KOVU LA MOYO 17 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 17




Robby alimtazama Jonas na Macho yao yakagongana na wakapena ishara fulani.
Mama yake Robby alikuwa bado anaendelea kumbwatiza Mwanae kitu ambacho kilizidi kumchefua Robby ... "Yani mimi nilikufungia ukaniona Mweu sindio?" ... Roby na Jonas walizidi kutazamana ghafla wakakurupuka mbio ... "We Robby wewe Robby nakwa...." ... Mama Roby alijaribu kumzuia Mwanae lakini ndiyo hivyo alichomoka kama mshale.
****
Muda mwingine Maisha yako unayoishi yanaweza kukutia simanzi na ukajikuta unalia mwenyewe .... Hakuna kitu kibaya sana hapa Duniani, kama shida. Wewe sikia au muone tu Mwenzako ana Shida ila usiombe shida ikukute.
Angelo na Poshie Walikuwa wakitembea huku wakiwa hawajui waendako. Robby alikuwa Mtu muhimu sana katika maisha yao, na kwa kitendo cha kupotezana naye, walikuwa wamefenya kosa kubwa sana, alikuwa kama kiungo katika maisha yao
"Angelo naomba usimame kwanza" ... Poshie alimwambia Mpenzi wake huku Machozi yakiwa yanamtoka .... "Mbona unanitisha Mpenzi wangu kuna nini tena?" ... Angelo alimwambia huku akiwa na wasiwasi na akimrudia pale alipo ... "Robby...!!" ..."Robby amefanyaje tena?" ... "Nahisi kuna jambo litakuwa limemtokea, maana siyo kawaida yake" ... Kilio kilizidi kumwagika kutoka kwa Poshie na kumpa kazi Angelo ambaye alikuwa akimnyamazisha, mwishowe na yeye akawa analia.... "Hallo nyinyi vipi katika nyumba yangu, Mmefiwa?"... Mzee Mmoja wa makamo alitoka ndani kwake na kuwafokea Poshie na Angelo ... "Hapana Mzee wangu ila tuna matatizo" ... "Wapumbavu wakubwa nyie, haraka sana sitaki niwaone nyumbani kwangu. Nendeni mkawachulie ndugu zenu" ... Angelo alichukia kutokana na kauli za yule Mzee na kutaka kujibishana naye lakini Poshie alimzuia na kumwambia waondoke eneo lile.
Hawakuwa na jinsi zaidi ya kuondoka pale na Poshie alimwambia Angelo Waende nyumbani kwa kina Robby ili Wajue kuna nini kilichomtokea Robby.
****
Robby na Jonas waliangaika kila sehemu kuwatafuta Angelo na mwenzake Poshie lakini wapi hawakufanikiwa kuwaona .... Robby alijisikia vibaya zaidi kutowaona kwasababu alijua kuwa yeye si mkaaji na endapo ataondoka bila kuwasaidia aliona kama amemtendea dhambi Poshie .... "Unaonaje twende tukawatazame kwenu?" ... Jonas alimwambia Roby huku akimtazama kwa makini ...."Angelo hawezi kurudi nyumbani hata kwanini labda sehemu nyingine lakini siyo nyumbani kwetu" .... Japokuwa Robby alimkatalia, lakini Jonas aliendelea kushikilia msimamo wake na wakakubaliana waende wakajaribu kuwabahatisha.
****
Baada ya kutembea sana, Angelo na Poshie walifanikiwa kufika mtaani kwa kina Robby ...."Nafikiri wewe unisubiri hapa, kwa sababu unamjua Mama yake Robby tabia zake" ... "Sawa we nenda Mimi nakusubiri hapa" ... Angelo aliongea na Poshie na wakakubaliana na Angelo akaenda kumtazama Robby.
Wakati Poshie akiwa pale kwenye uchochoro anamsubiri Angelo, ghafla akasikia anapigwa kibao cha aja kilichompeleka mpaka chini ... "Malaya mkubwa wee! Hivi kwanini unapenda kumfuatilia mwanangu?" ... Alikuwa ni Mama yake Robby ambaye baada ya kumpiga Poshie alifunga kanga yake vizuri kisha akamkamata Poshie na kumnyanyua juu ... "Majirani njooni mmuone kahaba mzoefu anamnyatia Mwanangu ili ampakazie Mimba" ... Mama Robby alimkunja Poshie huku akipiga kelele na kwenda naye nyumbani kwake .... "Mama nisamehe mimi nilikuwa namsubiri Angelo" .... Poshie alilia huku akiomba msamaha lakini wapi, Mama Roby aliendelea kumuitia watu na Watoto walijaa na kumzomea.
Angelo alifika kwa kina Robby na kuelezewa jinsi Robby alivyovunja mlango kisha akatoka na kuondoka na Mwenzake. ... Haraka sana Angelo aling'amua kitu na akageuza haraka na kuondoka. Wakati anataka kukunja kona ghafla akakutana na kundi la watu huku Mama Roby akiwa amemkunja Poshie na akikaribia kumvua nguo .... "Heee kumbe kuwadi wake upo huku? Hivi wewe umekosa sehemu nyingine ya kwenda kumuuza huyu changudoa wako mpaka kwa mwanangu" .... Mama yake Robby alimwambia Angelo huku akiwa amesimama mbele yake na akiwa bado amemkunja Poshie.
Angelo alipandwa na hasira na alitamani kumrukia Mama Roby, ikiwezekana hata amnyonge ...."Mama nakuomba fanya chochote lakini sitaki umchezee huyo binti, tafadhali nakuomba umuachie huyo binti" .... Angelo alimwambia Mama Robby huku akiwa amechukia.
Roby akiwa njiani akielekea nyumbani kwao akiwa na Jonas kuna Mdada alimkimbilia na kumwambia.. "Robby fanya uwahi nyumbani kwenu Mchumba wako naibishwa na Mama yako" ... Robby alistuka na kumuuliza ... "Mchumba wangu gani? Mimi mbona sina Mchumba?" ... "Robby wewe si una Mchumba yule Mjamzito?" ... Roby na Jonas walistuka na kutizamana kisha wote wakasema ... "Poshie huyo"... Kisha wote wakatimua mbio, kukimbilia kwa kina Robby
"Sikiliza nikwambie wewe Kuwadi, kuanzia leo nenda kamtafute Mwanaume wa kumuuzia malaya wako na siyo Mwanangu" .... Maneno ya Mama Roby yalizidi kumuuzi, Angelo na akatazama huku na kule na akaona chupa, akakimbia na kuikota ili akambutue Mama Robby .... Angelooooo!! ...
NINI KITAENDELEA?



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa