SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, December 7, 2019

SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)





MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 10



TULIPOISHIA: Ile naangalia pembeni sikuweza kuamini kuona kichwa kama cha mama flani ajabu alikuwa ametulia kama vile kasinzia, nilipomuangalia vizuri nikagundua ni nyoka yenye kichwa cha binadamu na pale niliposimama imejikunja ikawa kama mduwala flani Ndo maana nikahisi ni kisiki cha mtu mkubwa uliokatwa. 


SONGA NAYO! 

Moyo ulinishuka nikaanza kujiuliza Ntatoka tokaje pale, muda huo Derick na profesa Rodrigo pamoja na Chilunga na Dominic walifika, taratibu nikawapa tahadhari wasimame wasisogee ikiwezekana warudi nyuma taratibu kupitia ishara ya mikono. 

Aisee kumbe nyoka yule alikuwa anatuchola vizuri kwa kile tunachokifanya.

Wenzangu hawakuweza kuelewa nikipi kinaendelea wakawa wanajiuliza sasa yule vipi. 

Kabla sijafanya kitu chochote nyoka yule alinirusha nikawaangukia wenzangu, aisee huwezi kuamini alijikunjua ukubwa wake hata wakwambie upime urefu wake au upana wake hungeweza, sote tuliishia kushangaa nyoka yule alivyo wa ajabu, kilichotuua zaidi ni kile kichwa cha binadamu, muda huo zakayo na Amanda walifika vile vile na Abdul na Joyce, ile wao kushuhudia walirudi nyuma kimya kimya, tukiwa bado tunashangaa shangaa nyoka yule alipitisha mkia wake juu ya Vichwa vyetu matawi ya miti ikakatika. 

Hatukuchelewa tulianza mbio ili kujitetea na nyoka yule hakutaka kutuacha akaendelea kutufukuzia, nyoka yule mkukimbia nia yake anipate mimi, Dominic alianza kumpiga lisasi ila haikusaidia chochote, nyoka yule baada ya kuona dominic anataka kupinzana nae alimpiga mtama akaenda chini kisha nyoka yule akakata mti ukamdondokea kwenye miguu dominic ikamfanya asiweze kutoka eneo lile, wenzangu kila wakikatisha sehemu nyingine nyoka yule hakuwajali bali alizidi kunifukuzia mimi tu. 

Nilikimbia bila kujielewa kwa bahati mbaya nikadondokea kwenye bonge la kolongo, kina chake kilikuwa kirefu na chini sana kulikuwa na majabali makubwa mno, nikiwa nipo njiani huku nikizidi kuteremka kwa mbali sauti yangu ilisikika ninavyopiga kelele, nyoka yule alijinyoosha nikashangaa kuona mkia wake, na fasta ikajikunja kwenye mwili wangu kama kamba kisha ikanirusha juu kwa juu nikaangukia karibu ya Dominic Alipokuwa amegandishwa na muda huo wenzie walikuwa wanajaribu kumtolea ule mti, nikiwa bado sijanyanyuka aisee huwezi kuamini mbele yangu alikuja yule nyoka huku akiwa anajiburuta chini, sote presha ilipanda kukimbia tukashindwa nikaanza kurudi nyuma baada ya kuona kama vile ananilenga mimi, nilipoufikia mti flani niliusegamia huku nikijaribu kusimama, moyo ulinienda mbio tulipogonganisha macho na nyoka yule. 

Nyoka yule mwenye kichwa cha binadamu kama mwanamama wa kikongo flani, ilianza kutoa ndimi zake mbili huku ikitaka kunizuru, dakika mbili ilipanua mdomo wake ukawa mkubwa sana ili kunimeza, na mimi nikajiandalia kufa, taratibu nikafumba macho huku nikijiuliza je! Ntaenda peponi au motoni.

Nikiwa nimefumba macho nilishtuka kusikia kama kishindo cha mtu mbele yangu ndo nikaanza kujiuliza kuna mtu kati ya wenzetu amekuja kunikinga nisidhurike, taratibu nilifumbua macho yangu nikashangaa kumuona mtu akiwa yupo kifua wazi, kichwani alikuwa na nywele nyingi mno, nilipopitisha macho pembeni nikamuona yule nyoka bado yupo pale pale ila kama vile kuna kitu wapo wanaongea na mkaka yule ambae sikuweza kumtambua alakini bila kutoa sauti. 

Upande wa kina Derick jasho ilikuwa inawatoka kama mvua, muda huo Patrick, Safia, Amanda, Zakayo, Joyce na Abdul walifika eneo la tukio, aisee hawakuamini walichokiona. 

Nyoka yule Tulimuona akawa mpole kisha akaondoka kama vile kaambiwa kitu na kijana yule. 

Nilipomuangalia vizuri kijana yule aliekuja kutupa msaada alikuwa na asili ya kizungu licha alikuwa amechakaa sana. 

Baada ya muda tulikaa kikao huku yule kijana mzungu akiwa anatuambia mengi kuhusu msitu huo. 

Dominic: huyu nyoka kwanini anakichwa cha mwanadamu? 

Mkaka yule ambae hakuweza kutueleza jina lake akatuambia kwa kingereza: mwaka mia sita mama huyu alikuwa ni mwadamu wa kawaida, aliweza kutenda usaliti zidi ya kabila lake.

Rodrigo: kabila gani? na ilikuwaje? 

Akasema: zamani makabila yalikuwa na mfalme wao kipindi hicho kabila la kibembe lilikuwa ni kabila lipo chini sana lenye kumiliki vitu vya thamani mno, hivo makabila wengine walihitaji kuteka kabila lile ili kuwafanya watu wao ikiwezekana walifutie mbali kabila ile, ila wabembe walikuwa na malikia wao ambae walipenda kumuita malikia wa kibembe, malikia huyo alikuwa na nguvu za ziada wao waliamini aliteremshwa kutoka mbiguni, hivo makabila yenye nguvu yalipopata taarifa kuwa yupo kiziwizi ndie anawafanya watu wale wawe na jeuli walianza kumtafuta kwa njia yote, baada ya kabila lile la wabembe kupata taarifa kuwa malikia wao wanamtafuta ili waweze kumuua alienda kufichwa kwenye pango flani ya miungu yao, sasa huyu mwanamama ambae ni nyoka kwasasa hivi akaenda kutoa siri ya kabila lao kwasababu ya tamaa zake wakamfuata malkia yule wakamchukua ila kabla hajafa alimuachia laana hii, ndo maana yupo namna hio. 

Tulishusha pumzi kwa pamoja ndipo Amanda akamuuliza: ilikuwaje sasa kwa hio kabila la kibembe? 

Profesa Rodrigo akamjibu: hilo silo linalotufanya tuwe hapa sijui umenielewa? 

Amanda: nimekuelewa. 

Rodrigo: mbona profesa mkuu hajatokea? 

Patrick akamjibu: muda mrefu hatupo nae. 

Tulishtuka na kumuuliza: amekufa? 

Alitupa mkasa ilivyokuwa aisee kila mmoja aliumia maana mzee yule alikuwa anatufanya tuwe na nguvu. 

Rodrigo akamwambia yule kijana kwa kingereza maana alionekana hata hasikii kiswahili: sisi utuonapo hapa tumetoka nchi jilani Tanzania tumekuja huku kufuatilia maswala ya huu ugonjwa wa ebola sasa Tumekutana na kizaa zaa cha ajabu mpaka sasa niongeapo watu kama watano hatupo nao tena, kuna ndugu yetu tumekuja nae huku cha kushangaza amebadirika anatuua hovyo, sasa sijui unaweza kutusaidia nini hapo? 

Mkaka yule akasema: ndio wengi wanaokuja kwa lengo hilo la ebola huwa wanapotezaga maisha wote ila niwaambie tu kuwa tiba ya ebola ipo na ipo ndani ya msitu huu. 

Tulishangaa kwa pamoja huku tukiendelea kumsikiliza kwa pamoja, ndipo akaendelea kusoma: mwaka...... Kuna mzee flani alishtumiwa kuwa yeye nimchawi na Nikweli alikuwa mchawi makubwa zama hizo, enzi hizo wafalme walikuwa wakali mno mzee huyo baada ya kuzingiziwa kuwa yeye ndie kahusika na kifo cha mwana wa mfalme ambae alitarajiwa kuwa mfalme wa baadae, mfalme aliamua kuua wa toto wote wa huyo baba mchawi pamoja na mkewe kipenzi vile vile hata yeye pia ila kabla hajafa aliwatangazia wana nchi wanaoishi katika nchi nzima ya kongo milele watadhulika kwa malidhi hayo kwasasa tunayaita Ebola hicho ndo chanzo. 

Aisee kijana yule Tulimuona mtu mwenye hakili mno maana historia ile hakuna ambae aliweza kusikia kabla, ndipo nikamuuliza: ilikuwaje akapandikiza dawa ile?

Akanijibu: baada ya kufa walipokuwa Wamemzika fuvu lake lilitoka ndani ya kabuli lile likaja huku Kaskazini mwa kongo lilipofika ndani ya msitu huu wa equatorial lilitengeneza maji ya ajabu ambayo yana rangi ya bluu, zama hizo wengi walikufa mno bila kujuwa nini kinawauwa kwa wingi, maji hayo ndio ugonjwa tosha wa ebola na ndio tiba tosha ya ebola. 

Rodrigo akamuuliza: una maana gani ukisema ndio tiba na ndio maradhi? 

Akasema: yapo kwenye kibuyu flani ambacho kipo juu ya mti flani mwenye matunda mzuri ambayo matunda hayo nyani wanayapenda mno, sasa mti huo upo karibu na mto flani unaoteremsha maji uitwao Ebola, mwaka 1976 ndo ugonjwa Huo ukaja kuvumbuliwa na mtafiti mzungu akaamua kuupa Jina ya Ebola kutokana alifanya uchunguzi akagundua virusi ile inatoka ndani ya mto ule, sasa inakuwa hivi kibuyu kile huwa kinamwaga maji yale ndani ya mto ule baada ya mwaka kikisha mwaga maji fuvu ile inakuja inaongeza mengine na ndo maana utasikia wanasema ebola inakuja mwaka kwa mwaka. 

Aisee vichwa vilichanganyikiwa kwa dakika mbili ndipo profesa wetu Rodrigo akasema: watafiti wanatuambia ebola ni virusi vinavyopatikana ndani ya mwili wa nyani ambae amefariki kisha sisi binadamu tukamchukua na kumla vipi hapo unalizungumziaje? 

Akasema: Nikweli baada ya nyani wale kula yale matunda wakashiba huwa wanakunywa maji ya mto ule sasa siku wakija kunywa yale maji ikakutana siku hio yale maji ya ajabu yamejimwaga ndani ya mto ule madhara yake huwa nao virusi hio inawapata wanaporudi kwenye makazi yao wanaanza kuzoofika mwishowe wanapoteza maisha, ikiwa hivo watu wanaona nyamafu wanaichukuwa wanaikula, wakishakula ndo maradhi ya Ebola yanatoka hapo. 

Aisee kijana yule alijizolea sifa nyingi kutoka kwenye nyoyo zetu ndipo nikamuuzi: vipi kuhusu mdogo wangu anasumbuliwa na nini mbona amebadirika kuwa kiumbe cha ajabu? 

Akanijibu: fuvu lile la yule baba wa kale alieuwawa na mfalme kwa kesi ya uchawi yeye yupo ndani ya msitu huu ili kulinda laana ile alioiacha, sasa kila anaeingia ndani ya msitu huu akiwa na lengo la kuja kujuwa mengi kuhusu ebola huwa inamuua, mkiwa mpo wengi kama nyinyi hapo linamchagua mmoja wenu linamuingia mwilini kisha linaanza kutumikia ndani ya mwili wake ili kuua wenzie. 

Tuliangaliana usoni wenzangu ambao walikuwa wananilaumu muda wote wakatamani kuniomba msamaa. 

Patrick nae akamuuliza: kwanini akiskia mziki anacheza? 


Unahisi nini kitatokea! 
Usikose mkasa huu!


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa