KOVU LA MOYO 26 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

KOVU LA MOYO 26




Angelo alikuwa hajawahi kuona pesa nyingi kiasi kile, hivyo alikuwa kama mtu aliyekuwa amechanganyikiwa
Alikimbia mpaka ndani huku akiwa bado anamwita Boss wake ... Wakati anakimbia kwa bahati mbaya alijikwaa na kuanguka. Pale alipojikwaa aliigonga mbao iliyokuwa na kopo la rangi nyeusi na lile kopo likaanguka na ile rangi ikamrukia Boss na kumchafua katika shati lake jeupe .... Yule Boss alichukia na kumfuata akamnyanyua na kumzibua kibao ... "Unasemaje we mpuuzi unaona sasa ulivyonichafua?" ... Boss alimwambia huku akiwa amechukia.
Kwakitendo cha kumzibua kibao Angelo, kilimrudisha akili zake na haraka sana akampotezea Boss wake ... "Nilikuwa naulizia pesa yangu Boss inamana nimefanya kazi bure?" .. Angelo alimjibu baada ya kuona anataka kumpa utajili mtu ambaye hakupangiwa na mungu .... "Pesa yako ndio naenda kufua shati langu na nikifunba macho na kufumbua sitaki kuiona sura yako machoni mwangu. Kimbia haraka sana kabla sijakufanya kitu kibaya" ... Ama kweli husilolijua sawa na usiku wa giza, laiti angejua kuwa mwenzake alikuwa anamletea pesa zisizo na mwenyewe hata hasingekifanya alichoamua kukifanya.
Baada ya kutimuliwa Angelo alitoka nje huku akiwa na nguo zake chafu za kazi. Wakati anatoka akaokota kiroba, akakichukua na kwenda kuweka lile begi la pesa kisha akatoa noti ya Tsh 10,000 na kuishika mkononi.
Akachukukua bajaji iliyompeleka mpaka nyumbani kwake akashuka haraka na kiroba chake chenye pesa na kuingia nacho ndani kwake ... "Imekuaje Mke wangu mbona mtoto analia kiasi hicho" .. Angelo alimuuliza Poshie baada ya kumkuta Henry akiwa analia ... "Njaa inamuuma mtoto ameshinda bila ya kula, nimemchemshia maji ya chumvi ili ale lakini wapi bado anaendelea kulia, na mimi siwezi kumnyonyesha kwa sababu maziwa yangu yanatoa damu" ... "Pole sana mwanangu kweli una haki ya kulia lakini usijali mwanangu kwa sababu ujio wako hapa duniani kwangu ni mzuri na umekuja na bahati isiyo na kifani" ... Angelo aliongea kwa furaha huku akiwa anamrusha mwanae hewani huku akiwa na furaha ... "Bado sijakuelewa Mume wangu vipi huko mambo mazuri nini? Tuambie basi kama umeajiliwa?" ... Poshie alimwambia Angelo huku akiwa na shauku ya kutaka kujua Mumewe anafurahia nini
"Sikiliza nikuambie Mke wangu, Mungu ni mkubwa na anapaswa kushukuriwa kwa kila jambo, Mimi sina wa kumshukuru zaidi ya yeye lakini pia sina wa kumshukuru katika dunia hii zaidi ya wewe yani bila wewe mimi ningekuwa nimeshajiua siku nyingi lakini kwa moyo wako umekuwa mtu wa kunipa ushauri mpaka leo hii siamini kama sisi tumekuwa matajiri wakubwa" ... Angelo aliongea huku machozi yakiwa yanamtoka ... "Angelo niambie Mume wangu una nini mbona unanitia wasiwasi" ....
Angelo akaenda kuufunga mlango vizuri kisha akachukua kile koroba na kutoa lile begi na kumimina pesa zote kitandani ... Poshie alistuka kuona pesa nyingi kiasi kile na akataka kupatwa na wazimu .... Walifurahi kupita maelezo na mwisho wakajikuta wakikumbatiana kwa nguvu huku wakilia ... Wakati wakiwa wamekumbatiana ghafla mlango wao ukawa unagongwa
Walistuka na kuanza kupakia pesa katika kiroba huku wakiwa wamechanganyikiwa na kuzificha uvunguni mwa kitanda haraka sana na Angelo akalala kitandani akijifanya anaumwa ... 'Karibu mama Poshie alisikia akimkaribisha mtu baada ya kufungua mlango na Bi Dua akaingia
"Najuta kwanini niliamua kuwasaidia nyinyi? Mwanzo nilijua ni watu kumbe ni chui mliojivika ngozi ya kondoo" .. Bi Dua aliingia na kuanza kubwata bila hata ya kumsalimia Angelo ... "Saalamu kwanza Mama mengine yatafuata baadae!" ... Angelo aliinuka kitandani na kumjibu ... "Leo ustaarabu unaujua wewe? Kama ulikuwa unajua kuna ustaarabu duniani kwanini unanikimbia kila siku?" ... "Sawa nimekuelewa ongea shida yako usepe" ... Angelo alimjibu Bi Dua kwa dharau .... "Angelo kwanini unamwambia Mama maneno kama hayo?" ... Poshie alichukia na kumsema mumewe ... "Leo mimi niongee shida yangu kisha nisepe? Sawa nashukuru, ama kweli mfadhili mbuzi unaweza ukanywa mchuzi kuliko binaadamu lazima atakuuzi tu. Sasa nasemaje nataka chumba changu mpaka kufikia kesho muwe mmehama nyumbani kwangu" ... Bi Dua aliongea kwa hasira huku akiwa anatetemeka mwili mzima .... Angelo alicheka sana kwa dharau kisha akamwambia ... "Hii nayo nyumba au kibanda? Hivi wakiitwa wenye nyumba nawe utatoka? Unatunyanyasa sana na kajumba chako kwa sababu unauona sisi masikini sasa kwa taharifa yako nimekutana na ndugu zangu na wamesema watanisaidia" ... "Kumbe mlikuwa na ndugu kwanini mlikuwa mkinieleleza mimi na matatizo yenu? Kesho nataka chumba changu na kama hamjatoka naweza hata kuwashitaki" ... Bi Dua alichukia mpaka akafikia atua ya kulia na kuondoka zake.
japokuwa walikuwa na furaha ya kupata pesa na kuyaaga matatizo, lakini Poshie aliudhunika kutokana na majibu ambayo Angelo amemjibu Bi Dua na kuona amemkosea heshima mtu muhimu sana katika maisha yao ... "Kwanini umemjibu vile Mama wa watu?" ... Poshie alimjibu Angelo kwa unyonge kabisa huku machozi yakiwa yanamtoka ... "Nimemjibu vile kwa sababu yeye Masikini na mimi ni tajiri hivyo tuna tofauti sana ya majibu yetu" .... Huyo ndiyo alikuwa Angelo Mpya na tayari pesa zilikuwa zimeshamchanganya.
******
BAADA YA MIEZI MI 3 KUPITA
Maisha yaliyopita ya Poshie na Angelo yalikuwa kama Cinema .. Walifanikiwa kuhama pale kwa Bi Dua na kupanga nyumba kubwa pembezoni mwa bahari ya Indi huku wakiwa wanaishi eneo ambalo walikuwa wakiishi matajiri wakubwa wa nchi hii .... Angelo alkuwa muoga kwenda kuweka pesa zake Bank kwa kuofia kuhojiwa alipozitoa, hivyo alitenga chumba kimoja cha siri nyumbani kwake na kuziweka pesa zake.
Siku moja baada ya kupata chakula cha usiku Poshie aliamua kuongea na Mumewe kuhusu pesa walizozipata na jinsi ya kuziendeleza ... "Tumefanikiwa kupata pesa nyingi kiasi hiki mume wangu na sasa tumekuwa tukiishi kwa kuzifuja hizi pesa tulizopata mpaka lini? Inabidi tubu..." .... "Ishia hapo hapo Mpuuzi mkubwa wee nimeshakuelewa unachomaanisha, wewe unaonekana unapenda sana pesa na unaweza hata ukaniua ili urithi psa zangu kama ulikuwa haujui hizi pesa ni za kwangu na wewe hazikuhusu. Heti pesa zetu we unajua nilipozitoa pesa hizi" ... "Lakini mume wa...." ... Kimya tena sitaki uniingilie katika pesa zangu huli humu ndani? Huvai? kama gari si hiyo nimekununulia sasa unataka kitu gani zaidi?" .... "Mimi nina haki kama Mkeo, kwanza sijaona sababu iliyokufanya uje kupanga nyumba kwa bei kubwa kiasi hiki, kama si ufujaji wa pesa ni kitu gani? Pesa unayolipa hapa tulikuwa na uwezo wa kujenga nyumba yetu" ... "Kwahiyo unataka kunipangia matumizi pesa yangu? kama ulikuwa hujui sababu iliyonifanya nije kuhishi huku ni kwamba nilikuwa sitaki kuishi karibu na masikini, pia nilikuwa nataka upepo wa bahari kwa sababu mimi ni tajiri" ... Angelo alichukia na wakagombana sana na mkewe mwisho Poshie aliamua kuwa kimya na kumuacha aamue atakalo
*******
Poshie akiwa katika matembezi yake akiendesha gari yake aina ya vitara. Pembezoni mwa barabara akamuona kijana ambaye walikuwa wakisoma wote nzega .... "Mambo vipi Omega" .. alishusha kioo na kumsalimia ... Omega alistuka baada ya kumuona Poshie ... "Poshie alimwita na kumfuata alipo" .... Poshie aliegesha gari na kushuka kisha wakakumbatiana kwa furaha
Wakati Poshie anakumbatiana na Omega kumbe Angelo alikuwa akipita maeneo yale na kumuona.
Waliongea mengi na kukumbushana ya mkoani wakati wanasoma ... "naona maisha umeyapatia Poshie? Wenzetu nyinyi wenye bahati sisi tunaungua na mafuta kila siku na tutakufa tukiwa hivi hivi Masikini hata mkokoteni sidhani kama nitakuja kununua" ... Omega alimwambia Poshie na kumfanya Poshie acheke kisha akamwambia ... "Si kila mwenye maisha mazuri basi ameyapata kwa mkato, wengine tumetaabika sana we acha" ... Baada ya kuongea machache Poshie alitoa Tsh 30,000 na kumpatia kisha akamuaga na kuondoka.
*****
Alirudi nyumbani na kumkuta Mumewe amekaa huku akiwa amechukia ... Poshie alifika na kumbusu shavuni .. "habari yako Mume wangu?" ... "Sijaziandika, nenda kamuulize bwana ako" .... Angelo alimjibu Poshie na kutaka kunyanyuka akiingia ndani. Poshie alimshika mkono na kumvuta kisha akamwambia ... "Unamaanisha nini mbona sijakuelewa?" .... Angelo aligeuka na kibao cha nguvu na kumtandika Poshie ... "Malaya mkubwa wee sasa nyumba itakuwa imekushinda, yani unaliacha toto lako mwenyewe unaenda kufanya umalaya" ... Kisha Angelo alimuita mfanyakazi na kumwambia amlete Henry .... "Beba kinda lako na uondoke nyumbani kwangu sitaki kukuona naweza kukufanya kitu kibaya muda si mrefu, Nenda ukampe mwenye Mtoto wake mana naona mnanijazia wingi tu hapa nyumbani kwangu .....
NINI KITAENDELEA? ...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa