KOVU LA MOYO 7 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

KOVU LA MOYO 7






Mvua kubwa ilimnyeshea Poshie pale alipoanguka na hakupata msaada wa mtu yoyote. labda kutokana na muda alioanguka na mvua iliyokuwa ikinyesaha muda huo labda ilisababisha watu wasitembee kwa mguu kwa wakati huo.
Mnamo majira ya alfajiri, jogoo wa kwanza kuwika waswahili wanasema hivyo, baridi kali lilimpiga Poshie huku njaa kubwa ikimkamata ilimsaidia kurejesha faahamu zake ... Hakujua wapi alipo na amefikije hapo. Alichoweza kufanya kwa wakati huo ni kujikunyata na kuaendelea kukaa pale pale huku mvua ikimnyeshea ...
Baada ya kunyeshewa sana aliweza kupata fahamu na kukumbuka kila kitu kwa wakati huo kuwa alikuwa akimuwahi Mtoto wake aliyemuacha Hospital ... Poshie alitamani anyanyuke na aendelee kukimbia lakini wapi, kila alipokuwa akinyanyuka alikuwa akianguka kama Mzigo. Njaa ilikuwa imemshika sana, vidonda navyo vilikuwa vimenyeshewa na mvua na dawa yote ikatoka lakinikilichoku
wa kikimuuma zaidi ni Mtoto wake Henry sijui atakuwa katika mazingira gani masikini ... Poshie aliendelea kulia kwa uchungu na nguvu zikazidi kumuishia mpaka sauti ikawa haitoki kbisaa ...
Asubuhi kulipokucha huku mvua ikiwa imeacha kunyesha na kusababisha uaribifu wa mazingira katika eneo ambalo Poshie alikuwepo. Binadamu yoyote ambaye alikuwa ameumbwa na uungwana kamwe usingeweza kumpita mwanamke mzuri kama Poshie ambaye alikuwa amechakaa kutokanana matatizo ambayo yalikuwa yakimsibu .... "Habari yako Dada?" ... Mama mmoja wa makamo alimsalimia Poshie Baada ya kumkuta akiwa amejilaza karibu na mtaro wa maji machafu
Poshie alitamani kuongea lakini alishindwa kuongea na badala yake aliishia kunyanyua mkono na kutetemeka mwili mzia, kama kifaranga ambaye amemwagiwa maji ya baridi asubuhi.
Kadri kulivyokuwa kunazidi kupapambazuka ndivyo na watu walivyokuwa wanazidi kuongezeka pale alipokuwa yupo Poshie ... "Inawezekana atakuwa amekabwa na vibaka jamani si unaona jinsi alivyoumia" ... Jamaa mmoja aliongea na kumuonea haruma Poshie ... "Badala ya kumsaidia nyinyi mnamshangaa kama cinema amuoni jinsi mwanamke mwenzenu anavyofedheeka?
Yani hamna hata kanga ya kumpa ajifunike ili apunguze baridi. Tatizo lenu mnavaa viguo vya ajabu ndiyo mana mnashidwa kutoa msaada ambao upo hata katika uwezo wenu. Je mngemkuta hana nguo kabisa sijui mngefanyaje?" ... Mama mmoja wa makamo aliwafokea Wasichana ambao walikuwa wamejazana pale huku akitoa kanga ambayo alikuwa amejitanda kama ushungi na kumfunika Poshie na kusbabisha wengine waliokuwa nazo pia kutoa na kumvika mwanamke mwenzao ... {Naomba ujifunze ndugu msomaji kupitia hii story jinsi gani Mama zetu wanavyopata tabu katika kuangaikia uzima wetu. Mateso anayoyapata Poshie ni robo ya Mateso aliyoyapata mama yangu wakati ananilea mimi {Dee Lovee) baada ya kukimbiwa na Baba yangu mimi nikiwa na miezi miwili, tena nikiwa naumwa nusu ya kufa .. Mpende sana mama yako mpaka unaingia kaburini mwiko kumtoa Mama yako akili kwa kumfananisha na Mpenzi wako. Mama ataendelea kuwa Mama na mpenzi wako ataendelea kuwa Mpenzi wako. ukimaliza kusoma Episode hii nenda kamfanyie kitu chchote Mama yako kumuonesha kama unamjali hata kama ametangulia mbele ya haki}
Wasamalia wema walimsaidia Poshie na kumkimbiza Hospital kwa sababu hali yake ilikuwa ni mbaya, na hakuna aliyejua nini kimemsibu mwanamke yule huku kila mtu akiongea lake na wengine wakifika mbali zaidi kwa kudai kuwa alikuwa anajiuza ndiyo mana akapatwa na maswahibu hayo.
*****
Asubuhi na mapema Shakira aliandaa chai ya nguvu ili ampelekee mgonjwa wake. Masikini hakujua kama mgonjwa wake ametoroka kule Hospital.
Baada ya kuandaa chai alichukua gari ili kuelekea hospital kwenda kumuona Poshie. Alifika na kuegesha gari yake haraka sana na akashuka ili akamuone Poshie
Wakati Shakira anafika na Dr Ben naye ndiyo alikuwa akitaka kutoka zamu ... "Kumbe ningechelewa kidogo tungekuwa tumepishana?" ... Shakira alimwambia Dr Ben huku akitabasamu kwa mbali kuashiria alikuwa na hofu ya kutaka kujua Poshie anaendeleaje ..... "Ni kweli tungepishana, hata ivyo nimechelewa kutokana na tatizo la mgonjwa wako, mara nyingi muda huu huwa nishatoka kazini" ... Moyo wa Shakira ulifanya Paaaaaa! kwa mstuko na sura yake ikabadirika ghafla .... "Tafadhali naomba uniambie imekuaje ni mzima au ..." Dr alimkatisha na kumwambia ... "Punguza presha Shakira naomba ukae kisha tuongee" ... Dr Ben alimwambia na Shakira akakaa na akamuelezea kila kitu kama mgonjwa wake ametoroka.
Taharifa za kutoroka kwa Poshie zilimstua sana Shakira na kuanza kuwa na wasiwasi na Poshie ..."Kuna kitu nimegundua kutoka kwa yule binti" .... Shakira alimwambia Dr Ben huku machozi ya uchungu yakiwa yanamtlilika .... "Kitu gani? mana hiyo ni kesi kubwa sana kwetu mgonjwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha" ... Ben alikaa sawa na kumuuliza Shakira ili amwambie kuna nini kati yao.
Walitoka nje na Shakira akamuadisia kila kitu Dr Ben, jinsi alivyokutana na Poshie mpaka alipomgonga na gari .... "Mimi nahisi yule binti atakuwa amemtupa yule mtoto na ndiyo mana ameniogopa mimi alijua nitambana na kumwambia Prince au nitasababisha akamatwe na Polisi" .... Poshie alimwambia Ben huku akijipa haukika kuwa Poshie atakuwa amemtupa mtoto wake wa kumzaa ama kweli usilolijua ni usiku wa giza
****
Baada ya kutoka kulala na wasichana wapatao wanne Papaa Prince akiwa na walinzi wake alirudi nyumbani kwake na kujichia katika bwawa lake la kuogelea huku pembeni akiwa na Whiskey haina ya Jack Daniel's akinywa na kuburudika.
Siku zote fikra zako ndiyo ugonjwa wako. Shakira baada ya kujua Poshie ametoroka pale Hospital yeye aliamini kuwa ni lazima Poshie atakuwa amemtupa Henry ndiyo mana ametoroka pale kwa kumuofia yeye ...
Aliwasha gari yake haraka na kuelekea nymbani kwa Prince ili akamuelezee kila kitu.
Alifika nyumbani kwa Prince na kupaki gari kisha akamfuata Prince kule alipokuwa amejiachia ..."Vipi mbona unakuja kasi hivyo huku unahema kiasi hicho, kuna nini huko?" .... Prince alistuka na kumuuliza Shakira ... "Prince yule Mwanamke wako uliyezaa naye amemtupa yule mtoto aliyekuja naye siku zile" ... "Unasemaje?" ... Prince alistuka na kumuuliza Shakira Huku akiwa amemtolea macho kama haamini kwa alichokisikia ..........


NINI KITAENDELEA? .....



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa