KOVU LA MOYO 4 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

KOVU LA MOYO 4






Gari ilijibota kwa mbele na kufunuka, kioo kilivunjika na kumjeruhi Dereva na Poshie kidogo.
Poshie hakuwahi kupata ajali ya gari katika maisha yake. alichanganyikiwa sana kwa ile ajali waliyoipata ... Wakati akiangaika kujichomoa katika ile gari, watu walifika na kumsaidia kumchomoa. Poshie alikuwa ni mwoga sana wa damu na alipomuona yule dereva ameumia vibaya huku damu zikimmwagika kwa wingi alizidi kuchanganyikiwa... Maisikini bila ya kujua kama apo kulikuwa na watu wema na wengine wamekuja katika kujinufaisha wao, Poshie alipojisahau kidogo tu walimuibia zile pesa ambazo alipewa na Prince na kubaki kama alivyo ... "Nimeibiwa jamani nimeibiwa" .. Poshie alipiga kelele huku akilia. Lakini hakupatikana mtu yoyote yule.
Hali ya Henry ilikuwa inazidi kuwa mbaya, Poshie alipata msaada kwa wasamalia wema na kukimbizwa Hospital."Hali ya mwanangu mbaya sana Nesi, naomba msaada wako" .. Poshie alikuwa akimuomba msaada Nesi ambaye alikuwa kama amsikii akiendelea na mambo yake ... "Kaa kwenye foleni kila mtu aliyekuja hapa ni mgonjwa na ana hali mbaya, kwani kuna unayemuona aliyekuja kupiga picha hapa" .. Yule Nesi alimjibu Poshie kwa zarau na kuwafanya baadhi ya watu waliokuwa apo kuingilia swala hilo .... "Dada hivi unajua uchungu wa mtoto wewe au unaongea tu? Jaribu kuwa na majibu mazuri siyo vizuri kumjibu mtu utumbo, wakati hali ya mtoto wake ni mbaya je akimfia mikononi utafanyaje?" ... Jamaa mmoja alionekana kuchukizwa na kauli za yule Nesi alimjibu na watu wakaanza kumshambulia kwa maneno mpaka akaondoka.
Henry alikuwa na malaria kali sana hivyo moja kwa moja alikimbizwa wodini ... "Inaonesha hautumii chandarua nyumbani?" ... "Ndiyo Dokta" ... "Kwanini unafanya hivyo wakati unajua una mtoto mdogo?" ..."Ni story ndefu sana ila kama kutakuwa na msaada wa kutibiwa huyo mtoto naomba msaada huo" ..."Kwa mujibu wa Selikari Watoto kuanzia Mwezi 1 mpaka miaka 5 huwa wanatibiwa bure. Mwanao atapata baadhi ya dawa hapa na dawa nyingine itabidi ukanunue hapo nje kwa sababu Hospital haina dawa" ... "Mimi sina hata shiringi Kaka yangu naombeni msaada wenu" ... "Tatizo hizo baadhi ya dawa hakuna Dada kama zingekuwepo tungemuudumia mwanao nenda kalete dawa haraka hali ya mtoto ni mbaya" .. Dokta alisisitiza hili Poshie akanunue dawa
Poshie alitoka nje huku mvua kubwa ikinyesha ikiambatana na upepo mkali ... "Mama ni Mama hakuna kama Mama, hata akiwa mdogo mama ni mama" .. alikumbuka sana wimbo huo ambao alikuwa anaimba akiwa mdogo. Hakuwa na jinsi mtoto wa kike ilimbidi aingie kwenye mvua huku yeye mwenyewe akiwa na majerahaa aliyoyapata katika ajali, lakini aliona bora akatafute pesa ya kumnunulia dawa mwanawe. wakati anatembea kwenye mvua mawazo mengi yalitawala katika kichwa chake na alikumbuka jnsi alivyotoka mbali na Angelo lakini leo hii amemuachia mtoto anateseka peke yake .....NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA!!............
Baaada ya kufiwa na wazazi wake wote wawili, Poshie alikuwa akiishi na Bibi yake huko Nzega mkoani Tabora. yalikuwa ni maisha magumu sana ambayo Poshie alikuwa akiishi na Bibi yake kwa sababu uduma pekee zilikuwa zinatoka kwa mjomba wake aliyekuwa anaishi Dar es salam. Baada ya miaka miwili Bibi naye alifariki na katika kikao cha familia mjomba aliamua kumchukua Poshie ili aje kumsomesha jijini Dar es salamBaadaa ya kufika Dar, Mjomba hakufanya kama alivyohaidi katika kikao cha familia, hakumpeleka Poshie shule na badala yake alimfanya kama mfanyakazi wa nyumbani kwake ....
Baba yake Poshie alikuwa ni Mwarabu na mama yake alikuwa ni Mnyamwezi mchanganyiko huo uliwafanya watoe msichana mmoja aliyekuwa anasumbua mtaani kote. Poshie alikuwa ni Msichana mmoja mzuri sana na kila aliyemuona alitamani ampate aswa kwa kipindi hicho ambacho anabarehe, alikuwa akimvutia kila mwanaume aliyekutana naye.
Hakuwa msichana mjinga hata siku moja, kila mwanaume aliyemuona na kumtongoza alitoka kapa kwa Poshie. Kutokana na ugumu wake alipachikwa majina mengi na wavurana na kwakuwa alikuwa ni bikra na wanaume walikuwa wanazidi kuchanganyikiwana hiyo kitu kila siku wlikuwa wakiongezeka.
Siku moja akiwa anatoka sokoni akasikia anaitwa na Mvulana mmoja akageuka na kumtizama, alikuwa ni kijana mmoja mtanashati alikuwa amependeza baraa ... Poshie alirudi na kwenda kumsikiliza yule kijana .... "Samahani sana kwa kukusumbua sijui unaitwa nani?" ... Yule kijana aliongea na sauti yake ikammaliza kabisa Poshie ..."Salam huwa inaonesha jinsi gani mtu ni muungwa siyo kurupu tu unataka jina langu" ... "Mungu katuambia tusamehee kwa sababu alijua kutakuwa na watu wakosaji kama sisi sasa bila kukosea nitakuomba samahani saa ngapi. Samahani sana na ningeomba nijipe adhabu mwenyewe, leo usinitajie jina lako mpaka siku nyingine nikikusalimia" ... Akika yule kijana alikuwa ni mcheshi balaa na Poshie alikuwa hana mbavu kwa kucheka. akageuka na kuondoka na yule kijana akamwita tena ... "Sasa mbona wewe unajiazibu bilakosa wakati wewe ulinisalimia? Mimi naitwa Angelo. Ni haki yako kunifahamu jina langu" ... Yule jamaa aliongea na kumfanya Poshie azidi kucheka na akaondoka.
Poshie na Angelo walizoena na kuwa marafiki wakubwa na siku moja Angelo aliamua kumwambiala Moyoni mwake ... "Nimefurahi sana kukutana na wewe Poshie lakini kwa sasa nilikuwa nakuomba mimi na wewe tupunguze ukaribu ikiwezekana hata kwa mwezi tonane mara moja" .... "Kwanini unasema hivyo Angelo? Mimi nimekuzoea sana na siwezi kupitisha siku bila ya kukuona wewe" ... "Na mimi ndiyo sipendi tufikie hivyo kwa sababu najikuta moyo wangu unakupenda Poshie na mimi masikini siwezi kuishi na mwanamke mzuri kama wewe ni bora ujiturize unaweza kupata mwanaume"... Poshie alistuka na kunyanyuka ... "Nilijua siku zote unanipenda kumbe haunipendi? Sawa nashukuru" ... Poshie alitaka kuondoka na Angelo akamshika mkono na kumvuta kwake, wakakutana Vifuani na kutizamana. ... baada ya kutizamana kwasekunde chache Angelo alimfuata Poshie mdomoni na kumpa juice ya mahaba .....


Nini kitaendelea???.....



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa