Mama Sabrina naye akamtazama daktari na
kumwambia,
"Tunashukuru sana dokta, umetusaidia sana"
"Msinishukuru mimi tu, mshukuruni na mumewe
pia hapa"
Huku yule daktari akimtazama Jeff na kufanya wote
wamtazame Jeff.
Mama Sabrina na Sakina walijikuta wakiuliza kwa pamoja,
"Mumewe? Kivipi?"
Jeff akaona hapa hali ya hewa itaharibika muda sio mrefu kwahiyo akawaomba warudi nyumbani na huko ndiko atawaeleza vizuri.
"Jamani, twendeni tukaongelee nyumbani haya mambo"
"Kwani yana uzito gani hadi ushindwe kutuambia?"
Jeff akazidi kuwasisitiza kuwa wakaongelee nyumbani hata baba Sabrina nae akaafiki juu ya hilo.
Wakati wanatoka pale, Sakina akawaomba wamsubiri kidogo kwani anaenda maliwatoni, kwahiyo wakapanda kwenye gari ya baba Sabrina huku wakimngoja Sakina.
Sakina akiwa mule maliwatoni akawaona tena wale manesi wa jana ambao walikuwa wakizungumza mambo kama ya jana yake.
"Unaambiwa yule mdada alipofika mumewe tu akajifungua bila tatizo"
"Sasa hapo huyo mumewe ndio angekuwa sio muhusika wa ile mimba wee ingekuwa khabari nyingine"
"Kwani ingekuwaje?"
"Asingejifungua na sijui hata tungefanyaje. kwakweli hii hospitali kama mtu alichepuka hata usimshauri kuja. Yani huyu daktari huyu ni shida ndiomana watu wanaiita hospitali ya babu hii"
Sakina alitoka akiwa na maswali mengi sana kwenye akili yake huku akiwaacha wale manesi wakiendelea kuongea kisha yeye kurudi kwenye gari na safari ya kwenda kwakina Sabrina ikaendelea.
Walipofika tu wakashangaa kumuona Sam nae akiwa eneo lile.
Baba Sabrina hakujishughulisha hata kumsalimia wala kuitikia salamu yake na kumfanya mama Sabrina nae ampite tu.
Sakina alichofanya ni kuitikia salamu tu na kuingia ndani.
Ni Jeff peke yake aliyebaki pale na kusalimiana na Sam kwani hata Sabrina alipita na mama yake vilevile.
"Kwahiyo mnatokea wapi saizi Jeff? Kumbe umesharudi?"
"Ndio nilirudi jana na kukutana na haya maswahibu. Ila saizi ndio tumetoka hospitali na mamdogo hapo kajifungua mtoto wa kiume"
"Jamani, hivi mimi ni mwanaume mwenye roho mbaya kiasi gani? Kumbe nimekaa muda mrefu kiasi hiki bila kuja kumuona mke wangu hadi nakuta ameshajifungua tayari! Ila Mungu ni mwema, amemsaidia Sabrina. Mimi sifai jamani"
Sam alionekana kujisikitia kwa yote aliyoyafanya ya kumsahau mkewe.
Alijiona ni mpumbavu sana ukizingatia ni huyu mwanamke anayempenda sana.
Sam akataka kuingia kwakina Sabrina ila baba Sabrina akatoka na kumzuia.
"Tafadhari Sam nakuomba tu uende zako, sina hata haja ya kukuona hapa kwangu"
Sam akaona kuwa haitakuwa vyema kwa yeye kubishana na baba mkwe wake hivyo akaamua kurudi kwenye gari yake na kuondoka.
Kisha baba Sabrina na Jeff wakaingia ndani.
Walipokuwa ndani bado mama Sabrina akakumbusha swala la daktari kumuita Jeff mume wa Sabrina.
Ikabidi Jeff achekeche akili na kuanza kuwajibu,
"Jamani sikufanya hili kwa nia mbaya. Daktari alimuhitaji mume wa Sabrina na kwa wakati ule Sam hakuwepo. Mi nikaamua nijaribu tu kujitokeza kama mume wa Sabrina ila si kwa nia mbaya"
"Aah kumbe ndiomana tukakutafuta bila kukuona, yani mi nikamshangaa kweli daktari eti mume wa Sabrina bila kujua kuwa wewe ni kama mtoto kwa Sabrina. Ila tunashukuru umetusaidia sana"
Kisha Jeff akaamua kuondoka pale ili kuepusha kuzuka kwa maneno mengine.
Kwahiyo akabaki pale Sakina na wazazi wa Sabrina na wakati wote huo Sabrina alikuwa kimya kabisa kwani hakuongea kuhusu jambo lolote.
Jeff akiwa nyumbani akayatafakari maneno ya daktari na kutabasamu,
"Kumbe na huyu pia ni mwanangu, najua Mungu anamakusudi yake kabisa kwa haya. Nampenda sana Sabrina, nampenda kutoka moyoni najua yeye ndio mke wangu wa maisha. Japo hawatanielewa kwasasa ila ipo siku watanielewa tu"
Moyo wake ukafurahi sana, na kuanza kuvuta kumbukumbu kabla ya kuondoka kwenda nje.
Akakumbuka kuwa siku mbili kabla alilala na Sabrina.
Pia akakumbuka barua aliyoandikiwa na Sabrina.
Akatabasamu tena, kisha akaenda kwenye begi lake kupekua ile barua.
Wakati anapekua akamsikia mama yake akimuita na kugundua kuwa mama yake amesharudi ikabidi aache na kwenda kumsikiliza.
Sakina hata hakujua kuwa aanzie wapi kwa anachokihisi kuhusu mtoto wake.
Ingawa Jeff aliitikia wito na kusogea alipo mama yake ila Sakina hakujua kuwa amuulizaje.
Kisha Jeff akaamua kumuuliza mama yake,
"Nimekuja mama, mbona huniambii chochote?"
Sakina akatulia kidogo na kuuliza,
"Hivi ulivyoenda kwa dokta na kusema wewe ni mume wa Sabrina ilikuwaje kuwaje yani kitu gani kilitokea?"
Jeff akamuangalia mama yake na kumuuliza,
"Nikikwambia ukweli utaniamini mama?"
"Kwanini nisikuamini mwanangu? Niambie tu"
"Usijali, nitakwambia"
"Mmh! Niambie jamani mwanangu, kwanini uwe kimya"
"Tulia mama, nitakwambia tu yote niliyoyafanya kule"
Sakina akatamani kujua ila Jeff hakuendelea kuongea zaidi ya kumuaga na kutoka pale nyumbani kwao na kumfanya mama yake azidi kuwa na mawazo katika akili yake.
Neema akiendelea kuwa hoi, akajikuta akimuuliza Aisha kuhusu rafiki yake Sia.
"Vipi yule rafiki yako uliyekuja nae siku ile?"
"Namshangaa Sia kwakweli kwamaana aliniahidi vizuri tu. Alisema atakuwa anakuja kukuona ila hata namshangaa hadi leo kimya"
"Namuona macho juu juu sana, mwambie awe makini na wanaume"
"Halafu dada, kwanini wanaume unawasema kiasi hicho?"
"Ni historia ndefu mdogo wangu, ila sitaweza kukaa kimya milele. Roho inaniuma sana. Ipo siku nitasema tu. Ila jiepushe nao tafadhari"
Aisha alikuwa akimsikitikia sana Neema na akatamani sana kujua tatizo alilonalo Neema ila ilikuwa ngumu kujua kuwa Neema anasumbuliwa na nini ingawa kila siku alimuona akizidi kudhoofika tu.
Sam aliamua kwenda baa kwaajili ya kupoteza mawazo dhidi ya mke wake Sabrina na kupoteza yale mawazo ya kutimuliwa kwakina Sabrina.
"Kweli tenda mema uende zako, yani mema yote niliyofanya kwa Sabrina na familia yake, yamesahaulika kabisa sababu ya kosa moja tu nililofanya"
Kisha akajifikiria tena,
"Ila kwanini nilifanya vile? Kwanini nilikuwa simpendi Sabrina tena? Kwanini nilibadilika?"
Hakupata jibu ila moyo ulimuuma sana na kujiona mtu asiye na thamani kabisa.
Wakati Sam yupo pale baa, akatokea Sia ambaye alifurahia sana uwepo wa Sam mahali pale na kujiaminisha katika moyo wake kuwa siku hiyo ni lazima ampate huyo Sam kwani alimuona kuwa ni mwanaume anayevutia sana ila kilichompendeza zaidi kwa Sam ni pesa alizokuwa nazo.
Alikaa pale na kujaribu kuzungumza nae mawili matatu huku akimbembeleza kuwa waende nyumbani.
"Sam, pombe hata haisaidii chochote zaidi utajiumiza tu"
"Sasa nini kinachosaidia?"
"Twende nyumbani nikakuonyeshe kinachosaidia ukiwa na mawazo"
Sam akakubali kwani tayari akili yake ilikuwa imevurugika vilivyo.
Safari ya kwenda nyumbani kwa Sam ikaanza huku Sia akiamini kuwa sasa ni muda muafaka wa yeye kuwa pamoja na Sam.
Walienda mpaka nyumbani kwa Sam na kuingia ndani pamoja na Sam.
Kisha wakaenda sebleni kukaa na kuongea mawili matatu.
Sia akatamani atoe nguo zake ili Sam apate kushawishika na mwili wake ulivyo, kwani yeye alijiona kuwa na silaha kubwa ya kushawishi mwanaume wa aina yoyote ile nayo ni makalio yake.
Alikuwa na makalio makubwa ya kupendeza ambayo hata akitembea lazima yatingishike, naye akaona wazi kama akitoa nguo na kuanza kumkatikia Sam lazima apagawe.
Ila kabla wazo lake hilo halijazaa matunda, wakasikia hodi yani mlango wa Sam ukigongwa ambapo Sam aliinuka na kwenda kufungua, mgongaji alikuwa ni Jeff ambapo Sam alimkaribisha vizuri ndani.
"Afadhari Jeff umeamua kuja huku moja kwa moja yani, naamini wewe ndie mwenye uwezo wa kunipa tumaini juu ya mke wangu"
Jeff akatabasamu tu ila maneno yale yalimkera sana Sia.
Jeff naye aliketi na kumsalimia Sia ambapo Sia naye aliamua kuaga na kumuomba Sam kuwa aondoke kwani Sam alimwambia pale pale kuwa atakuwa na maongezi marefu kidogo na huyo Jeff.
Sam hakusita kumruhusu, kisha akamtoa nje kama ishara ya kumsindikiza kidogo na alipofika nae nje akampatia pesa ya kuweza kupanda gari ya kukodi ili aweze kurudi kwao.
Kisha Sam akarudi ndani kwaajili ya mazungumzo yake na Jeff.
Sia akiwa njiani akajikuta akijiwa na sura ya Jeff na kuona kama mtu anayemfahamu vizuri ila tu hakumbuki ni wapi aliwahi kumuona ila hisia zake zingine zilimuonyesha kuwa yule Jeff aliwahi kumuona akiwa mdogo ila tu hakukumbuka ni wapi.
"Duh! Basi amekua mkubwa sana saivi halafu kamekuwa kazuri zaidi mmh!"
Sia akajikuta akitabasamu na kuona wazi moyo wake ukivutiwa na muonekano wa Jeff pia.
Sam aliamua kumueleza Jeff kile anachodhani kuwa kitaweza kumsaidia kwaajili ya kumrudisha Sabrina kwake.
"Yani naomba unisaidie Jeff tafadhari, najua mke wangu hana kumbukumbu kwasasa ila najua wazi kuwa wewe ni mtu pekee unayeweza kumsaidia aweze kurudi katika hali yake ya kawaida ila hata kunisaidia katika kuwashawishi wazazi wake wanisamehe"
"Ni kweli naweza kufanya hivyo, ila je unaniruhusu?"
"Nakuruhusu Jeff na ndiomana nimekuomba, kwanza nimeshukuru sana kuja kwako kwani sikutegemea kama ungekuja huku kwangu kweli"
"Hakuna ulichonikosea kabisa, nina kila sababu ya kuitikia wito wako. Hata hivyo nilirudi bila kukutaarifu kuwa ni siku flani narudi. Ndiomana nikaja huku"
"Kwanza kuna mambo nimekosea, naomba nikiri kwako jambo hili"
Jeff akashtuka kidogo na kumsikilizia Sam kuwa ni jambo gani alilokosewa.
"Kwanza nikuulize, Dorry yupo?"
"Hayupo, na hata mimi sijamkuta kwani siku niliyofika nasikia ndio siku aliyoondoka."
Sam aliamua kumueleza alichokifanya baada ya kusoma barua ya Dorry na jinsi alivyomshawishi adanganye kuwa ana mimba ya Jeff na jinsi mpango wao ulivyokuwa hapo mwanzoni.
"Nisamehe sana kwa hilo Jeff tafadhari"
Jeff hakuona kama hili ni kosa kubwa kiasi hicho kwake hadi kuombwa msamaha kwani yeye ndiye aliyekuwa na kosa kubwa zaidi dhidi ya Sam.
"Kumbe ndivyo ilivyokuwa! Usijali kaka, ila hiyo barua uliipata wapi?"
Sam akaamua kumuelezea Jeff mazingira ya yeye kuipata hiyo barua.
"Nilimuona Sabrina wakati akikuaga alikuwa amekuchomekea kitu kama barua, roho ikaniuma na kunifanya nitake kujua kuwa alikuwekea nini. Ndipo nilipotoka na hiyo barua ya Dorry"
Jeff akabaki kuduwaa tu kwani yeye hakuelewa kuwa hayo yote yalitokea wakati akisafiri.
"Basi bamdogo, hakuna tatizo mi nishakuelewa. Tusaidiane tu juu ya hili lililopo"
Kisha Jeff akaamua kuaga kwani aliona wazi kuwa akiendelea kukaa hapo basi Sam anaweza akamuhoji vitu ambavyo angekosa majibu kwa wakati huo.
"Sawa Jeff, ila tafadhari sana nakuomba ujitahidi kunisaidia hili swala nililokuomba"
"Hakuna tatizo juu ya hilo na nina kuahidi kuwa kila kitu kitakuwa sawa"
Kisha akaondoka zake na kumuacha Sam pale kwake.
Kwavile ilikuwa tayari usiku, Jeff alifika kwao na kwenda kulala moja kwa moja ila wazo la barua dhidi ya Sabrina halikuisha kwenye akili yake kwani alikumbuka maneno ambayo Sabrina alimuandikia kwenye ile barua na hicho kitu ndicho kilichomfanya alipofika kusoma akachagua kozi za muda mfupi ili aweze kurudi mapema kumuona Sabrina.
"Hivi huyu Sabrina kama nikimsomea ile barua yake hawezi kukumbuka kweli?"
Akatafakari hilo na kuona kuwa ni jambo linaloweza kumfanya Sabrina arudiwe na kumbukumbu zake.
Akatafakari hilo na kuona kuwa ni vyema kama kesho yake afanye hivyo.
Kulipokucha Sakina aliamka akifanya usafi ila maneno ya wale manesi bado yakarudi katika akili yake.
Akakumbuka kuwa walisema kuwa mdada aliyehitajiwa mumewe aje na kama mimba isingekuwa yake basi asingejifungua.
Akatafakari kuwa Jeff ndiye aliyesema kuwa alienda kujifanya kama mume wa Sabrina na kuwezesha Sabrina ajifungue.
"Mmh! Kuna nini hapa kati hapa? Kuna nini mbona sielewi? Eeh Mungu tafadhari isiwe kama ninachowaza mimi jamani"
Akafikiria kidogo tena,
"Hivi inawezekana kweli kwa Sabrina kutembea na mtoto aliyemlea mwenyewe? Hapana, hapana nakataa. Sabrina hawezi kufanya kitu kama hiki jamani"
Jeff naye akawa ametoka ndani muda ule na kumuaga mama yake kuwa anaenda kumuangalia Sabrina jambo ambalo likamtia mashaka Sakina kuwa anawaza vingi na iweje mwanae huyu kuamka tu na kudai kuwa anaenda kumuangalia Sabrina.
Alimuangalia tu akienda lakini akasema kuwa lazima amfate.
Jeff aliona kuwa ile asubuhi ndio ingekuwa muda muafaka wa yeye kuzungumza na Sabrina na hata kumsomea ile barua ili aone kama ataweza kurudisha kumbukumbu zake.
Alifika na kuwagongea ambapo mama wa Sabrina ndiye aliyemfungulia mlango na kumkaribisha ndani huku yeye akiendelea na shughuli zingine za usafi na huku akimuandalia Sabrina chakula cha asubuhi.
Jeff aligonga chumbani kwa Sabrina na kukaribishwa kwani Sabrina alikuwa ameshaamka tayari na mwanae yule mdogo kwani yule mwingine alikuwa akilala na mama Sabrina.
Jeff alikaa na kumsalimia Sabrina kisha akamwambia,
"Kuna kitu kidogo nataka nikueleze."
"Kitu gani?"
"Niambie kwanza kama upo tayari kunisikiliza"
"Yeah, nitakusikiliza"
Jeff akatoa ile barua na kuanza kuisoma,
"Ni usiku sana nimeamka na kuandika haya. Kwako Jeff mpenzi......."
Jeff akakwamia hapo na kushtuka kwani mlango ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Sakina.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment