KOVU LA MOYO 30 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

KOVU LA MOYO 30




Prince alimjibu Shakira huku akicheka kwa madaa.
Shakira alimtazama kwa hasira huku midomo yake mizuri ya kunyonya koni akiichezesha mithili ya simba mwenye njaa kaona swala .... Prince alimsogelea na kumshika kiuno kisha akamwambia ... "Hauwezi kuamini Shakira, Mr Love anajua sana kufanya mapenzi na ukijaribu utapenda ufanye tena na tena" ... Prince aliongea huku akikipandisha juu kigauni kifupi cha Shakira ... Konde moja zito la hasira lilimtoka Shakira na akamtwanga Prince ... "Mshenzi Mkubwa wee uliyelaanika ... Mimi siyo sawa na wanawake wako wa buku unawaokota huko mitaani" ... "Jamani heti anasema yeye siyo wa buku wakati nimemshuti mara kibao tukifanya mapenzi hahahahaha We Malaya tu" ... Prince aliongea na kuangua kicheko na kuwafanya Walinzi wake wote waangue kicheko
****
Asubuhi na Mapema Dr Ally aliamka na kumtazama Aisha akagundua kuwa alikuwa amelala ... Akachukua funguo ya gari na kutoka haraka ... Wakati anaondoka Aisha aliamka na kumtazama kisha akasema ... "Lazima nimuoneshe huyu binti, haiwezekani mimi nilale na mpenzi wangu usiku kucha na hasinifanye kitu inamana kaniona mimi gogo?" ... Aliongea mwenyewe kisha akachukua simu na kuonekana akiongea na mtu akimuelekeza kuhusu Poshie.
Kwakuwa ilikuwa ni Asubuhi na mapema hata foleni haikuwa kubwa siku hiyo ilimchukua kama dk 30 na kufika The green Love Park ... Hotel kubwa na ya kisasa aliyokuwa amempangia Poshie. Alifika na kumkuta Poshie ameamka muda mrefu akiwa amekaa kitandani huku akilia .... Kitendo cha kumkuta Poshie akilia, kilimstua sana Dr Ally na haraka akamkimbilia Henry ... "Kuna nini kilichotokea tafadhali naomba uniambie?" ... Dr Ally alimwambia Poshie huku akiwa na wasiwasi umemjaa moyoni na akizidi kumkagua Henry ... "Hata usijali Dr, Henry yupo salama na anaendelea vyema" .. Poshie alimwambia Dr Ally huku machozi yakizidi kumtililika zaidi na kujikuta akilia kwa kilio cha kwikwi.
Dr Ally alimtazama kisha akajisikia kama mwili wake unasisimka kwa kumuonea huruma, kisha akamfuata na kukaa karibu yake na kumshika mashavu kisha akamfuta machozi ... "Tafadhali nakuomba usilie Poshie kwa sababu ukilia unanikumbusha mbali sana" ... "Niache nilie Ally kwa sababu kulia ndio njia pekee inayonifanya nipunguze sumu iliyo moyoni mwangu ... Silii kwa sababu ya kuteswa na Aisha, nalia kwa sababu yangu najuta kwanini nilipenda? Kwanini nilimuamini Mwanaume? Hayo ndiyo makosa niliyofanya mpaka leo Maisha yangu yapo hivi Ally" ...
Kiukweli Poshie aliongea kwa uchungu mpaka Dr Ally alijisikia vibaya na kujikuta akimchukia Huyo Angelo japokuwa hamjui ... "Mimi sipendi kukuona ukiishi katika hali hiyo naitaji nikupe furaha ya milele na umsahau huyo Angelo naamini utakuja kupata Mume bora siku za usoni na akaja kukuoa tena mimi nikikusimamia kwa kila jambo. Maisha gani unapenda kuishi Poshie ambayo unahisi yanaweza kukupa furaha" ... Dr Ally aliongea huku akimfuta Machozi Poshie na kumfanya walau ajisikie faraja kwa mara nyingine anaguswa na mwanaume ambaye kidogo mstaarabu ... Poshie alinyanyua sura yake na kucheka kicheko furani cha majonzi ... "Nashukuru sana kwa maneno yako matamu yenye kutia faraja .. Nimefurahi sana kukutana na wewe kwa sababu unaonesha ni jinsi gani ulivyodhamilia kunipa furaha lakini nasikitika kukwambia unajaribu kuokoa kiroba cha sukari iliyomwagika baharini"... Dr Ally alimtazama kisha akamwambia ... "bado sijakuelewa ulikuwa unamaanisha nini?" ... "Namaanisha hivi Kunipa Mimi furaha basi labda unibadilishe moyo .. Angelo ameutia moyo wangu kidonda na inapotokea mtu akanitonesha basi lazima nilie, kwa sababu ninapolia huwa natoa machozi ambayo kwangu ndiyo unipa faraja. Nahisi km damu inatoka moyoni mwangu. Niombee mungu kidonda changu kipone na likibaki Kovu naamini stolia tena"
Dr Ally alimwambia kuwa yeye atajitaidi walau amponeshe kidonda chake ... "Unajua Mimi ndiyo Mtoto wa Mwisho kuzaliwa kwa Mama yangu ... Siku niliyozaliwa Mimi ndiyo siku ambayo Mama yangu aliyofariki .. Chozi lake la uchungu lilimtoa duniani najisikia vibaya kukuona unalia" .. Dr Ally aliongea na kujikuta akilia na Poshie akawa na kazi ya kumbembeleza yeye
Baada ya kuongea sana Dr Ally aliwachukua na kurudi nao nyumbani
"Dada yako yupo wapi?" ... Dr Alimuuliza Dada wa kazi kisha akamjibu ... "Yupo chumbani" ... Dr Ally akamshusha Poshie na kumuingiza chumba cha Mfanyakazi haraka ... "Umetoka kufanya umalaya wako ndo unarudi?" ... Aisha alimwambia Dr Ally na Dr Ally hakumjibu kitu badala yake akaingia chumbani na kujiandaa, kisha akatoka ili aende zake kazini ... "Unaondoka bila kunipa pesa mimi naishi vipi leo" ... Dr Ally akatoa Laki 3 na kumpa ... Aisha akachukua na kumtupia ... "Pesa hiyo nenda kampe malaya wako mimi hainitoshi ... Dr Ally akachukua na kumwambia ... "Sina pesa muda huu pitia kazini baadae" .. Aisha akachukua na Dr Ally akaondoka
Baada ya Dr Ally kuondoka Aisha akaleta watu wake na wakamteka Poshie ... "Leo lazima nikung'oe meno ili nione huyo bwnaaako atakupenda ukiwa na mapengo? .. Aisha alimwambia Poshie huku akiwa amemkunja
NINI KITAENDELEA?



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa