KOVU LA MOYO 6 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

KOVU LA MOYO 6




"Mamaaaaa nimeua' ... Sauti ya kike ilisikika kutoka katika gari ambayo ilikuwa imemgonga Poshie.Aliamua kushuka katika gari ili kuja kumuona mtu ambaye alikuwa amemgonga.
Alikuwa ni Shakira ndiye aliyekuwa amemgonga Poshie .... Shakira alistuka baada ya kugundua kuwa aliyemgonga alikuwa ni Poshie, alimkimbila na kujaribu kumuamsha lakini wapi Poshie hakuweza kuitika ...Watu walimzonga Shakira wakimtuhumu kwa kuogonga Poshie lakini baada ya kugundua kuwa walikuwa wakijuana waliamua kumuacha na kumsahuri amkimbize Hospital. Wasamalia wema walimsaidia Shakira kumbeba Poshie na kumpakia katika gari kisha akamkimbiza Hospital ili apate uduma haraka iwezekanavyo ...Shakira aliumia sana kumgonga Poshie na alikuwa akimuomba mungu ili Poshie hasife. anakumbuka wakati Poshie alipoenda kwa Papaa Prince alikuja na mtoto, lakini apo hakuwa na mtoto ... Kitu ambacho kilimuumiza sana Shakira na akataka kujua wapi Poshie alipomuacha Henry ... "Dada naomba uamke ili uniambie wapi umemuweka mtoto? Kama utakuwa umemtupa utakuwa umefanya kosa kubwa katika maisha yako, kwa sababu hujui mungu amemuandikia nini yule Mtoto"... Shakira hakujua matatizo ambayo yalikuwa yamemkuta Poshie na yeye alijua labda kutokana na kukataliwa na Prince atakuwa ameamua kumtupa yule mtoto ... masikini hakujua kama Poshie alikuwa akitafuta pesa ili kumnusuru mwanawe ambaye alikuwa anaumwa, baada ya pesa alizopewa na Prince kuibiwa katika ajali.Shakira alifanikiwa kumpelaka Poshie Hospital na kwa bahati mbaya hakumpeleka katika ile Hospital ambayo Poshie alikuwa amemuacha mwanawe, yeye alimpeleka katika Hospital binafsi ambayo uwa anatibiwa yeye.
Poshie alipokelewa na kupelekwa katika wodi mahututi huku akiwa bado hajapata fahamu na alikuwa akimwagika damu nyingi sana ... "Tafadhali sana Dr Ben, nakuomba umsimamie ipasavyo ndugu yangu huyu" ... Shakira alimwambia Dr Ben huku akiwa amechanganyikiwa .... "Usijali Shakira tupo kwa niaba yake na yako tunaamini tutajitaidi kwa uwezo wetu wote ili kufanikisha afya ya ndugu yako" .... Dr Ben alimjibu Shakira na kumsihii apumzike ili wao wafanye kazi yao.
Japokuwa alikuwa hamjui Poshie na wamekutana kwa mwanaume wake huku Poshie akiwa amekuja na mtoto huku akidai kutelekezwa na Prince lakini Shakira alitokea kuguswa sana na matatizo ya Poshie japokuwa alikuwa bado hajajua kiundani matatizo ya Poshie ... Alishindwa kuamini kama Poshie amezalishwa na Prince kwa sababu Yeye anamwita Prince ni Angelo wakati Shakira yeye hajawai kusikia kama Prince anajina lingine la Angelo na alipojaribu kumbana zaidi Prince alikana kamfahamu Poshie.
Shakira alikaa mpaka usiku pale Hospital na kuamua kuondoka huku Poshie akiwa bado hajapata fahamu ... aliapa kumsaidia Poshie na Mtoto wake hata kama hamjui ila yeye aliamua kufanya hivyo kwa sababu ni mwanamke mwenzake
*******
Wakati Poshie akiwa katika matatizo huku ikiwa haijulikani hatma yake na yote yamemkuta kwa kutaka Mtoto wake wa pekee aweze kupona na kundelea kukuwa kama watoto wengine japokuwa Baba yake amemtelekeza na kumuachia yeye. Kwa upande wa Papaa Prince ukipenda mwite mpenda sifa siku hiyo alikuwa katika ukumbi mmoja maarufu ambapo kulikuwa na bendi kubwa ilikuwa ikipiga. Wasanii na wanenguaji wa Bendi huwa wanapenda kumsifia Papaa Prince mpenda sifa huku Wanenguaji wakienda kumkatikia Papaa Prince pale alipo.
Baada ya kusifiwa sana na kunogewa Papaa Prince,alinyanyuka huku akiwa ameshika kibunda cha pesa, alipanda jukwaani na kuanza kuzigawa kwa kila mwanamziki aliyekuwa katika bendi hiyo huku akicheza kwa madahaa ... "Sanda kalawe ... Amina...Papaa Prince mutu ya watu anataka kumwaga pesa wote tuseme ... Mwaga pesa ... Papaa ... Mwaga pesa Papaa mwaga Pesaaa" ... Ni wimbo ambao Papaa Prince alikuwa akiupenda sana na pindi akiimbiwa wimbo huo, Papaa Prince alikuwa akichukua vibunda vya pesa na kuanza kumwaga Sanda kalawe. Watu waligombea pesa za Papaa Prince Wakati Poshie amegongwa na gari kwa kutafuta pesa kiduchu ya kumnunulia dawa mwanawe ili kunusurumaisha ya mwanawe.
Baada ya kumwga pesa kwa watu ambao walikuwa hawana hata faida kwake sasa ilikuwa ni zamu ya kuchukua wanawake ambao walikuwa wakijiuza ... Kwa wale Wasichana ambao walikuwa na tamaa yapesa Papaa Prince alikuwa akiwapenda sana alikuwa akiwachukua kibao na kuwajaza katika gari yake na kwenda nao katika nyumba ambayo alikuwa amepangisha. Huko Shakira alikuwa hapajui na alichokuwa akifanya huko ni haibu hata kusimulia ... "Msiwe na shida ya pesa, hapa ni mahala pake kila mtu nitampa pesa mpaka achanganyikiwe na maisha yake kwa sababu nina pesa nyingi na sina kazi ya kuzifanyia" ... Prince aliwaambia wale Wasichana baada ya kuwakusanya kule ukumbini na kuwapeleka katika nyumba yake ya siri, Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Papaa Prince aliyokuwa akiishi kila siku
****
Usiku wa manane mvua kubwa ikiwa inanyesha ikiambatana na upepo mkali pamoja na ngurumo. Ilipiga radi moja kubwa iiyomstua Poshie nakupiga kelele ... Alijishangaa kujikuta sehemu ambayo hakuijua ni wapi lakini baada ya kufikiria sana alikumbuka ile ajali aliyoipata na akagundua alikuwa yupo Hosipital .... "Masikini mwanangu Hanry" ... Poshie alimkumbuka mwanawe na kuanza kulia kwa uchungu. Japokuwa alikuwa na majeraha mwili mzima lakini hakuyasikia maumivu yale zaidi ya kusikia tumbo la uchungu likimkamata. Akiwa kama mwanamke hakutamani kumuona mwanawe henry akifa ama kuoneshwa kaburi lake kwa sasa labda afe yeye na siyo mtoto wake.
Poshie alichomoa zile dripu alizokuwa amewekewa na kutoroka pale Hospital ili kwenda kumuona mwanawe ili ajue kama mzima au amekufa .... Akiwa njiani anakimbia huku mvua ikiwa inamnyeshea kwa wingi, Poshie alianza kuona kizunguzungu lakini alijikaza na kuzidi kukimbia hivyo hivyo .... Baada ya kukimbia sana Poshie alizidiwa na kuanguka chini kama mzigo ..... Pwaaaaaaaaaaa .....NINI KITAENDELEA? ... POSHIE ATAKUFA? VIPI KUHUSU HANRY? JE UNATABIRI NINI?



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa