Nililia sana moyo wangu uliuma mno baadaye tuliambiwa mama kilicho sababisha kifo chake ni maini yalijaa maji.
Taratibu za mazishi zilifanyika niliazima simu kwa mtu nikampigia Martha na kumpa taarifa kisha nikamwambia anifungie nyumba yangu nilitoka kwa haraka sikuweza kufanya kitu chochote kile. Alifanya nlivo mwagiza akaja msibani mazishi yalifanyika matanga yalikalika na hatimaye msiba ulikwisha.
Duuuh baada ya msiba ndo nakumbuka kwamba kuna safari nilitakiwa kwenda na sijatoa taarifa na sijaenda. Nilikuta simu yangu imezima maana ni muda mrefu tangu nimeiacha usiku ule. Nili iweka charg na kuiwasja kulikua na missed call nyingi sana kutoka kwa boss wangu sikutaka kumpigia simu ila nilienda kazini moja moja.
Kufika kazini boss hataki kuonana na mimi na secretary alisema kuna ujumbe wangu kutoka kwa boss. Well ilikua ni barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la kuifelisha kampuni na kutoweka bila taarifa yoyote dah... Nilifanya jitihada za kuonana na boss lakini zilikwama tena alikua mwarabu yaani akisema neno moja hataki maelezo pamoja na hayo niliandika sana barua za kujielezea na kuomba msamaha lakini sikupata majibu chanya hivyo niliacha maana kisicho riziki hakiliki.
Niliendelea na maisha yangu kma kawaida na balance ndogo nliyo kuwa nayo ndo ilinisaidia kusukuma siku nilikua nahangaika kutafta kazi bila mafanikio. Siku moja natoka kanisani nikakutana na mjeda paaaap kavaa gwanda na yuko na mabegi kama ametoka safari. Kiasi flani nilifurahi kumuona ila nikaweka sura ya mbuzi tu nikawa nampita akasema "Kwaiyo pesa yangu hutaki kuilipa au?" Nikamwambia "Nahisi nitakua na nembo ya crdb usoni kila ukiniona unawaza pesa tu alafu hela yako si nilikulipaga au?" Akasema "Bado una ujeuri umekujaa kwa staili hiyo huwezi kufanikiwa kwa lolote" lile neno lilinikera na kuniuma sana "ujeuri? Nimemkufanyia ujeuri gani? Kwani kila ukiniona unakua na ibilishi gani wakati haupo nilikua na amani ungefia huko huko" nikawa naondoka kwa hasira kumbe na yeye lile neno lilimuuma sana.
Nikafika nyumbani mda kidogo Mlango ukagongwa kutoka mjeda nikamwambia "Unasemaje?" Akasema "Unahitajika jeshini" Heee "Kiaje tena imekuaje mpk nihitajike jeshini?" Akasema "Utaenda kujua mbele ya safari" nikamwambia "Kaka naomba unieleze ili nijue naenda kufanya nini?" Akasema "Utaenda au unaleta ubishi? Sina muda wa kupoteza hapa" Duuh nikaona mambo siyaelewi nikasema "Nitaenda" akasema "Namaanisha sasa hivi..Naongozana na wewe yaani mimi ndo nakupeleka na si vinginevyo"
Tena sura yake imejaa hasira macho ameyakaza kias kwamba anataka anivunje vipisi vipisi..
Sikuweza kubisha wala kuweka pingamizi japo sina hakika nini kinaendelea. Moyo unadunda nna wasi wasi yaani sijui hata niwaze nini kila ninacho otea haki make sense.
Nilifunga mlango wangu nikatii sheria bila shuruti nikajue huko jeshini kunaniiii....
Itaendelea..
No comments:
Post a Comment