KOVU LA MOYO 11 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 7, 2020

KOVU LA MOYO 11





Maneno ya Robby yalizidi kumvunja nguvu Poshie, akageuka na kumtazama Robby huku machozi yamkimwagika kwa wingi Robby alijisikia vibaya sana baada ya kumuona Poshie akilia kiasi Kile aswa kutokana na hali yake ilivyokuwa ..
Alimuona kama Dada yake ndio yupo katika mateso kama yale ... "Mimi nina wazo Angelo! Kwanini tusimtafute mtu mzima ambaye ana heshima zake na twende naye kule kwa Mzee Makasi na akaongee naye, anaweza akamuelewa".... Robby alimwambia Angelo kwa sauti ya chini huku akiogopa Mama Yake hasIje kumsikia ... "Yule Mzee hawezi kumuelewa mtu yeyote Robby, ni bora tutazame mipango mingine kuliko kurudi tena nyuma kwasababu ameshaongea mdomo mpana kuwa yeyote atakayerudi katika nyumba yake anaweza hata akamuua. Sasa huwezi jua kwanini ameongea maneno makali kiasi kile, tena ukizingatia Poshie ni Mtoto wa Marehemu Dada yake" ... "Tatizo lako Angelo unapenda kupanga kushindwa kabla haujashindwa. Alivyokufukuza wewe tofauti na tutapoenda na mtu mzima" .... Robby liendelea kusisitiza na Poshie akaunga mkono ili wamtafute mtu angalau akajaribu kuwaombea msamaha.
Walifanikiwa kuangaika na kumpata mzee mmoja ambaye mwenye busara zake na kwenda naye kule kwa Mjomba wake Poshie. Mzee Makasi alipomuona Poshie ameungana na watu wanakuja nyumbani kwake akaingia ndani na kutoka na panga, kisha akawatimua na kutangaza mtaa mzima kuwa atakayemsaidia Poshie basi yeye atakula naye sahani moja.
Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili na hapo sasa Angelo alitakiwa aoneshe kwanini amezaliwa Mwanaume
Poshie alilia sana mpaka akaanza kujisikia vibaya kutokana na hali yake jinsi ilivyokuwa. Hakuwa na Kaka wala Dada ambaye labda angemfuata na kumlilia matatizo yake ili amsaidie, lakini wapi alizaliwa mwenyewe na alitakiwa apambane mwenyewe ... "Lolote litakalokuwa na liwe ila kwa tukio ambalo nimelishuudia kwa macho yangu ni bora tu niwasaidie. Mama kama atachonga chochote basi mimi nitajuana na yeye" ... Robby aliona bora Poshie na Angelo pamoja na yeye mwenyewe walale chumbani kwake na kama Mama yake akijua kinachoendelea basi yeye atajua jinsi ya kumjibu.
Vilio vilitawala kutwa nzima huku kukiwa hakuna wakumbembeleza mwenzake kati ya Poshie na Angelo. Wakati huo Robby alikuwa ametoka ili kwenda kujaribu kutafuta mpango wa kuwasaidia Angelo pamoja na Poshie ....
Usiku ulifika huku Robby akiwa hajafanikiwa kupata kitu chochote cha kuwasaidia.... "Njaa inaniuma mpenzi wangu sasa tutafanyaje?"... Poshie alimuuliza angelo na kumfanya akune kichwa akifikilia cha kumjibu ... "Naona hata haibu mke wangu sijui nikujibu nini? Kiukweli sina hata kipande cha pesa mfukoni kwangu na sijui utakula nini?" ... Angelo alimjibu Poshie huku akijisikia haibu.... "Kama hauna kitu Mume wangu ndio mipango ya Mungu wala usijali. Kwakuwa leo tumekosa nitakunywa maji na kumshukuru Mungu, naamini kesho atatupa kikubwa zaidi ya tulichokuwa tunakitaka leo" ... "Poshie wewe ni zaidi ya mwanamke najiona mtu mwenye bahati kukupata mke kama wewe! Kila mtu kwenye ndoa yake angefanikiwa kupata Mwanamke kama wewe nafikiri usaliti katika Ndoa husingekuwepo kabisa" ..."Nani kakudanganya hivyo? Siku zote nyinyi Wanaume hamridhiki na mnachokipata mimi naamini Wanawake wengi ni wavumilivu katika ndoa zao tatizo ni nyinyi Wanaume" ...
Poshie na Angelo walianza kubishana juu ya mambo ya ndoa huku kila mmoja akivutia upande wake kuwa ndiyo upo sahihi.
Kwa kitendo hiko cha kubishana kwa dakika kadhaa, kiliwasaidia kiasi fulani kusahau matatizo yao na wakijikuta wakibishana, Huku wakiwa makini wasije wakasikika kama kuna watu mule chumbani kwa Robby.
Robby alirudi na kuwakuta wakiwa wamelala Chini ..."Kaka vipi mbona hapa?" ... "Usijali ndugu tumekupisha wewe" ... "Hapana usifanye hivyo jembe, huyu ni mjamzito hatakiwi kuumwa na mbu kwa sababu ya malaria muamshe mwende kitandani bwana kule ndio kuna net." .... Maneno ya Robby yalimgusa sana Poshie aliyekuwa yupo macho lakini akijifanya amelala, Roho ilimuuma sana kuona wanamlaza chini mwenye kitanda ili wao walale kitandani ... Pale pale akiwa amefumba macho na machozi yakimtoka aliamua kumuomba Mungu amjalie Mpenzi wake ili siku moja naye apate pesa na wawe na maisha yao" ... Angelo alimuamsha Poshie na akasalimiana na Robby ..."Vipi shemeji unaendeleaje?" ... "Mimi naendelea vizuri sijui wewe Shemeji yangu huko utokako?" ..."Namshukuru mungu nimetoka salama, japokuwa sijafanikiwa kitu, ila usijali Shem langu la ukweli Matatizo yataisha na yule Mjomba wako siku moja atakuja kukuangalia kwa haibu sana" ... "Nashukuru kusikia hivyo Roby, Mungu akupe moyo huo huo wa huruma katika maisha yako naamini utakuja kufanikiwa" ... "Vipi mbona unataka kulala Shemu chakula vipi?" .. "Hapana Shem mana tumekusumbua sana we acha tutalala tu" ... Poshie alimjibu Robby kwa haibu lakini njaa ilikuwa ikimuuma sana ... "Haiwezekani ulale na njaa wakati mimi nipo bwana shemu. Ngoja niende kwa bimkubwa huko nikawaibie chakula naamini kitakuwa kimebaki" ...
Robby alienda Nyumba kubwa na kuwaibia chakula kisha akawaletea
****
Maisha ya Poshie na Angelo yalikuwa yapo mikononi mwa Robby na yeye ndiye aliyekuwa akiwasaidia
Poshie hakutakiwa kutoka nje, kwa sababu walimuogopa Mama yake Roby hasije akamuona Alikuwa kama mwali na kila kitu alikuwa akifanya ndani, hata kujisaidia ilikuwa ni ndani na wao walikuwa wakimwaga .... Mama yake Robby alianza kuhisi kama ndani kulikuwa na mtu ambaye mwanae amemficha. alijaraibu kufanya uchunguzi na kweli alifanikiwa kumuona Poshie bilaya yeye kumuona.
Robby kama kawaida yake siku hiyo alikuwa anaenda kuiba chakula ndani na wakati anataka kutoka akakutana na Mama yake ...."Naona unafanya kazi ya kuchukua chakula changu na unampelekea yule mfugo wako?" ... Kauli ya Mama yake ilimstua sana Robby na alijua lazima Mama yake atakuwa amegundua kila kitu ..."Sijakuelewa Mama unamaanisha nini?" ..."Mpumbavu mkubwa heti unamaanisha nini? Wewe hauna akili hata kidogo na nakwambia dawa yako ipo jikoni inachemka" ... Mama yake Roby alimwambia na kuondoka zake Robby aliporudi kule aliogopa kuwaambia kama Mama yake amegundua kama wao wapo mule kwa kuhofia Poshie anaweza kupandwa na presha .... Siku hiyo waliongea sana mpaka wakachelewa kulala.
Kwakuwa Walichelewa kulala jana usiku na walichelewa kuamka asubuhi yake.
Kumbe Mamayake Robby alimfuata mwanae mkubwa Dada yake Robby anayeitwa Maria. Mama Roby alimwambia kila kitu Maria juu ya Roby na kina Poshie jinsi anavyowafuga mule ndani
Maria na Mama yake walikuja na wakamgongea mlango Robby na akatoka... "Shikamoo Mama" .. Roby alimsalimia Mama yake lakini Dada yake alimsukuma pembeni na kuingia ndani huku akiwa ameshika ndoo iliyokuwa na maji ya baridi yaliyokuwa yamechanganika na Barafu ... Maria alifika na kuwamwagia Poshie na Angelo waliokuwa wamekumbatiana ..."Mwaaaaaaaaa" .... Poshie na Mpenzi wake walistuka huku wakitetemeka ... "Shikamoo Mama"... Poshie alimwamkia, Mama yake Robby huku akitetemeka na kuogopa ...
"Shikamoo Mama!!!" ... Mama yake Robby alimgezea Poshie huku akiwa amembania pua, kisha akamsonya na kumwambia... "Malaya Mkubwa weee!! Sina Mtoto aliyelaanika kama wewe na sidhani kama utakuwa umezaliwa labda utakuwa umetapikwa. Yani katika maisha yangu nilikuwa sijawahi kumuona Changudoa mjamzito ila leo ndio nimekuona. Haya na limimba hilo, unawezaje kuwamudu Wanaume wawili kwa wakati mmoja? ....
NINI KITAENDELEA? ...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa