KOVU LA MOYO 21 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

KOVU LA MOYO 21




Poshie alimtazama Angelo kwa hasira huku machozi yakimtoka.
Kiukwelili alijisikia vibaya sana kuambiwa kitu ambacho hajawai kukifanya, lakini aliumia zaidi kuitwa Malaya .... "Haiwezekani hata kidogo yani ... Sijawahi kutembea na mwanaume yeyote katika maisha yangu zaidi ya wewe, lakini yote bure bado unaniona mimi ... Hapana siamini kama Wewe Angelo unaweza kuniambia maneno ya kipuuzi kiasi hicho yani..." ... Poshie alimwambia Angelo huku akilia kwa jazba kiasi ambacho alishindwa kuongea... "Sikiliza nikwambie Poshie, usijifanye kulia na kunizugisha. Bado haujanijibu swali langu, nimeakuachia Tsh 500 ule maandazi cha kushangaza nimekuta ubwabwa, pesa ya kupika chakula hiki umepata wapi kama siyo umalaya?" ..."Tokea nianze mausiano na wewe, leo ndio umenikosea sana! Yani unaniita Mimi Malaya?" ..."Kama hauna majibu yaliyonyoka unataka mimi nikuiteje zaidi ya kukuita Malaya? Hata marafiki zangu wananiambiaga kuwa, kama hauna pesa Mwanamke hawezi kukupenda kwa sababu wanawake wa siku hizi pesa mbele kama mfuko washati na kama hauna pesa, utaishiwa kuchukuliwa tu" ...
Maneno ya Angelo yalimchoma sana Poshie yani kama Mtu kaingiza msumari wa moto katika kidonda. Poshie alichukia sana kiasi ambacho alishindwa kuongea na muda wote alikuwa Angelo akibwata kama mnywa mataputapu .... "Sikuwahi kufikiria kama kuna siku Angelo unaweza kunidhalilisha kiasi hiki? Kwanza hao marafiki zako wote wanafki, rafiki yako Mmoja tu, ambaye ni Robby. Unaposema Wanawake wanapenda Pesa nimekupenda Angelo una nini wewe?" ...
Poshie alijitaidi masikini na kujibishana naye. Majibishano yalizidi kiasi ambacho hakuna aliyekuwa akimsikiliza mwenzake ... Kitendo cha Poshie kujibishana na Angelo kilimuuzi Angelo na akajikuta akimzibua kibao kilichompeleka Poshie mpaka chini .... Masikini Angelo anampiga mkewe wakati akijua fika mwenzake ameshinda na njaa kutwa nzima "Angelo unanipiga? Nakuuliza umeamua kunipiga? .. Niuwe basi Angelo nimekwambia niuwe" ... Poshie alimkamata Angelo huku akimtikisa na Angelo alikuwa akiendelea kumpiga vibao ili amuachie.
Bi Dua aliweza kuwasikia muda mrefu lakini aliwachunia kwa kujua ugomvi wa wapendanao. Lakini walipoanza kupigana aliogopa, tena ukizingatia Poshie alikuwa na mimba kubwa, ivyo aliogopa wasije wakauwana na yeye akapata kesi nyumbani kwake ....
Alitoka ndani kwake na kwenda kuwagongea.
Poshie alitoka na kukimbilia nyuma ya nyumba ambapo kulikuwa na migomba mingi iliyosababisa kiza kinene ... Bi Dua alizidi kuchanganyikiwa na aliona labda Poshie anaweza kujifanyia jambo baya kule alipo. Alimfuata na kumbembeleza ..."Nyamaza Mwanangu, hali yako na machozi ni vitu viwili tofauti, lakini pia nakuomba utoke huku kwa sababu pia kuna wadudu, kwanza mbu wengi, lakini pia kuna nyoka hapa" ...
Japokuwa Poshie alikuwa na jazba huku akiwa analia kwa kilio cha kwikwi alikuwa mwoga mkubwa wa nyoka, ivyo aliposikia mdudu huyo anatajwa aliona mwili mzima unasisimka ... "Bora nibaki hapa kuliko kwenda tena kule kugombana na Angelo Mimi siwezi kwanza sijazoea ugomvi" ... "Basi nyanyuka twende ndani kwangu" ... Hiyo ndiyo kauli ambayo Poshie alikuwa akiiombea ... Alinyanyuka na kwenda ndani kwa Bi Dua.
Walipofika ndani Bi Dua alimbembeleza anyamaze lakini pia alimsihi sana wasipende kugombana haswa ukizingatia Poshie alikuwa ni mjamzito ... Pia Bi Dua alitaka kujua nini kilichosababisha mpaka wasemezane mpaka wanafikia atua ya kupigana. Poshie alikuwa ni Mwanamke aliyefundwa akafundika, hakupenda kumsimulia mambo yake yandani Bi Dua kwa sababu hakumjua fika kiundani Mama huyo ... Poshie alizidi kulia kwa kwikwi kitu kilichofanya Bi Dua amuache na kwenda kumfuata Angelo.
Angelo alipoulizwa na Bi Dua alimueleza kila kitu mpaka akaamua kumpiga ... "Unamuonea bure Mtoto wa Watu Mwanangu ... Kwa muda ambao Mimi nimeishi na nyinyi, mimi nakupongeza kwa kupata mke mwema tena unatakiwa kumshukuru mungu. Sijawahi kumuona na marafiki, yeye kutwa ndani na akitoka yeye yupo na mimi. Sasa umalaya huo anaufanya na majini?" ... Bi Dua alimsema sanaAngelo na kumueleza kila kitu jinsi Poshie alivyomuomba vichwa vya dagaa pamoja na maganda ya nyanya huku yeye kwa huruma yake akamsaidia moto ... Angelo alijisikia vibaya kwa kosa ambalo amelitenda na akamwambia Bi Dua ..."Nimemkosea sana Mke wangu, naitaji kumuomba msamaha" ... Angelo alimwambia Bi Dua kwa haibu huku akiwa ameinamia chini .... "Ukisikia uanaume ndio huo, piga moyo konde twende ukamuombe Mkeo Msamaha" ... Bi Dua alimwambia Angelo kisha wakatoka na kuelekea alipo Poshie."Samahani sana Mke wangu najua nimekukwaza ila naomba unisamehe" .... "Imekuaje tena unakuja kumuomba Malaya Msamaha?" ... Poshie aligeuka na kumjibu Angelo kwa hasira ... "Hapana Mwanangu vibaya ivyo, jaribu kurudisha moyo nyuma. Ukiona mpaka mumeo anakuomba Msamaha ujue naye ameshajua makosa yake, samehe saba mara sabini hata vitabu vina tuambia... Bi Dua alidakia na kumsihi Poshie ili amsamehe Angelo ... "Mama inaniuma sana Angelo kuniita Mimi Malaya, yani kua ... Basi siwezi, bora aniache tu. Kuanzia leo Angelo Mimi na wewe basi"
NINI KITAENDELEA??



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa