_ Unafanya kazi, uko bize kweli kazini, unaamka saa kumi unarudi saa sita usiku. Lakini kama mwanamke uko kwenye ndoa ni lazima kuweza kuhudumia chumba chako, kila kitu muachie dada wa kazi lakini hakikisha kuwa unahudumia chumbac hako hiyo ni lazima. Ukishindwa kufanya mambo haya na unaishi na mume, ukiachana na wale waliopo mbali kikazi basi ni rahisi ndoa yako kuvunjika.
_ (1) Binti wa kazi hatakiwi kuingia chumbani kwako, wakati mwingine hata kumtuma acha, akijenga mazoea ataanza kupaona pakawaida, mwisho wasiku ataingia mume yupo na watazoeana. Hata kama mna mtoto mdogo, labda kama mazungira hayaruhusu kumlaza kwingine lakini asiingie, ila kama ni lazima akamlaze mtoto chumbani kwako basi hakikisha kuwa ni kumlaza mtoto hagusi hata nguo iliyodondoka chini.
_ (2) Usafi wa chumbani kwako ni jukumu lako, kuanzia kufagia mpaka kupanga nguo. Ni sumu binti wa kazi anaingia chumbani kwako kufanya usafi, kuna siri za mumeo, boxer chafu, anatupa nguo chini, soksi zinanuka anaingia anaokota. Lakini kuna vitu vya mumeo, ni vya kazini labda ni muhimu, mume aliweka kitu sehemu flani, anakiulizia unaaanza kumuita dada wa kazi, eti ile miwani wa Baba wakati unafagia uliiwekeka wapi?
_ Mwanamke mwingine hata kitanda unasikia dada akatandike, ndugu yangu ni heri tukae mwezi hatutandiki kuliku kutandika binti wa kazi. Najua mwanaume anaweza akafanya hivi vitu lakini ukweli nikuwa kuna vitu vinngine vinaladha vikifanywa na mwanamke mwanaume akisaidia.
_ (3) Nguo za mume wako hakikisha unafua wewe, ziwe za ndani, au za nnje mpaka za pembeni fua wewe. Kwenye nguo kuna vitu vingi, mwanaume unamlundikia tu dada, mwanaume kasahau cheki yake kwneye mifuko basi anafua hata hakagui au akiona hajui ni nini? Fua mwenyewe, lakini hata kama uko bize basi kuliko kumpa dada wa kazi tafuta mtu aje kufua.
No comments:
Post a Comment