KOVU LA MOYO 31 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

KOVU LA MOYO 31





Poshie alistuka na kuanza kuogopa huku akiwa analia.
Aisha alimzibua kibao na kumuamuru anyamaze ... "Nyamaza wewe malaya. Hivi wewe unajiona mzuri sana si ndio?" ... Aisha alimwambia Poshie huku wakizidi kumpiga ... "Dada unanionea bure Mimi sitembei na Ally wala simjui, ameamua kunisaidia kwa moyo wake tu mimi sina mahusiano naye" ... "Sikiliza nikwambie, mimi siwezi kukuamini hata kidogo hivi Mwanamke gani anaweza kukuruhusu ukaishi na mpenzi wake? Ally anashindwa kunioa siku zote kumbe wewe ndio unaemfanya hasinioe?" ... "Kweli tena Dada yangu mimi siusiki nae" ... Poshie alimjibu Aisha huku akiwa bado anaendelea kulia
Aisha alimwambia Poshie kuwa anaweza kumuachia lakini kwa masharti ... "Mimi nipo radhi kwa chochote Dada yangu naomba uniruhusu ili nikamnyonyeshe Mwanangu" ... "Mimi nitakuachia ila ukitoka hapa naomba uondoke mara moja nyumbani kwa Ally na Endapo utaendelea kuwepo, nitakufanyia kitu kimoja kibaya sana katika maisha yako na ole wako ukamwambie Ally" ... Aisha alimchimba mkwala Poshie na Poshie akamwambia atafanya kama alivyomuagiza.
Walimchukua Poshie na kwenda kumbwaga karibu na nyumba ya Dr Ally ... Poshie alimshukuru mungu kwa kuweza kuponyoka ktk mikono yao
Poshie aliingia ndani na kumkuta Msichana wa kazi ... "Yupo wapi mwanangu?" ... "Mwanao amelala Dada, kwani kuna nini mbona upo hivyo?" ... "We niache tu mdogo wangu, wewe upaswi kujua chochote kuhusu mimi" ... Poshie aliongea na yule Msichana na hakutaka kumwambia kitu kwa kuofia anaweza kumwambia Aisha ....
Poshie aliingia ndani na kumchukua mwanae kisha akamwambia ... "Akija Dr Ally naomba umwambie kuwa mimi nimeondoka naenda kutafuta Maisha yangu na naomba hasinitafute, nashukuru sana kwa msaada wake alionisaidia" ... Baada ya kumpa maagizo Poshie alimbeba mwanae na kuondoka anapopajua
****
Dr Ally alijitolea kwa moyo wake wote kumsaidia Poshie pamoja na mwanae lakini tatizo kubwa lilikuwa kwa mchumba wake aliyekuwa akitaka kumuoa ...
Dr Ally akiwa anatoka kazini alipitia dukani na kuwachukulia nguo Poshie pamoja na Henry huku akiwa amembebea vitu vya kuchezea Henry Pasipo kujua nini ambacho kimetokea nyumbani
****
Baada ya kutoka nyumbani kwa Dr Ally Poshie alitafuta sehemu na kukaa na mwanae na kutafakari wapi aende kwa wakati huo ... Baada ya kutafakari sana aliona sehemu pekee ambayo anaweza kukimbilia na kupata msaada aliona ni kwa Bi Dua pekee.
Poshie hakuwa hata na senti mfukoni ambayo ingeweza kumpeleka kwa Bi Dua ... Mbaya zaidi Poshie alikuwa ametoka kupigwa na njaa ilikuwa ikimuuma yeye pamoja na mwanae ... Alipiga moyo konde na alimbeba Mtoto wake na kuelekea kwa Bi Dua
Ilikuwa ni safari ngumu lakini ilimbidi atembee ... Alitembea sana na kufanikiwa kufika nyumbani kwa Bi Dua akiwa hoi taabani ... Alipofika pale hakuamini kwa alichokiona mbele yake ... Nyumba ya Bi Dua ilikuwa imevunjwa na inaonesha kuna nyumba inataka kujengwa ... "Habari yako Kaka?" ... Poshie alimsalimia kijana mmoja aliyekuwa maeneo hayo ... "Nzuri sijui nikusaidie nini?" ... "Nilikuwa nakuja kwa Mama yangu lakini nashangaa kuona nyumba yake ikiwa imevunjwa?" ... "Mama yako? Huyo mama yako anaitwa nani?" ... Yule jamaa alistuka na kumuuliza ... "Ndiyo Mama yangu! Anaitwa Bi Dua. Kwani vipi mbona umestuka kiasi hicho?" ... "Unanishangaza kuniambia Mama yako Bi Dua alafu usiwe na taharifa zake" ... "Sina taharifa zake Kaka yangu hata mimi nimeshangaa kukuta hapa pamevunjwa" ... "Bi Dua ni Mama yako kivipi Dada yangu?" ... "Ni Mama yangu wa hiyari, mimi nilikuwa Mpangaji wake na alikuwa akinilea kama mwanae" ... Poshie alimuelezea kwa ufasaha na yule kijana akamuelewa ...
"Hapo sasa nimekuelewa Dada yangu. Pole sana nasikitika kukuambia kuwa Huyo aliyekuwa Mama Yako, hatunaye tena duniani" ... Poshie alistuka na kumuuliza vizuri ... "Unasema!! .. Bi Dua amefariki?" ... "Ndiyo amefariki katika mazingira ya kutatanisha na hii nyumba yake ilikuwa imezua utata mkubwa ndio mana ndugu wakaamua kuiuza. Hivyo hapa pameuzwa na Bi Dua amefariki muda tu, ndiyo mana nikashangaa wewe kuwa Mtoto wa Bi Dua.
Ilikuwa ni vigumu sana kwa Poshie kuweza kujizuia baada ya kupokea taharifa hizo.
****
Dr Ally alifanikiwa kufika nyumbani kwake salama usalimini ... Akaegesha gari, na kuchukua mizigo yake na kuingia nayo ndani ...
"Kabla ya yote naomba umuite kwanza mjeda wangu, mana nimemkumbuka kweli" ... Dr Ally alimwambia mfanyakazi wake wa ndani lakini yule Msichana alitizama chini na kuanza kulia ....
"Nisamehe Kaka kwa yote niliyoyafanya" ... Dr Ally machele yalimcheza kama kuna tukio limetokea ndani mwake ... Akaingia katika vyumba kadhaa na kujarbu kumuita Poshie kila eneo lakini wapi, Poshie hakuwepo ktk nyumba yake Muda mrefu ... "Yupo Wapi Poshie?" ... Dr Ally alirudi huku akipumua kwa shida na kumuuliza yule binti ... "Samahani Kaka, Dada Aisha, alimteka Poshie na sijui alimpeleka wapi. Kasema na anaondoka na anaomba husimuadisie mtu" ... Dr Ally aistuka na kuzidi kupagawa...


NINI KITAENDELEA



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa