KOVU LA MOYO 28 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

KOVU LA MOYO 28






Dr Ally alistuka na kumgeukia Poshie kwa haibu.
Dr Ally alikuwa ni Mtu mmoja mpole, ambaye alikuwa hawezi kupigizana kelele kama afanyavyo Aisha ... "Lakini Aisha mambo gani unaongea mbele ya mgeni? Kwanini usingemsalimia mgeni kwanza kisha mimi na wewe tukaongea Chumbani?" ... Dr Ally alimwambia Aisha kwa upole na usataarabu wa hali ya juu huku akimtazama Poshie kwa haibu ... "Siliza Ally, Mimi nimeshapata habari zako kwamba wewe unamwanamkee umezaa nae nje huko. Sasa umeamua kunithibitishia, kwa taharifa yako huyu hakai humu ndani"...
Aisha alikuwa ni Mwanamke anayependa ugomvi kupita malezo na mara kadhaa alikuwa akimchokoza Poshie ili amjibu na wapigane lakini alimkuta Poshie Mwanamke mwengine kabisa japokuwa alikuwa akimtukana lakini hakufungua kinywa chake hata mara moja
****
Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri, mwanzo wa story nafikiri tuliona jinsi Papaa Prince alipofanya sherehe ya kuuaga umasikini na kuwaalika mabinti Warembo nyumbani kwake na kufanya nao kufuru.
Papaa Prince hakuwa mwingine bali ndiyo Angelo ndiyo aliamua kujibatiza jina lile ili kujiweka mbali na watu wanaomjua ... Baada ya kuonesha jeuri ya pesa kwa sehemu tofauti ikiwemo kubadili wasichana kama nguo lakini kulikuwa na Mwanamke mmoja ambaye kidogo alidumu nae kama mwezi mmoja huyu si Mwengine bali alikuwa ni Shakira.
Kwa kitendo cha Shakira kumsaidia Poshie na kumlazimisha Prince ampe pesa Poshie kilikuwa kimemchongea sana Shakira.
Pembezoni mwa nyumba ya kina Robby kulikuwa na uwanja mkubwa uliokuwa ukimilikiwa na Mama Roby ... Prince alituma watu wake ili wakaukodi ule uwanja kwa sababu kulikuwa na sherehe anaitaji kuifanya hapo ... Mama Robby hakukataa pesa, bila kujua Prince ni Kijana aliyemnyanyasa siku nyingi na siku hiyo alikuwa akiitaji kumuonesha jeuri ya pesa
Ilikuwa ni sherehe ya kuzaliwa kwa Shakira ... Prince alizialika bendi kazaa za mziki na kuwafanya watu wafurike eneo ilo ... Ulipikwa Mchele kama kilo 600 na vijana wapenda kula bure walijaa eneo hilo.
Mnamo majira ya saa kumi jioni huku watu wakiwa wamejazana eneo hilo ... Msafara wa magari yapatao 15 uliingia huku gari moja kubwa la kubebea magari likiwa limebeba gari moja ya kifahari ... Watu wote walipigwa na butwaa baada ya kumuona huyo Papaa Prince waliyokuwa wakimsikia kumbe ni Angelo ... Mama Robby alichanganyikiwa zaidi na kutamani ardhi ipasuke ili aifiche sura yake.
Prince aliongea machache na kuwashukuru Wananchi wa Eneo ilo kwa kuja kushuudia tukio lake muhimu katika maisha yake .... Aliwasaidia kikundi cha kina Mama wa mtaani pale, kiasi cha Tsh milioni 2 na kuwasihi katika pesa hiyo hasiwemo Mama Robby ... Pia alitoa pesa kwa vijana wa mtaani hapo na kuwaaidi kuwa atawasaidia zaidi.
Ulifika wakati wa tukio ambalo lilikuwa likisubiriwa na wengi ... Prince alimkabidhi gari mpya ya kisasa Shakira, ambayo ilikuwa imeletwa hapo kama zawadi yake kwake .... Shakira alifurahi sana na kumkumbatia Prince kwa furaha huku machozi yakimtoka.
Watu wengi wa Mtaa ule walikuwa wakimjua fika Angelo na walitambua kuwa mpenzi wake alikuwa ni Poshie. Lakini kwa kitendo cha Kumzawadia gari Shakira na kubusiana hadharani kiliwachanganya watu wengi na walikuwa wakitamani kujua Poshie alipo ... Kwa wale waliokuwa wakijua maisha aliyopitia kijana yule hawakusita kudondosha machozi yao
****
Gari ya Shakira ililetwa mpaka nyumbani kwao na wakati anapekua ule mfuko uliokuwa na kadi ya gari akakuta karatasi iliyoandikwa ... "Nimefurahi sana kukushuudia ukitimiza miaka kadhaa huku mimi na wewe tukiwa Wapenzi ila kwa tabia yako ya kuingilia maswala yangu na kunilazimisha nimpe pesa yule mwanamke ambaye simjui ... Nasikitika kukuambia kuwa mapenzi yetu yamekufa na hiyo gari ndiyo mpenzi wako kwa sasa ... Sijapenda tuachane vibaya ndiyo mana nimekufanyia sherehe" ... Ujumbe wa Prince ulikuwa umeishia hapo na kumfanya Shakira achanganyikiwe na hasiamini kwa kile alichokuwa amekisoma ... Alirejea mara kazaa kuisoma ile karatasi na akatoka mbio kuelekea nyumbani kwa Prince
****
Hekima na busara ni kitu muhimu sana katika maisha ya Binadamu. Ila kwa bahati mbaya Vizazi hivi vya sasa havina kabisa vitu hivyo muhimu. Mpaka Wazee Wasasa hawana Hekima na busara ... Dr Ally alikuwa ni binadamu pekee mwenye hivyo vitu kwa kizazi cha sasa. Alijitaidi kumpoza Aisha na kumpeleka chumbani.
Baada ya kumpeleka Aisha chumbani akamfungia kwa nje kisha akamchukua Poshie na kuondoka nae ... Kwa bahati mbaya kwa Dr Ally apakuwa na Mlinzi kwa muda huo, hivyo ilimbidi atoke mwenyewe na afungue geti.
Wakati anaangaika kufungua geti Mdada wa kazi alimfungulia Aisha na akatoka nje akaingia katika gari yake na kuanza kuwafuatilia ... Dr Ally bila ya kujua km anafuatiliwa alifika katika hotel moja kubwa na akamchukulia chumba Poshie kisha yeye akaondoka kumuwahi Aisha.
Baada ya Dr Ally kutoka Hotelini, Aisha alichukua wembe katika gari yake na kuingia mule hotelini na kupania kwenda kumuaribu uso Poshie ...
NINI KITAENDELEA ...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa