KOVU LA MOYO 19 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 19






Poshie na Angelo walikuwa makini kumsikiliza Robby "Nafikiri mnafahamu kama mimi natakiwa kusafiri na kesho ndio siku yangu ya kusafiri" ...
Robby aliongea kwa uchungu sana huku akijisikia vibaya kuwaacha katika hali ile, Poshie halishindwa kujizuia na kujikuta machozi yakimmwagika ... "Sina cha kukulipa Robby zaidi ya kukwambia Asante sana kwa moyo wako wa kujitolea. Mungu akujalie huwe na Moyo huo huo. Ukifika Kampala naamini utakutana na Wanawake wengi Warembo walioumbika, nakuomba ujiweke mbali sana na Mapenzi. Hata Mungu anapenda binadamu tujifunze kupitia Maisha ya Watu tulio nao karibu kwa sababu hiyo ni moja ya njia zake za kutuonya juu ya jambo fulani. Nafikiri unatuona jinsi sisi tunavyopata tabu na hii ni kwasababu tumekurupuka kuanzisha mahusiano kabla ya kupanga maisha" ... Poshie alimuhusia Roby ajiweke mbali na Mapenzi huku Angelo pia akimsisitiza asome kwa nguvu zake zote ili aje kuwakomboa
(NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUKUOMBA NDUGU MSOMAJI HASWA KM WEWE KIJANA NDIO UNAINGIA KATIKA MAPENZI, JIFUNZE SANA YALIYOMKUTA POSHIE NA ANGELO.)
Baada ya kila mmoja kumuhusia mwenzake, huku Robby akiwaomba wasitengane na ikiwezekana waje kuoana, Robby aliwaaga na Angelo akamsindikiza.
****
Baada ya Robby kusafiri, Angelo na Poshie Waliendelea kuishi kwa upendo wa hali ya juu huku wakipanga mipango lukuki juu ya maisha yao ya baadae. Angelo aliendelea kumfuatilia yule jamaa lakini alikuwa akimzungusha kila siku na huakika wa yeye kupata kazi ulikuwa ukiyayuka kama barafu Iliyo anikwa juani.
Baada ya Mwezi mmoja, vyakula viliisha ndani na pesa ilikata. Angelo hakuwa na sehemu ya kupata kazi huku mimba ya Poshie ikiendelea kuwa kubwa. Siku hiyo Angelo aliondoka Asubuhi huku akiwa hana hata kipande cha pesa cha kumuachia mkewe. Poshia alishindia maji kutwa nzima na kuishia kulala ndani kwake. Usiku ulivyofika Angelo alirudi na kumkuta Mkewe amelala, alifika na kumuamsha. Poshie aliamka huku akiwa hana nguvu ... "Habari ya huko utokako Mume wangu" ... "Za huko mbaya tu, nimezunguka karibia jiji zima leo, lakini sijabahatika kupata kazi mke wangu. Sijui hata tutaishi vipi" ... "Ridhiki mafungu saba naamini na letu lipo Mume wangu, wala husikate tamaa siku moja mungu atakujalia" ...Poshie alimwambia Angelo kisha akamsogele na kumfungua vishikizo vya shati na kumvua shati. Baadae akamvua viatu pamoja na soksi kisha akamwambia ... "Pole kwa uchovu wa kutwa nzima, mpenzi wangu. Nyanyuka ukaoge maji yapo tayari"... Angelo alinyanyuka na kwenda kujimwagia maji.
Wakati Angelo anaoga, Poshie alitazama jiko na kugundua lilikuwa na mafuta kidogo ... Akatoka nje na kwenda katika duka ambalo walikuwa nalo karibu na akamwambia yule muuzaji ... "Samahani kaka nikopeshe unga robo Mume wangu akirudi nitakuletea Tsh 300 yako" ... Yule Muuzaji alimuamini na akampimia ... Poshie alirudi mpaka nyumbani na akapika ugali.
Angelo alitoka kuoga na kumkuta Mkewe akipika ugali ... "Umepata wapi pesa ya kununulia unga?" ..."Samahani Mume wangu kwa kutokushirikisha, nimeenda kukopa hapo dukani kwa Mangi mana hali yangu mbaya sana" ... Poshie alimjibu mumewe kwa upendo wa hali ya juu kana kwamba hakuwa na njaa.
Angelo alimuelewa na kumpongeza kwa kuwa na moyo wa ubunifu .. Ugali uliiva lakini hawakuwa na Mboga, Poshie alichukua chumvi na kumimina katika bakuli na kukoroga na maji kidogo kisha akamwambia Angelo ..."Karibu tule Mume, sema mboga hakuna itabidi tule na chumvi" ... "Asante sana Mke, we usijali mbona chumvi mboga nzuri tu" .. Poshie alimnawisha Angelo na akataka kula lakini Poshie akamshika Mkono .... "Bado hatujakiombea chakula kinaweza kuwa sumu kwetu, pia tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutuletea chakula katika nyumba hii, ili na kesho atuletee tena" ... Poshie alimwambia Angelo kisha wakakiombea chakula na wakala .... Kama isingekuwa kujitoa kwa Poshie basi wasingekula siku hiyo.
Baada ya kumaliza kula, walishukuru na kupanda kitandani kulala.
Wakiwa kitandani Angelo alimtazama Poshie na kujikuta akitabasam ... "Unanicheka hee?" .. Poshie alimtazama Mumewe na kumwambia .. "Hapana Mke wangu, bali nafurahi kupata Mwanamke wa shoka yani sijui nikupe zawadi gani?" .. "Hakuna zawadi utakayonipa Angelo nikaridhika zaidi ya upendo wa dhati. Siku zote Mwanamke anapokufanyia Wema we Mlipe upendo daima atakupenda na kukuheshimu mpaka anaingia kaburini ila ukimvunja Moyo utampa kumbu kumbu mbaya na atakufanya kama Mtu wa mfano kwa kila atakapojisikia kuongea nani alimuumiza" .. Waliongea sana na hawakujua usingizi uliwapitia muda gani akika yalikuwa ni maisha ya furaha amani na upendo.
Asubuhi na mapema kulipokucha, Angelo aliamka na kwenda kujimwagia maji ... Baada ya kutoka kuoga Angelo alirudi na kumuamsha Mkewe na kumuaga huku akiwa hana hata senti ya kumuachia mkewe ... "Mimi naenda kutafuta Kazi Baby wangu"... "Safari njema mpenzi wangu, mungu atakujalia" ...Poshie alimjibu huku akiwa bado na usingizi.
Angelo aliondoka nyumbani huku akijisikia vibaya kwa kutomuachia kitu ....
Wakati Angelo akiwa njiani anatembea huku mawazo kibao yakiwa yamemzonga na muda mwingine akiongea mwenyewe ghafla mbele yake aliona Tsh 500. Aliisogelea na kuiokota, kisha akamshukuru mungu.
Japokuwa alikuwa amefika mbali lakini aliamua kurudi nyumbani ili akamuachie Mkewe .... Alifika nyumbani na kumkuta Poshie akiwa ameamka lakini bado amejilaza katika kitanda chao cha mabox ..."Ama kweli Mungu siyo Mzee Mkumba, nimeokota mia tano hii ununue hata maandazi utafune" ... Angelo alimwambia Poshie na kumpa ile pesa kisha akaondoka zake.
Poshie alimka na akajiuliza ile Tsh 500 akanunue maandazi kama Angelo alivyomwambia au akalipe lile deni la jana?
NINI KITAENDELEA? ..



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa