JE HAYA NI MAPENZI!! 57: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 18, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 57:






Kisha Jeff akasogeza midomo yake karibu na
midomo ya Sabrina.
Wakashtuliwa na mlio wa mlango ambapo aliyeingia
alikuwa ni Sam.
Kisha Sam akawaambia,
"Msishtuke endeleeni tu nimeshajua kila kitu"
Wakajikuta wakitazamana kwa aibu.
Jeff akamuachia Sabrina na kubaki ameduwaa huku akimtazama Sam, ambapo Sam akawaambia,
"Nimesema endeleeni na mlichokuwa mnataka kufanya"
Jeff akaona utakuwa msala sasa, akataka kuondoka ila Sam akamzuia na kusema tena,
"Kwanini unataka kukimbia Jeff ikiwa kitu mlichokuwa mnataka kufanya ni kitu cha kheri?"
Sabrina hakuweza hata kumtazama Sam usoni kwani aibu ilimjaa tu huku wakisubiria hatma yao kwani wote walishindwa cha kusema.
"Kumbe mna ishara zenu siku hizi eeh!"
Wakaendelea kukaa kimya na kumfanya Sam aendelee kuongea,
"Jeff, uliponiambia kuwa Sabrina amekuita sikupata mashaka sana ila kuna kitu ambacho hukukigundua, mi katika simu yangu nimeweka huduma ya kurekodi mazungumzo yote yanayofanyika kwa kupitia simu yangu ili hata kama nimesahau basi nijaribu kusikiliza tena. Na ulipoondoka tu, nikaamua kusikiliza tena yale mazungumzo yenu na kumsikia Sabrina akikwambia kuwa uende nyumbani kwenu mama yako anakusubiri. Sasa kilichonishtua ni wewe kuniaga na kuniambia kuwa Sabrina anakuita na ndiomana nikaamua kurudi ili nikamate uongo wako. Haya sasa nataka kujua, je Sabrina ulimwambia Jeff kuwa mama yake anamuita kama ishara ya yeye kuja hapa? Au Jeff uliamua tu kuja kwa mazoea yako binafsi? Nijibuni sasa"
Sabrina alikuwa akitetemeka tu kwani hakuelewa hata ajieleze vipi ili aweze kueleweka kwa Sam,
"Inamaana leo mmekosa kabisa jibu la kunishawishi mimi?"
Jeff akaanza kujitetea,
"Hapana sio hivyo, mi nilikuja tu kumuaga mamdogo"
Sam akacheka sana na kusema,
"Kweli wewe mtoto hamnazo, yani katika kujitetea kote wewe umeona huo ndio utetezi mkubwa sana? Ok, kwa mfano nikakuuliza kwani asubuhi hukumuaga? Na kwanini usimuage kwenye simu? Na kwanini mimi usiniambie ukweli wakati unaondoka kule?"
Jeff alibaki kimya tu kwani kwa vyovyote vile alihisi kuwa ni wazi Sam ameshaujua ukwe li ila anawasanifu tu kwa maswali anayowauliza.
Kisha Sam akamuangalia Jeff kwa makini sasa na kumwambia,
"Haya nakuruhusu uende kwa mama yako, najua anakungoja"
Jeff hakuamini masikio yake na kujikuta akitoka kimya kimya bila ya kusema chochote.

Sabrina sasa, alibakia yeye na Sam mule ndani.
Alikuwa kasimama tu huku akingoja hatma yake.
Sam akamsogelea Sabrina na kumkumbatia vilevile ambavyo Sabrina alikuwa kasimama na kumwambia,
"Nakupenda sana mke wangu, eeh umeniandalia chakula gani leo?"
Sabrina alikuwa akijibu huku midomo ikimtetemeka kwani aliona wazi kuwa anaweza kutendewa jambo lolote baya na Sam kwa wakati ule.
Kisha Sam akaenda kukaa kamavile mtu anayengoja chakula kiandaliwe.
Naye Sabrina aliandaa kile chakula huku akiwa bado hana amani moyoni mwake.
"Chakula kitamu sana hiki Sabrina, asante kwa kuniandalia chakula kizuri kama hiki. Namshukuru Mungu kwa kunipa mke mwema na mzuri anayejua mapi shi"
Sabrina alikuwa akimkodolea macho tu Sam,
"Tena kesho kutwa ndio harusi yetu, hivi hiyo mimba inamiezi mingapi mke wangu ili niandae nepi za mtoto?"
"Ina miezi sita unaenda wa saba"
"Ooh miezi mitatu imebaki, nina hamu sana ya kumuona mwanangu. Najua atakuwa wa kike tu"
"Hapana ni wa kiume"
"Kwanini tuandikie mate wakati wino upo? Baada ya harusi, wiki ijayo nitakupeleka hospitali ukapige ultrasound hapo ndio tutamaliza utata wa jinsia ya huyo mtoto"
Sabrina akaitikia tu na kujichekelesha kiuongo uongo kwani furaha hakuwa nayo kabisa.
Muda kidogo kupita Sabrina akamuomba Sam kuwa aende nyumbani kwao ili siku ya harusi atokee nyumbani.
Sam nae hakuona kama lile ni jambo la kupinga, kwani aliona ni kheri tu tena italeta picha nzuri ingawa biharusi mwenyewe tayari alikuwa mjamzoto.
Kwahiyo Sam akajiandaa kwaajili ya kumpeleka Sabrina nyumbani kwao ingawa muda wote Sabrina alikuwa na mawazo tu.

Kwavile, waliondoka kwao jioni kwahiyo wakaingia kwakina Sabrina wakati muda nao umeshaenda ambapo mama wa Sabrina alifurahi na kuwaambia kuwa wamefanya vyema.
"Ni busara sana atokee hapa nyumbani kuliko mtoane huko huko"
Sam alikuwa akitabasamu tu muda wote ingawa Sabrina alikuwa kanyong'onyea.
Kisha Sam akawaaga na kuondoka.
Ila Sabrina hakukaa sana zaidi ya kujibeba na kwenda kulala, kwani aliona kichwa chake kuwa kizito kwa mawazo.
Wakati amelala, akajiwa na njozi kuwa wameshaenda kanisani kwaajili ya kufunga ndoa, ila watu wakaanza kuulizana,
"Jamani bwana harusi hayupo, hajafika mpaka saa hizi au haji tena?"
Akamuona shangazi yake akipayuka,
"Nilishayajua yote haya, kiburi chako kimekuponza Sabrina unaona sasa?"
Akajikuta akilia kwa uchungu, mama yake naye akamfata na kumwambia,
"Pole sana mwanangu, jikaze ndio ukubwa huo. Hata mimi mamako nimepitia hayo"
Akatokea na Jeff na kumwambia,
"Usijali Sabrina, ha ta wote wakutenge mimi nitakuwa pamoja nawe"
Ila Sabrina bado alikazana kulia, mara akamuona Sam kashika bastora na kuwaelekezea yeye na Jeff kisha akawaambia,
"Na mkapendane huko akhera, kwaheri"
Sabrina alishtuka huku jasho jingi likimtoka, hakutaka kuamini kuwa ile ilikuwa ni ndoto tu.
"Lazima ina ukweli ndani yake, masikini Sabrina mimi. Nimekosa nini jamani? Mbona naonewa? Yani hii mimba hii inanitesa mimi, bora hata ingejitokea tu nijiepushe na aibu"
Sabrina alijikuta akibubujikwa na machozi tu na hakuweza kulala tena hadi panakucha.

Kulipokucha aliamka na kumfata mama yake kisha akamwambia,
"Sitaki tena kuolewa mimi mama"
"Wee Sabrina una kichaa au? Na hiyo mimba utaipeleka wapi? Mbona una mabalaa mwanangu?"
"Sina mabalaa mama ila tu sijisikii kuolewa"
"Yani harusi kesho halafu wewe unasemaje Sabrina? Huo upuuzi kamwambie baba yako mi sitaki hata kuusikia"
"Nina maana yangu mama"
"Maana gani hiyo? Tushakula hela za watu sie. Unataka utaolewa, hutaki utaolewa tu. Hizo sababu zako ukazitoe ndani ukiwa na mumeo"
Sabrina alimuangalia mama yake na kumuona kamavile ni mtu asiyemuhurumia ila alijilaumu mwenyewe kwakutokumwambia ukweli mama yake.
Akatoka na kujikalisha nje tu kwani mawazo yalimjaa.

Sam akiwa anamalizia mambo yake ya siku hiyo ili akajiandae kesho yake kwaajili ya harusi, njiani akakutana na kijana Francis ambaye alihitaji kuzungumza naye.
Kwanza kabisa Francis alimpongeza Sam kwa kumpata Sabrina,
"Hongera sana kaka, una bahati kwakweli. Sabrina ni dhahabu ambayo wengi wameitafuta bila mafanikio, ila wewe umebahatika hadi kumpa mimba dah hongera sana"
Sam alitabasamu kinafki kwani alijua wazi kuwa mimba ya Sabrina sio yake.
Kisha Sam akamuuliza Francis,
"Inamaana Sabrina ni binti aliyetulia sana eeh!"
"Tena sana, mimi nina mifano iliyohai kabisa kwani nina ndugu yangu aliwahi kuwa hadi kipofu kwaajili ya Sabrina lakini bado hakuweza kulala na Sabrina. Yani hakuna mwanaume aliyebahatika kulala na Sabrina, nakupongeza sana kaka."
Sam akamshukuru Francis kwa kufunguka kwake, tena akamkaribisha kesho yake kwenye harusi yao ambapo bila kinyongo Francis aliahidi kuwa ataudhuria tu.
Kisha Sam akarudi nyumbani kwake huku akiwa na tabasamu usoni ingawa moyoni alikuwa na mawazo kupita maelezo ya kawaida.

Jeff akiwa nyumbani kwao jioni ya siku hiyo alishangaa kupigiwa simu na Sam,
"Tafadhari Jeff nina mazungumzo na wewe. Naomba tuonane tafadhari"
Jeff aliogopa na kukataa ila Sam alimsisitiza kuwa hana nia mbaya na amemuita kuzungumza naye mambo mema tu.
Mwisho wa siku Jeff akakubali kwenda kuzungumza na Sam.
Kisha akamuaga mama yake,
"Haya wapi muda huu?"
"Jamani mama, yani hata nisiende kutembea"
"Haya nenda ila uwahi kurudi"
Jeff akakubaliana na mama yake ingawa mama yake alitambua wazi kuwa anadanganywa kwa muda ule kwani mwanae sio wa kurudi mapema wala nini.

Mida ile ya jioni pale kwakina Sabrina walianza kufika baadhi ya ndugu zao kwaajili ya kujiandaa na harusi ya kesho yake.
Sabrina akainuka na kumuaga mama yake kidogo,
"Nafika hapo kwa Sakina mara moja"
"Usiniletee balaa Sabrina, kesho mambo yananukia hapa. Kwa Sakina unaenda kufanya nini?"
"Kuna kitu naenda kumwambia"
"Kwanini asije yeye hapa? Kama unaenda uende na mtu"
Sabrina hakutaka kubishana sana na mama yake zaidi ya kuongozana na ndugu yake mmoja kwenda kwa Sakina.
Lengo kubwa la Sabrina lilikuwa ni kutaka kuzungumza na Jeff ila alijua wazi huyo nduguye atambania nafasi hiyo sema akaona ni vyema kama atumie ishara ya kuweza kuonana na Jeff hata badae wazungumze kwani hakutaka kumpigia simu wala kuzungumza nae kwenye simu akimuhofia Sam kuwa anaweza kufatilia mazungumzo yake.
Walipofika, walimkuta Sakina akiwa anamalizia kazi  zake za hapa na pale, na alipowaona akaanza kuongea kwa kujishuku,
"Jamani biharusi hadi umenifata jamani, mi ndio nilikuwa namalizia hapa halafu nije angalau kusalimia wageni"
"Ndiomana nimekufata ili twende wote"
Wakaongea mawili matatu kisha Sabrina akamuulizia mtu aliyemfanya aende pale,
"Na Jeff naye yuko wapi?"
"Utamuweza yule? Yani wanawake watamponza mwanangu, hata hatulii hadi namuonea huruma. Hapa hayupo sijui kaenda kwa yupi leo."
Sakina aliongea bila ya kujua jinsi gani Sabrina ameumia, na muda huo huo Sabrina akaaga na kuondoka zao.
Na walipofika nyumbani moja kwa moja Sabrina alienda kulala kwani aliona kichwa chake kikichanganyika na mawazo.

Wakati yupo kitandani akitafuta usingizi, alijikuta akitafakari
"Hivi kwanini naumia nikiambiwa kuwa Jeff ameenda kwa wanawake? Inamaana namuonea wivu? Na kama namuonea wivu basi inamaanisha kuwa nampenda. Uwiii Mungu wangu, niepushe na hili janga tafadhari maana nahisi kuchanganyikiwa tu"
Sabrina alikuwa akiwaza na kuwazua pale kitandani mpaka pale usingizi ulipomchukua.

Kulipokucha, Sabrina alikuwa wa kwanza kuamka kwani wengine walichelewa kidogo kutokana na mkesha ambao waliufanya usiku wake.
Na wao walipoamka ilikuwa ni maandalizi tu, amcpo Sabrina alipelekwa saluni kwaajili ya kupambwa na kuvaa shela.
Wakati anamalizia kupambwa, alitokea dada mmoja na kumfata Sabrina kisha akamsalimia na kujitambulisha,
"Naitwa Sara"
Sabrina naye akajitamburisha kwa jina ambapo yule dada akamwambia,
"Usijali Sabrina, mi nakufahamu tena sana tu na pia nafahamu kama unaolewa na Sam ila kilichonisogeza hapa kwako ni kuhusu jambo moja tu"
Sabrina akamuangalia kwa makini yule dada na kumuuliza,
"Jambo gani hilo?"
"Hivi unamfahamu vizuri huyu Sam anayetaka kukuoa?"
Sabrina akashtuka sasa na kumuuliza yule dada kwa makini,
"Kwanini unaniuliza hivyo dada?"
"  Ninachotaka kukwambia mimi ni kuwa, unatakiwa uwe makini sana kwani huyo Sam kashawaliza wadada wengi sana hapa mjini. Kwaheri"
Sabrina alitaka kumuhoji vizuri huyu dada ila ndio hivyo alishainuka na kuondoka.
Sabrina alitamani kughairi kuvaa lile shela ila aliamua kuheshimu mawazo ya mama yake.

Muda wa kwenda kanisani ulifika, na karibia wote wakakutanika eneo la tukio ila Sabrina hakumuona Sam wala Jeff na kuanza kuhisi kuwa ndoto aliyoiota huenda ina ukweli ndani yake na kumfanya ajawe na uoga.
Ila muda haukupita sana, Sam na wapambe wake wakaingia pale kanisani na ndoa yao ikafungwa bila pingamizi kutoka kwa mtu yeyote yule.

Ndoa ilipomaliza kufungwa pale kanisani, kama kawaida wakaenda ukumbini kwa ajili ya kusherehekea kwa kula na kunywa na kupongezana kwa pamoja.
Hadi hatua hiyo ilipofika, Sabrina alikuwa na amani sasa moyoni ingawa mashaka kiasi bado yaliendelea kuutafuna moyo wake.
Baada ya tafrija kuisha, maharusi walitakiwa kusimama ili wawaage wageni waalikwa na waweze kwenda kupumzika.
Walipokuwa wamesimama, moja kwa moja Sabrina alifatwa na Jeff kisha yule Jeff akamkumbatia Sabrina kwa nguvu na kumfanya Sabrina amshangae kwani hakuonekana tangia harusi ile ianze ndio anaonekana muda huo.
Jeff akiwa kamkumbatia Sabrina, akaanza kumwambia,
"Kuwa makini Sabrina, Sam anaujua ukweli wote"
Muda huo huo Sabrina akaanguka chini na kuanza kutokwa na damu.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa