KOVU LA MOYO 20 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 20





Dawa ya deni ni kulipa deni na si kulikimbia deni.
Huo ndio msemo pekee uliokuja katika kichwa cha Poshie baada ya kufikiri sana. Alinyanyuka na kwenda kujimwagia maji kisha akavaa na kuchukuaile Tsh 500 na kuelekea dukani. Alifika na kumpa pesa yake kisha akamwambia .... "Asante sana Kaka yangu, ila samahani sana kwa kukucheweleshea pesa yako, kwasababu Mume wangu alichelewa kurudi" ... "Usijali Dada, mimi pia nashukuru kwa kuwa muaminifu" ... Poshie alichukua chenji yake ambayo ilikuwa ni Tsh 200 nakurudi nyumbani.
Masaa yalizidi kusonga huku njaa ikizidi kumuuma Poshie .... Jiko halikuwa na mafuta na mkononi akiwa na Tsh 200. Kila alipokuwa akiumiza kichwa hesabu zilikuwa haziungi na mwisho kabisa aliamua kulala.
Hakuna kitu kibaya katika Maisha kama njaa, wakati wewe unaposema hujisikii kula, kaa ukijua kuna binadamu wenzako wanakufa kwa sababu ya njaa... Poshie alilala mpaka majira ya saa 10 jioni na kuamua kuamka kwa sababu usingizi ulikuwa haupatikani kabisa.
Baada ya kuamka Poshie alikuwa akifikiria kuwa atakula nini yeye na mumewe siku hiyo ... Alitafakari sana lakini akupata jibu lolote, akajiambia Mwenyewe ... "Mimi ni Mwanamke na ndiyo Mama wa Familia lazima nipambane ili kuleta faraja katika nyumba hii na kama sijapambana basi njaa inaweza ikatawala katika nyumba hii na faraja ikapotea" ... Poshiea aliongea mwenyewe kisha akatoka nje na kutafakari ni vipi wataishi.
Akiwa nje, alikuja Mama Mwenye nyumba akiwa na dagaa na kuzichambua huku wakiwa wanaongea maneno machache na Poshie ... "Mama samahani naomba unipe hivyo vichwa vya dagaa husivitupe".... Poshie alimwambia Bi Dua baada ya kumuona akitaka kuvitupa vile vichwa vya dagaa ambavyo ametoka kuvichambua .... Bi Dua hakutaka kumuuliza maswali mengi Poshie kwa sababu kwa muda mfupi alioishi nao aliwajua fika maisha yao. Poshie alichukua vile vichwa vya dagaa na alimuomba pia Bi Dua maganda ya nyanya alizomenya na akaingia ndani na kuviosha vile vichwa kisha akachukua maganda ya nyanya na kuyakatia pembeni .... "Poshie kuna Moto Mwanangu kama utakuwa na kazi nao" ... Bi Dua alimwita Poshie aje kuchukua moto baada ya yeye kumaliza kupika ... "Nakuja Mama yangu" ... Poshie alimjibu Bi Dua na kumshukuru Mungua kuwa amesikia Maombi yake.
Poshie alitoka nje na kulibeba lile jiko la mkaa na kuliingiza ndani kwake ... Alipoutazama ule moto aliona anaweza kupika mboga pamoja na chakula ...Alichukua chupa ya mafuta ya kula na kuelekea dukani .... "Kaka Mchele Tsh ngapi?" ... "Mchele kilo Tsh 2000" ... "Samahani naomba unikopeshe kama jana mume wangu akirudi nitakuletea" ... "Sawa Dada usijali" .... Poshie alikopa mchele nusu na mafuta ya kula ya Tsh 600, hivyo akawa anadaiwa Tsh 1,600 Alirudi nyumbani haraka na kuanza kuuchagua mchele ... Aliuchagua na kuanza kupika ubwabwa na akaupalilia ... Alichukua sifuria na kuibandika juu kwenye moto ule aliopalilia, na kuchemsha maji ya kuoshea vile vichwa vya dagaa. Baadae akabandikasifuria ya kupikia mboga na ilipopata moto, akamimina mafuta ya kula na yalipochemka akachukua yale maganda ya nyanya na kuyamimina kisha akaweka vile vichwa vya dagaa na kupika mboga.
Baada ya kumaliza kupika Poshie alienda kuoga na kwa kuwa muda ulikuwa umeenda aliona bora amsubiri mumewe ....
Mnamo majira ya saa 2 usiku, huku miguu yake ikiwa imejaa vumbi na akionesha fika kuwa ametembea sana, Angelo alirudi na kumkuta Poshie akiwa amelala. Poshie aliamka na kumpokea mumewe ... "Habari ya huko ulikotoka Mpenzi wangu?" ... Poshie alimsalimia Angelo huku akimvua shati .... "Yani mpaka naona haibu mke wangu kukuambia yaliyotokea huko. Leo nimetukanwa sana katika ofisi moja niliyoingia kwenda kuomba kazi, isitoshe njaa ilinishika mpaka nilikuwa nasikia kizunguzungu yani bado kidogo nianguke" ...."Pole sana Mume wangu mungu atakujalia, kwahiyo haujapata hata kitu?" .... "Sijapata chochote Mke wangu sijui tutaishi vipi" ... Angelo alisononeka sanajuu ya maisha aliyokuwa akiishi lakini Mkewe alikuwa akimpa Moyo na kumwambia kuwa watafanikiwa .... "Vipi Babaangu hajambo humu? Au ameshaanza kucheza soka" ... Angelo alimtania Poshie huku akimshika tumbo na kulisikiliza ...."Toka zako, nani kakudanganya kuwa mimi nazaa Mtoto wa Kiume? Huyo mtoto wa kike lazima aje kunisaidia kazi mwanangu" ... Poshie na Angelo waliendelea kubishana, baadae Poshie akamuwekea maji angelo ili aende akaoge.
Wakati Angelo anaoga Poshie aliamua kuandaa chakula kabisa ili mpenzi wake akija wale wote ... Angelo alimaliza kuoga na akarudi, alipoingia ndani alistuka kukuta mkewe ametenga Ubwabwa ..."Ame kweli hakuna Mwanamke mvumilivu ktk hii Dunia! Yani hata wewe umeshaanza umalaya si ndio? Nimekuachia Tsh 500 ule maandazi, pesa ya ubwabwa umeitoa wapi Kama si umalaya?" ... Angelo aliongea kwa hasira na kuipiga sahani ya chakula teke na ubwabwa ukamwigika kabisa ...."Angelo Mimi Malaya?" Poshie alistuka na kumuuliza kwa uchungu ... "Ndiyo wewe Malaya ....
NINI KITAENDELEA??



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa