SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, December 7, 2019

SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)





MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 07



TULIPOISHIA: Tulipowafikia wenzetu walipokuwa wametusubiri aisee walikuwa wamepondeka na kichapo cha sokwe wale, Derick aliponiona Nipo kwenye mgongo wa Dominic moyo ulimuuma sana, nilipomtazama niligundua ameumia ila nikapotezea, aliponiweka Chini tu, aisee huwezi kuamini kilitokea kitu juu kikadondoka Chini, watu wote wakapiga kelele huku wakitazama kitu kile......... 

SONGA NAYO!

Tulipoangalia vizuri kilikuwa ni kitoto cha Nyani kilitoka juu kikadondokea Chini, waschana wote waliogopa Ila wanaume Walitupa moyo, professor mkuu alikasogelea katoto kale ka Nyani akaanza kukashika shika huku akikapa pole ndipo akatuambia: mmemuona mama yake kule... 

Tuliangalia juu ya Mti uliokuwa pembeni yetu tukaona Nyani dike akiwa anamtazama mwanae kwa Hofu ndipo professor mkuu akaendelea kusema: alikuwa anamfundisha mwanae jinsi ya kuruka miti sasa mwanae bado hajazowea matokeo yake Ndo haya.

Professor aliomba tumpishe Nyani Yule aje kumchua mwanae, Nyani Yule alipoona tumempisha alitoka juu ya Mti ule taratibu akaanza kusogea pale tulipo, alipoona hatuoneshi hali yoyote ya Kutaka kumzuru alimchukua mwanae akaondoka zake. 

Joyce alishusha pumzi kwa kishindo Mpaka kila mmoja akacheka.

Tulikaa hapo wakucheza Wakaanza, wakupiga story wakaendelea. 

Nikiwa nipo mwenyewe huku nikimfikiria mama yangu mgonjwa ambae nimemuacha kwenye mikono ya watu ambao sio ndugu yangu nilikuwa nahofu Sana nikihisi Labda hawatomjali ipasavyo. 

Derick alisogea pale nilipo akanisalimia na kusema: mguu vipi? 

Nilimtazama na kumjibu: nipo sawa Kidogo. 

Derick alikaa kisha akatoa dawa flani ya maji maji akaomba anifanyie huduma ya kwanza, nilimruhusu akaanza kunipaka dawa ile. 

Muda Huo professor Rodrigo alianza kutupiga story ilivyokuwa muda ule sokwe walipowavamia, ndipo Zakayo akasema: naskia huu msitu unasifika kwa sokwe wakubwa kama wale. 

Professor mkuu: huu msitu una wanyama wengi wakali ila tumuombe Mungu. 

Hamisa alimfuata Abdul akamuomba wakapiga nae picha pembeni ya maeneo Yale ndipo Patrick akacheka na kusema: Subutu ndugu yangu kwasasa utakuja unakimbizwa na  tembo.

Abdul: siwezi kufanya huo ujinga aende mwenyewe. 

Chande alinyanyuka na kusema: achana nao waoga tu, twende zetu. 

Waliongozana kwa Pamoja. 

Chilunga muda Huo alikuwa amekaa na Sofia huku wakipiga stori. 

Chilunga: hii kazi ambayo mumekuya kufanya iko ngumu Kidogo alakini muko na asilimia mia ya kufanikisha. 

Sofia: kwanza niambie kuhusu zahabu naskia huku kwenu zinapatikana Sana!

Chilunga: kwa mutoto muzuri Kama weye ni rahisi kupata. 

Sofia alitabasamu kwa maringo Baada ya kusifiwa ndipo akamuuliza: una maana gani na wewe!

Chilunga: shie vijana wakongo tuko na makuta ya mingi sana. 

Sofia: makuta ndo nini? 

Chilunga: madolale. 

Sofia: wow! Vipi kuhusu zahabu?

Chilunga: tuko nayo ya mingi, ni weye tu. 

Sofia alicheka na kusema: mimi tena kiaje! 

Chilunga: Ukisema niko tayari Mbona mimi mwenyewe ntakupashiaga. 

Sofia: I'm sorry kupashiaga ndo nini? 

Chilunga: it's mean I'll give you. 

Sofia aliachia kicheko kikali Mpaka wote wakamuangalia, ndipo akatuambia: Jali yenu.

Tulimpotezea tukaendelea na mambo yetu. 

Chilunga: banamuke bote banakusikilia wivu. 

Sofia: hata sijui Kwanini.

Chilunga: si juu uko mkuongea na mtu mkubwa. 

Sofia alitabasamu na kusema: kweli? 

Chilunga: Eee bale ba filles bote ni bambaya ndo maana siongei nabo. 

Sofia: filles ndo nini? 

Chilunga: banamke.

Sofia: Mbona wewe Upo unaongea na mimi haliyakuwa Nipo wa Kawaida? 

Chilunga: shiweji ongea na fille mbaya weye kuongea na mie juwa uko wa bien zaidi yao utapata madolale mama! 

Sofia raha ilimuua akamuuliza: Kwani Yule namzidi? 

Alimnooshea kidole Amanda maana Yeye alikuwa mrembo tena mwenye pesa ndipo chilongo akamwambie: eeee! mbona Iko wa Kawaida Sana mbele yako mamaa! Yule si chochote kwanza Iko mukokuogopa sana njo maana Hawezi kujongea ulipo weye, Nimeshakwambia weye ni Jolie kuliko bote hapa. 

Sofia aliendelea kutabasamu kwa furaha, upande wa Abdul na zakayo story ziliendelea.

Abdul: Duh! Sofia anaonekana amemuelewa sana Jamaa. 

Zakayo: sound za wa Kongo unaziweza. 

Abdul: Demu bado tupo DSM nimemuomba namba kanitolea nje ila Huyu Jamaa wanacheka nae Mpaka siamini kama Ni yeye. 

Zakayo: kama ulikuwa unamfukuzia huyo manzi mteme tu maana huwezi kupata ubavu wa ku share mschana na mkongo. 

Abdul: una maana gani? 

Zakayo: wanapetepeti sana Hawa majaa sijui waliubwa je! 

Upande wa Chilunga story ziliendelea mwishowe akamtongoza. 

Sofia kwa furaha akasema: Aku mi siwezi! kwanza Nyinyi wa Kongo mnaoa sana. 

Chilunga: banafanyaga hivo juu habayapataga bamomo saa weye, ngoyela Nikwambie Hakuna kijana wa hapa Kongo au wa dunia nzima anaweza pata mrembo ambae ameumbika kama weye Halafu akamuowea mwanamke wa pili juu Haiwezekani mama!
Bako mukuoae ba bimdogo juu babimkubwa ni babaya saa hibi bibinti hapa, umenielewa cherie! Usiwe na probleme Ntakupa ma diamond, ma or ma dollar ya kimarekani utaishi saa malikia Elizabeth. 

Sofia kwa maneno Yale alijikuta anamkubali Chilunga mia mia. 

Muda Huo Dominic alikuwa bize anaimalisha ulinzi kama Kawaida ya majukumu yake. 

Upande wetu Derick alimaliza na kuniambia: utulie Kama saa nzima. 

Nikamjibu: Asante. 

Derick alinitazama usoni na kuniuliza: Yule Jamaa Kwanini anakujali sana? 

Nikamuuliza: Nani? 

Derick: Dominic. 

Nikamuuliza: Kwanini unaniuliza? 

Derick: by the way! why ulikuja huku? 

Nikamuuliza: na wewe Ulianza anzaje kuja huku na uprofeshino ulionao? 

Derick: Nimekuja huku kwa ajili ya kuokoa mamilioni ya watu. 

Nikasema: hata mimi nipo hapa Kwa ajili ya mama na baba. 

Derick: mengi nahitaji kuongea na wewe ila nafasi sipati. 

Nikamuuliza: kama? 

Derick: I love you. 

Nilitabasamu nilipomtazama Amanda niligundua hajafurahia kuniona nikiwa nipo na Derick ndipo nikamuambia: mfuate Rafiki yako ana upweke. 

Derick alipomtazama akagundua kweli anajiona mpweke sana, aliniacha hapo na kumfuata Amanda. 

Baada ya masaa kadhaa hatukuweza kusonga tena maana wengi walikuwa na maumivu kutokana na kichapo kile cha sokwe, hivo wakaomba tuweke makazi hapo ikiwezekana kesho tutaanza safari. 

Latina alinifuata na kuniambia: dada Nipe ruhusa nikapige picha ndege. 

Nikamjibu: Hapana kaa hapa. 

Latina: please dada sichukui muda nawafuata Kina Hamisa. 

Nikamjibu: Hapana Latina. 

Latina: unanibania sasa! 

Nikamjibu: basi nenda ila usikawe. 

Latina alifurahi kisha akanikiss na kuondoka na simu yake tu. 

Tukiwa tupo hapo nilijaribu kunyanyuka kwa bahati nzuri nikaweza aisee dawa ya Derick ilinisaidia sana. 

Professor mkuu akasema: nendeni mlete kuni za usiku si mnaona giza inaanza kuingia. 

Watu wote walipotezea ndipo nikasema: Ntaenda Mimi. 

Professor mkuu: utaweza mwenyewe? 

Nikamjibu: ndio. 

Professor mkuu: Chagua mtu Mwende nae. 

Nilimchangua Joseph maana Kidogo yeye nilikuwa nimeanza kumzowea. 

Tukiwa tupo mbali Kidogo na hapo, Tulianza kucheza mimi na Joseph taratibu.

Upande wa Latina alipoona muda unazidi kwenda alianza kurudi alikotuacha, kabla hajapiga hatua tano alishangaa kuona pembeni yake kuna kimvuli cha mtu akageuka kuangalia akihisi Labda kina Hamisa wamekuja Ila cha ajabu kimvuli Kile kilitoweka na mtu yule hakumuona, Hofu ilimuingia akaanza kuita kwa sauti ya uoga: dada Hamisa ni wewe? We Chande ni Nyinyi Mpo hapo?

Ukimya ulitawala kwa sekunde kadhaa, ghafla akashangaa kuona fuvu la mtu likiwa lipo mbele yake, kuongea alishindwa vile vile na kupiga kelele alishindwa, akiwa anajiuliza afanye nini fuvu lile lili.......... 


Unahisi nini kitatokea! 
Usikose mkasa huu!


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa