STORY:PENZI LA MJEDA EP 15 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 12, 2020

STORY:PENZI LA MJEDA EP 15





Baada ya mda kidogo dactari akawa amefika mimi nipo tu najifanya sina fahamu lakini kwa hali inavoonyesha kila mtu anawasi wasi maana dactari alivo fika kachangamkiwa sana Baba mkwe akasema "Samahani kwa usumbufu ndugu yangu hebu mcheki huyu binti nini tatizo" Dactari akasema "Salamu kwanza mzee" baba mkwe akasema "Aiseeh nimechanganyikiwa nisamehe bure huyu ni mkwe wangu mwanamke wa huyu kijana wangu sasa kumetokea kutokuelewana kidogo bahati mbaya nikampiga kofi sasa nadhani kapoteza fahamu sijui nini kitakuwa kimetokea" nilivo skia baba mkwe kanitambulisha kama mkwewe nikajua hapa ruhusa imesha patikana..

Yule dactari akanishika mkono hapa kwenye maungio ya kiganja kama anapima kitu.. Akanifumbua jicho moja kisha akasema muamsheni nikasema dah huyo dactari atakuwa amejua kama najifanyisha huyu Omary kaniita kama mara tatu nimekausha kimya kaniita akanitikisa ndo nikajifanya napata fahamu naitikia kwa mbaaaali.. nikaamka nikakuta watu wamenizunguka wanaonekana wana presha nika kaa kitako dactari akasema "unajiskiaje?" Nikasema "Kichwa kinauma sana" Dactari akasema "tofauti na kicha hakuna kingine chochote?" Nikasema "Nimechoka tuu" akawaambia wengine "tupisheni kidogo tuzungumze" bila ubishi wakaondoka dactari akanipa kichupa akasema nenda kalete mkojo.. Kha nikasema huyu vipi tena mambo ya mkojo hapa yanaingiaje? Ila sikubisha kwakua chumba kilikua self contained nikaenda chooni nikakojoa kidogo nikampa akasema "sawa pumzika" akanipima na vipimo vingine vingi vingi akasema "pumzika" akawaambia wengine "Muacheni binti apumzike naenda nitarudi badae na majibu ya vipimo vyote"

Basi mama mkwe akaniletea chakula lakini nikashindwa kula ile nimeonja kidogo tu nikaenda kutapika akasema "Mwanangu nini shida?" Nikasema "Sijui mama ila sijiskii kula" akasema "Au una mimba?" Nikasema "Haiwezekani mama" akasema "Unajua mm ni muuguzi ila mme wangu hapendi nifanye kazi" akanishika kwenye maungio ya kiganja akasema "Usiongee" akaskilizia akasema "Mmmh" nikasema "Mbona unaguna mama" akasema "Tulia usiongee" akanishika chini ya kidevi siyo kidevuni chini ya kidevu hapa kwenye ngozi laini akaskiliziaaa akatoa akaweka vidole kwenye maskio yangu akafumba macho kama kuna kitu anaskilizia..

Akanyanyuka akatoka nje nikajiuliza huyu mama ananifanyia mambo gani tena.. Kurudi karudi na vipimo viwili vya mimba.. nikamwambia "mama vipi tena?" Akasema "Nna pharmacy yangu ila natafta binti wa kumuweka ndo mana unaona nna vitu vingi" nikasema "Simaanishi hivyo namaanisha hivyo vipimo vya mimba" akasema "Kwa uhakika tu" akaangalia huku na huku akachukua kimfuniko cha mafuta akakifuta vizuri na kitenge chake akasema "Kojoa humu kidogo tu" nikawa namwangalia akasema "Nenda chooni kama unaona aibu,au unataka nifumbe macho?" Nikaenda chooni kukojoa nikarudi nikampa basi mm mwenyewe pale presha ikanishika au nna mimba nini? Nikamwambia "Ukipata majibu utaniambia mama" nikageukia pembeni nasubiri niambiwe naskia mama anaita kwa sauti "Omaaaaary! Omaaaary!! Omary njoo" ile sauti ili washtua watu wote siyo omary peke yake mm mwenyewe nilishtuka Watu wamekuja fasta fasta omary akiwa mstari wa mbele "Kuna nini mama?" Mama mkwe kamkumbatia "Hongera mwanangu mwanangu umekuwa baba yeleeewiii Asante mwanangu" watu wote mama mkwe wifi na omary wakanigeukia na mm nikamwangalia mama mkwe..

Mama mkwe ndo akawaonyesha kile kipimo cha mimba..Heeee nna mimba? Tina mimi nna mimba? Nikamwangalia Omary..Omary akaangalia chini kwa aibu flani baba mkwe hakusema kitu akatoka akasema Omary nifate. Omary akatoka mama mkwe akasema "hee mbona nimefurahi peke yangu wengine wametulia tu" mimi nikageukia pembeni kulala.. mama mkwe akasema "Ukisjikia unataka chochote niambie" nikasema "Sawa" na yeye akatoka..

Wifi akanisogelea akasema "Malaya wengi wa mjini wakitaka kuforce ndo wanategesha mimba,Usidhani hicho ndo kigezo cha wewe kuolewa" Kauli ile iliniuma sana ukizingatia nilikua sitaki kupata mimba kwa wakati huu alafu naambiwa nategesha mimba? Nikanyamza tu wanasema funika kombe mwanaharamu apite.. nikatulia badae dactari alikuja akaleta majibu nna mimba na damu yangu ni chafu akaacha dawa kwa ajili ya kusafisha damu akasema nipate mda wa kutosha wa kupumzika..

Badae natoka chumbani kwenda sebleni nikakuta sebleni kumetulia mno nikajiuliza watu wako wapi.. nikaskia sauti kwa nje nlivo sogea dirishani nikaskia wifi anasema "Baba unadhani yule mwanamke tuliye mchagulia Omary atatuonaje? Na si unajua baba yake ni mtu mkubwa sana hii ni connection nzuri kwa familia yetu" Omary akasema "Mimi sitaki kuziskia hizi habari tena naomba tina asijue lolote kutokana na hili" na mama mkwe akasema "Ni kweli muacheni mtoto amuoe anaye mtaka" Baba mkwe akasema "Unajua nini wewe mama wa nyumbani kaa kimya kama hujui unacho kiongea" Mama mkwe akasema kwa hasira "Mimi ni mama wa nyumbani lakini usingeniachisha kazi nisinge kua mama wa nyumbani.. Omary usilazimishwe kuoa mtu usiye mtaka ukaja kujuta kama mimi" Akasimama na kuondoka Omary akawa anamftaa mama yake nyuma anasema mama subiri yaani nlijiskia vibaya sana nikawa nimesimama tu pale..

Ghafla mama mkwe akaingia ndani akifatia na Omary walivo niona wote walishtuka na mimi nilishindwa kuchangamka maana nimeumia moyoni kwa kikao chao walicho kua wanazungumza nikaondoka kuelekea chumbani Omary akanifata..

Nikaingia chumbani nikaa kitandani hapo ilishakua jioni Omary akasema "Tina ulikua unafanya nini pale?" Nikasema "Samahani kwa kuskiliza yasiyo nihusu" hapo machozi yanatoka..
Akasema "Umeskia yote?" Nikasema "hapana kwanzia pale unapotakiwa kuoa mke ulio chaguliwa"

Omary akasema "Naomba tuongee nisikilize" Nikamwambia "Haina haja naomba begi langu nataka kurudi kwangu" Omary akasema "Tina samahani kwa ajili ya familia yangu" Nikasimama nikachukua Begi langu..

Nataka nianze safari ya kurudi kwangu.. siwezi kuvumilia maumivu haya wallah..



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa