STORY:PENZI LA MJEDA EP 17 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 12, 2020

STORY:PENZI LA MJEDA EP 17






Basi bwana kwakua nilisha fanya maamuzi ya kuishi pale na Omary mpaka baba yake atakapo tupa baraka tuoane.. kule jeshini nilipo kua nafanya kazi kwenye ile supermarket nilifukuzwa kazi bila sababu ya msingi lakini sikujali mama alikua ananitia moyo yani akanipenda na mimi nikampenda mpaka nikawa nahisi marehemu mama angu labda anatumia mwili wa yule mama.. maana upendo wake kwangu ukikua wa kweli kabisa..

Mimba yangu ilianza kukua na tumbo lilianza kutokeza Omary alikua anaenda kazin na kurudi pale nyumbani tunaishi vizuri kwa amani. Siku moja nikiwa nimekaa chumbani wifi akagonga nikamruhusu Omary alikua sebleni wifi akasema "Tina una mpango gani na maisha yako?" Nikamuuliza "una maana gani?" Akasema "Baada ya kujifungua una mpango gani?" Nikasema "Sijaelewa swali lako..Nikijifungua si nnatakiwa kulea au?" Akanipa simu nikasema "Hii si ni simu ya omary?" akasema "ndio" Nikaichukua nikaweka pembeni akasema "fungua msg" nikamwambia "Za kazi gani? Unataka kufanya nini?" Akasema "Akili kichwani mwako" akaondoka dah pale nikapata ushawishi sijui nifungue msg sijui niache ila nikaona dah nisijitaftie presha za bure nikaiacha ile simu kama ilivyo mda kidogo Omary akaja akasema "Umenionea simu yangu?" Nikasema "uliiyacha hapa kitandani" akaichukua fasta kama ana mashaka flani mimi nikapotezea tu..

Baadae usiku wakati tunakula baba mkwe akasema "Omary umefikia wapi?" Wifi akajibu "Baba usiwe na mashaka Omary atakufrahisha soon" baba mkwe akatabasamu akasema "Kweli eeh,Nakutegemea sana" Mimi na mama mkwe tuka angaliana kisha tukamuangalia Omary, Omary alikua kama ni mtu ambaye hana amani Akaangalia chini tu akasema "Nimeshiba..Asante mama chakula" akanyanyuka akaelekea nje.. mimi na mama mkwe tukaangalia yani tunaona hapa sign ya hatari inapiga kabisa..

Tulivo maliza kula nikatoka nje kumwangalia Omary alikua amekaa kwa mbali anaongea na simu kageuzia mgongo nikawa natembea kuelekea kule sijui alihisi kuna mtu anakuja akakata simu fasta.. Alafu akageuka akasema "Nambie mke wangu" sauti yake haina kujiamini kabisa nikamwambia "Unafanya nini huku usiku peke yako? Tamthilia yako inayo ipenda imekaribia kuanza" Akasema "Ooh saa tatu tayari..Tangulia nakuja" mda ule ule simu ikaita akaiangalia hakuipokea.. Nikamwangalia Machoni.. Akasema "tangulia ndani" nikamwambia "Nakusubiri twende wote" akasema kwa ukali kidogo "Nenda ndani nataka kuongea na simu" nikamwambia "Hee tangu lini unajitenga ukiwa unaongea na simu?" Akakata ile simu alafu akaelekea ndani kwa kuchukia bila kunijibu chochote..

Nikawa namfta nyuma akafungua mlango kwa hasira akaingia ndani wengine walikua sebleni wana angalia Tv wakageuka kuangalia nini kinaendelea maana Omary alivo fungua lango na kuingia ni kama vile tulikua na ugomvi.. Wakati nataka kumfata chumbani mama mkwe akasema "Tina vyomboo" nikasema "abee?" Mama akasema "Vyombo unataka na leo tena nioshe mimi?" Nikasema "Nakuja mama" Akasema "Osha kabisa ndo uendelee na mambo yako.. We nakujua huchelewi kusema umesahau au umepitiwa usingizi" Baba mkwe akasema "Agh jaman kelele mpaka hatuskii"

Nikaelekea jikoni kuosha vyombo vile vya usiku ki ukweli mama alikua hapendi vyombo vichafu vilale.. Nikaanza kuosha mama naye akaja akasema "Nini kinaendelea mbona sielewi hapa hii hali ya hewa ya humu ndani inanichanganya" nikasema "Mimi mwenyewe hata sielewi sote tupo gizani usinge niita kuosha vyombo labda ningejua Agh mama na wewe una timing mbaya" Akasema "Pole nlidhani unajua kitu ili unieleze" nikasema "Sijui chochote ila kuna kitu kitakua kinaendelea" akasema "Usije kuta Omary kamkubali yule binti" Nikasema "Binti gani mama" akasema "Ah si yule anae lazimishwa kumuoa ni mtoto wa mtu mkubwa sana" nikasema "Mama hujui jinsi Omary anavo nipenda hawez kufanya hivo" mama akasema "Kweli..Aya maliza vyombo ukapumzike" Nikasema "Daah nikajua utasema unanisaidia" akacheka akasema "Usipende raha kama paka"

Akaondoka...
Nimemaliza kuosha vyombo nikawa naelekea chumbani ila kufika mlangoni nikawa naskia Omary anaongea na simu kama anabembeleza kitu.. Nikiskiliza kwa makini lakini siskii Vizuri nikafungua mlango Omary alikua amelala chali huku amejiachiiia kama anabembeleza kitu nilipo ingia akashtuka akakaa kitako alafu aka kata simu..

Nikamuuliza "Vipi" akasema "Naenda kuoga" akavua nguo wakati ndo anaingia tu bafuni simu ikaanza kuita ile nataka kuishika tu sijui hata alitokea wapi akaikwapua fasta akatoa betri akasema iache kama ilivo akarudi bafuni kuoga..

Mmmmgh kengele ya hatari ikaanza kuwaka kichwani nikasema hapa kuna ulakini maana siyo kawaida..

Inabidi nianze ufukunyuku mpaka nijue nini kinaendelea hapa..



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa