KOVU LA MOYO 3 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

KOVU LA MOYO 3






Maneno ya Poshie yalimgusa sana Shakira, alimtazama Prince na kujikuta akilia Baada ya kumuona Mpenzi wake analia Prince alijisikia vibaya na kuamua kumbembeleza Shakira.. "Naomba uniamini mpenzi wangu mimi simjui huyu masikini ameamua tu kuja kunichafulia jina" ...Prince alijitetea kwa Shakira huku akimtazama kwa jicho baya Poshie ... "Sikiliza wewe Masikini kama unashida ya pesa sema nikusaidie lakini siyo vyema kumgombanisha mtu na mpenzi wake. Mimi sikujui naomba toa huu uchafu wako kabla sijaukanyaga" .."Mimi siyo mjinga mpaka ni vuke kote huko mpaka nikufuate wewe! sina shida ya pesa yako japokuwa nimezaa na wewe isipokuwa nimekuja hapa kufuata maitaji ya mtoto kwa sababu ni wajibu wako kumuhudumia na kama kweli huyu siyo mwanao naomba umruke, apo nitajua kuwa umemkana mwanao na mimi nitaondoka katika nyumba yako"...
Damu nzito kuliko maji Wahenga walinena. Roho yaPrince ilikuwa nzito kumruka Henry sijui kwanini? uenda alikuwa ni mtoto wake kweli, lakini kwanini Poshie amwite Angelo badala ya Prince? siyo bure kutakuwa na kitu ndani yao ... Prince alimtizama Poshie kisha akamtizama Shakira na kumgeukia Henry aliyekuwa chini. kwakuwa Shakira alikuwa akizidi kulia Prince alijua labda analia kwasababu anahisi yule mtoto ni wake na yeye alitaka kumdhihirishia kuwa yule si mtoto wake. alivuta pumzi kwa wingi na kuzia chia kwa mkupuo kisha akaamua kumruka ..
Kabla hajafanikisha tendo lake Shakira alitoka na kumsukuma ili hasimruke Henry na kweli Prince hakumruka mtoto ... "Siamini kama Prince una roho mbaya kiasi hiki! Yani unataka kuikana Damu yako mbele yangu? Siwezi kukubali hata siku moja kuona mwanamke mwenzangu akinyanyasika mbele yangu. Kama unaweza kumfanyia huyu hivi hata mimi unaweza kunifanyia zaidi ya hivi siku moja. Naomba mpe pesa ampeleke Mtoto Hospital" ... Shakira alimwambia Prince kwa uchungu huku akilia .... "Lakini Shakira mpenzi wangu mimi simjui huyu" .. "Huyu siyo chizi Prince naomba umpe pesa mtoto anaumwa huyu"... Prince alijisikia vibaya sana kwa maneno ya Shakira aliamua kwenda ndani huku akiwa amechukia
Shakira alimuokota Henry pale chini na kumpa Poshie kisha akamwambia ... "Pole sana Dada yangu nimejisikia vibaya sana kwa jinsi alivyokujibu Prince, lakini ni kweli umezaa nae?" ... Shakira alimwambia Poshie huku akiwa amemkumbatia Henry ... "Nashukuru sana kwa ukarimu wako. Ni wanawake wachache sana wenye moyo kama wewe ndio mana wanaume wanatuonea na kutukandamiza kila siku, kwasababu tu Wanawake hatupendani. Huyu ni mwanae na yeye ndiyo Baba wa mtoto huyu Nashukuru sana kwa yote ambayo amenifanyia Angelo ila mimi naamini mungu analipa hapahapa Duniani" ... Poshie alishindwa kuongea zaidi nakujikuta akilia sana.
Prince alitoka na kumtupia pesa Poshie kama mbwa kisha akamwambia ... "Sikiliza nikuambie wewe changudoa, mnazaa ovyo huko mitaani alafu mnatafuta wa kuwapakazia ukome kuja nyumbani kwangu, na ukija tena hapa nakupiga risasi" .. Poshie alitaka kuokota zile pesa Shakira akamzuia kisha akampa Mtoto na kuziokota yeye zile pesa na kumpa kisha akamwambia ... "Siku moja mungu atakulipia machozi yako, usikate tamaa katika kutafuta maisha yako na ya mtoto wako. Wanaume si chochote katika maisha yetu. Wanatupenda sisi tukiwa wazima na tukipendeza mbele yao lakini tunapokuwa na badiriko yoyote ikiwemo mimba basi wao sijui wanatuonaje na kutuachia mizigo ya kulea familia ambazo wao ndio chanzo kikubwa chafamilia hizo" .... Poshie alimshukuru Shakira na kuondoka zake.
Kitendo cha Shakira kumsaidia Poshie na kuongea maneno mengi ya kumpa ushauri kilimkela sana Prince na akamuuliza Shakira .. "Sikutegemea kamasiku moja ungekuja kuniusisha na wanawake wa ajabu hivi wewe unanichukuliaje mimi?" ... "Naomba usiniuzi Prince yule ni mtoto wako na kama siyo mtoto wako basi siyo mbaya utakuwa umemsaidia mtu ambaye hata mungu atakulipa kuliko wale wasichana ambao wanacheza uchi uliokuwa unawapa pesa jana, naomba tuongee mambo yetu tuachane na yule msichana ila siyo vyema kumpachika majina ya ajabu mwenzako na kama kweli ulimpa mimba utakuwa umefanya kosa kubwa sana kumtukana
"****
Hali ya Henri ilizidi kuwa mbaya sana, Poshie aliamua kuchukua Tax na kumkimbiza Hospital. Akiwa njiani alikumbuka kashifa ambazo alikuwa akipewa na Mzazi mwenzie aliumia sana na kuzidi kulia ... "Nawachukia sana Wanaume na nitaendelea kuwachukia maisha yangu yote. Kama Angelo amenitukana na kunikashifu mbele ya mwanamke mwnzangu sidhani kama kutakuwa na Mwanaume ambaye atakuwa na mapenzi ya dhati katika Dunia hii" ... Alikuwa aniongea mwenyewe huku akilia
Wakati akiongea mwenyewe ghafla macho yaHenry yalibadilika na mwili wake ukakakamaa ..."Dereva ongeza Mwendo mwanangu anakufa" ... Dereva aliongeza mwendo lakini Poshie alikuwa bado akilia na kupiga kelele kuwa mwanawe anakufa. Dereva aligeuka ili kumtizama mtoto huku anaendesha gari. Masikini kulikuwa na mtu anavuka barabarani na Dereva alikuwa hajamuona. "Dereva unauwaaaaaa!!!" Poshie alipiga kelele na Dereva akamkwepa ghafla ... gari iliacha njia na gari ikaingia kwenye mtalo na wakapata ajali .....NINI KITAENDELEA? .. JE POSHIE NA MTOTO WAKE WATAKUFA? ANGELO NI NANI NA PRINCE NI NANI? VP KUHUSU OMEGA?



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa