KOVU LA MOYO 2 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

KOVU LA MOYO 2




Poshie alianguka kama gunia la viazi ... "Pwaaaa"Alifikia mdomo na kujing'ata ulimi. Damu zilimtoka kama amechinja kuku kwa mdomo ... Wanasema uchungu wa Mwana aujuae Mzazi. Ndivyo ilivyokuwa kwa Poshie hakujua hata kidogo kama ameumia badala yake alijisikia uchungu mwanawe kutupwa kwenye mvua ...
Alimuokota mwanawe kwa uchungu huku akilia na kumkumbatia.
Henry alikuwa akitetemeka kwa baridi huku sauti ikiwa imemkauka kabisa. Poshie alijitaidi kumvika nguo nyingi Henry ili kumnusuru na baridi lakini wapi hali ya Henry ilizidi kuwa mbaya."Tafadhali Omega naomba unifungulie Mlango hali ya Mtoto ni mbaya sana" ... Masikini Poshie alijitaidi kumgongea Omega lakini wapi Omega aliuchuna kama amsikii ... Baada ya kumgongea sana Omega na kumchunia Poshie alimchukua Henry na kujibanza nae ukutani huku Mvua ikimuangukia mgongoni mwake.
****
Pesa haiwezi kukununulia furaha lakini hata umasikini nao hauwezi kukupa furaha ...
Japokuwa Shakira alikuwa amechukia sana kumkuta Prince akifanya mambo ya kipuuzi lakini hakuwa na hoja ya nguvu zaidi. Kwa sababu yeye pia amempendea pesa Prince ... "Najua umenuna ila kuna taharifa moja nzuri naitaji kukuambia kidogo kisha utaendelea kununa" ... Prince alimwambia Shakira huku akiwa anaendelea kunywa ... "Sema nakusikia"... Shakira alimjibu Prince huku akiwa bado kaendelea kununa ... "Naitaji kufunga ndoa na weweangani tukiwa ktk ndege kubwa ya kisasa" ... Shakira alistuka kisha akageuka na kumtizama huku akiwa anatabasamu ... "Siamini Prince kama itakuwa kweli" ... "Amini kuanzia sasa kwamba itakuwa kweli" ... Papaa Prince aliongea huku akijiamini ..."Lini unafikiria kutimiza ndoto yangu?" ... "Hata ukisema kesho mimi nipo tayari kukuoa Shakira na nafanya hivi kwa sababu nakupenda ... Shakira alifurahi na kumkumbatia kwa nguvu Prince na kumwambia ... "Nakupenda sana mpenzi wangu" ... Shakira alimwambia Prince huku akimfuata mdomoni na kuanza kumbusu mdomoni huku akimpapasa.
Ulikuwa ni usiku mzuri wa haina yake huku kila mmoja akimuonesha mwenzake kwamba yeye si wa kupita bali anatakiwa waishi wote ... Hakuna mwanamke ambaye hasingependa kuolewa na Papaa Prince na ndio mana Shakira kwake aliona kama mtende umeota jangwani.
****
Asubuhi na mapema poshie alidamka na kumpeleka mwanawe Hospital ili apate uduma yoyote ... Pesa ndiyo kila kitu ktk maisha ya sasa na kama hauna pesa unaweza kufa na usipate msaada wowote.
Japokuwa alimpeleka mtoto Hospital, lakini kwakuwa Poshie hakuwa na pesa hakupata uduma yoyote pale Hospital ... "Kwanini lakini Angelo ananitesa kiasi hiki? Angelo alikuwa akiniambia maneno matamu yenye kusisimua, leo ameniacha nateseka na Mtoto peke yangu?" ... Poshie aliongea peke yake huku akiwa hana la kufanya.
****
Ukiwa na pesa kila jambo ambalo uwa unapanga linaenda kama ulivyopanga na muda mwingine unaweza ukaishi kama mtoto ... Baada ya kuamka Asubuhi Shakira na mpenzi wake waliingia Gym iliyokuwa humo humo nyumbani kwa Prince na kufanya mazoezi.
Baada ya kujiona wamefanya mazoezi ya kutosha, Shakira na Prince walitoka na kuja ktk bustani ya maua na kupumzika lakini baadae wakaanza kucheza kwa kumwagiana maji kupitia mpira uliokuwa unamwagilia mauwa.
Wakiwa wanaendelea kumwagiana maji kwa furaha mara wanamuona mwanamke akiingia ndani kwa uchungu huku mikononi akiwa ameshika mtoto na alikuwa akilia yule mwanamke huku akimkazia macho Prince.
Hakuwa Mwanamke mwengine bali alikuwa ni Poshie aliyekuwa amembeba Henry ...
Prince alitizamana na Shakira kisha akamuuliza ..."Unamjua huyu?" ... "Hapana simjui labda unajuana naye wewe" ... "Mimi pia simjui labda atakuwa amekosea njia"Poshie alizidi kumkazia jicho Prince huku akilia ndani ya moyo ... "Dada leo siyo siku yangu ya kutoamsaada labda ungekuja siku ya Ijumaa" ... Poshie alimtizama Prince kisha akaguna na kufuta mafua yake kwa mkono wake ... "Unajidanganya sana Angelo heti leo mimi unijui au kisa huyu malaya wako?" ...
Kitendo cha kuitwa Malaya kilimchoma sana Shakira na akataka kupigana na Poshie. Prince alifanikiwa kuwazuia na hakuna aliyempiga mwenzake."Sikiliza nikwambie wewe msichana. Mimi sikujui na naomba uondoke nyumbani kwangu" ... "Sawa nashukuru kwa kunisahau ila tambua kama mimi nina damu yako. Vipi kuhusu mtoto nimekuja kuchukua pesa ili nikamtibie kwa sababu hali yake mbaya" ... "Dada ondoka kwangu mimi sikujui" ..."Angelo unasemaje?" ... "Kwanza sitaki uniite sijui Angelo mimi sitaki. Alafu mimi sina mtoto na wala sikutambui naomba utoke nyumbani kwangu kabla sijakufanya kitu kibaya" ...
Hali ya Henry inazidi kuwa mbaya. Poshie alitegemea apo alipoenda anaweza kupata msaada ... "Nashukuru kwa kunikana mimi pamoja na Damu yako mwenyewe. Kwa mimi haina shida hata kama umenikana ila nataka kuona kwa huyu mwanao kama kweli unamkana na humjui kama huyu ni mtoto wako. Naomba umruke mwanangu apo ndipo nitaamini km kweli umemkana na siyo mwanao" .. Poshie aliongea na kumuweka mtoto chini.



NINI KITAENDELEA?



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa