STORY:PENZI LA MJEDA EP 4 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, February 10, 2020

STORY:PENZI LA MJEDA EP 4






Nilijiskia vibaya sana kwa alicho kifanya Martha ukizingatia mimi na huyo mjeda hatupatani hata kidogo kwaiyo kama vile kampa ushindi mjeda. Ila nikasema sawa nitajua jinsi ya kukabiliana naye..

Kesho yake ilikua weekend wakati naenda sokoni asubuhi nikamona mjeda anakuja usawa ule nnao pita mimi nikabadilisha njia fastaaa..kumbe kaniona akawa ananifata mm sijui nikafika mpk kwenye kona nikajibanza ili yeye akipita tu na mimi niendelee na safari zangu.. Naona mbona hapiti sasa nachungulia ili nione amefika wapi nakutana na sura yake na yeye ananichungulia nilishtuka nikapiga kelele "Mamaaaa" akasema "Ndo alio kwambia ujifiche?" Nika kaa kimya nikasimama vizuri kutoka katika pozi la kujificha..

Nikasema "Shikamoo" alafu ghafla nikajishtukia hee nimemsalimia? Akaniangalia tu nilikua nimeinamisha kichwa akasema "Kwani wewe una matatizo gani?" Nikamwambia "Sina matatizo yoyote" akasema "Hudhani kma kuna maelezo unatakiwa kunipa?" Nikamwambia "Hapana sina maelezo yoyote" akasema "oooh kwaiyo kila alichosema rafki ako ni kweli?" Nikamwambia "Hebu acha kuniuliza maswali kma vile mimi ni mtuhumiwa kamuulize alie ongea vyote vilivyo ongeleka hakuna hata kimoja kinacho husiana na mimi,kwa heri"

Wakati naondoka akasema "Hela yangu unanizurumu?" Nikamgeukia nikamuuliza "hela ipi?" Akasema "Unajifanya umesahau kwenye chips siku ile" nikamwambia "Takupa nikitoka sokoni" akasema "Nipe saivi" nikamwangalia kwa hasira nikarudi nikampa elfu tano nikamwambia nipe chenchi.. akasema "Twende ukachukue chenchi nyumban wewe siku ile si ulitaka nikachukue hela kwako" nikamwambia "Achana nayo..Mimi siyo mbinafsi kama wewe hata chenchi kaa nayo" nikaondoka kwa hasira.. akasema "Wewe chukua hela yako" Nikaondoka kurudi nyumbani nikiwa na hasira hata siku geuka nyuma..

Nikafika nyumbani nikampigia Martha "Wewe mwanamke mchana unapika nini?" Akasema "Ugali na nyama" nikamwambia "weka share yangu nakuja" akacheka akasema "Nilidhani umeninunia" nikamwambia "Achana na mimi,wewe jua nakuja kula" nikakata simu.

Kwakua ilikua asubuhi nilifanya shughuli zangu zote zinazo nihusu pale nyumbani nilifua nikafanya usafi mida ya sa 6 nikaenda kwa martha sa kwa martha ni jirani na kwa mjeda.. Wakati napita pale kwa mjeda nikamuona anafua kavaa Vest na pensi ya kijeshi.. Kaweka earphone maskion anafua huku anaimba..

Ilibidi nisimame aiseeh yule mkaka mzuri wallah najikuta tu natamani kumuangalia nikajisema _Mkaka mzuri ila roho mbaya kama nini_

Ile ndo nataka kuondoka mala kainua kichwa akaniona namuangalia nikashtuka nikaendelea na safari yangu fastaaa..Nikaingia kwa martha huku nahema juu juu.. Akasema "Wewe vipi una kimbizwa au?" Nikamwambia "Haikuhusu mabalaa yote haya sababu ya mdomo wako usio kua na break huo" Akasema "Jamani si yaishe nishaomba msamaha au..Eh Tina unapenda kuongea jamani" nikamwambia "Tatizo hujuagi kusoma nyakati" akasema "Basi mama chakula kinapoa"

Tukawa tunakula akasema "Ila yule mkaka anakaa nyumba hiyo karibu na yangu hapa" nikamwambia "Najua..Na wala sijakuuliza" akacheka akasema "Ila kiukweli unajua mnaendana" nikamwambia "Hata wanaume wote waishe duniani siwezi kuwa na uyo mtuu" akasema "Maneno hayo unayatupa ujue" Nikamwambia "Bwana kma umeshiba niache mimi nile"

Ila kichwani picha ya mjeda alivokua pale nje inajirudia tu eti natabasamu peke yangu.. Sijui mududu kaingia kwenye hii kichwa yangu?






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa