STORY:PENZI LA MJEDA EP 5 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, February 10, 2020

STORY:PENZI LA MJEDA EP 5






Ile picha ya mjeda ikawa yani inanirudia kichwani tu lakini nilikimbuka hatupatani basi picha yote inapotea hasira zinanishika.

Basi mambo yaliendelea na mfa ukapita sijaonana na mjeda wala sijamfatilia yaani nikaendelea na ratiba zangu kama kawaida siku moja ikatokea business trip kwenda arusha kampuni nlio kua nafanyia kazi wakaniteua mimi kwenda kama mwakilishi wa kampuni kwaiyo kila kitu kikaandaliwa nikakabidhiwa ticket ya bus na pocket money. Nikauliza nafikia wapi nikaambiwa si mimi peke angu kuna kampuni mbali mbali zinaenda ila tutafkia kwenye kambi ya jeshi na tutakaa kwa muda wa siku tatu.. Basi mtoto wa kike nikajiandaa vyema kwa ajili ya safari kesho ambayo ndo kesho yake natikiwa kwenda

Usiku nikiwa nimelala nikapigiwa simu mama yangu amezidiwa ghafla na sasa yupo ICU..Nilikurupuka nikasahau hata simu wala kufunga mlango nikakimbia kuelekea kwa hospital niliyo elekezwa nilikumbuka nauli tu yaani nilipanda pikipiki fasta mpka hospitali..

Kufika naambiwa hali ya mama yangu ni mbaya sana kilicho baki ni kusali tu yaani Mungu afanye muujiza nilikaa pale nje ya wodi ya ICU mpk kunakucha maana sikuruhusiwa kuingia madaktari walikua bado wanapambania uhai wa mama yangu. Mpaka madaktari wanakuja kutoka nje ya ile wodi ya ICU kumekucha asubuhi tena bado sikuruhisiwa kumuona mama kila anayetoka mle nikimuuliza anapita tu baba akawa ananitia moyo "Tulia mama atakua sawa,usiwasumbue madaktari"  nilimkata baba jicho kali sana maana hakuwahi kumjali mama sababu kubwa iliyo nifanya niondoke nyumbani ni baba alikua mlevi sana na kila akilewa basi mama anapokea kipigo mpaka basi mama hata umshauri vipi anasema hiyo ni ndoa yake na ndo mwanaume alie mchagua siwezi kuelewa mpka nitakapo olewa kwakweli mama sikua namuelewa na kuendelea kumuendekeza baba licha ya unyanyasaji wote niliamua kuondoka nyumbani.

Nakumbuka siku hiyo naondoka mama alipigwa mpka akawa anatema damu na mwisho wa siku alizimia baada ya matibabu nilimshawishi mama tuondoke Mimi nitamtunza hataki nilimwambie basi twende polisi au stawi wa jamii jibu lake lilikua "Huyu ndo mume nilio mchagua kama kufa wacha nifie mikononi mwake" nilimwambia mama "Huyo mume wako mimi namfunga" mama alisema "Hajakugusa hata kidogo na kama ni polisi ushahidi huna na mimi siwezi kukubali mume wangu afungwe bora nipoteze mtoto kuliko mume" Mimi niliamua kuondoka kuwaachia ndoa yao.

Lakini kila siku mama alikua anazidi kukonda na kulalamika nikimpa ushauri hataki anasema kua uyaone. Nilimwambia mama "Huyo unaye sema mumeo na baba yangu siku moja atakuua"

Tikiwa pale dactari mmoja akasema "Nyie ni ndugu wa marehemu?" Tulisimama kwa mshangao sana nikauliza "Marehemu? Doctor marehemu gani? Mama yangu yupo huko ndani" Akauliza "Marysiana Mapunda?" Nikajibu haraka haraka "Ndio doctor huyo ndo mama angu..Saivi naruhusiwa kumuona?" Doctor hakujibu ila alipisha mlangoni akimaanisha tuingie.

Nikakuta wauguzi wengine wamesimama pembeni kwa wakati huo sikutaka kujua wala kufatilia chochote zaidi ya kujua hali ya mama.. Ila kila nikisogea naskia kama miguu inakufa ganzi na nguvu zinaisha maana mama kafunikwa shuka jeupe mpaka usoni. Nikamuuliza doctor "Mama yangu atapumuaje ukimfunika hivo" nikasogea taratibu mpaka nikamfikia mama nikawasukuma wale wauguzi wengine wanipishe doctor nliskia anasema "Poleni sana,saa moja na dkk 36 asubuhi tarehe 11 mwezi wa 3 mwaka 2010 marysiana Mapunda amepoteza maisha innah lillah waihna lillah rajiuni" nguvu ziliniisha miguu ilishindwa kusimama tena aiseeh nilipoteza fahamu nakuja kushtuka kitu cha kwanza namuona mama mdogo nikasema "Yesu wangu mamdogo umefika sa ngapi bila tarifa?nimechelewa aiseeh ninatakiwa kwenda arusha leo kikazi utanisaidia kuaga kwa mama mwambie nitampigia nikifika ngoja nikajiandae" naona mamdogo kasimama tu haongei wakati kawaida yake angesha nitukana nimechelewa kuamka.

Mala mamdogo anisogelea ananikumbatia anasema "Tina tufanyeje? Tina dada hayupo tena Tina dada yangu amekufa" mamdogo ana angua kilio kabla sijauliza dada ako yupi namuona baba anaingia kuangalia vizuri nipo hospital nimelala kumbu kumbu zinanirudia khaaaa Mama!! Mamaaa!!! Mama yangu!!! Mama amekufa mamdogo!!! Kilio kikaanza hapo...

Itaendelea.....



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa