KOVU LA MOYO 12 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 12






Kitendo cha Mama yake Robby kumuita Poshie Malaya kilimuuma sana Angelo lakini kilimuuma zaidi Poshie, aliona kama kuna kitu kimeshika kooni na kujikuta akilia kwa kilio cha kwikwi
"Mama mimi siyo changudoa" .. Poshie aliongea kwa uchungu huku akitetemeka kutokana na maji ya baridi aliyokuwa amemwagiwa, lakini pia alikuwa na uchungu uliochanganyika na hasira ya kuitwa malaya ... "Koma kama ulivyokoma kwa Mama yako msehnzi mkubwa wewe ukome kuniita Mama sijawahi kuzaa shetani kama wewe" ... Mama Robby alimzibua kibao Poshie na kumsindikiza na manenomakali kama kawaida yake ... "Hivi Robby unamatatizo gani mpaka unaamua kuchangia Mwanamke na huyu Rafiki yako? Haujui kama kuna magonjwa siku hizi?" ... Dada yake Robby alimuliza mdogo wake aliyekuwa naye machozi yakimtoka kutokana na vitendo ambavyo alivyokuwa akifanyiwa Poshie na Mama yake.
"Tatizo lenu Dada Maria, nyinyi hamuulizi tatizo nini mnafikia kuchonga tu! Huyu ni Mchumba wa Angelo na amefukuzwa na Mjomba wake ndio mimi nimeamua kuwasaidia isitoshe huyu Dada ni Yatima" .. "Kwahiyo wewe ni Shirika la misaada au wewe ndio Kituo cha Watoto yatima?" ... "Naombeni mnisamehe sana pia naombeni mumsamehee Robby kwa kujichukulia maamuzi bila kuwashirikishan
yinyi kiukweli sisi tuna matatizo tulikuwa tunaomba msaada wenu" ... Poshie aliongea huku akiwa amepiga magoti na akilia ... "Sikiliza nikuambie Binti bila shaka Nyinyi mmefanya tendo la ndoa mpaka wewe ukapata huo ujauzito si ndio?... Mama yake Robby alimuuliza Poshie na Poshie akamjibu kwa kichwa kuashiria ndio ... "Safi sana kama mliamua kufanya tendo ambalo linawahusu wanandoa na mkaamua kulifanya nyinyi bila ya kujua nini kitafuatia. Tendo la Ndoa limewekwa Mahususi ili kutafuta watoto na kuijaza Dunia hii ni kwa wana Ndoa tu, Nyinyi mna bahati sana kwakuwa mmefanya upuuzi wenu na mmebahatika kupata hiyo mimba, wenzako huwa wanaambulia magonjwa. Msaada wangu kwako ili hiwe fundisho kwa wasichana wengine wapuuzi kama wewe wasiojua hata umuimu wa kujikinga ni kwamba, naomba mtoke nyumbani kwangu kabla sijawaitia wezi na mkachomwa moto".
Angelo alijaribu kupiga magoti ili kumuomba msamaha Mama yake Robby, lakini wapi yule Mama alishaamua kuwatimua nyumbani kwake.Kama unavyojua Uswahilini huwa hakuna dogo, kitukidogo tu watu wanajazana na kuacha shughuli zao muhimu ili kuja kushudia kinachoendelea
Masikini Angelo na Mpenzi wake Poshie hawakuwa na njia nyingine zaidi ya kuondoka pale kwenye nyumba ya kina Robby ... "Tafadhali Mama usifanye hivyo nipo chini ya miguu yako mama nakuomba. Dada Maria tazama msichana mwenzako anavyofedheeka Dada jaribu kuwa na moyo wa huruma" ... Masikini Robby aliongea kwa uchungu huku akilia kama mtoto mdogo lakini wapi hakuna aliyemsikiliza
Kwenye matukio kama haya kila mtu anakuwa na mtazamo wake tofauti. Kuna watu waliguswa sana na tukio la kutimuliwa wakina Angelo na kutamani kuwasaidia ila ndio hivyo kama unavyojua maisha ya mjini, Mtu kapanga chumba chake kimoja na anaishi na mkewe au mumewe unafikiri atawasaidia vipi? Kuna wengine walikuwa wapuuzi wenye mtazamo wa karibu, waliwazomea wakina Poshie na Angelo huku wakiwatupia mawe kiasi ambacho jiwe lilimpata Poshie na kumpasua usoni na kuanza kutokwa na damu, huku wenye visimu vyao vya Facebook na mitandao mingine wakichukua picha na video utafikiri waandishi wa habari.
Robby alitamani kuondoka nao lakini ndio hivyo tena Mama yake alimzuia na kumwambia kuna kazi nyingi anapaswa kufanya na sio kujitia Msamaria Mwema
Katika Maisha haya kama umempata Mama mstaarabu mwenye kujali Watoto wake na Watoto wa Mwanamke mwenzake Mshukuru sana Mungu kwa sababu kuna Wamama wana Mambo ya ajabu, na mengine mpaka yanaweza kukufedheesha hata wewe mwenyewe mbele ya jamii inayokuzunguka... {Asante Mungu kwa kunipa Mama Bora}
Mama Roby hakuwa Mama mzuri ambaye ni Mfano wa kuigwa na kama kuna Mwanamke ambaye anasoma story hii ambaye ni Mama au una ndoto ya kuja kuwa Mama tafadhali usije kuwa kama Mama Roby, Ambaye pia kwa namna moja aliamua kumlisha sumu Mwanae {Maria} ili awachukie Poshie na Angelo, Wakati yeye kama Mama alitakiwa kuonesha yeye ni nani katika jamii.
*****
Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kufedheeka. Yani usiombe ukaja kukutana na hali hii, kama ubongo wako hafanyi kazi inavyotakiwa unaweza hata kuchukua maamuzi ambayo hata ukuwahi kufikiria kuyachukua kwa sababu unaweza kupatwa na msongo wa mawazo na ukipatwa na Msongo wa mawazo, kujiua kwako ni jambo la kawaida sana, Ndio mana simlaumu mtu yeyote ambaye amejinyonga kutokana na msongo wa mawazo.
Walikuwa ni Vijana wadogo ambao walikuwa wamejibebesha mzigo ambao hawakusthili kuwa nao kwa wakati huo. ... {HII INAWAHUSU SANA NDUGU ZANGU MNAOYAKIMBILIA MAPENZI SIJUI KAMA MNA PLAN B AU KILA SIKU MPO FB KUOMBA USHAURI MJIFUNZE SANA KUPITIA HII STORY}
Wakati wanatembea Angelo na mwenzake Poshie, nyuso zao zilitawala huzuni na kila mmoja alikuwa akilia japokuwa vilio vilikuwa vinatofautiana kati ya kilio cha Poshie na kile kile ambacho alichokuwa analia Angelo. Angelo alikuwa analia kama mwanaume na muda mwengine alikuwa na kazi ya kumnyamazisha mpenzi wake lakini ndio kama alikuwa akizidisha kumliza na wote walikuwa wakilia.
Kiukweli hakuna aliyejua wapi wanakwenda wakati huo huku wakiwa hawajapata chochote tokea kumekucha yani hata Mswaki walikuwa hawajapiga. Mimba ya Poshie ilikuwa kubwa na hakuwa na uwezo wa kutembea sana alisimama na kushika kiuno kisha akamwambia mpenzi wake ..."Nimechoka Angelo, sijajua tunaelekea wapi Mpenzi wangu" ... Poshie aliongea huku macho yake yakiwa yameiva na kuvimba kwa kulia sana ... "Hata mimi bado sijajua wapi tunaenda kwa wakati huu? ila kama utaweza twende ufukweni kwanza tukapumzike mpenzi wangu" ... "Mimi siwezi Angelo labda tutafute sehemu na tupumzike" .... Poshie aliongea huku akiwa amechoka na kukaa chini kabisa ... Angelo alimwambia amsubiri ili akatafute sehemu na aje kumchukua wakapumzike
Baada ya kuangaika sana Angelo alifanikiwa kupata sehemu ambapo kulikuwa na jumba bovu na akamfuata Poshie wakapumzika hapo.
Walikaaa takribani nusu saa hakuna mtu ambaye alimuongelesha mwenzake kila mtu akiwa ametingwa na mawazo akijaribu kuwaza na kuwazua .... "Mimi nilihisi haya tokea mwanzo, na ndio mana nilikuwa naogopa kuanzisha mahusiano na wewe Poshie. Tazama sasa ninavyokutesa mpenzi wangu?" ... Angelo alivunja ukimya na kumwambia Poshie .... "Hakuna chochote unachonitesa mpenzi wangu na hii yote ni mitihani ya Mwenyezi Mungu, mimi naamini wewe ndiye Mwanaume wangu ambaye nimeandikiwa hivyo usijali naamini majaribu tutayashinda" .... "Mimi nilikuwa na wazo mpenzi wangu" ... "Wazo gani tena ilo Angelo?" ...."hunaonaje mimi na wewe tusijiue?" ... "Kwanini tujiue Angelo?" ... "Wewe Huoni aibu tuliyopata leo? Pale mtaani watu wote wale wananijua sijui nitaiweka wapi sura yangu?" ... "Sikiliza nikuambie Angelo kijiua ni dhambi hata Mungu amekataza katika vitabu vyake, istoshe kwanini unaishi kwa sababu ya watu? Wewe unaweza kuishi kila mtu anavyotaka? Siku zote ukitaka kumkosoa Mungu, basi mtazame wa chini yako, hapo ndio utaona ni jinsi gani mungu alivyokupendelea wewe. Kuna watu wana maisha magumu na wanateseka sana kiasi ambapo wewe ungekutana nao na ukawaadisia maisha yako yani wangetamani walau mungu awape hata maisha yako wewe" ..
Maneno ya Poshie yalimuingia kiasi fulani Angelo na akabadilisha mawazo yake.
Walikaa pale mpaka usiku kumbe kwa bahati mbaya pale palikuwa na walinzi wanapalinda, hivyo walipoingia na kuwakuta wamekaa pale wale walinzi waliamua kuwatimua ... Angelo na mkewe walichukuzana mpaka katia kiwanja cha mpira na kujiweka katika upande mmoja wa goli kwa sababu kulikuwa na kiza na wakakaa hapo.
Mchana kutwa walishinda bila ya kula chochote wala kunywa maji... Poshie njaa ilimshika mpaka sasa akawa anaishiwa nguvu ... "Naenda kukutafutia chakula mpenzi wangu naomba unisubiri" ... Angelo alimwambia Poshie na akatoka eneo lile na kumuacha Poshie peke yake.
Baada ya kuzunguka sana alitokea katika mtaa mmoja ambaow alikuwa wanauza vitafunwa
Wakati anapita pale alimuona ntoto mmoja anatoa Tsh 1000 na kununua Maandazi ... Angelo aliaona bora lawama kuliko fedhea. yule mtoto wakati anatoka pale na mfuko wake wa maandazi alimfuatiria na walipofika kwenye kiza akampokonya ule mfuko na kukimbia nao .... "mwiziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii" ..... Mtoto alipiga kele na raia wema wakaanza kumfukuza Angelo .....Nini kitaendelea.......like na kushare iwahi kuja.....



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa