yetu tukaanza safari.
Tukiwa tupo njiani, Hamisa na chande walikuwa mbele ndipo zakayo akawauliza: mbona mpo mbele yetu?
Chande: eeee wanyuma ndo wanapataga tabu siku zote.
Abdul: kwahio mnatugeuza chambo si eti.
Wote walicheka huku wakiendelea kutaniana, tukiwa tunazidi kusonga mbele huwezi kuamini mbele yetu Latina alikuwa amesimama kama vile kuna mtu kamsubiri.
Hamisa na Chande ndio walikuwa wa kwanza kumuona aisee hakuna cha kupoteza muda tulianza mbio huku tukirudi nyuma, hata kina Hamisa hawakutaka kupoteza muda.
Hamisa akiwa yupo nyuma yetu sisi wote kwa bahati mbaya latina alitokea mbele yake na kumshika kwenye koo huku akiziingiza kucha zake.
Kelele za Hamisa akiomba msaada tulizisikia ikatubidi kusimama ili kuangalia nyuma, masikini mwenzetu alikuwa anarusha rusha miguu na mikono huku akituomba Msaada.
Chande uzalendo ulimshinda ukija kuangalia ni kama walikuwa wameanza mahusiano yao, ndipo akaamua kumfuata huku sisi wote tukimsisitiza aache twende ila hakuweza kutusikiliza, alipomfikia Latina alivuta gogo ndogo kiasi akaanza kumpiga nalo ila cha ajabu Latina hata kutikisika hakuweza kutikisika bali aliendelea kumumalizia Hamisa, haikuchukuwa muda Hamisa alikata roho kisha Latina akamrusha pembeni.
Tulipoona anamgeukia Chande aisee kila mmoja alimuombea kwa Allah amlaze mahali pema sote tukakimbia, tukiwa tupo njiani huku tukikimbia kwa kasi sauti ya mwisho ya Chande Tuliisikia akipiga kelele ishara anauwawa, wengi walianza kukimbia huku wakilia mno.
Baada ya muda baadhi yetu walikaa wengine wakawa wamesimama huku tukiwa tunaulizana nini kimetokea.
Zakayo alianza kunilaumu mpaka wengine wakamuunga mkono ndipo profesa mkuu akasema: yeye sio chanzo.
Patrick: ukisema yeye sio chanzo mbona mdogo wake ndo anafanya mauaji? Mimi naona huu Mchezo tupo tunachezewa maana haiwezekani mtu kubadilika tu inaonekana kwao wachawi.
Baadhi ya wengine wakakubali maneno ya Patrick.
Hapo sikuwa na cha kujieleza mbele yao tena Niliendelea kulia, wakiwa wanazidi kuongea huwezi kuamini Latina alitokea katikati yetu kabla hatujakaa sawa profesa ambae alijitambulisha kuwa jina lake ni husband yeye ndie alikuwa kati kati yetu kwa muda huo, Latina hakutaka kupoteza Muda alimkata na kucha tumboni profesa wetu damu ikaturukia, mwanajeshi Dominic alichomoa bastola yake ili kumshtuti Katina ila nilimuwahi akajikuta anapiga lisasi juu, utumbo tumbo wa profesa ukamwagika, hakuna Aliebaki hapo Tulitoka hapo tunakimbia bila hata uchovu.
Kila mmoja alienda na njia yake kwa wale waliobahatika kwenda wawili wawili ilikuwa bahati kwao, ila mimi nilienda njia yangu.
Patrick akiwa yupo na profesa mkuu kwa mbali waliona Simba dume inawafuata kwa kasi sio ya kawaida, bila kupoteza muda wakakimbia, kwa kuwa patrick alikuwa ni kijana hakujuwa ni saa ngapi kapanda mti alijikuta yupo juu ya mti ndipo akamuambia profesa mkuu awahi aje kupanda ila profesa alishindwa maana umri kidogo ulikuwa umeenda, simba yule aliruka juu akaja kutua kwenye kichwa cha profesa, yote Patrick alikuwa anashuhudia kwa macho yake mawili.
Profesa mkuu alianza kupalangana na simba yule huku akizidi kupaza sauti aje kusaidiwa, maskini profesa nguo Pamoja na Ngozi yake vilichanwa chanwa na simba yule mwishowe akazidiwa nguvu akafariki hapo hapo, Patrick nusu ageuke kichaa akitetemeka hali ya kwamba akashindwa kujizuia akaanza kulia kama mtoto mdogo.
Akiwa yupo hapo alishangaa kuona vitoto vya simba yule kama visita hivi vikaja vinamkimbilia baba yao ila simba yule baada ya kuviona vina hamu sana ya nyama alianza kuvitishia kisha akaanza kuburuza mwili wa profesa wetu vikatokomea nae msituni.
Upande wangu machozi zidi ya mdogo wangu yalikuwa yamekata ilikuwa imebaki mimi kujitetea mwenyewe, nikiwa nazunguka zunguka niliona kitu kama mti mkubwa mno ambao ulikatwa yaani umebaki Kama kisiki ndipo nikaona acha nikapande ili kuomba msaada kwa wenzangu nilipofika nilipanda juu nikaanza kuwaita wenzangu kwa sauti kubwa, ajabu nikiwa naita kama vile pale nilipo panabonyea kimtindo flani, nilipojaribu kuangalia nashangaa sehemu ile inabadili marangi tofauti, nikipeleka mguu pembeni nashangaa rangi inakuwa ya bluu, nikitoa mguu inakuwa rangi ya kawaida nyeusi, nikawa najiuliza Kulikoni hichi kitu.
Ile naangalia pembeni sikuweza kuamini kuona kichwa kama cha mama flani ajabu alikuwa ametulia kama vile kasinzia, nilipomuangalia vizuri nikagundua ni nyoka yenye kichwa cha binadamu na pale niliposimama imejikunja ikawa kama mduwala flani Ndo maana nikahisi ni kisiki cha mtu mkubwa uliokatwa.
Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu!
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment