KOVU LA MOYO 27 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

KOVU LA MOYO 27




Kauli ya Angelo ilimstua sana Poshie. Akanyanyuka na kumtazama kwa makini"Unasemaje Angelo?" .. Poshie alimwambia Angelo huku akiwa haamini kauli ya Angelo .."Inamana haukunisikia au jeuri yako?" .. "Sijakusikia Vizuri Baba Henry ndiyo mana nikakuuliza" .. "Kwa ufupi ni kwamba, wewe siyo Mwanamke wa adhi yangu na siwezi kuishi na wewe"... Hakuwa Angelo yule ambaye unamjua wewe, Angelo alikuwa amebadilika na kusahau kabisa alipotoka.
Poshie alijitaidi kushuka na kujaribu kumbembeleza Angelo hasichukue uamuzi ambao alikuwa anataka kuuchukua ... Angelo hakutaka kumuelewa Mkewe hata kidogo alishikilia mawazo yake na kuamua kumfukuza Poshie nyumbani kwake ... "Angelo hebu jaribu kumuogopa mungu, mateso yote niliyopitia nawewe leo tumefanikiwa unataka kunifukuza? Sawa mimi naweza kuondoka hapa nyumbani kwako lakini vipi kuhusu huyu Mtoto wako Mimi nampeleka wapi usiku huu?" ... Poshie alimwambia Angelo huku akiwa analia ... "Wewe unanichekesha sana. Mimi sina Mtoto ktk hii Dunia wewe na Mwanao Mtajua wapi pa kwenda" ... Aliongea kwa jeuri ya hali ya juu km sisi yeye ambaye alikuwa akimsifia na kudai hatomuacha ktk Maisha yake
Angelo alimpiga sana Poshie na kumtupa nje ya nyumba yake.
****
Wanaume wakorofi, siku zote wanapata Wanawake wapole na Wanawake Wakorofi mara nyingi upata Wanaume wapole.
Ndivyo ilivyokuwa kwa upande wa Poshie na Angelo. Poshie alikuwa Mpole sana na Angelo alikuwa mkorofi kupita maelezo.
Poshie akiwa nje alilia sana na hakujua wapi aende kwa muda ule ... Angelo alimpokonya kila kitu ikiwemo funguo ya gari na apo ndiyo alikuwa amemmaliza kabisa ...
Baada ya kutafakari sana Poshie alitamani arudi kwa Bi Dua ili akamuombe lakini akakumbuka jinsi Walivyoondoka na Angelo.... Sehemu pekee ambayo aliona anaweza kupata msaada wa haraka ilikuwa ni kwa Omega na aliamini Omega anaweza kumsaidia kwa sababu alikuwa kama ndugu yake, kutokana na sehemu waliyokuwa wakitoka .... Akatizama ktk pochi yake kulikuwa na Tsh 50,0000. Akachukua na kukodi bajaji iliyompeleka mpaka pale anapouza miogo Omega. Kwa bahati mbaya Omega alikuwa amefunga biashara yake kwa muda huo. Haraka aliwaulizia vijana wa pale na wakampeleka ... "Vipi mbona usiku sana?" ... Omega alistuka na kumuuliza Poshie baada ya kufika nyumbani kwake .... "Ni story ndefu Kaka yangu naomba nipumzike kwanza kisha nitakuadisia kila kitu" ... Poshie alimwambia Omega na huku akiwa bado analia ... Omega alimkaribisha ndani kwake huku akiwa na shauku ya kutaka kujua nini kilichomsibu.
Poshie alimuadisia Omega kwa ufupi ila aliogopa kumuelezea mazingira ambayo Angelo alipozipata pesa kwa sababu alikuwa hamuamini Omega ..."Pole sana Poshie kwa matatizo yaliyokusibu. Sasa ulikuwa unataka msaada gani kutoka kwangu?" ...."Mimi nilikuwa naomba ifadhi tu kutoka kwako Omega mana sina pa kuishi" ... "Sawa Mimi nitakusaidia kwa ilo lakini utaweza maisha ya hapa? Mwenyewe si unaona jinsi ninavyoishi?" ..."Nimeishi maisha magumu haya ya kwako ni mazuri sana, we usijali" ...
Omega alimshauri Poshie akamshitaki Angelo kwa jambo alilo mfanyia lakini Poshie alikataa na kuamua kumuachia mungu.
*****
Maisha ya kwa Omega yalikuwa ya kawaida lakini yalikuwa magumu kwa Poshie kwa sababu alikuwa amesahau kuishi maisha hayo ...
Mwanzoni Omega alikuwa msataarabu sana na wakawa wanaishi kama mtu na Dada yake. Lakini baadae baada ya Poshie pesa kumuishia, Omega alibadilika na kuanza kumnyanyasa Poshie ... Siku Moja Omega alimbaka Poshie huku Henry akiwa anaumwa na akilia kwa sauti ... Baada ya kumaliza kufanya kile kitendo Poshie aliogopa kumshika mwanae kwa kuogopa kumualibu na akakimbilia kwenda kuoga ...Alipotoka kuoga akamkumta Mwanae ametupwa ktk Mvua huku akiwa amelia mpaka amekauka sauti ... Omega alimtupia mizigo yake na kumfukuza nyumbani kwake ...
POSHIE ALIMALIZA KUMSIMULIA DR ALLY MKASA WA MAISHA YAKE
Baada ya kumaliza kumsimulia Dr Ally, Poshie alilia sana na Dr Ally akawa na kibarua cha kumbembeleza ... Ally alisononeka sana kwa kitendo ambacho Poshie alifanyiwa na Angelo ..."Pole sana naamini mungu amekusikia kilio chako na siku moja atajibu maombi yako. Ila ningependa kukushauri ukacheki afya yako kwanza kwa sababu haujui huyo Omega ana maradhi gani" ... Dr Ally alimwambia Poshie na Poshie akamjibu yupo tayari kucheki afya yake.
Baadae Ally aliamua kumchukua na kuondoka naye nyumbani kwake ... "Samahani Dokta! Haujaniambia Mwanangu yupo Wapi?" ... "Husijali Poshie Mwanao yupo nyumbani, tena yupo ktk mazingira mazuri" ... Poshie alitabasam kidogo kisha akamwambia ..."Yupo na Mkeo?" ... "Hapana Mimi bado sijaoa ila nina Mchumba anaitwa Aisha. Henry yupo na Dada wa kazi ila hata Aisha pia anapenda sana Watoto atafurahi akimuona" ... Dr Ally alimwambia Poshie huku akiwa anaendesha gari
Baada ya Mwendo wa Dakika kazaa Walifanikiwa kufika nyumbani kwa Dr Ally na akamkaribisha Poshie ndani ... "Mage Huyu ndiyo Mama wa yule Mtoto" ... Dr Ally alimwambia Dada wa kazi na akadakia Aisha kumbe alikuwa ndani ... "Yani umefanya huko umalaya wako sasa unakuja na machangudoa ndani na kuniletea kinda la changudoa? ...
NINI KITAENDELEA?



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa