KOVU LA MOYO 8 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

KOVU LA MOYO 8





Kitendo cha Prince kustuka kiasi kile, kilimstua Shakira na kuingiwa na wasiwasi juu ya Prince ..... "kwanini ulimkana mwanao mbele yangu? Kwanini uliamua kunificha kama wewe ndio Angelo?" ... Shakira aliongea, huku midomo ikimtetema kwa hasira
Prince alinyanyuka kwa hasira na kuomsogelea Shakira huku akitafuna meno kwa hasira ... "Maneno gani unayoniambia wewe Mwanamke? Nani unayemwambia maneno yako ya kipuuzi?" ... "Siitaji maswali yako yasiyo na kichwa wala miguu .. Aliongea huku akiwa amemtolea lakini haikusaidia kumfanya Shakira apunguze msimamo wake ... "Naitaji uniambie kwanini ulimkana mwanao mpaka yule mwanamke ameenda kumtupa?" ... "Pumbavu mkubwa wee" ... Prince alimzibua kibao Shakira kilichompeleka mpaka chini ... "Unataka niongeaje ili uniamini kama yule simjui? Kwahiyo wewe hautaki kuniamini kwa kile nikisemacho si ndio?" ... "Kama kweli sio mwanao kwanini umestuka kiasi hicho? Inamana kukuambia ukweli ndio mpaka unipige?" ... "Nimekupiga kwa sababu wewe ni mpuuzi na tena ukizidi kuniuzi nitakupiga tena sasahivi. Mwanamke gani una akili hata ya kuzaliwa? Yeye alisema Mwanae anaumwa na mimi nimemsaidia pesa ili ampeleke mwanae Hospital sasa iweje tena akudanganye amemtupa? wewe uoni kama yule mwanamke anamfanya Mtoto wake kama mtaji wa kumuingizia pesa?" ... Prince alichukia sana na kumfokea Shakira ... "Kama Hautaki kuniamini mimi basi nenda katafute mwanaume mwengine ambaye unaisi wewe utaendana nae" ... "Samahani sana Mpenzi wangu najua ni jinsi gani nilivyokukosea" ... Shakira alimwambia Prince huku akiwa amempigia magoti kumuomba msamaha mpenzi wake.
*****
Baada ya kutibiwa kutwa nzima na kutundikiwa dripu kazaa Poshie alifanikiwa kupata nafuu na kurejesha fahamu ... "Habari yako Mama Henry? Vipi unaendeleaje na hali yako? ... Poshie alisikia sauti ya mtu ambaye alikuwa ni mwanaume aliyeonesha kumfahamu kwa sababu alimuita kwa jina la Mama Henry.
Alitamani kugeuka Haraka ili amuone huyo mwanaume lakini alishindwa kutokana na maumivu aliyokuwa anayasikia na alikuwa anageuka kama Bibi wa miaka 90, kumbe alikuwa ni Dada wa miaka 24 tu ... alipogeuka alikutana na kijana mmoja mtanashati mweupe ambaye alikuwa akionekana mtu mwenye kujali sana ... "Namshukuru mungu mimi sijambo, japokuwa nasikia maumivu makali mwili mzima .. Yule Kijana akitabasam na kumwambia .."Pole sana, nilazima utajisikia kutokana na ajali uliyopata Jana, hata hivyo sindano ulizochoma zitakusaidia na utajisikia vyema ningeomba upumzike" .. "Samahani sana sijajua naongea na nani mwenzangu? na nimefikaje hapa?" ... "Pole sana Dada, mimi naitwa Dr Ally kama utakuwa unakumbuka vizuri juzi ulivyomleta mwanao mimi ndie Dokta ambaye nilikuambia ukanunue dawa na ulivyoondoka ndio haukurudi tena mpaka ukaletwa ukiwa katika hali hiyo" .... Kitendo cha Dr Ally Kumtajia Poshie mwanae kilimstua na kujikuta akipata nguvu ya ajabu na kunyanyuka kitandani kama mtu aliyestuka kutoka ndotoni .... "Mwanangu? .. Yupo wapi? .. Tafadhali Dr niambie kama mzima au amekufa?" ... "Poshie alimuuliza Dr Ally Maswali kibao tena kwa sauti ya juu kama alikuwa mtu ambaye alikuwa haumwi .. "Usijali Dada Nilijitolea kumsaidia mwanao baada ya wewe kutoonekana na mpaka sasa yupo katika hali nzuri na hali yake inaendelea vyema tu" ... Maneno ya Dr Ally yalimsisimua Poshie na kujikuta akilia kama Mtoto Mdogo kisha akanyanyua mikono yake juu na kumshukuru mungu kwa kumpa nafasi nyingine ya kujaribu kumlea mwanae aliyemzaa kwa uchungu japokuwa alikuwa bado hajakutana nae.
Poshie aligeuka na kumtazama Ally na kutamani kumwambia kitu chochote kile ambacho kingeendana na Msaada wake kwake, lakini kila kauli iliyokuwa imejaa katika kinywa chake alikuwa anaona kama anakosea ... "unajua Mwanao ni mzuri sana, kwanini umpi malezi bora? Unajua sijaamini kama Ningekuja kukuona tena hapa? niliamini kuwa utakuwa umemtelekeza mwanao" ... Ally aliongea kwa Upole na kuzidi kumtia simanzi Poshie ... "Napenda Mwanangu kumpa kila uduma muhimu ambayo mtoto anatakiwa apate lakini ndio hivyo Kaka yangu nina mengi yanayonisibu hata nikisema nikuambie hapa sidhani kama utanielewa. Japokuwa nina matatizo mengi lakini kamwe siwezi kutupa mwanangu niliyemzaa mwenyewe hata kwa nini" ...
Dr Ally alimpa pole sana Poshie na kuahidi kuwa atamsaidia kwa lolote kwa kipindi chote ambacho angekuwa apo hospital.
Baada ya kuongea naye mawili matatu Dr Ally alimuaga Poshie na kuondoka. Poshie alimtazama na kumuombea dua Ally na kutamani walau Angelo angegeuka na kuwa Ally
******
Baada ya kutibiwa kwa siku tatu hali ya Poshie iliendelea kuwa vizuri huku Dr Ally akimsaidia kwa kila jambo kama jinsi alikuwa amemuahidi
Baada ya hali ya Poshie kuimalika aliruhusiwa kutoka Hospita na Dr Ally alimchukua na kumpkia katika gari yake ndogo haina ya GX100 kisha akamuuliza ... "Haujawahi kuniambia unaishi wapi Poshie? Sasa sijajua nakupeleka wapi?" ... "Ni story ndefu kaka lakini mbona haujaniambia Mtoto yupo wapi?" ... "Usijali Mtoto Yupo salama kabisa na anaendelea vyema japokuwa ananyonya ziwa la Mama yake wa kufikia ambaye ni Ng'ombe" .. Ally alimwambia Poshie na kumfanya Poshie acheke mdomoni lakini moyoni alikuwa na majonzi tele ... "kwakuwa una hamu sana na mwanao ngoja nikupitishe nyumbani umchukue mwanao kisha nitakupeleka nyumbani kwenu" ... Dr Ally alimwambia Poshie kisha akawasha gari na wakaondoka eneo lile.
Sura imeumbwa na haya kama hauana haya basi wewe sio kiumbe hai kwa sababu hata Panya pia ana haibu ndiyo mana hata chakula anachoiba ulia shimoni ... Wakati wapo njiani wakitembea Poshie alikuwa na mawazo mengi sana juu ya aendako kwa sababu hakujua amwambie Dr Ally ampeleke wapi kwa sababu kwa Omega ndiyo ivyo tena amemfanyia unyama na kumfuza .. Prince naye ndiyo hivyo amemkana hamjui na kusema kuwa yeye si Angelo
Baada ya kutafakari sana aliona bora avunje ukimya na kuzungumza na Dr Ally "Kaka mimi ninamatatizo mengi sana na nilikuwa nahitaji msaada wako wa hali na mali" ... Poshie alimwambia Dr Ally huku akiwa na haibu kubwa sana na machozi yakimmwagika ... "Usijali Dada yangu ngojea basi nitafute sehemu ili uniambie kila kitu amabacho kinakusibu.
Baada ya kutembea kwa umbali kidogo Dr Ally alipata sehemu na kupaki gari kisha wakaingia kwenye mgahawa mmoja ili waongee ... Poshie alimuadisia kila kitu Ally kuanzia alipotoka pale Hospital na akagongwa na gari, pia alimwambia jinsi alivyotoroka kule hospital
Baadae Poshie alianza kumuadisia jinsi alivyotoka Nzega mpaka akakutana na Angelo na sisi tutaendelea pale Poshie na Angelo walipokuwa ufukweni.
>>>>
Poshie alimtazama Angelo aliyekuwa machozi yakimtoka kwa wakati ule kisha akamwambia kwa sauti fulani ya kusisimu .... "Sijawahi kumpenda Mwanaume yeyote yule katika maisha yangu Angelo na nipo tayari kwa lolote we niambie tu unachojisikia" ... Poshie alimwambia Angelo na kumfanya afarijike kisha akamwambia ... "Nimefurahi kukutana na mwanamke kama wewe katika maisha yangu Poshie na sidhani kama nitakuja kumpata mwanamke mwengine zaidi ya wewe ... Poshie mimi ni masikini ambaye nahisi sitoweza kuishi na wewe kwa sababu hapa mjini kwanza sina ndugu, sina kazi, wala sina makazi. Usione napendeza nje tu lakini mimi kulala kwangu ni kwa kusaidiwa na Rafiki yangu" ... Angelo alimwambia Poshie na kuendelea kumuadisia kuhusu maisha yake ..... "Mimi nilikuwa naishi na Mama yangu wa Kambo Jijini Mwanza ambapo nilitoroka na kuja hapa Dar es salaam nikiwa na miaka 15, kosa ambalo nimewahi kulifanya katika maisha yangu ni kuacha shule kitu ambacho kimenifanya mpaka sasa nikose kupata kazi ya kumudu maisha yangu sasa je nitaweza vipi kuishi na wewe Poshie wakati sina kazi wala sina pa kuishi?" ... "Pole sana mpenzi wangu, kwanza nakuomba usiseme wewe masikini wakati umetimia kila kiungo. Mimi nipo Tayari kuishi na wewe kivyoyote hata kama itakuwa ni nje ya nyumba. Maisha ni kutafuta na naamini mimi na wewe tukiamua na kupendana kwa dhati tanaweza kuyatafuta maisha na kila kitu kikabaki kama history kwa Watoto wetu. Mimi ni mwanamke na nitakubadilisha kwa kila jambo mpenzi wangu na utafanikiwa" ... Poshie alimwambia Angelo na kumfanya Angelo amrukie na kumpiga mabusu kwa mkupuo
******
Kuanzia siku hiyo Angelo na Poshie walianzisha mapenzi yao Rasmi na walikuwa wakikutana na kuongea mambo yao kwa siri ... Siku moja Angelo alimuita Poshie kwenye chumba cha Rafiki yake na kumwambia kuwa alikuwa na maongezi na yeye.
Poshie alifanya kazi za nyumbani haraka na jioni ilivyofika alivaa na kupendeza na kumfuata Angelo alipo.
Alifika na kumkuta Angelo akiwa hayupo sawa kabisa. Poshie alijaribu kutaka kujua Mpenzi wake alikuwa na tatizo gani ndipo Angelo alipomwambia .... "Tumekuwa Wapenzi jina mimi na wewe kwa mwezi wa sita sasa, leo nataka kufanya mapenzi na wewe, ili tufungue ukurasa wetu wa wapendanao" ... Angelo aliongea na kumstua Poshie kwa sababu hakuwahi kufanya mapenzi katika maisha yake.


NINI KITAENDELEA? ...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa