STORY: PENZI LA MJEDA EP 7 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, February 10, 2020

STORY: PENZI LA MJEDA EP 7






Nikatoka kumfata mjeda akaniongoza mpaka kwenye gari tena gari la jeshi.. yani hapo sielewi kabisaaa..
Hatimae tumefika kwenye kambi ya wajeda kashuka kaanza kuondoka sa najiuliza huyu mtu namna gani kashuka ananiacha? Ile nashuka tu wakaja wajeda wawili wakike mmoja akasema "Habari yako binti" nikasema "Safi shikamoo" hakuitika akasema "Nifuate" nikamwambia "Nikufate wapi mm nimeletwa na yule kule anaye ondoka" akasema "Unadhani ningejuaje kma angekua hajanambia? Acha maswali nifate"  Basi nika kaa kimya nikamfata..

Akanipeleka mpanga kwenye chumba kimoja ofisi siyo ofisi store siyo store yani hapaeleweki..
Akasema "Unaitwa nani?" Nikamwambia "Naitwa Tina" akasema "Tina mana ake nini christina au martina au nani?" Nikasema "Jina langu ni Tina tuu halina kirefu" akasema "Kwaiyo wewe ndo master plan wa mambo yote yaliyotokea arusha si ndio?" Nikasema "hapo sijakuelewa dada" akanipa kofi.. akasema "Huu sio wakati wa kubembelezana tubu makosa yako na adhabu yako itapungua" nikamwambia "Dada mimi nashindwa kukuelewa unazungumzia nini?"

Mda hule hule akapigiwa simu akaweka loudspeaker nikaskia sauti ya mjeda inasema "Uko wapi mbona humleti kiongozi ana msubiri" akasema "Nakuja" yule dada akaniangalia kwa hasira alafu akasema "Ukienda kwa kiongozi ongea ukweli la sivyo utapambana na mimi umenielewa?" nikasema "ndio" akamwambia yule mjeda mwenzie wa kike "msindikize huyo" yule mwenzie mda wote alikua kimya wakati ananipeleka ndo nikamuuliza "Dada eti nini kinaendelea au ninakosa gani? Samahani kama unajua naomba uniambie nipo gizani yani najiskia vibaya sana na nnaogopa mno" Akasema "Omary alikua katika kambi ya arusha yapata kama mwezi lakini kule amenusurika kufa mala nyingi sana nje na hata ndani ya kambi kwa madai yake mitego yote alikua anategewa ilikua ya kawaida hivyo kwake ilikua rahisi kutegua ila kwa upande mwingine alikua na hatari kubwa ya kupoteza maisha sasa alikua anataka aanze kufanya uchunguzi wewe ni mmoja kati watu alio kuwa anawahisi wanatumiwa na watu wabaya kumdhuru na amethibitisha kwamba hivi karibuni ali ku provoke na ukasema bora angefia huko alikokua sasa wewe ulijuaje kama alitaka kufa kama hauhusiki?"

Heeeh nguvu ziliniisha nikamuuliza kwaiyo mimi hapa ni mtuhumiwa? Hivi huyu kaka anawazimu au? Nikamuuliz yule dada "Dada kwaiyo na wewe una amini hivyo?" Akakaa kimya nikamwambia "Dada akyamungu mimi sijui chochote mimi mwanamke mwenzako nisaidie yule kaka ana matatizo" yule dada akasema "Mimi sihusiki na chochote ofisi ile ndo unatakiwa uingie" alafu akageuza akaondoka..

Dah ikabidi nifike mpka pale nikasema "hodi" nikaskia sauti nzito inasema "ingia" nikaingia nikamkuta mbaba wa makamu tu amekaa kwenye kiti na Yule mjeda sasa ambaye ndo nshajua anaitwa Omary amekaa kwenye kitu kingine pembeni.

Nikamsalimia yule mbaba "shikamoo mzee" akasema "marahaba keti(akinionyesha kiti nikae)" nikimwangalia Omary sipati majibu yaani huyu amenichukulia mimi jambazi au kitu gani?

Itaendelea...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa