KOVU LA MOYO 25 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

KOVU LA MOYO 25






Angelo hakuamini hata kidogo kilichotokea, alivuta pumzi kwa nguvu na kuziachia taratibu na kukaa chini huku akitamani kulia
Angelo alijilaumu mwenyewe kwa uzembe alioufanya kulala pale kazini, alijisikia vibaya sana atakaporudi nyumbani akamwambie Mkewe kuwa amefukuzwa kazi kwa uzembe wake ... Alitamani sana kulia aswa alipokuwa anakumbuka deni la yule Mama na kwa jinsi Mkewe alivyokuwa hana amani kwa jinsi alivyokuwa akidaiwa na Bi dua .... Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi peke kwa yeye kuweza kuikomboa familia yake lakini wapi ndiyo kwanza alifanya uzembe aliwa kazini ... "Ama kweli Ng'ombe wa Masikini hazai" .... Angelo alijisemea mwenyewe huku akiwa bado anaendelea kujilaumu.
Hakuna kitu kibaya maishani kama kuishi kwa fikra kwa sababu ni mara chache sana Mtu akamfikiria mwenzake kitu alafu kikawa cha kweli. Mara nyingi Mtu anapomfikiria mwenzake kuwa yupo hivi anakuta mwenzake yupo vingine.
Baada ya Boss wake kuingia ndani, Angelo alikaa na kufikiri sana na akahisi kuwa Boss wake hawezi kumfukuza kazi kwa kosa la kizembe kiasi kile na kwa vyovyote atakuwa amempima akili yake tu ... Baada ya kupata akili hiyo Angelo alitabasamu na kunyanyuka kisha akakimbilia vifaa vyake na kuanza kupiga kazi kwa nguvu zote ili Boss wake akija amkute anavuja jasho na atajua Angelo siyo mvivu .. {Je fikra zitamsaidia Angelo? Ngoja tuone mbele ya mchezo}
*******
Mzigo unauma karibu ya kufika na usipokuwa makini unaweza ukaubwaga kabla haujafika uendapo" ... Uvumilivu ulimshinda Bi Dua na akaenda kuogongea Poshie, wakasalimiana kisha akamuuliza ... "Mumeo nimemkuta" .... "Angelo ndio amepata kazi leo ameenda kuanza ili tulipe hayo madeni Mama yangu" ... "Lakini nilikuambia kuwa akifika ni lazima umwambie nionane naye, naona wewe na Mumeo wote mnadharau ndiyo mana mnaniona mimi kama mpuuzi fulani. Kama msaada nimeshatoa sana lakini kwa hili wacha nipate dhambi, toa vitu vyenu nje mimi nataka kukifunga chumba changu sina mjadara na wewe" ... Bi Dua aliongea huku akiwa amechukia zaidi ya siku zote wanavyoishi nae kiasi ambacho hata Poshie alimshangaa
Yalikuwa ni maamuzi mazuri sana kwa upande wa Bi Dua lakini yalikuwa ni Maamuzi mabaya kwa ile familia kwa sababu ndiyo hivyo kama unavyoona Poshie alikuwa na mtoto mdogo alafu hawakuwa na pesa ambayo ingewafanya watoke pale na kwenda kupanga chumba kingine sehemu popote
Maisha ya Poshie yalikuwa yametawaliwa na vilio vya kila siku kitu ambacho kilikuwa kikimfanya awe anakonda kila siku. Lakini pia uzazi ulikuwa unachangia na kama hivyo alikuwa hapati zile uduma ambazo mzazi anazipata pindi anapotoka kujifungua ... Poshie alishindwa kujizuia hisia zake na kujikuta akiangua kilio baada ya kujibiwa vile na Bi Dua .... "Mama mimi nitaenda wapi Mama yangu na wewe ndiyo kimbilio langu Mama!! Mama fikiria mara mbili mimi mwanamke mwenzako naenda kufedheeka wapi nitaenda mimi ikiwa hata wewe uliyenishika mkono tayari unataka kunitupa kama Jongoo na mti wake. Yote yananikuta kwa sababu Mimi sina mama na laiti ningekuwa na Mama basi yote yasingenikuta haya labda na mimi ningemfuata Mama yangu na kumlilia shida zangu lakini sijui kwanini Mungu umemchukua Mama yangu mapema huku akiwa hajanifunza ya urimwengu na ukiniacha urimwengu ukinifunza" ...... Poshie aliongea kwa kilio cha uchungu huku akiwa amempigia maoti Bi Dua na kumshika miguu yake.
Maneno ya Poshie yalimchoma sana Bi Dua na alijisikia vibaya sana pindi Poshie alipompigia magoti na kumlilia kama Mungu wake. Aliona kama ndiyo mwanae wa kumzaa ndiye aliyekuwa akiyapata mateso hayo .... Kitendo cha Poshie kuwa analia kilimsababisha Henry alie zaidi mpaka sauti ikawa inapotea. Bi Dua aliona kama yule Malaika wa mwenyezi mungu pia alikuwa akimlilia ili hasiwafukuze katika nyumba yake ... Alimnyanyua Poshie na kumkumbatia na wote watatu wakawa wanalia kwa sauti kiasi ambacho majirani waliwakimbilia wakijua kuna msiba umetokea
********
Katika Maisha ya binadamu kuna watu wanapenda kujitafutia kwa jasho lao lakini kuna watu ambao upenda njia za mkato katika maisha na wengi wao ujikuta wakipoteza maisha kwa kupenda mambo mazuri kwa haraka sana aswa sisi vijana wa kipindi hiki ... Katikati ya jiji la Dar es salaam Majambazi waliivamia bank moja kwa niaba ya kupora pesa na kuanza kurushiana risasi na mapolisi waliokuwa wakiilinda bank hiyo.
Ilikuwa kama Mchezo wa kuigiza uliokuwa ukichezeka pale bank baina ya polisi na majambazi hao wa tatu waliokuwa katika gari fulani yenye rangi nyeusi .... Baada ya majibizano ya hapa na pale Majambazi walifanikiwa kuchota pesa na kupakia katika begi lao na kuanza kukimbia kurudi katika gari yao huku wakiwa bado wanarushiana risasi na mapolisi waliokuwa wameongezeka ... Wakati wanarudi katika gari yao yule Jambazi analiyekuwa na lile begi la pesa alipigwa risasi ya kichwa na kufa pale pale.
Jambazi Mmoja aliyekuwa wakike akaamua kujitoa muanga na kulirudia lile begi huku akiwarushia mapolisi risasi kama njugu na kufanikiwa kuwajeruhi baazi ya mapolisi huku akiwauwa wengine pamoja na Wananchi waliokuwa wakikimbia ovyo ... Yule Dada alifanikiwa kupata Begi na wakati anakimbia alipigwa risasi za tumbo lakini alikimbia na kuingia katika gari lao
alipofika katika gari alimkuta yule mwenzao mwingine aliyekuwa dereva naye amepigwa risasi na kufa. Akamsukuma pembeni na kukaa katika kiti cha dereva na kutulia akijiuliza ajisalimishe au vipi ... Alichukua lile begi na kufungua alipoziona pesa zimejaa alisema ... "Hii ndiyo sehemu pekee ya kuuaga umasikini" ... Kisha akalifunga vyema na kujiandaa kwa shambulizi la mwisho.
Mapolisi walijua wameshamaliza kazi hivyo wakawa wanalisogelea gari huku wakiwa makini. Ghafla yule Dada akatia gia na kuondoka kwa kasi ya ajabu ... Mapolisi waliingia katika gari yao na kuanza kumfukuza.
*****
Angelo hakutaka kukata tamaa aliendelea kufanya kazi kama hana akili nzuri ilimradi Boss wake akija hasimfukuze kazi ... Akiwa anapiga Kazi ghafla aliona gari inasimama mbele yake na kuna Mdada anamwita.
Hakuwa mwingine alikuwa ni yule Jambazi. Angelo akaenda mpaka pale na alistuka kuona ndani ya gari kuna damu nyingi huku kukiwa na mtu aliyekuwa amelala na alijua kuwa atakuwa amekufa ... "Kimbia haraka sana" ... Yule Jambazi alimpa lile begi na kumwambia akimbie haraka kisha yeye akaondoka na gari huku hali yake ikionekana kuwa mbaya huku akimuachia lile begi Angelo.
Angelo aliogopa na akalitupa lile begi nyuma ya kifusi cha udongo aliokuwa akiusambaza
Yule Dada alikuwa amemwaga damu nyingi ivyo alijiona hawezi tena kukimbiza gari na anaweza kutiwa mbaloni muda wowote na istoshe yeye anaweza kufa hivyo aliona bora amtunuku mtu kuliko kuwaachia Polisi zile pesa ambazo zimewauwa wao ... Alipofika mbele alishindwa kuendesha garia na akaipaki pembeni.
Angelo hakutaka kudiri na lile begi na badala yake akawa anaendelea na kazi ... Boss wake alitoka na kuzidi kumfokea ... "Bila shaka wewe kijana utakuwa unavuta bangi si bure? Mimi si nimekwambia sikutaki kazini kwangu sasa unafanya kazi nani atakulipa?" ... Wakati yule Boss akimfokea Angelo ghafla ilikuja gari ya polisi na kusimama kisha wakamwita yule Boss ... Angelo aliogopa na kuzuga anaendelea na kazi .... Walimwita na kumuulizia ile gari lakini yule Boss aliwajibu kuwa hakuwa makini kwa sababu zimepita gari nyingi na wao walikuwa na shughuli zao
Baada ya mapolisi kuondoka yule Boss alitoa Tsh 2000 na kumwambia nenda nyumbani sikutaki hapa beba vitu rudisha ndani na wewe kazi basi ... Angelo hakutaka kumbishia tena aliona siyo bahati yake. akachukua vitu na kuingiza ndani huku lile begi akiwa ameliacha pale
Yule Dada alikuwa amezidiwa sana na alipoona mapolisi wanakuja yeye hakutaka shida akajipiga risasi ya kichwa ili kupoteza ushaidi ... Mapolisi walifika na kuchanganyikiwa baada ya kutokuta lile begi la pesa
Angelo Baada ya kutoka kuoga alivaa na kutoka nje akakague begi lake. Lakini wakati anataka kutoka na ile gari ya polisi ikawa inarudi ikiwa imeongozana na ile gari aliyopita nayo yule Dada. aliogopa na kujibanza sehemu ... Walipopita akaenda na kulifungua lile begi hakuamini macho yake baada ya kuliona limejaa pesa .... Alipatwa na mstuko na hakujua hazifanyaje na akaona bora akamwambie Boss wake akatoka mbio huku akiwa ameziacha na kukimbia akielekea ndani huku akimwita Boss .... Boss ... Boss" ..........
NINI KITAENDELEA?? ...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa