KOVU LA MOYO 13 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 13





Kila aliyekuwa amesikia kelele ya Mwizi alitoka alipokuwepo kwa wakati huo huku akichukua silaha yoyote iliyokaribu naye na kukimbilia kwenye kelele za wizi, bila ya kujua mwizi huyo ameiba kitu gani?
Angelo aliona akifanya mchezo anaweza kufa na akamuacha Poshie akiteseka peke yake, yani kama kufa bora wafe wote.
Aliushika vyema mfuko wa maandazi na kutimua nao mbio kama kuna medari anashindania ... Watu walizidi kuongezeka wakimfukuza na aliona sasa anaweza kufa, alifika sehemu na kukuta kuna ukuta ambao juu ulikuwa na chupa lakini hakujali, aliushika na kuruka upende wa pili. Japokuwa aliumia sana kwenye ule ukuta kiasi ambacho aliacha ngozi lakini hakuacha ule mfuko.
Hakuna aliyeweza kuruka pale na wengi ilibidi warudi na kupitia njia nyigine na hapo Angelo alifanikiwa kuwaacha na kutafuta sehemu kisha akajificha kwanza ..... Akiwa yupo sehemu amejificha, aliwasikia watu wakiwa wanapita na kumtafuta yeye
Angelo aliogopa sana na aliona sasa lazima afe. Angelo alikumbuka sana msemo usemao hata kibaka naye umuomba mungu ili afanikiwe jambo lake, Haraka sana aliamua kuomba Mungu ili amnusuru na hatari ya kuuwawa hapo alipo, kwa sababu alikuwa akitaka kuokoa maisha ya yule mjamzito na mtoto wake aliye tumboni.
"Vipi Mbona unakuja hivyo Angelo? Unajua umenistua sana mpenzi wangu" ... Poshie alimwambia angelo baada ya kuja kwa kasi na kujitupa alipo yeye .... "We niache tu mke wangu, kwanza Mshukuru Mungu kwa kuniona nimelejea tena nikiwa mzima?" .... "Kwani kuna nini Mbona unanitisha?" ... "Nimetoka kuiba maandazi na raia walikuwa wananikimbiza wakitaka kuniua" .... Poshie alistuka na kujikuta palepale machozi yakimtoka .... "Husije ukarudia tena Angelo, wizi siyo jambo zuri mpenzi wangu. Unaweza kufa kwa sababu ya wizi" ... Poshie limwambia Angelo huku akiwa na wasiwasi akihofia wasije wakakutwa pale walipokuwepo.
Alimtazama mikononi na kugundua anavuja damu. Haraka aliamua kuchana kanga yake na kumfunga mule alipokuwa ameumia na damu zikimwagika.
Angelo alimtizama usoni wakati Poshie akiangaika kumfuta damu na kumwambia .... "Tutaishi maisha haya mpaka lini Mpenzi wangu?" ... "Mungu ndie anayeijua kesho hakuana ajuae zaidi ya yeye pekee leo tumelala hapa lakini yeye ndiyo anayejua wapi tutakuwa kesho" .... "Siku zote umekuwa ukinipa maneno ya kunipa moyo mpenzi wangu, lakini mimi naona tuna mzigo mkubwa sana mbele yetu na unayeteseka zaidi ni wewe mke wangu. Sasa ikitokea leo umejifungua ghafla, huyo mtoto utakaye mzaa ataishi wapi?" ... "Mungu anaweza yote na ukimkabizi kila jambo anaweza kukutatulia, siku zote maisha ni kuyatafuta na ukipanga kuyatafuta naamini utayapata tu mpenzi wangu. Tujipe moyo siku moja tunaweza tukafanikiwa na Maisha haya tunayoishi yakaja kuwa kama simulizi" .... "Nakupenda sana Poshie kwa sababu unanifanya kuwa mimi kila siku, naamini angekuwa mwanamke mwengine hasingeweza kuishi maisha ambayo mimi na wewe tunaishi leo hii. Leo tupo hapa kiwanjani na tunaumwa na mbu pamoja ukichanganya na matatizo ambayo tumekumbana nayo mimi na wewe na bado umenivumilia, mimi nakula kiapo siku ambayo nitakuja kukusaliti wewe basi Mungu anifanyie jamo lolote baya" .... "Husiseme hivyo Angelo wewe ni Binadamu kaa ukijua haujakamilika, hujui nini kitakuja mbele yetu" ... "Lazima niseme hivyo Poshie unafikiri nitastahili nini kama siyo adhabu, endapo nitakutenda kutokana na matatizo ambayo tunayapitia?" .. Poshie alicheka na kumwambia ... Haya bwana kama umeamua mwenyewe, njoo tule ili tulale muda umeenda huu" ... "Hapana hayo ni yako mpenzi wangu, mimi nitalala na njaa" ... "Hapana bwana mimi siwezi kula peke yangu" .. Poshie alimlazimisha Angelo na wakala yale maandazi kisha wakalala.
Kwakuwa ilikuwa ni kiwanjani Poshie alikuwa akipigwa na baridi sana na ilimbidi Angelo ampakate mpenzi wake ili kumsaidia kumpa jotojoto
******
Robby hakuweza kupata usingizi usiku huo hata kidogo, na muda wote alikuwa akiwafikilia Poshie na Angelo watakuwa katika mazingira gani kwa wakati huo. Aliyekuwa akimuonea huruma zaidi alikuwa ni Poshie kwa sababu alikuwa ni Mwanamke, lakini pia kutokana na hali yake aliyokuwa nayo. Alimuona kama Dada yake Maria ndiyo anapata matatizo yale ... Alijaribu kuipiga simu ya Poshie ilikuwa haipatikani, alitaka kumpigia Angelo akakumbuka kuwa hakuwa na simu na alikuwa ameiuza siku nyingi.
Robby alikuwa katika michakato ya kwenda kusoma chuo Uganda na aliona kama yeye hajawasaidia kwa chochote anaweza kuwaweka katika matatizo zaidi ... Ilipofika saa 11 alfajiri, aliamka na kuanza kuwatafuta. Aliamini lazima watakuwa wamelala katika majumba mabovu tu na si kwenginepo.
Aliangaika sehemu tofauti kuwatafuta lakini wapi hakuweza kuwaona, lakini wakati anarudi akiwa anapita maeneo ya kiwanjani aliwaona na kuwakimbilia pale walipo, alifika na kuwaamsha.
Walistuka na kutaka kukimbia lakini walitulia baada ya kumuona Robby.
Robby alistuka kumuona Angelo akiwa na vitambaa mkononi, na akamuuliza kuna nini kimemsibu .. Poshie alimfuata na kumkumbatia Robby na kumuadisia kila kitu ambacho kimetokea jana yake. Wakati Poshie anamuadisia Robby jinsi Angelo alivyonusurika kufa, alishindwa kujizuia na kujikuta akiangusha kilio na kumfanya Robby azidi kujisikia vibaya na atimaye machozi yakawa yanamtoka na yeye.
Angelo alijitaidi kuwanyamazisha na wakafanikiwa kunyamaza ... Robby aliwachukua na kuwapeleka kwenye mgahawa ulio karibu na kwenda kuwanunulia chai.
Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa, Robby aliwachukua na wakatafuta sehemu na wakapumzika kisha akawaambia kitu ambacho kilimuuma sana Poshie pamoja na Angelo ... "Poleni sana nduu zangu kutokana na matatizo ambayo yamewakuta na mimi nakusihii sana Angelo usije ukarudia tena swala la kuiba kama utakuwa na shida ni bora uombe kuliko kuiba, lakini pia nakuomba umpende sana Poshie na usije ukamuacha hata siku moja, kwa sababu hautokuja kumpata mwanamke mwengine katika maisha yako ambaye atakaribia kuwa na sifa za Poshie. Mimi na wewe Angelo ni Marafiki wa muda mrefu kiasi ambacho sasa umekuwa kama ndugu yangu, ningependa muda wote kuwa karibu na nyinyi ili niweze kutoa msada wangu wa hali na mali, lakini kwa sasa nasikitika kuwaambia mimi nimepata chuo nchini Uganda na nina siku mbili tu kuanzia sasa natakiwa kusafiri" ...
Maneno ya Roby yaliwaumiza sana Poshie pamoja na Angelo kwa sababu mtu pekee ambaye alikuwa akiwasaidia kwa uwezo wake wote ndio huyo alikuwa akitakiwa kusafiri kwenda kusoma je wataishi vipi? ... "Mimi nakutakia safari njema shemeji najua fika unaenda kutafuta maendeleo yako ya leo na kesho utakapokuja kuwa na familia yako. Usiha wangu kwako ni kwamba utakapofika uko jitaidi ukae mbali na mapenzi, mpaka utakapokuja kuwa na maisha yako, nafikiri unatuona sisi tabu ambazo tunazipata kwa sasa" ... "Nashukuru sana Poshie kwa maneno yako mazuri yenye kujenga. Na mimi siwezi kuwaacha mkiwa mnalala pale kiwanjani kwa sababu siyo sehemu salama kwenu aswa wewe mjamzito.
Angelo aliwachukua na kuwapeleka kwa Rafiki yake ili kwenda kujaribu kuwaombea japokuwa wawe wanalala kwake ....
"Mambo vipi Jonas" ... Robby alimsalimia kisha Poshie na Angelo pia wakafanya hivyo ... "Jonas huyu si unamfahamu?" .... Robby alimuuliza huku akimuoneshea Angelo ... "namjua ndiyo si Angelo huyo" ... "Vizuri kama unamjua. Huyu Mshikaji bwana alikuwa na matatizo yeye pamoja na mpenzi wake, kwa ufupi ni kwamba Mpenzi wake amefukuzwa kwao na amesusiwa yeye. Mimi niliwasaidia ila Bi Mkubwa amegoma na amewatimua, sasa mshikaji hana pa kulala na mimi naondoka naelekea Uganda naenda kusoma, sasa nilikuwa naomba wajishikize katiika geto lako mpaka Mshikaji atakapo pata kazi basi atachukua chumba chake" ... Robby alimwambia Jonas kwa umakini sana lakini cha ajabu alipomaliza kuongea Jonas alicheka sana na kumwambia ... "Hapa mtaani watu wanakusifu sana Robby kuwa una akili lakini kwa ili umechemka mchizi wangu. Unapata tabu kwa matatizo ya kujitakia? Yeye kajitakia majukumu mwenyewe basi muache aangaike mwenyewe, yani chumba kimoja niende kulala na hawa mataira je demu wangu akija mimi nitalala nae wapi?" ..... "Usiseme hivyo Jonas matatizo yapo kwa kila mtu leo kwako kesho kwa mwenzako" ... "huyu akili hana Angelo wenzake wote tunajipanga kutafuta maisha yeye kaona kumtia mimba mtoto wa watu ndiyo dili., muache ateseke mbona apo bado sana. Kama matatizo yatakuzidi sana, kuna Mzee mmoja yupo Mombasa anawapenda sana vijana kama nyinyi nitakupeleka lazima atakusaidia ila lazima atakuoa ....
Kauli ya Jonas ilimchefua sana Angelo na hakupenda kudhalilishwa mbele ya mpenzi wake, alimfuata Jonas na kumvamia ...
NINI KITAENDELEA ....



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa