KOVU LA MOYO 15 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 15







Angelo alimtazama Robby na kushusha pumzi kisha akachoka kabisa.
Robyy alimtazama na kumfuata pale alipo kisha akamwambia ... "Mbona umechoka sana Kaka?" ..."Lazima nichoke Robby, yani tunapiga atua 5 kisha tunarudi nyuma atua 10. Sasa pesa yote tunalipa Hospital, nini atma yetu? Au ndio tutaendelea kulala katika viwanja vya mpira?" .... Angelo alimwambia Robby huku tayari macho yakiwa yameshaiva na machozi yalikuwa yakimtoka ....
Robby alikuwa ni kijana ambaye mara nyingi alikuwa hapendi kukurupuka pindi anapotaka kutoa maamuzi ... Alinyanyuka na kutafakari kisha akapiga atua kadhaa na kugeuka na kumtazama tena Angelo na kumwambia ... "Poshie amekaa siku 2, tayali inatakiwa zaidi ya Tsh 50,0000. Kama tukimuweka zaidi hapa, inamana tutatumia pesa zaidi na tutakuwa tumerudi nyuma zaidi. Lete hiyo pesa" .... Angelo alitoa pesa na kumpatia Robby.
Robby alichukua pesa na kwenda kulipia, kisha akachukua dawa kabisa na akarudi walipo. Walimchukua Poshie na kutoka pale Hospital.
Alipofika nje walichukua Tax na Wakaondoka kuelekea mitaa ya kwao .... "Tuache hapo mbele Dereva" ... Robby alimwambia Dereva ambaye naye aliegesha gari yake vyema na wakashuka.
Robby alitoa noti ya Tsh 10,000 na kumpatia yule Dereva tax. Japokuwa alilalamika sana, kuwa walipokuja ni mbali, lakini Robby alimuomba sana na akamuelewa na akaondoka zake."Bado sijaelewa hapa tumekuja kufuata nini?" ... Angelo alimuuliza Robby huku akimtazama .... "Muda mwengine Maswali yako hayana nafasi Angelo, ngoja tu utajua tumekuja kufanya nini?" ....
Baada yakumwambia maneno hayo Angelo, Robby alivuka barabara na kuingia katika nyumba moja ... Alikaa kama dakika 5 kisha akarudi kuwachukua na akaenda nao kule. Kumbe ilikuwa ni nyumba ya kulala Wageni ... "Shemeji karibu sana, kwa siku ya leo mtapumzika hapa na Mumeo, kwa ufupi zile simu tumefanikiwa kuziuza, ila kwa bahati mbaya kile chumba alichosema Jonas tumekuta kimepangishwa" ... Robby alimwambia Poshie kisha akaendelea ... "Jamani katika kile kiasi chetu, mpaka sasa nimetumia Tsh 90,000 na tumebakiwa na Tsh 90,000" ... Roby alitoa kiasi cha pesa kilichobaki na kumpatia Angelo na kumwambia ... "Utachukua pesa kiasi na mtanunua chakula. Ngoja leo kila mtu akapumzishe akili kisha kesho tutakutana ili kujua tunajikwamua vipi" ....
Poshie aliwashukuru sana Angelo na Mwenzake Jonas kwa moyo wao wa kujitolea.
Baada ya kuongea maneno kadhaa, Roby na Jonas waliaga na kuondoka .... Angelo aliamua kuwasindikiza mpaka nje na Roby aliitumia nafasi hiyo kumfunda Rafiki yake ... "Angelo wewe ni Mwanaume, na sifa kubwa ya Mwanaume ni kutokata tamaa! Epuka kuongea kauli za kumkatisha tamaa Poshie tumia nafasi hii kumuonesha mapenzi yako kwake, jitaidi kumsifu kwa uvumilivu wake lakini jitaidi kumpigisha story tofauti na Matatizo yenu" .... Jonas pia alimwambia... "Mapenzi ni ugonjwa mbaya sana kuliko ugonjwa wowote unaoujua wewe, mdogo huwa Mkubwa, Mfupi urefuka na mgonjwa anaweza kupona kama ugonjwa wake unaruhusu. Hivyo nakusihi sana Kaka tazama usije kufanya mapenzi na Poshie na ukifanya basi uwe makini sana kwa sababu yule Mgonjwa mara mbili" .... Maneno ya Roby na Jonas yalimuingia ipasavyo Angelo. Waliagana na kuachana nae.
****
Ulikuwa ni usiku mzuri kwa Poshie kuwa na Angelo siku hiyo ... Wakiwa kitandani huku Poshie akiwa amemlalia Angelo miguuni huku Angelo akichezea tumbo la Mkewe na Poshie akiwa anajisikia raha, Angelo alimwambia .... "Kuna kitu naitaji kukwambia lakini naona haibu mke wangu" .... "Kitu gani icho we niambie usijali" .... "Fumba macho nikwambie" ... Haraka Poshie alifumba macho na kuwa na shauku ya kutaka kujua .... "Nina hamu kweli ya kukiona Kimwanya chako pindi unapochekaga, cheka basi nikuoene" .... Angelo alimtania Poshie na kumfanya atabasam kidogo kwa mara ya kwanza tokea wapatwe na matatizo ....Waliendelea kutaniana lakini ghafla Poshie alianza kulia na akanyanyuka kutoka kitandani ... Angelo alimfuata na kumuuliza ... Poshie aligeuka na wakakutana uso kwa uso na Angelo .... Akauchukua mkono wa Angelo na kuugeuza ktk kiganja kisha akakiangalia kiganja cha Angelo na Mchozi wake ukaangukia pale kwenye kiganja cha Angelo ...."Ndoto zangu zilikuwa ni kuutoa usichana wangu katika ndoa yangu. Angelo umebahatika kutibua malengo yangu ambayo nimeyapanga na umenitoa bikra kabla. Je machungu ya bikra yangu nimeyapata kwa Mwanaume sahihi? Ni kweli utaendelea kuyakinga machozi yangu na kuyamwaga au utayakinga na kuyamimina?" .... Poshie aliongea kwa Uchungu kiasi kwamba machozi yalizidi kuanguka pale kwenye Kiganja cha Angelo ....
"Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunipa zaidi ya mke Mwema ktk maisha yangu na kunifanya niwe Mwanaume Mwenye bahati. Thamani ya Machozi yako ni zaidi ya Damu yangu sina cha kukupa zaidi ya kukupenda daima" .... Maneno ya Angelo yalimkosha Poshie na kumpachika mikono yake kwenye Shingo na kumfuata mdomoni, na kuanza kupeana mabusu mfululizo. Wakarudi nyuma mpaka kitandani .....
NINI KITAENDELEA?? ...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa