STORY:PENZI LA MJEDA EP 18 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 12, 2020

STORY:PENZI LA MJEDA EP 18







Mimi nikasema ngoja nilale katoka kuoga kapanda kitandani kulala kaanza uchokozi anataka mpwipwi namuangalia anavo hangaika yaani hata hamu ya mpwipwi naitoa wapi?? Nilikua nimelala zangu na kitisheti tu chepesi kirefu kidogo mpka mapajani akahangaika mpka kakivua mimi nimetulia sioneshi ushurikiano wala nini.. akinisemesha mie kimya.. akauliza "kuna kitu nimekukwaza?" Kimoyoni nikasema "Hivi anauliza hajui au anauliza ujeuri tu" nikakaa kimya alivo ona nipo kimya akaendelea na shughuli yake ya kutafta mpwipwi.. Kaanza kunipapasa kifuani kashuka mpaka tumboni aaaah mkono ushafika kunako makazi ya mpwipwi.. mie nimetulia tu kama siskii kitu.. kumbe moyoni natamani aendelee japo nna hasira ila mpwipwi ni swala jingine bhana..

Kafanya zake utalii wa ndaani alipo ona ametosha kampanda farasi wake kaanza kuendesha kwa raha zake hana wasiwasi mie nmetanua miguu tu wala sioneshi ushirikiano ila moyoni najua yaani hapo ulipogusa ndo penyewe na yeye anajituma ili niongee lakini mimi walaaaa..Natamani kuongea nashindwa natamani kutoa sauti lkn ndo nimefanya maamuzi ya kumkaushia nimetulia tuuuuli..

Mpaka bwana mkubwa kamaliza shughuli yake na mie nishakunwa vya kutosha wala sikuongea chochote nikanyanyuka nikaenda bafuni nikajimwagia maji nikarudi kulala.. Na yeye akalala alivo pitiwa usingizi nika amka nikachukua ila simu pale mezani nikatoka nayo mpka bafuni nikafunga mlango kwa ndani nikaweka betri nikaiwasha..

Kuiwasha tu nikaitoa sauti nikafunika sink la choo alafu nikakaa sasa nianze upekuzi sehemu moja baada ya nyingine.. nikaangalia simu ya mwisho kuongea nayo namba imeseviwa "Kamanda" bila shaka ndo ile alikua anaongea nayo kabla sijaingia chumbani.. Nikaenda kwa msg Mtumeeee simamaaaaa.. Naona mbona kama nguvu zinaniisha? Mbona kama naota? Au kweli naota nikafungua bomba kwanza ninawe uso labda wenge la usingizi linanipeleka kushoto..

Msg kati ya kamanda na Omary..
"Kadi ziko tayari waalike watu unaotaka waje alika wote kasoro huyo mwanamke wako" omary kajibu "Sawa usijali" msg ingine "Lini tunaenda kununua nguo za harusi?" Omary kajibu "Maliza wewe kila kitu mm nitakua busy kdg ila takutumia size zangu za nguo na viatu"

Na msg nyingine nyingi ila yote kwa yote omary anafunga ndoa tena wiki ijayo yaani wiki hii inaisha inayo fata ndoa? Nikiangalia chatting zao mbona mawasiliano hayana muda mrefu? Nikaangalia ile namba WhatsApp kwenye simu ya Omary Heeeeh huyu? Kumbe huyu dada ndo anaolewa na Omary? Nilishtuka sana maana ni mtoto wa mtu mkubwa sana katika nchi na ni mrembo si kidogo pesa ipo sio kitu cha kuuliza na yule dada ni mtu mkubwa yeye mwenyewe anajishughulisha na mambo ya fashion yaani ni maarufu pia..

Roho iliniuma sana nililia mno mle bafuni ila nikasema ngoja nilale tutaona itakavo kuwa. Nikarudisha kila kitu kama kilivo kua alivokua ametoa betri na kila kitu nikarudisha nikapanda kitandani..

Kila nikifkria Omary anaoa naumia.. kwaiyo mimi na mama ndo hatujui kinacho endelea wengine wote wanatuchora tu? Omary wa kunifanyia hivi kumpenda kote huku? Mimi mjinga sana.. Kiherehere cha kupenda kimeniponza.. kwaiyo itakuwaje maisha yangu.. Mtoto wangu? Daaah siamini macho yangu...

Usingizi sijui ulikuja sa ngapi ila nilishtuka Omary ananiamsha na ilikua tayari asubuhi macho yamenivimba hatari akasema "Ulilia?" Nikasema "Kwanini?" Akasema "Macho yamevimba kama mtu aliokua analia" nikasema "Hapana kwani hujui kama huwa naumwa macho?"

Akasema "kwanini uliwasha simu yangu wakati nikikwambia uiache kama ilivo?" Nikamwambia "mimi sijawasha cm yako!" Akasema "Unadhani kuna kitu unaweza fanya mimi nisijue? Simu nilivo iweka sivyo nilivo ikuta usisahau kama mimi ni mwanajeshi"  Nikasema "Ni kweli mimi siwez fanya kitu wewe usijue ila wewe unaweza fanya vitu mimi nisijue na siwezi kusahau kama wewe ni mwanajeshi kwasababu ndo kitu pekee kinacho nikumbusha kama sistahili kuwa na mtu mkubwa kama wewe"  Aka kaa kitandani akanisogelea akasema "Kuwasha simu niliyo kwambia usiwashe umeona haitoshi mpka ukague na mambo yangu?" Nikamwambia "Ungejua kuna vitu vya siri havitakiwi kuonekana ungeweka password"

Basi mzozo ulikua mkubwa nashangaa Omary anapandisha sauti kana kwamba anataka nyumba nzima wajue tuna gombana akawa anapandisha sauti anafoka namfatilia namuingilia kwenye mambo yake hanitaki tuachane nna kihere here adabu sina sijui nafasi yangu..yani mambo kibao mpka nikawa nashindwa kuelewea nikasema "Kwakua umepata mwanamke tajiri wa kuoa ndo mana unasema maneno hayo?" Akasema "si maneno tu leo takuonyesha.." nikasema "Nisamehe kwa kufatilia mambo yako naomba usinipige nna mimba Omary" akasema "Utajua wewe mimba yenyewe nna mashaka kama ni yangu kweli mwanamke unaonekana hujatulia upo juu juu tu siwezi kuishi na mwanamke kama wewe" yaani anaongea kwa kelele kana kwamba anatangaza matangazo jamani..

Nikamwambia "Omary unaniumiza na maneno yako mimi nitaondoka naomba usiniongelee mambo nisiyo yajua unawezaje kuongea maneno hayo kwa mwanamke aliye kubebea mimba?" Akasema "Unadhani hilo tumbo ndo kifungo kwangu? Dada angu alikua sawa umenitegeshea mimba ili nikuone na pengine mimba si yangu hiyo"

Nikaskia mama anasema "Omary fungua mlango Omary nakuita kama mimi mama yako nisikilize" Wifi anasema "Mama waache wamalizane wenyewe" nikawa nanyanyuka kwenda kufungua mlango Omary akanisukuma chini nikaangukia matako nikatoa sauti ila ya kushtuka na maumivu Omary akavuta mkanda wake wa jeshi akaukunja nikajua leo mimi na mwanangu tumboni tunakufa..

.....Inendelea....



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa