PETE YA KIKE Sehemu Ya 7 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 1, 2020

PETE YA KIKE Sehemu Ya 7




MWANAUME MSAFI

Sasa hapo kichwa moto mana anapenda hela kuliko maelezo, suria aliingia bafuni, sasa ile anaanza kuoga anagundua ana pete kwenye kidole, na huezi kuoga na pete kidoleni mana itakuchubua chubua au kukugasi wakati wa kuoga... Sasa wakati huo asha kaduaa, mana kapewa hela lakini pete haipo, na huezi kumvua mtu... Sasa huku bafuni suria kaishika ile pete huku akisema...
"ayaaaaa kumbe sijavua hili lipete"
Aliongea kwa sauti mpaka asha akasikia,... Sasa asha huku anaomba hio pete ivuliwe mana hata akivua hawezi kuiacha huko bafuni, bali ataiweka mahali...

Sasa huku kwa maimati akiwa katulia, ghafla akapata ishara kuwa pete imevuliwa,... Kwa ishara hio aliona kuna umuhimu wa kwenda alipo surian... Maimati akajiandaa kuruka ili akaangalie kulikoni pete ivuliwe,.. Lakini kabla hajaruka, akapata ishara tena kua, pete imevaliwa, hivyo akaahirisha kwenda

ENDELEA..........

Suria liingia bafuni akiwa na pete kidoleni, pete ambayo ina uwezo wa ajabu pindi uivaapo,... Kitu cha kwanza kwa surian baada ya kuivaa pete hio, kapigiwa simu ya kazi,... Hio ndio faida ya hio pete,... Na kingine ni kwamba kama kuna mapepo yanakuandama, ukivaa pete hio hakuna kiumbe yeyote atakaye kusogelea, na pia vile vile, ukivaa pete hio, hakuna kiumbe kitakachoweza kukudanganya kwa namna yeyote ile, hata kama ni jini mzuri, pia hawezi kukurubuni mana una pete kidoleni mwako,...

Sasa surian alipogundua kuwa hajavua ile pete, aliivua kisha akaiweka kwenye kadirisha kalichopo hapo bafuni,.. Sasa kule maimati akapata ishara kuwa pete imevuliwa, maimati akajiandaa kupotea katika mazingira yao... Lakini kabla hajaruka, alipata ishara kwa mara nyingine kuwa pete imevaliwa... Hivyo akaahirisha kuruka, ikabidi akae kwa kutulia

Sasa huku kwa asha,.. Kumbe asha ndio kaivaa ile pete,.. Baada ya kuwekwa tu kwenye dirisha, asha akaichukua na kuivaa... Sasa kule kwa maimati akapata tena ishara kua Pete imevaliwa, lakini imevaliwa na mtu wa jinsia yake, yaani mwanamke mwenzie, bila kupoteza muda maimati aliruka hapo hapo kuja kwa akina surian,... Lakini alipopita hapo nje alimwona shaimati akiwa katulia katika mti,... Akajua tu yeye ndio sababu ya surian kuvua pete,... Sasa hajakaa vizuri mara asha katokea huku akifurahi kwani mtihani aliopewa kaufaulu...
Maimati aliweza kuiona pete aliompa surian ili imkinge,...
"shit, shaimati... Umefanya nini"
Maimati alikasirika na kumfuata shaimati huku akimwambia hayo maneno....
"sasa mimi nimefanya nini"
Sasa wakati huo wakibishana, maimati hakuwa akionekana (invisible), sasa asha anakuja anamshangaa shaimati kama anabishana na hewa, mana hakukua na mtu wa kitu mbele yake, lakini alikua akiongea....
"lazima umemtuma huyu msichana akachukue pete"
Aliongea maimati huku shaimati akijibu kua
"hao ni ndugu, wajuaje kama wamepeana"
"kama ni ndugu wamepeana, je wewe unafanya nini hapa"
"napunga upepo tu, kwani huoni kuna kivuli kizuri"
Sasa asha anazidi kushangaa, shaimati anaongea na nani...
"we dada, kwani unaongea na nani"
Asha alimuuliza shaimati ambao kwa sasa ni marafiki, lakini asha hajui kuwa shaimati ni jini...
"aahhhhh mawazo tu... Wala siongei na mtu"
Shaimati alimjibu asha kuwa ni mawazo tu lakini hakuwa akiongea na mtu
"mmhh ok, ila punguza mawazo dada.. Afu kazi yako ulionipa nimeimaliza"
Aliongea asha sasa shaimati bado anajibalaguza, mana aliambiwa na maimati kuwa yeye ndio sababu ya hio pete kuwepo kwa huyo msichana,
"umeona eee, nilikwambia wewe ndio sababu ya hii pete kuwa kwa huyu mwanamke"
Aliongea maimati lakini shaimati hakujibu kitu,... Pale pale maimati akaingia ndani chumbani kwa surian, na anae ona kuingia kwa maimati, ni shaimati peke yake, mana ni jini mwenzie...

Sasa maimati ile anataka tu kuingia, alimuona surian akiwa anaitafuta ile pete,... Hapo ndipo maimati akajua ile pete ilichukuliwa wakati anaoga,.. Maimati aliumia sana mana hawezi kuichukua hio pete ikiwa kidoleni mwa mtu, ni mpaka aivue ndipo aichukue... Na hio pete ndio ilikua kinga ya surian ili asiende kule kwenye himaya yao,... Surian alitafuta pete mpaka kachoka,.. Alikwenda kuvaa vyema kisha akamfuata mama yake,.. Wakati huo maimati yupo nyuma lakini haonekani,...
"mama"
"abeee"
"hujaona kijipete flani hivi"
Aliuliza surian lakini kabla mama yake hajajibu ghafla asha akaingia...
"mimi sijaona... Kwani nawe skuizi wavaa pete"
Aliuliza mama yake, mana surian hajawahi na hua hapendelei kuvaa pete au cheni,...
"hapana mama... Ni pete ya mwanafunzi wangu... Niliibeba kimakosa wakati machukua chaki kwa ajili ya kufundishia madrasa"
"mmhh mimi sijaona, labda umuulize dada yako"
Aliongea mama yake, kisha surian akamuuliza asha...
"eti hujaona pete hapa kama ilidondoka"
Suria alimuuliza asha ambaye ni dada yake kabisa
"hio pete ni ya kike au ya kiume"
"ni ya kike"
"heeeeeee sasa wewe na PETE YA KIKE wapi na wapi"
Asha alianza kumkandika wakati yeye ndio anayo hio pete na mkono aliovalia pete hio, kauficha ili surian asione
"lakini si nimesema hapa kuwa ni pete ya mwanafunzi wangu"
Wakati huo maimati katulia tu, mana hairuhusiwi kumnyang'anya mtu pete, mpaka aivue mwenyewe,...
"mmmhhh mimi sjaiona nikiiona nitakwambia"
Aliongea asha, na hapo hajui hio pete ina faida gani na uzuri ni kwamba pete hio haina ubaguzi, yeyote atakaye ivaa lazima aneemeke....
"asha simu yako inaita huko chumbani kwako"
Aliongea mama yake,... Huku suria akaamua tu kuwahi msikitini mana ilikuwa ni wakati wa jioni kwenda kuswali magharibi,... Sasa kwakua suria hana pete, hivyo maimati ana kazi ya kumfuata nyuma nyuma ili shaimati asije kumrubuni... Mana mwanzo suria alikataa kazi aliopewa na shaimati kuwa kwa wiki atalipwa milioni kumi,.. Lakini bado kakataa kwasababu alikua na pete, na pete hio haikubaliani na uongo,... Lakini kwa sasa suria hana pete hivyo akikutana na shaimati lazima akubali tu, hivyo maimati kaamua kuwa mlinzi badala ya ile pete.... Shaimati kweli hakua mbali, kana kwamba alijua tu suria atatoka kwenda msikitini hivyo atamvizia.. Lakini kwa bahati mbaya maimati yupo nae, hivyo akashindwa kwenda kumrubuni

KESHO YAKE ASUBUHI MIDA YA SAA NNE

Suria siku hio hakwenda kazini, kule shule kufundisha mana jana alipigiwa simu ya kwenda kupata kazi ya kulipwa milioni tano mpaka nane kwa mwezi,.. Sasa leo hakwenda shule, ili aende kwenye intaviu ya kazi hio aliopigiwa simu jana... Lakini kabla hajatoka akaitafuta ile namba iliompigia simu jana,...
"hallo boss hali yako"
Suria alimsalimia boss huyo wakiwa katika mazungumzo ya simu...
"salama tu hali yako kijana"
"Tunamshukuru mungu kwa rehma zake"
Alijibu suria huku akitabasamu kwa mbaali
"inshallah, sasa kijana mbona una haraka, sisi tulikwambia tutakupigia simu"
"lakini boss, jana jioni mlinipigia kuwa leo nije saa nne"
"hapana... Labda tulikosea namba tu"
"boss, namba ni hii hii"
"hapana bwana... Unataka kituuzi tena"
"basi boss wangu, Nasubiri wito wenu"
Aliongea suria kisha boss huyo akakata simu kwa hasira....

"alaaaa.... Huyu si alinipigia jana huyu"
Aliongea suria huku akiwa kama haelewi,... Mana Jana akapigiwa simu kuwa leo saa nne aende kwenye intaviu kwa ajili ya kazi, sasa leo anaipiga ile namba inamjibu tofauti,... Suria alichoka na kuchoka... Hata hamu ya kutoka tena ikawa hakuna,... Akarudisha baisikeli yake ndani na kukaa kwa kutulia,..

Sasa kumbe ile pete iko hivi... Kama kuna mahali ulikwenda kuomba kazi,. Alafu ukaambiwa tutakupigia simu... Sasa kama ile nafasi ya kazi ipo lakini wahusika wanataka rushwa, basi ukivaa ile pete, inakuwa kama inamlazimisha yule mhusika kukupa kazi,... Mana nafasi ipo lakini unabaniwa kuipata... Lakini kama haipo basi haipo... Lakini kama ipo afu unabaniwa usiipate, basi ile pete inafanya kazi,.. Kwahio jana suria alipigiwa simu kwakua alikua kavaa ile pete, sasa hivi hana ile pete ndio mana boss hamuelewi...na suria hajui kuwa ile pete ni kwa ajili yake na ndio sababu ya kuitwa kazini... Yaani laiti angelijua kuwa pete ile ndio sababu,.. Angempokonya mtu ambaye yuko nayo... Mana suria au mtu yeyote anaweza kumpokonya asha ile pete, lakini kiumbe kama shetani au hawa hawa akina maimati na shaimati hawawezi kumpokonya asha ile pete, ni mpaka aiache mwenyewe,.. Kwahio hata kama ingelikua kidoleni kwa suria, pia hakuna kiumbe kitakacho weza kumpokonya ni mpaka aivue..
"mama..."
"abeeee... Ah bado hujaenda huko kwenye intaviu"
Mama huyo Alimuuliza mtoto wake
"ah mama... Ni mitihani tu... Jana kanipigia mwenyewe, lakini nashangaa leo ananigeuka"
Aliongea surian huku akitamani hata kulia, mana ni kazi inayo endana na elimu yake, na anaipenda kwelikweli
"pole mwanangu, labda sio riziki yako"
"aahhh sasa si angesema toka jana.. Mana leo sijaenda kazini kule shule kwa kujua kuwa nakwenda kupata kazi"
Aliongea suria huku mama akimuonea huruma mtoto wake
"sasa kwanini usiwahi huko shule, ili usipoteze kote kote.. Wahi baba"
"saa hizi mama ni saa nne hii, ni mwalimu gani anakwenda shule saa nne"
"Sikiliza mwanangu, wewe ukifika useme nilipata dharura kidogo"
Aliongea mama yake, ndipo suria akachukua baiskeli yake...
"hivi dada asha yuko wapi"
"si kaenda huko saluni kwake, eti watu wamejaa mlangoni wanataka kusukwa"
"eeehh ndio katoka asubuhi hivyo"
"kapigiwa simu toka jana"
"eehh... Haya mi wacha niende"
Basi suria alipanda baiskeli yake kisha huyooo....

Sasa huku saluni kwa asha... Duuuu kumejaa wanawake,.. Wengine wanafumua nywele ili wasukwe na madraya... Wadada wanafanya kugombea anzee yupi amalize yupi, kiufupi leo asha alikua na wateja utafikiri soko... Hajawahi kuweka wasaidizi lakini leo kaweka wasaidizi kama watano hivi, tena kapandisha na bei ya kusuka sijui kushonea, ah mimi sijui misiko ya kile mnaitaje... Lakini asha siku hio mpaka yeye mwenyewe anashangaa, tena anafanya kuuliza kuwa huko mitaani umeme umekatila au vipi,.. Mana watu wanazidi kujaa saluni kwake..

Sasa wale ambao wanamjua asha alivyo, leo wanashangaa...
"kumbe mwenzetu ukivaa kiheshima unapata wateja hivi"
Aliongea mmoja wa rafiki zake, mana hawajawahi kumuona asha kavaa hijabu,... Sasa leo kavaa afu ana wateja wengi mpaka hawataki Tena

Lakini sasa mbali na hapo pia maimati yupo hapo habanduki, anasubiri asha avue ile pete ili aichukue, lakini asha havui wala nini anafanya kazi akiwa na pete, na yeye pia hajui kuwa hio pete ndio sababu ya wateja kuongezeka katika biashara yake, yaani ukiwa na hio pete riziki zako zote zinafunguka..

Sasa huku barabarani, suria akiwa anakwenda zake shuleni kufundisha, japo kachelewa lakini ana kisingizio, japo uongo hapendi kuongea lakini leo itambidi ili alinde kibarua chake
Lakini alipokua anawahi kwa kuchanganyia baiskeli yake ili ikimbie... Alipishana na mwanamke mmoja ambaye anamkumbuka lakini hamfahamu
"samahani dada"
Aliongea suria na yule dada akasimama bila tabu... Lakini sasa dada mwenye ni shaimati
"bila samahani"
Shaimati alijifanya hana mpango nae kabisa, wakati hata hapo kajipitisha makusudi tu ili suria amuite, na kweli ndivyo ilivyokuwa...
"natumai jioni ya jana tuliongea tukiwa jirani na pumziko letu"
Aliongea suria akimaanisha jana waliongea na huyo dada wakiwa jirani na kwao...
"enhehehe, ni kweli, afu una kumbukumbu kweli.. Enhe niambie kaka yangu"
"safi tu... Sasa ile kazi uliosema jana, inapatikana wapi mana sijakuuliza jana"
Aliongea suria kana kwamba anajiingiza mwenyewe bila kujua...
Sasa shaimati akachanganya kichwa haraka haraka na kusema
"mimi naishi dubai, na hio kazi pia ipo dubai"
Aliongea shaimati na aliamua kusema dubai kwasababu suria ni muislamu na anaipenda dini yake hivyo akiskia mambo ya dubai dubai, kidogo anaweza kushawishika mana ni sehemu iliotawala imani yake
"ok safi sana... Aahh unajua jana nilikataa nikajua ipo ulaya huko, mana mimi sipendi kwenda ulaya"
Sasa suria yeye anajua kuwa jana alikataa kwa akili yake, kumbe ni pete ndio ilikua ikimuongoza akatae, sasa leo anasingizia eti alikataa kwakua hapendi kwenda nchi ambazo zimekithili utandawazi na fasheni za ajabu...
"ok poa"
Sasa shaimati akajifanya kama hana muda nae
"sasa dada... Mbona hunipi jibu sahihi"
"jibu gani tena.... Kama upo tayari jiandae twende"
"lini sasa tunakwenda"
"kesho"
"kwsho?"
"ndio, kwani hujajiandaa bado"
"ss.. Ss. Sawa tu, hata leo twende"
"kesho mapema..."
"sasa, twende kwetu basi ukapajue vyema, na wazazi wajue kuwa wewe ndio tajiri yangu"
"usijali,... Tutakwenda"
"lakini wazazi wangu wanatakiwa kufahamu hili"
"kwani nimekataa?"
"sawa"
Shaimati aliondoka, lakini alipofika mbele akakumbuka kua mwenzake maimati kafuatilia pete yake, hivyo anaweza kuipata leo leo afu akampa suria na akisha mpa tu,. Suria haendi popote hata kwa kwa nini haendi... Shaimati akaamua kupanga safari siku hio hio,... Mana ilikua waondoke kesho ikiwa ndio siku yao ya saba toka waje duniani, sasa shaimati kaamua kuindoka mchana huo huo kabla maimati hajaipata hio pete...
"mbona unarudi dada"
Suria alimuuliza shaimati au shamimu. Mana kaenda mbele afu karudi...
"nataka tuondoke sasa hivi"
Aliongea shaimati huku surian akianza kutabasamu...
"basi twende kwetu"
Aliongea suria, lakini shamimu au shaimati alimsogelea na kumwambia
"hapana... Twende leo, kesho tunarudi rasmi kuwaaga wazazi"
Aliongea shaimati lakini suria hakupenda kuondoka bila kuwaaga wazazi wake...
"lakini ni vyema nikawaage... Ili niweke na hii baiskeli yangu"
"sikiliza we surian... Wazazi wako wamekusomesha kwa hali na mali ili upate kazi, sasa umepata kazi unaringa ringa... Sawa we nenda lakini ujue kazi ndio basi"
Aliongea shaimati kisha akaondoka... Sasa suria na wazazi wake humtoi,.. Aliachana na shaimati kisha akapanda baiskeli yake mpaka kwao.. Lakini alipofika kwao geti lilikua limefungwa kuashiria mama yake hayupo, mana baba yake kaenda kijiweni... Ila mama yake hayupo hivyo huenda kaenda sokoni... Suria aliegemeza baiskeli yake kwenye geti lao la mabati kisha akawa anakimbilia kule walipo achana na shaimati, au shamimu kama anavyo mjua yeye. Lakini wakati huo shamimu anamuangalia tu huku akicheka.... Suria alikua anawahi huku akiwaza maneno alio yasema shaimati kua
"hapana... Twende leo, kesho tunarudi rasmi kuwaaga wazazi"
Aliyakumbuka maneno ya shamimu, na shamimu akatokea mbele yake kama vile hakumuona.....
"dada? ... Dada?... Dada.?... Nipo tayari, twende sasa"
Shaimati alifurahi sana huku akicheka katika moyo wake,... Leo ikiwa ni siku yao ya sita toka siku wanaingia duniani,... Lakini shaimati anailazimisha safari ili suria asije kupata kinga ya pete...

Sasa huku kwa maimati kakaa kwa kutulia akivizia pete ivuliwe, ili ampe suria aivae... Na kesho wakiondoka waondoke bila mwanaume msafi, lakini bila kujua leo shaima anaondoka na suria... Mwanaume aliopendwa na jini mwenzie....

Je? Itakuwaje pale maimati akijua kuwa suria yu safarini kwenda ujinini?






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa