Nikakaa baada ya kuwa nimekaa yule mzee akaniuliza "unaitwa nani?" Nikasema "Naitwa Tina" akamgeukia omary akamwambia "Huyu ndo binti ulisema?" Omary akasema "Ndio mkuu" Yule mzee akaniuliza "ulikuwa unafanya shughuli gani hapa katikati?" Nikamwambia "Nilikua nafanya kazi katika kampuni flani ila nimefkuzwa kazi baada ya kukosa kwenda arusha kwenye trip ya kikakaz kutokana na msiba wa mama yangu ulioteka siku chache zilozopita nilishindwa kutoa taarifa ofisini na hivyo nilifkuzwa kazi" akasema "Una uhakika na unachokisema unatakiwa ujue hapa unaongea na nani" nikaona sina maelezo tena ya kumpa nikamwangalia Omary amenikazia macho. Nikaangalia pale mezani kuna pen nikamwambia yule mzee unaweza "kunisaidia karatasi?" Akanipa nika andika namba za martha namba za baba namba za boss na namba za Secretary pale kazini kisha nikamwandikia email na website ya kazini.
Nikamwambia "Sijui kwanini niko hapa na sijui kwanini nahojiwa kiukweli hapa nilipo mimi najiskia vibaya sana maana sielewi kwanini majanga yananiandama mama yangu kafariki hapo hapo kazi nimefukuzwa hapo nahangaika kutafuta kazi kodi inaisha bado sijajua cha kufanya naingizwa kwenye mambo ambayo hata siyaelewi" Hapo machozi yananitoka naona ndo natonesha donda. Nikamwambia Omary "Sina hakika kama kuna kitu nimewahi kukukosea mpaka unafikia hatua ya kunichukia namna hii kama una bastola hapo si unie tuu jamani mbona nateseka nasielewi nilikosea wapi?" Omary akainama chini kama vile ameguswa na maneno yangu na yale machozi nikamwambia yule baba "Hao ni watu ambao unaweza kuwauliza kuhusu chochote unachotaka kujua" akasema "Pole samahani sana.." Akamwangalia omary akamuuliza "Una kipi cha kusema?" Akasema "Sina chochote mkuu" nikauliza "naruhusiwa kuondoka?" Akasema "Ndio samahani sana sijui hata cha kusema kwa mokosa aliyofanya kijana wangu,Mimi nimekuelewa na maelezo yako yanatosha" akachukua ile karatasi akatia kwenye dustbin nikasema "kwanza yule mdada alienifata pale kwenye gari kanipiga kibao kinauma sana pili omary amenivunjia heshima na kunidhalilisha sana ndivyo hivyo jeshi linatakiwa kuwa?" Akamgeukia omary kwa hasira akamuuliza "nani alie mfata kwenye gari?" Omary akajibu "Helena" akamuuliza "Nyie mlipewa wapi haki ya kuonea raia?" Omary akakaa kimya yule mzee akasema "Binti sina hata cha kusema samahani sana" nikamwambia "Hii siyo mala ya kwanza mala nyingi Omary ananifanyia vituko vya ajabu ajabu kwakua yeye ana mamlaka na sina uwezo kwa kufanya chochote lakini kilicho niuma sana Omary alisema siwezi kufanikiwa kwa sababu ya ujeuri wangu..Hajui nafanya jitihada kiasi gani kuendesha maisha yangu bila msaada wa mtu yeyote hajui napitia magumu kiasi gani anatoa wapi uwezo wa kunitamkia kauli kama hiyo? Maisha yake si sawa na yangu mimi napambana nahangaika nile au nilale njaa yeye hajui lakini kaenda mbali sana na kunihisi vibaya hanijui hata kidogo na bado kila akiniona haishi kuniumiza" nilianza kulia kwa uchungu aiseeh.. Yule baba akasema "Omary nita deal na wewe badae" akasema "kwaiyo binti nifanye kitu gani cha kukupa ahueni wewe ni kama mwanangu na umenigusa sana" nikamwambia "naomba kazi" huku bado nalia..
Akashangaa "kazi? Sasa hapa jeshini unadhani kuna kazi gani" nikafuta machozi nikamwambia "kwani jeshini maduka ma supermarket hamna?" Akacheka akasemaa "anhaa sawa ila tatizo kuna supermarket inajengwa hapo nyuma haijamalizika utatakiwa usubiri ila kwa sasa chakua nauli hii na ilo swala lako likisha kamilika takupigia simu ach namba yako ya simu na jina pale getini"
Nikachukua ile pesa nikashukuru nikaondoka nikafika getini nikaacha namba yuleeee nikasepaa..
Usiku nikaskia mlango unagongwa nikasema sijui nani tena.. Kufungua Omary huyooo.. kapitiliza mpka ndani kabeba mamifuko nikamuuliza "wewe unaingiaje ndani kwa mtoto wa kike anaye ishi peke yake bila ruhusa?" Akasema 'Kwa sababu anaishi peke yake unadhani ungekua unaishi na mtu ninge ingia?" Nikamwambia "Lakini sijakuruhusu toka" akasema "ningeomba ruhusa usinge kubali..Huna hata kochi kwaiyo wageni tunakaa kitandani" nikamwambia "Siko na mood ya kugombana na wewe naomba utoke" akaweka mifuko chini akajitupia kitandani akasema "nna kiu" nikamwambia "Kufaaa" akasema "Ilo neno unalipenda sana siku nikifa utalia" nikamwambia "Labda kma nitakua nimechanganyikiwa hebu toka mme wangu anakuja yuko njiani usiniletee matatizo" akacheka akasema "Martha kasema upo single alafu ukiangalia kwa upande mwingine na mimi nipo single ujue"
Nikawa namvuta miguu namwambia "Toka toka tokaa ondoka" mara akanivuta nikamdondokea kifuani..😩😩 nikataka kuamka akanivuta akawa kama kanikumbatia akasema kwa upole "Tina nisamehe sana nilikuelewa vibaya nisamehe nimekosea" sa nilikua namwangalia machoni kabla sijajibu mlango umefunguliwa wote kuangalia nani.. Martha.. alivotuona akashtuka akarudi nje.. Nikanyanyuka martha akabamiza mlango akaongea kwa nje "Samahani tina sikujua kama upo na shemeji kwaheri nyie endeleeni mimi naondoka" nikamgeukia Omary kwa macho makali akageukia pembeni..
Nikamwambia "unaona sasa mpka martha kafkiria vibaya?" Akasema "si umemskia kasema tuendelee sasa mbona umesimama tu hapo?" Nikamwambia ww hunijui nikachukua mfagio nikaanza kumpiga nao kanyanyuka kashika mfagio kauvuta tupa kule kanivuta mkono kanikumbatia.. Kamwili kamotrooooooo... Aaaah nini tena hiki namskumiza anasema "Umenisamehe tina?" Nikanyamaza akasema "usipo jibu nalala hapa hapa.." kimoyoni nikasema "sijibu ngoja tuone kama kweli utalala hapa"...
Mjedaaaaaaa mweeeh!!!
No comments:
Post a Comment