Nikatoa begi langu niaondoke omary akasema "Tina kama una niamini na unajua mm nakupenda basi naomba uniskilize na unisaidie tina sitaki kuoa mwanamke mwingine tofauti na wewe na ukizingatia una mimba yangu" Nikasema "Omary kama swala ni mimba wala isiwe sababu hili ni janga langu nitakula na wa kwetu" Mama mkwe akaingia mle chumbani akasema "Tina mwanangu naomba umuelewe mwenzio alafu mimba ni swala la baraka usiseme ni janga mama nakuomba hata ukitaka nipige magoti nitafanya chochote" Nikashangaa nikamuuliza "Mama mbona unanisihi sana niwe na Omary?" Akasema "Samahani kama utafkiria mimi ni mbinafsi lakini kila mzazi anapenda kumuona mwanae ana furaha nyie nyote ni wanangu na nnajua furaha yenu nikuwa pamoja na pia sitamni Omary aje kuishi maisha kama nliyo ishi mimi mama yake maisha ya kulazimishwa kuoa au kuolewa kwenye familia flani hata kama wewe ni mwanaume ukisha ingia hapo tu basi nguvu zako na mamlaka yako yote yanaisha na unaanza kutawaliwa maana unakua umeshaolewa na watu wenye nguvu na haupo pale kwa ajili ya mapenzi bali kwa ajili ya matakwa na faida za watu wengine unakua mfungwa mimi siwez kuangalia mwanangu anaishi maisha kama yangu nilifanya makosa mimi inatosha" Mama aliongea kwa uchungu mpaka akalia alilia sana akasema "Kuna siri kubwa sana ambayo hakuna mtu yeyote anaijua ila nawambia nyie ili Tina tuunganishe nguvu pamoja tushinde hili swala" Tukasikiliza kwa makini mama akaenda ku lock mlango aka lock madirisha kashusha mapazia alafu akafungulia mziki kisha akatusogeza karibu akasema "Baada ya hili nitakalo waambia naomba msionyeshe tofauti yyt kama mnataka niendelee kuwa hai" Tukakubali...
Mama akaanza kutusimlia
"Hapo zamani wakati nipo binti nilikua na mahusiano na kijana mmoja ambaye kiukweli tulipenda sana na tulikua na mipango mingi kama wapenzi lakini kutokana na uwezo mkubwa wa familia yangu hawakutaka niolewe na yule kijana kwa madai kwamba nitaleta umaskini katika ukoo,walinilazimisha kuolewa na baba yake Omary kwa vitisho kwamba nikiwa mbishi watamuua yule kijana,Basi ili kuokoa maisha ya yule kijana nilikubali kuolewa na nilimweleza ukweli japo alisema yeye yupo tayari kwa lolote ila tusiachane, Niliingia kwenye ndoa moja kwa moja na kuanza maisha na huyu baba yako kila kitu nilikua napangiwa mpaka idadi ya watoto nilipangiwa nilipangiwa mda wa kula mda wa kulala mda kufanya kila kitu mimi nilikua naishi kwa Amri na si kwa mapenzi nikilalamika nyumbani wanasema fanya kile wakwe zako na vile mmeo anataka.. kwaiyo sikua na jinsi, siku furahia ndoa na hata wakati wa tendo nilikua kama nabakwa lakini sikua na namna"
Tukawa tunaskiliza kwa makini mno huku tukimhurumia mama..Akaendelea
"Hapo ndipo nilipo mmisi yule kijana nlie kua na mahusiano nae na tukakutana na kufanya tendo la ndoa hapo tayari Dada yako Omary alikua na miaka mitano basi siku ile nilivo kutana na yule jamaa tulishiriki tendo la ndoa na tulikua na Furaha sana na kuahidiana kuendelea na mchezo huo au kutoroka kwenda kuishi mbali lakini sikujua kama ninafatiliwa kila hatua nilivo rudi nyumbani nilimkuta baba yako amechukia sana na nilipigwa mpaka nikalazwa na kwanzia siku iyo baba yako alionywa kumpiga mtu yeyote baadae alinioyesha picha tulizopigwa mimi na yule jamaa akasema hata nikitoka kwenda sokoni kuna macho ya watu zaidi ya mia moja yananiangalia kwaiyo bora nitulie la sivyo ataniua na huyo jamaaa lazima ampeleke panapo stahili sikuelewa ana maana gani lakini baada ya kama wiki lilitokea tukio la ajabu mtu aliuwawa kikatili kwa kukatwakatwa kiungo kimoja kimoja na kumbe alikua yule kijana..😢😢 Na wakati huo nilikua na kila dalili ya ujauzito mimba ambayo nilikua nimembeba Omary Tumboni mwangu, ili kuficha siri nililazimisha kwa kipindi kile kukutana na huyu mzee kimwili ili niseme mimba ni yake na kweli nilifanikiwa huku nikijua wazi mwenye mimba halali ameuliwa na nilikua namuhisi huyu mzee ndo kamuua japo mpaka leo sijajua ukweli haswa ni upi.. Tangu iyo sikuruhusiwa kutoka nje ya geti bila sababu maalum na kile chumba ulichotaka kuingia Tina hakuna mtu yyt amewahi kuingia wala anaye jua kuna nini"
Mama mpaka anamaliza kuongea mimi uwoga umenijaa na Omary analia maana tulimuelewaa kila sentesi aliyo sema hakukua na Swali zaidi.. Tukaskia mlango unagongwa mama akasema "mimi naingia kabatini Omary vua tishet nenda kafungue mlango mazingira yaonyeshe kama mlikua kwenye tendoo.." Mama akaingia ndani ya kabati Omary akavua tishet nikamzuia kwenda nikalegeza nguo yangu na kuvuruga nywele alafu nikatoka kwenda kufungua mlango alikua ni wifi akasuma mlango ili aingie nikamuuliza "Unataka kumuona kaka ako akiwa uchi?" Akanikazia macho akasema "Siamini kama umepata ujasiri wa kufanya mapenzi katika wakati kama huu" nikamjibu "Asemacho Ommy kwangu sawa hakuna nnacho pinga labda umlaumu yeye" akaniangalia akaondoka..
Nikarudi ndani mama akatoka tukamwambia aende nje sisi tujadili tutaongea nae kesho na usiku ushaingia sana kwaiyo tutalala..
Omary alikua na wakati Mgumu nikamwambia "Omary mimi siondoki mpaka tufikie muafaka" akasema "Si umeskia baba yangu mzazi aliuliwa je na wewe wakitaka kufanya hivyo?" Nikasema "Nimezaliwa siku moja nitakufa siku moja..Tumependana na tutapambana"
Sasa hatuko ukweni.. Tuko vitani.. yewooooomiiii...
Itendeleaaaaaa...
Insta:epiphaniafrancoofficial
No comments:
Post a Comment