KOVU LA MOYO 5 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

KOVU LA MOYO 5




Iliwachukua kama sekunde 30 wakipeana Juice ya mahaba ... Poshie alimsukuma Angelo na kumtoa mwilini mwake kisha akatazama pembeni huku akitamani kulia. aliona haibu sana kwa kile kitendo alichofanya na Angelo.
Hakuwahi kuwa na Mwanaume katika maisha yake. Hakutegemea kama siku moja angekuja kubusiana na Mwanaume ... Poshie alimtazama Angelo kisha akamwambia ... "Kwanini umenibusu wakati umeniambia nijitulize ili nipate Mwanaume wa kunioa?" ... Lilikuwa swali gumu kwa Angelo na kujikuta akikwama akiwa hana cha kumwambia, mwishowe akalopoka ... "Nimefanya hivi kwasababunakupenda Poshie, ila najuta sana kwa nini nimekufanyia hivi" ... Angelo aliongea kwa uchungu na kumpigia magoti Poshie .. "Nisamehe sana Poshie nakuahidi sitorudia tena kukufanyia hivi kama nilivyokufanyialeo.
Poshie alitokea kumpenda sana Angelo na kwa kitendo alichofanyiwa na Angelo alijisikia raha isiyo kifani moyoni mwake. lakini aliumia tu kwa manenoambayo Angelo amekuwa akimwambia na kumuomba msamaha.
*****
Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kupenda mpaka ukapitiliza. Ni bora upende lakini ombea usipitilize ... Poshie alitokea kumpenda Angelo mpaka ikapitiliza ikafikia atua bila kusikia sauti ya Angelo basi alikuwa apati usingizi siku hiyo {Ulishawahi kupenda kama Poshie wewe} ... Angelo pia alikuwa akimpenda sana Poshie laikni alikuwa akiogopa kwamba anaweza kumuaribia maisha yake ... "Kwanini leo haujapita nyumbani?' ... poshie alimwambia Angelo katika simu baada ya kutomuona kwa siku hiyo akikatiza mtaani kwao..."Kuna mambo yalinibana Poshie, alafu kwanini unapenda unione kila siku mimi naogopa kukupenda Poshie naweza kukuaribia maisha yako"... "Husiseme hivyo Angelo unaweza kuniua jamani naomba utambue mimi nakupenda mpaka basi" ..."Tatizo haujui kuhusu maisha. Nakuomba tuonane kesho ili nikuambie kila kitu kuhusu mimi" ... Kitendo cha Angelo kumwambia Poshie waonane kesho yake kilimfurahisha sana Poshie na kujikuta akishangilia kama mtu aliyepandishwa cheo ... Aliona usiku ulikuwa unachelewa kucha siku hiyo ili akakutane na mtu ambaye alikuwa akimpenda kutoka moyoni mwake
****
Ilikuwa siku ambayo alikuwa akiisubiri kwa hamu bibie Poshie, siku hiyo alivaa na kupendeza zaidi ya siku zote ... Angelo alikutana na Poshie na kuamua kwenda nae ufukweni mwa bahari ya hindi ili kuongea nae mawili machache ... Poshie alisikia furaha sana kutoka na Angelo siku hiyo ..."Mmependezana sana jamani" ... Dada mmoja ambaye walikutana naye kule ufukweni aliwaambia na kumfanya Poshie ajisikie furaha zaidi na kumkumbatia Angelo.
Angelo alimtembeza kwanza Poshie na kucheza nae michezo tofauti ya ufukweni .... Baadae walitafuta sehemu wakatulia ili Angelo amwambie kwanini yeye hataki kuwa na mahusiano na yeye ...."Nimefurahi sana Angelo kutoka na wewe leo yani najiona mwanamke mwenye bahati sana kuwa na wewe" .... Angelo alicheka kidogo kisha akamwambia ... "mimi nafikiri nina bahati zaidi kuwa na wewe kwa sababu ni wanaume wengi sana ambao wanatamani kuwa na wewe na kila siku wanakufuata lakini unawakataa" .... "Sawa bwana wewe si mwanaume najua amkubali kushindwa hata kwanini! ila mimi nitabaki kuendelea kuwa mwenye bahati zaidi sidhani kama kuna msichana yoyote wa mjini ambaye hasingependa kuwa na Mvulana mtanashati kama wewe" ..
Baada ya kutaniana kidogo Angelo aliamua kumwambia Poshie kwanini yeye hasingependa kuwa na yeye kimapenzi .... "Kiukweli mwanzo mimi nilikuwa nakutamani tu wala nilikuwa sina shida ya kuwa na wewe kimapenzi ila baada ya kuwa karibu na wewe na kuyajua maisha yako nilitokea kukupenda kweli na niliona haibu kukuchezea Poshie' .... "Nashukuru kusikia umeongea ukweli wako kuwa ulitokea kunitamani na ukajikuta umenasa kweli. Kama tatizo ndiyo ilo sasa si limekwisha, na tunaweza kuwa wapenzi" ..."Mimi napenda sana kuwa na mwanamke mrembo kama wewe lakini kinachonisumbua Mimi Poshie ni maisha yangu. Mimi sipendi kuwa na wewe nikuache, kwasababu nikifanya hivyo nitakuwa nimekuchezea na mimi sipendi hiwe hivyo" ... "Kwa nini uniache sasa wakati unanipenda Angelo" ... Angelo alikuwa mgumu kufunguka kwanini hataki kuwa na Poshie ila baada ya kuona Poshie anang'ang'ania sana, hakuwa na budi ilibidi amwambie ukweli. .... "Poshie nakwambia wewe siri yangu kwa sababu nakuamini sana. tafadhali naomba usimwambie mtu yoyote kuhusu maisha yangu" ... "Usijali Angelo mimi nakupenda mpenzi wangu haibu yako ni yangu mpenzi wangu na kamwe siwezi kuitoa nje hata siku moja" ....."Nashukuru sana kusikia hivyo Poshie na kama utakubaliana na mimi naahidi kukupenda mpaka naingia kaburini' ... Angelo aliongea na kutimzama Poshie na kujikuta machozi yakimtoka ... "Angelo kwanini unalia mpenzi wangu mbona unanitisha? Naomba ufute mchozi wako na uniambie kimoja baada ya kingine nini kinachokusibu na ikiwezekana tukitoka hapa mimi na wewe tuwe mke na mume watarajiwa" ... "Inaniuma sana poshie Naomba unihaidi kama utanipenda mpaka kifo kitutenganishe,Mpaka kifo kitutenganishe,mpaka kifo kitutenganishe,
Mpaka kifo kitutenganishe"
Sauti ya Angelo ilikuwa ikijirudia kichwani mwa Poshie huku mvua kubwa ikimnyeshea akiangaika kumtafutia pesa ya kumnunulia Dawa mwanawe. Mawazo yalijaa kichwani mwake akimkumbuka mwanaume ambaye aliyebadili Dira ya maisha yake .... Mvua ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba ilikuwa vigumu sana kuona kitu ambacho kinatoka mbele yako. ... akiwa anavuka barabara ghafla ilisikika gari ikifunga breki za ghafla na ikamvaa Poshie na kuanguka chini Pwaaaaaa!! ......

 NINI KITAENDELEA? ..



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa