KOVU LA MOYO 18 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 18




Angelo akiwa na Chupa mkononi, aligeuka ili kumtazama aliyekuwa akimpigia kelele.
Alikuwa ni Robby ndiye aliyemuita Angelo ili asimpige chupa Mama yake ... Angelo alijisikia uchungu sana kwa mambo waliyokuwa wakifanyiwa na Mama yake Robby, alitupa chupa chini na kulia kwa uchungu .... "Unajihaibisha sana Mama, kwanini unafanya mambo tofauti na heshima yako?" .... Robby alimsema sana Mama yake kwa kitendo ambacho alimfanyia Poshie kiasi ambacho hata Majirani zake hawakukipenda ...
Mama Robby alikuwa akimbwatiza Mwanae na kumwambia anatembea na Mvuta bangi.
****"
Kuwa uyaone" ... Ni Msemo ambao Poshie aliukumbuka sana, kwa sababu Marehemu Bibi yake alikuwa akipenda kumwambia. Na kweli sasa alikuwa akiyaona kila haina ya maisha ambayo binadamu wanaishi. Ilikuwa ni Tsh. 60,000 pekee ndiyo ilikuwa imebaki katika bajeti yao na uwezekano wa kupata chumba ambacho wangeweza kuendesha maisha yao ulikuwa unazidi kutokomea ....
Waliangaika sana bila mafanikio na baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu, Jonas aliamua kujitoa katika mchakato huo na kusingizia kuwa amepata kazi ya kusafiri na gari ya mafuta kuelekea Nchini Burundi .... Walimshukuru sana kwa moyo wake wa kujitolea kwa kipindi chote ambacho alijitolea. Robby alijua fika kuwa Jonas aliamua kujitoa baada ya kuona majukumu yanaweza kumuangukia yeye Baada ya Robby kusafiri. Robby alijitaidi kuwatia moyo na kuwaambia kamwe hatoondoka na kuwaacha katika mazingira magumu.
Mungu hamtupi mja wake, Wahenga Walishanena. Baada ya kuangaika sana atimaye waliweza kupata kijichumba angalau cha kuanzisha Maisha yao.
Chumba kilikuwa maeneo ya bondeni na kilikuwa kidogo sana na kutokana na mazingira ya nyumba mwenye nyumba aliwaambia .... "Kusema kweli wanangu, icho chumba kinavuja wala siwadanganyi na kama mngekuwa na pesa ya kutosha basi ningewajengea" .... "Sawa Mama tumekuelewa ila kama tulivyokuambia hapo Mwanzo sisi tuna Matatizo na tulikuwa tunaomba msaada" ... Robby alimuaomba Bi Dua na akawakubalia Walipe 15,000kwa mwezi na wampe pesa ya miezi mitatu. Walitoa kiasi cha Tsh 45,000 na wakalipia.
*****
Kwa bahati Mbaya Angelo na Poshie hawakuwa na chochote katika Maisha yao, hivyo ilimbidi Robby akauze baadhi ya vitu vyake muhimu, ikiwemo radio yake na kuwanunulia sifuria chache, jiko pamoja na sahani.
Alitaka pia kuwapa kitanda chake pamoja na godoro, lakini Mama yake alikataa na kuzuia visitoke kisa tu Amemnunulia yeye .... Robby aliwapa shuka zake na wakatafuta mabox usiku ule na wakasafisha ndani kisha wakatandika ndani vizuri.... Roby alitoa kiasi kilichobaki ambayo ilikuwa ni Tsh 40,000 na kumpatia Angelo kisha akamwambia... "Kitu muhimu ambacho unachotakiwa kufanya kwa sasa, akikisha unamnunulia Poshie vifaa vya kujifungulia na kiasi kitachobaki nunua vyakula na bakisha kama Tsh 5,000 itakusaidia siku za usoni".... Robby alimwambia Angelo na kumsisitiza kuwa hawe makini sana kwa kila jambo ambalo ataliamua kwa sasa kwa sababu anaweza kuigharimu familia yake ..."Nakushukuru sana Robby na nitaendelea kukushukuru kwa maisha yangu yote kwa msaada wako ambao umejitolea kutusaidia, kiukweli nimejifunza kitu kupitia wewe na sasa najua ni jinsi gani nije kuishi na marafiki zangu ukiwemo wewe"... Poshie alimwambia Roby huku machozi yakiwa yanammwagika ... Robby pia alimshukuru sana Poshie na Angelo kutokana na uvumilivu wao kwa kipindi chote ambapo Mama yake alikuwa akiwanyanyasa.
****
Usiku ulikuwa umeingia na Robby akamchukua Angelo na kwenda naye maeneo ya kwao na kwenda kuonana na jamaa mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi za ujenzi ili amsaidie Angelo apate kazi ili waweze kujikimu kimaisha .... "Ataweza kazi zetu huyu jamaa yako mbona anaonekana Sharo?"... Yule rafiki yake Robby alimvuta pembeni na kumwambia huku akimtazama Angelo asimsikie ... "Yule anaweza kukomaa we mwenyewe mbona utamkubali" ... Robby alimjibu na kummwagia sifa kibao Angelo ... "Basi sawa ngojea nikamfanyie mipango kisha mi nitakujulisha" ..."Mimi kesho nasafiri ila atakuja yeye mwenyewe kukucheki" ... Baada ya kuongea na yule jamaa walimuaga na kuondoka.
****
Mke mwema ni yupi? Wanaume wengi wanajiuliza kabla ya kuingia katika ndoa, hata mimi najiulizaga sana lakini nitapenda mke wangu akiwa na tabia kama za Poshie .... Baada ya kina Angelo kuondoka
Poshie aliingia jikoni na kuandaa chakula cha usiku ili Mpenzi wake na shemeji yake wakija waje wale chakula alichopika.
Angelo na Robby walifika na wakaongea machache kisha Poshie akawatengea chakula ... "Kwanini shemeji umeamua kujitesa?" ... "Inamana Shemeji yangu haupendi kula chakula nilichopika mimi Mkeo?"... Poshie alitaniana na Robby huku akitenga chakula.
Kilikuwa ni chakula kitamu sana ambacho Poshie alikuwa amekipika japokuwa alitumia muda mchache sana ... Baada ya kumaliza kula Roby alimshukuru Poshie kwa chakula kisha akaongea kitu kilichowatia simanzi .... "Najua ni jinsi gani inavyoniuma ila ndiyo hivyo sina jinsi ....
NINI KITAENDELEA?



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa