STORY:PENZI LA MJEDA EP 19 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 12, 2020

STORY:PENZI LA MJEDA EP 19






Kabla hata hajanipiga nikawa nalia "nakufaaa nakufaaa mama weeeh.. Omary usinipige..Omary utaniua"
Omary akasema "Kufa.. Kufaaa kafie mbali" cha ajabu badala ya kunipiga mimi akawa anapiga kitandani.. anasema "Leo nakumaliza" mimi kwa uoga nalia "Nisamehe,Niache niondoke" Kasema "Hakuna kuondoka na kwenye harusi lazima kuja" kaanza kupiga chini sasa mimi nashagaa mbona hanipigi mimi yaani hapo machozi yanatoka naogoga hatari. Nikaskia sauti ya baba mkwe "Omary fungua mlango" Omary akanisogelea akanivuruga vuruga nywele akanitupia shuka maana nlikua na kishati tu alafu akanibana   akaishua ile shati kidogo bega moja likawa wazi hapo anafoka tu mimi simuelewi..

Baba mkwe akasema "Omary fungua!!" Omary akanitupia ule mkanda miguuni akafungua mlango baba mkwe akaingia na mama mkwe na Wifi mama mkwe alivo niona pale chini akanisogelea haraka akasema "Mwanangu nini kimetokea pole mama umeumia wapi?" Akawa ananifuta machozi kiukweli sijaguswa na sijaumia popote ila najiuliza nini kinaendelea? Nikifkiria kuoa kwa Omary nikaanza kulia kwa sauti mama ananinyamazisha mama akasema "Kama huwez kukaa na mtoto wa watu acha kumtesa mrudishe nyumban kwao" Baba mkwe akasema "Akiona hawez kuvumilia aondoke mwenyewe" mama mkwe alishikwa na hasira akachukua ule mkanda pale miguuni kwangu wacha awatandike watu si wifi si baba mkwe wala Omary aliwachapa mpka wakatoka nje baba mkwe anasema "Wewe mwanamke umepandwa na kichaa unanipiga utajuta" Mama mkwe hajali akasema "Nijute? Nijute mala ngapi? Mpka saiv maisha yangu yote ya majuto nlikua naishi kwa ajili ya Omary lakin Omary mwenyewe nimesha mpoteza amekuwa mnyama kama baba ake siogopi tena chochote"  Baba mkwe anasema "Utajutia nakwambia" Mama mkwe anamfata baba mkwe anampiga anasema "Utanifanyaje? Utania kama baba ake Omary ulivo muua?"

Heeeeh mama leo karopoka kumbe wifi alikua hajui baba mkwe akasema "Acha kuongea uoumbavu mbele ya watoto" mama mkwe akasema huo sio upumbavu Bali ni ukweli wanatakiwa wajue kwamba wewe ni mtu wa aina gani na wanatakiwa wajue mama yao nauwawa mda wowote"

Baba mkwe akamkamata mama mkwe akampokonya ule mkanda akautupa chini akamuangalia kwa hasira sana mama mkwe akacheka akasema "Haha unataka kuninyonga? Kunipiga risasi? Unadhani nakuogopa wewe muuaji mbwa wewe?" Baba mkwe akamkata kibao mama mkwe akasema "Badooo hapo badooo? Hizo ndo nguvu zako? Ndo umenipiga hapo? Unapigaga hivo? Nivue nguo wanao waone unyama na ukatili wako? Nipige mpk uniue mbele ya wanao usije kusingizia nimekufa ghafla mala niliumwa niue hapa hapa" yaani mama mkwe anaongea kama amechanganyika hana uoga wala ule upole tulio kuwa tumeuzoea..

Baba mkwe akasema "Nitakuaa wewe" Mama mkwe akasema "Mmesikia? Mmesikia alivo sema? Omary umeskia? Nyote mmeskia ataniua..haya utaniua lini? Sema kabisa nijiandalie jeneza zuri mwenyewe au na mm utanitupa majini? Fanya haraka nikaungane na mpenzi wangu huko aliko unanichelewesha khaa nimechoka nimekaa kama mfungwa miaka karibu thelathini leo hatimae nimepata ujasiri wa kuongea tena najua ni kwasababu nakufa mda si mrefu.. kwanini? Kwasababu wewe ni shetani.. mnyama unaejifanya malaika machoni pa watu gaidi lilijificha kwenye gwanda za jeshi"

Wifi alikua analia kama kuna msiba Omary mwenyewe kama vile amepigwa na butwaa kwa yale anayo yaona na kuyaskia wifi akasema "mama ni kweli unayosema?" Mama mkwe akasema "Umemskia akibisha? Muulize we si ndo mwanae kipenzi?  Si unafatisha kila anacho sema? Mpaka sasa mmeshaua watu wangapi pamoja nae? Amesha kufundisha uovu kiasi gani?" Wifi akawa analia "anasema mama si kweli sivyo unavyosema" mama akasema "Mimi na Omary mnatutenga mnafanya yote mannayo jiskia eti Omary mtoto wa mama eti mimi sijasoma kwaiyo akili sina? Haha heri heri hivyo Omary mtoto wa mama lakini hajawahi mwaga damu.. Mimi sijasoma lakini nnajua jema na ovu siamini kama wewe ndo mwanangu nilie kuzaa kwa uchungu hivi unajua umenitesa kiasi gani mimi?kujifanya kila kitu wewe na baba yako? Kujichukulia maamuzi juu yangu? Sina sauti kwako? Hunipi heshima ya mama siamini kama wewe ni yule nilie kuzaa" mama mkwe aliongea huku analia yaani alikua analia vibaya sana kiasi kwamba hata mimi nilishindwa kujizuia..

Mama mkwe akamkumbatia Omary akasema "Asante mwanangu Asante kuwa mtoto bora kwangu siku zote niliheshabu nna watoto wawili lakini sikujua mwingine yuko wapi maana hajawahi kuniangalia mimi kama mama yake" wote na Omary walikua wanalia baba mkwe alitoka nje akawasha gari akaondoka... Mama mkwe alilia mpka akaishiwa nguvu mikononi kwa Omary.

Omary alimbeba akampeleka Chumbani kwake akamlaza.. Wifi alikua sebleni analia nilimwangalia sijui hata cha kusema nnashindwa kumbembeleza nashindwa kufanya chochote.. Baada ya mda kidogo Omary aliniita akasema "Naomba umwangalie mama mimi ninatoka" nikamwambia "unaenda wapi?" Akasema "natoka nitarudi" akaondoka wifi nae akaondoka.. kwakua ilikua asubuhi nikafanya shughuli zote za nyumbani na kumwangalia mama..

Mchana Omary alikuja akatoa taarifa kwamba haijalishi nini kimetokea ila mipango yake ya ndoa itaendelea kama kawaida na tena ndoa itafungiwa hapo hapo nyumbani maana kuna uwanja wa kutosha alivo maliza kuongea aliondoka bila kuskiliza maoni ya mtu yyt mama mkwe alijiskia vibaya sana na aliniangalia kwa huruma lakini hakuwa na chakufanya.

Baba mkwe alirudi nyumbani jion na kuendelea kama hakuna kitu kilicho tokea jambo ambalo lilimtia hofu sana mama mkwe hata mimi kwakweli niliogopa na kuhisi baba mkwe labda anampango wa kando..

Usiku mama mkwe alikua anaogopa kwenda kulala na kuhofia labda chochote kinaweza kumtokea lakini wifi alikuja sebleni akasema "Mama kama unaogopa kwenda kulala baba hawezi kufanya chochote" Mama akasema "Hujui unachokisema kaa kimya" wifi akasema "Hapana baba ninamjua hawezi kukurupuka kufanya chochote maana harusi ya Omary wiki ijayo labda Harusi ikiisha ndo ataweza fanya chochote ila saivi hawezi"

Mama akasema "sawa" wifi alivo ondoka mama akasema "Hata huyo simuamini yeye na baba yake kitu kimoja" nikamwambia "Hata mimi sitaki kulala chumbani na Omary" mama akasema "Unaonaje tukichukua godoro kwenye chumba cha wageni tukatandika hapa tukalala? Maana hata chumba cha wageni naogopa kulala" nikasema "Sawa" tumemaliza tu kutandika godoro tunataka tulale Omary kaja akasema "Tina kulala chumbani nyanyuka hapo" ndo kwanza nikajiliza nikalala..

Hapo bado siku kadhaa tu ndoa inafungwa daaaaah..

....Instagram:epiphaniafrancoofficial



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa