Mjeda akauliza tena "Umenisamehe Tina?" Nikamwambia "Toka kwangu bhana" akaniachia kidogo akanishika mashavu akainama kidogo yaani yupo close mpka pumzi yake naisikia kabisaa akasema "Unajua kuna vitu vinakuja bila kutarajia sijawahi kuwaza kama nitakuja kukupenda" nikashtuka hee Mjeda ananipenda nikajifanya mgumu kumbe kama vile namuelewa ujue.. nikamsukuma nikamwambia "Ondoka bhana" nikaenda kumfungulia mlango atoke nikiwa nimesimama pale mlangoni Omary kaja kanishika kiuno akapitisha mikono yake mpaka ikafika tumbo ikakutana akaniinamia yaani kidevu chake kipo begani alafu akasema "Nimejikuta nakupenda Tina" alafu kwa mkono wake mmoja akaurudishia mlango akanigeuza yaani mimi najihisi wa moto kama nataka kulipuka akasema "Naomba tuwe wapenzi" nikamwambia "Sitaki" sauti yangu inatetemeka haiendani hata na nnachokiongea..
Akauliza "Hutaki kwanini si nimeomba msamaha kwa kukuelewa vibaya nimekukosea tuachane na mambo ya nyuma au una sababu nyingine?" Nikasema "Ndio" akanambia "niambie" nikamwambia "Wanajeshi malaya watu wanasema" akaniinamia mpaka pua zetu zikagusana akasema "Nipe nafasi ukihakikisha kwamba mimi malaya utaniacha mwenyewe kama kuna kitu unataka nifanye ili uniamini niambie" Nikauma midomo maana sina cha kujibu mala kesha fikisha mdomo wake mdomoni kwangu.. Akanipa boooonge la kissssss..
Nikasema liwalo na liwe bwana..Nikaanza kuonyesha ushirikiano si mnajua busu kama hilo linazaaga mambo mengine ila wakati tupo kwenye harakati sasa za kuvuka mipaka ya kiss nikajiambia mwenyewe "Jishkilie mtoto wa kike ndo kwanza mmeanza mahusiano unataka umtunuku tayari" Nikakata pale pale kwenye kiss..
Akauliza "vipi?" Nikamwambia "Tusivuke mipaka hatujaoana" akasema "si tumesha kuwa wapenzi?" Nikamwambia "Ndo ulivo zoea kufanya uko au?" Akaniachia akasema "Kwanini unanifikiria vibaya?" Nikamuuliza "kwani nahitaji sababu ya kukufkiria vibaya nipe wewe sababu ulio kua nayo ya kunifikiria vibaya" akasema "Daaah hayo si yameisha Tina?" Nikamwambia "Niliwahi kusema yameisha au kama nimekusamehe yote umefanya wewe kuomba msamaha na kujisamehe umefanya mwenyewe" aka kaa kitandani akaniuliza "Niambie basi natakiwa kufanya nini ili nisamehewe?" Nikamwambia "Niazime hela nilipe kodi nikipata kazi takulipa" akacheka..
Akasema "Yaani kila ukipata nafasi unataka uitumie kule ilikua kazi saivi hela" nikamwambia "Kwani mimi nilikutuma unikosee?" Akasema "Sawa yaishe..Unataka kiasi gani?" Nikamtajia akasema "Takupa kesho mpenzii" nikamtania "Sijakubali bado kuwa mpenzi wako" akasema "Khaaa nahapo natakiwa nifanyeje? Nikununulie private jet au?" Nikamwambia "Hilo taamua mimi baada ya kuona mwenendo wako umebadilika ukiendelea na ule ukatili wako basi mimi umenikosa" akasema "Ndio mkuu nimekuelewa" akanipigia saluti nikacheka..
Nikamwambia "hii mifuko yote umeleta nini?" Akasema "Fungua uone" nikafungua kuna matunda kuna mchele kuna maharage kuna dagaa kuna ungaa duuh.. nikamuuliza "Kwaiyo imekuwaje mpka umeleta vyote hivi?" Akasema "Hauna kazi chakula unatoa wapi? Hii ni zawadi yangu ya kuomba msamaha ila kwakua umetaka kingine basi mifuko yangu narudi nayo" nikamwambia "Unanitania ww huwezi letea mtu kitu na ukaondoka nacho" akacheka..
Mapenzi kati yangu na Omary yameanza..Tumeamua kusahau yaliyo pita sasa tunataka kujenga mahusiano..Je kwa mwenendo wake na hasira zangu tutafika kweli? Maana kila mtu anataka kuwa top kwa mwenzie yeye kwa mamlaka yake mimi kwa pride yangu..
Ep 10...Will tell you everything as for now..Bye Bye.!!
No comments:
Post a Comment