Basi maisha yakaanza upya mimi nikiwa kwa mahusiano na mjeda wangu.. kwake kwangu kwangu kwake.. mala nyingi alikua akinambia nihamie kwake tukae wote ila sikua tayari nilimwambia tuna hitaji kujuana zaid na kila mmoja akiridhika na mwenzie basi afate taratibu zinazo takiwa kisha mengine yatafata..
Hatimae lile jengo la supermarket lilikamilika na hatimae nikapata kazi jeshini pale ndo tumezidi kusogezwa karibu.. Kazini tunaenda wote kama siku akiwa anaenda na kurudi tunarudi wote.. kama siku haendi bas mm naenda lakini kila siku lazima tuonane..
Jumamosi moja bwana mjeda alikua kazini mimi nikasema ngoja nikamfanyie usafi unaoeleweka leo na ikiwezekana nipange vitu upya si unajua nyumba akikaa mwanaume bwana..
Nikaenda zangu nikaanza kufanya usafi kupiga deki mtoto wa kike.. dikaka chache baadae nikaskia mlango unafunguliwa mtu anaingia.Nikasema Omary karudi mala hii tuu..Nikasema "Hee umewahi kurudi dear" Nikaskia sauti ya kike "Wewe nani?" Nikasema "Kwani wewe nani?" Kumuangalia vizuri..nikamkumbuka ndo yule mjeda wa kike alonitia kofi siku ile..
Nikamuuliza "umefata nini hapa?" Akanisogelea Akaniangalia kwa dharau sana akaondoka. Nikashindwa kuelewa ila nikahisi kuna kitu kinaendelea pale kati ya Omary na yule dada maana kma sivyo angewezaje tu kuingia kama vile ni nyumbani kwake? Nikaacha pale pale ndoo ya kudekia sebleni na shughuli yenyewe ya usafi ikaishia pale..
Nikarudi kwangu nikiwa nawaza nini kinaendelea hapa kati ya hawa watu wawili ila nitajua tu..Badae mjeda akanipigia simu nikawa sipokei katuma msg "Uko wapi?" Sikujibu nikapanda kitandani nikalala.. Akaja nyumbani "Tina Tina" nikaamka "Unasemaje?" Akaniuliza "Una matatizo gani?" Nikamwambia "Kwani ww unaonaje?" Akasema "Mbona nyumbani umekuacha vile kma ulikua hujiskii kufanya usafi si ungeacha kabisa?" Nikawambia "Usafi ndo pekee unachojua? Una uhakika gani kama mimi ndo nimeacha kwako kuko ovyo kwani mm ndo peke yangu naendaga?" Akasema "Una maana gani?" Nikamuuliza "Tofauti na mm nani mwingine huwa anakuja kwako?" Akasema "Nini wewe tu tina mbona sikuelewi?" Nikamwambia "Toka toka kwangu..Yaani unanidanganya mbele ya uso wangu? Kwaiyo mm ni mwendawazimu?" Akasema "Tina hebu ongea lugha ya binadamu ili tuelewane unajua sikuelewi?" Nikamwambia "Mimi no mdudu lugha ya binadamu naijulia wapi? Enda kaongee na binadamu wenzio naomba uondoke na usirudi tena na wala usinitafute endelea na watu wako" akasema "Daaah aiseeh okay poa ila dah haya bhna kwaheri" akaondoka nikafunga mlango nikatia na lock kabisa nikalala..
Jumapili nikaendelea na ratiba zangu kama kawaida wakati natoka kanisani nikawa napita ile njia ya kwa Martha ambayo pia lazima nitapita kwa mjeda nikamuona yule mjeda wa kike tena kasimama pale mlangoni anaongea na simu huku anacheka nikajua tu anaongea na Omary nikapitiliza moyo unauma mpaka kwangu..
Nasema kwaiyo Omary alikua ananidanganya kisa anatembea na mwanajeshi mwenzie siyo? Aah sawa nimeelewa mimi ni kamisikini fulani ambako hakana thamani..si ndio? Kwaiyo kumbe wote ulikua uongo? Kha wanaume kwa kuigiza..Wajeda kweli malaya yani yote naongea huku nalia chumbani peke yangu.
Ep 11 coming up next!! Stay tuned!!
No comments:
Post a Comment