KOVU LA MOYO 16 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 16






Angelo alimbeba Poshie na kumuweka kitandani huku wakiendelea kubusiana na kila mtu kuutawala mwili wa mwenzake.
Poshie aliishika nguo ya Angelo na kumvuta kwake kisha akampokea na busu mwanana!!
Poshie alikuwa yupo hoi taabani akiwa hajiwezi kimahaba .... Alizidi kumvuta Angelo ili ampe haki yake ..... "Tusifanye mapenzi Mpenzi wangu kwa sababu hali yako bado siyo nzuri" ... Poshie hakutaka hata kidogo kuisikiliza kauli ya Angelo, na muda wote akili yake ilikuwa inawaza mapenzi ..."Angelo tafadhali unaweza ukaniua jamani, naomba unipe haki yangu mpenzi wangu hee!!" ... Poshie aliongea kwa sauti ya mahaba huku macho yake makubwa yakirembua na kummaliza kabisaa Angelo. .... "Lakini Poshie.... " ... Angelo alishikwa na kigugumizi na hakuwa na chakuongea zaidi ya kuchojoa nguo yake moja baada ya nyingine ili ampe haki yake mpenzi wake.
Hakuna kitu kizuri katika mapenzi kama kufanya mapenzi na Mwanamke mjamzito, yani hata ukiwa goigoi vipi, unaweza ukajikuta unarudia mara nyingi zaidi kuliko kawaida yako .... Angelo na Poshie walikuwa hawajawahi kukutana kimwili tokea Poshie ashike ujauzito na siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yao ya kwanza kufanya na kuushudia utamu wa ujauzito ....
Siku zote mapenzi uleta faraja katika chuki lakini yanaleta amani katika dhiki ndiyo mana starehe ya masikini ni Mapenzi. Masikini hana zaidi ya hilo ndiyo mana Masikini wanajua kuudumisha upendo....
Kitendo cha kukutana kimwili siku hiyo, kiliwafanya Poshie na Angelo wasahau kwa muda matatizo yao na kujikuta watu wenye amani kama hawakuwa na matatizo yeyote ambayo yalikuwa yakiwazonga.
Waliongea mambo yao mengi na kupangilia mipangilio ya maisha yao ya baadae utafikiri wapo nyumbani kwao .... "Ukifanikiwa kujifungua salama Mpenzi wangu, nimepanga kufunga ndoa na wewe kama shukrani yangu kwako" ... Angelo alimwambia Poshie na kumfanya Poshie astuke na kumshangaa, kisha akamrukia kana kwamba hakuwa na ujauzito tumboni mwake. Poshie alimkumbatia Angelo na kujikuta akilia kisha akamuuliza ... "Angelo ni kweli hayo uyasemayo au unanitania?" ... "Ni kweli kabisa mke wangu, ila wasiwasi wangu kwako unaweza ukanisaliti tu" ...."Mimi siwezi kufanya hivyo Angelo kwa sababu hakuna Mwanaume katika Dunia hii ambaye nimetokea kumpenda kama wewe Angelo. Nafikiri unatambua kuwa wewe ndie umeutoa Usichana wangu, na moyo wangu umeufungua wewe na wewe ndie mmiriki halali wa Moyo wangu" .... Poshie alimjibu mpenzi wake na kumshukuru kwa uamuzi wake wa kuamua kufunga ndoa na yeye.
******
Wakati Angelo na Poshie wakiufurahia usiku huo na kujikuta wakifanya mapenzi na kujaribu kujisaurisha matatizo yao, kwa upande wa Robby, mambo yalikuwa tofauti kwa upande wake. Usingizi ulikuwa hauji kabisa na muda wote alikuwa akiwaza na kuwazua jinsi ya kuwasaidia hao jamaa zake. Kitu kilichokuwa kikimuumiza zaidi ni kwamba alikuwa amebakisha siku moja ya yeye kubaki Tanzania na siku inayofuata alikuwa anatakiwa aelekee Uganda.... Aliumiza kichwa sana na akupata jawabu haraka kila wazo alilokuwa akiliandika kama mpango wa kuwasaidia hapo baadae aliona halifai na kuishia kulichana.
Robby alikuja kupata usingizi mnamo majira ya saa 9 usiku bila ya kupata wazo lolote. Alichelewa kuamka kesho yake kwa sababu hakulala mapema jana usiku.
Alikurupuka na macho akayatupa ukutani na kuona ilikuwa imeshatimia saa 4 asubuhi, Haraka alinyanyuka na kuchukua mswaki kisha akaweka dawa ya meno na kutaka kutoka nje ili akaoge na kupiga mswaki .... Akiwa anafungua mlango, alishangaa kuuona haufunguki na alipouchunguza aligundua kuwa ulikua umefungwa kwa nje ...
Robby hakuwa na lengine zaidi ya kupiga kelele akiomba msaada .... "Mama yako amesema tusikufungulie labda nikuitie Mwenyewe uongee nae" ... Mdada Mmoja ambaye alikuwa ni Mpangaji wao, alimwambia baada ya kuchoshwa na kelele zake ..... "Fanya hivyo Da Sharifa, naomba uniitie wangu" ... Robby alimwambia yule Dada na akanyanyuka na kwenda kumuitia."Unasemaje wewe mpuuzi" ... Mama Robby alifika nakuongea nae dirishani ... "Sasa Mama kosa langu nini mpaka unaamua kunifungia ndani kwangu?" ... Robby alimuuliza Mama yake aliyekuwa nje na yeye alikuwa ndani .... "Nimekufungia huko kwa sababu wewe ni mpuuzi. Yani mimi napoteza pesa zangu ili mwanangu usome, wewe Kazi yako kuangaika na yule malaya? Sasa basi nimekufungia na hautoki na hizi funguo hauzipati wala nini na Tayari nimeshaongea na Mjomba wako na anakuja kesho mnaondoka wote" ...
Mama yake Robby alimwambia Mwanae na kuzichukua funguo kisha akaziweka katika Matiti. Robby alilia sana kama mtoto mdogo na aliona kama Poshie na Angelo wataona amewafanyia makusudi lakini ndiyo hivyo Mama yake alikuwa na roho mbaya. Simu yake alikuwa ameuza na hasingeweza kupata mawasiliano kwa sababu hata Simu ya Poshie nayo walikuwa wameiuza na Angelo hakuwa na simu siku nyingi tu
******
Jonas alimsubiri sana Robby na kuona kimya, alijua labda Mama yake anaweza kuwa amempa majukumu fulani au atakuwa ameshaondoka kwenda Uganda .... Baada ya kuona kimya sana Jonas aliamua kumfuata Robby nyumbani kwao ili akaakikishe kuna nini kimetokea? ... Wakati anapita mlangoni kwa Robby akasikia kama mtu anamuita na akarudi nyuma kwenda kuchungulia ... Kumbe alikuwa ni Robby ndie aliyekuwa akimuita. Robby akamuadisia Jonas yaliyomkuta na kumwambia afanye akili ya kuzaliwa ili yeye atoke mule ndani,mana wale wanaweza kuganda kule guest.
Jonas aliamua kutafuta misumari ili kuona kama anaweza kuitegua ile kufuri iliyofungwa pale
******
Kama ilivyo ada ya nyumba za wageni, inapofika muda fulani kama hauendelei na chumba unatakiwa kukikabidhisha kwa wahusika kisha wewe unatimka zako, na kama ulikuwa unaendelea kukaa hapo, basi ulitakiwa ulipe mapema haraka iwezekanavyo ....
Baada ya kukaa sana Pale katika nyumba ya Wageni bila ya kumuona Robby wala Jonas wakitokeza eneo lile, Huku wahudumu wakiwasumbua kuwagongea kila mara, Angelo na Mpenzi wake waliamua kurudisha chumba na kuondoka zao .... "Sasa tunaenda wapi Mpenzi wangu" ... Poshie alimuuliza Angelo huku akiwa amesimama .... "We nifuate tu tutajua tunaenda wapi. kuliko kukaa kumsubiri mtu ambaye hatujui hatakuja saa ngapi" ... Angelo alimjibu Poshie na kumrudia kisha akamshika mkono na kuishia zao
Jonas alifanikiwa kuiangaikia ile kufuri mpka akaifungua kupitia chuma fulani haraka walitoka na kukimbilia kule kwenye Nyumba ya kulala Wageni.
Wakati wao wanavuka na kutazama kwengine na Angelo na Poshie nao walikuwa wakivuka na kuishia zao .... "Dada wale watu wangu wa Jana niliokuwa nimewaleta jana usiku wapo wapi? ..."Angelo alimuuliza Mdada mmoja ambaye alionekana ni muhudumu wa hapo ... "Walikuwepo sana hapa ila wameondoka muda si mrefu" ... Yule Dada aliongea na kumchosha Robby.
Alitazamana na Jonas na kumpa ishara waondoke lakini ile wanafungua mlango wa nje anageuza wakakutana uso kwa uso na Mama yake Robby .... "Nimewaona muda mrefu sana, Mjomba wako amefika nenda kajiaendae kesho Safari .... Mama yake Robby alimwambia Mwanae na kumfanya nguvu zimuishie kabisaa .... "Sijui nitawasaidiaje Angelo na Poshie? Bila ya mimi wanaweza hata kunywa sumu" .... Robby alijiuliza kuchwani na kukosa majibu na kuamua kujibwaga chini
NINI KITAENDELEA? ....



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa