STORY:PENZI LA MJEDA EP 20 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 12, 2020

STORY:PENZI LA MJEDA EP 20






Omary akawa ana force nikalale chumbani.. nikamwambia "siwezi kumuacha mama hapa.." akasema njoo kuna kitu nataka tuzungumze.. nikasema "Sitaki niache nilale" akachuchumaa akasema "Hivi unadhani kweli mimi naoa au? Njoo tuongee" mama akasema "Nenda hakuna shida"

Basi nikanyanyuka tukaongozana mpaka chumbani akasema "Samahani mpenzi wangu siku hizi nimekua nakuumiza sana nisamehe lakini nna plan ndo mana nilifanya yote hayo" nikasema "una plan gani?" Akasema "Hiyo utaijua tuu ila kikubwa we endelea kuonyesha kama umenichukia kabisa" nikasema "Sawa ila usiniambie maneno makali kama yale unajua mimi maneno huwa yananiumiza sana" akanikumbatia akasema "usijali mke wangu nisamehe" nikaanza kulia huku akiwa amenikumbatia akasema "Unalia nini tena?" Nikamwambia "Nilijua ndo umeniacha kweli.." akasema "hiko ni kitu kisicho wezekana ila kuna mtego nilitega ndo mana nilisababisha ugomvi kati yetu na badae ugomvi ukawa mkubwa kiasi kile na mtego wangu ulifanikiwa zaidi ya nnlivo dhani nasubiri siku maalumu ya kulipua bomu" nikamwambia "Hebu nitoe gizani niambie tu ukweli" akasema "Baba aliweka Cctv camera ambayo inaweza kurekodi maeneo yote ya nje na mwisho ni sebleni yani kama mtu anaingia kupitia mageti yote maana kuna mageti matatu anaonekana na mpka sebeleni inachukua kasoro tu vyumbani. Hiyo iko active masaa 24 na inarekodi mpaka sauti sasa mimi ule ugomvi wote wa sebleni mpaka mama kusema matendo ya baba ime kua recorded unadhani hiyo familia itakubali kunipa mtoto wao na istoshe baba kadanganya kwamba kuna mwanamke ananifatilia ila hajasema kama nna ishi na mwanamke tena ni mja mzito"

Nikamwambia "kwaiyo unataka kufanyaje?" Akasema "Usijali utaona kwani si bado siku tatu tuu"   mtoe mama wasiwasi.. usijali kuhusu dada angu yeye ndo anatakiwa abadilike asikuumize kichwa" nikasema "Sawa nimekuelewa" tukakumbatiana tena.. Tukalala..
Asubuhi kila mtu kaendelea na mishe zake kama kawaida nikamwambia mama kila kitu.. mama akapata amani ya moyo akatulia kabisa mchana baba mkwe akasema anamtuma mtu analeta mzigo nyumban ilikua ni nguo pamoja na viatu akasema tujalibishe kisha tutoe majibu mimi na mama tulijaribisha na nguo zikatukaa fresh tukatoa majibu nguo tumezipenda tunashukuru.

Jion Omary katoka kazini kaja na begi ila linaonekana limejaa akaniita chumbani kwa njia ya msg nikaenda weeeh napewa shera naambiwa "Tina hata kama hujalipenda mimi ndo nimelipenda na nnajua litakupendeza" nikavaa nikajiangalia kwenye kioo yani nikabaki mdomo wazi akasema "vipi" nikamwambia "yani umenipatia aiseeh nguo imenikaa kama ulinipima"

Akanipa na viatu,viatu vina meremeta hatari akasema "niliangalia saiz ya mguu wako kwaiyo usiseme havikutoshi" nilipendeza sana mpaka nikawa natamani yani tufunge ndoa mda huo huo aiseeh.. hapo tumebakiza siku moja inayofata ndo harusi ya Omary.. Nilivo jaribu nguo na viatu akanipa na crown ya kichwani yani doh nilipendeza sana. Basi badae nikarudi zangu sebleni mda wa kula Omary akasema "Tina kesho ndo siku ya kwenda clinic?" Nikamwangalia maana kwa kumbukumbu zangu sija anza hata clinic ila nikajua huyu ana mpango wake labda.. nikasema "ndio" akamgeukia mama akasema "Mama si unaweza kunisaidia kumsindikiza kesho kuna sehemu naenda na mchumba wangu nnaye takiwa kumuoa" mama akasema "Hivi wewe una akili kweli? Mimi nimpeleke clinic ndo mme wake? Wewe uende kwa mwanamke mwingine umechanganyikiwa au?"
Omary akasema "Basi kama hutaki ataenda baada ya ndoa" nikasema "Mama naomba tu unipeleke haya mambo yaishe amesha amua kuoa tusimuingilie si unajua mapenzi hayalazimishwi" Wifi akaniangalia akasema "Takupeleka mimi" mama akasema "Wacha tampeleka mwenyewe" Omary akasema "Imeisha iyo tawapeni lift nikiwa natoka" hakuna aliye jibu wakati wote baba mkwe alikua anakula tu..

Tukiwa chumbani nikamuuliza Omary "Una mpango gani kuhusu kesho?" Akasema "Ndoa" nikamuuliza "Ndoa kiaje?" Akasema "Kukuoa" nikasema "sijakuelewa" akasema "Tulale mke wangu" Kesho yake nikajiandaa asubuhi na mama pia akajiandaa Omary alikua anatusubiri kwenye gari tukaingia safari ikaanza mama akauliza "Tunaenda wapi Omary?" Omary yupo kimya mama akaniangalia kama najua chochote nikatikisa kichwa kuonyesha kama sijui kitu tumeenda mala gari inapaki nje ya saluni kuangalia vizuri Martha yule rafiki angu yupo nje amesimama alipo ona lile gari akaja akafungua mlango nikabaki nashangaa akasema "Yani kunisusa kote kumbe sababu ya ndoa watu mna roho mbaya jamani" Omary akasema "Mama shukeni" Tukashuka tunashangaa Martha akasalimiana na mama alfu akamshika mkono kumuongoza ndani nikabaki na Omary pale nje nikamwambia "nini kinaendelea?" Akasema "Argh akayanani Tina una maswali mpaka basi" nikasema "Sasa unataka nisiulize au?" Akanivuta mkono kunipeleka ndani nakuta mama amesha anza kupambwa na Martha pia Mmmgh nikaonyeshwa kiti nikae na Mimi nikaanza kupambwa Omary akasema "Jamani umakini unahitajika mke wangu huyo" mama mkwe akasema "Kwaiyo mama ako hahitaji umakini? Omary akasema "Bwana wewe usha zeeka unataka nini tena wewe mama?"
Tukacheka wote..

Inaendeleaaaa...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa