JE HAYA NI MAPENZI!! 56: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 18, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 56:





Kisha Sabrina akarudi tena chumbani.
Alipotazama kitandani, akamuona tena amelala
akiwa amejifunika gubigubi kama sebleni.
Sabrina akajikuta akipiga kelele na kuanguka.
Kelele za Sabrina zikamshtua Sam pale kitandani na kumfanya aamke kwa kukurupuka kisha akamfata Sabrina pale chini alipoanguka huku akijaribu kumpa huduma ya kwanza.
Sabrina alipozinduka akamuona Sam akimpepea, kwanza kabisa akapumua kwa uoga huku akimuangalia Sam kwa jicho la wasiwasi na kumfanya Sam amuulize,
"Kwani tatizo ni nini Sabrina?"
"Kwani wewe Sam ni mchawi?"
Sabrina akajikuta akiropoka na kumfanya Sam amshangae.
"Mchawi? Mchawi kivipi jamani Sabrina?"
"Kwakweli Sam hapana, mi siwezi kuendelea kulala humu ndani nataka nirudi kwetu sasa hivi"
"Mbona ni usiku sana Sabrina, una matatizo gani? Sikuelewi"
"Wewe mtu gani? Kwanza una mambo ya ajabu hueleweki, unajiweka sebleni na chumbani. Sam wewe utakuwa mchawi tu"
Sam akacheka na kuanza kuhisi kitu kinachomtatiza Sabrina, kisha akamuuliza,
"Hivi Sabrina unaweza kupata ujasiri wa kuzungumza na mchawi kiasi hiko? Hivi siku ukimuona huyo mchawi katika kazi yake, utaweza hata kujikaza na kumwambia maneno hayo? Na kama ningekuwa mchawi si ningeshafanya jambo la kukusahaulisha! Najua linalokutatiza, nenda tena sebleni ukamuone aliyelala pale."
Sabrina bado alikuwa na uoga huku akinyanyuka na kumuomba Mungu kimoyo moyo kuwa amsaidie kwa wakati huo.

Sabrina akainuka na kwenda sebleni ili kujiridhisha na moyo wake, akamkuta yule wa sebleni akiwa amelala vilevile huku kajifunika shuka gubigubi.
Sabrina akasimama tu huku akisita kumsogelea, Sam akamfata Sabrina kwa nyuma na kumsogeza mpaka kwa yule mtu,
"Mfunue mwenyewe uone kama ni mimi huyo"
Sabrina bado akasita kumfunua mtu yule, ikabidi Sam amsaidie mwenyewe kumfunua.
Sabrina akashangaa kumuona kuwa ni Jeff tena amelala fofofo.
Sabrina akamuangalia Sam na kumuuliza kwa mshangao,
"Jeff amefikaje hapa? Ameingia saa ngapi? Na mbona amelala hoi sana?"
"Hayo maswali Sabrina naomba  kesho umuulize mwenyewe huyo Jeff ndio atakujibu kwa usahihi zaidi. Tafadhari turudi ndani tukalale"
Sabrina hakubisha muda huu zaidi ya kuwa mpole na kuanza kuelekea chumbani kwao.
Ila kiukweli Sabrina usingizi haukumjia kwa wakati kwani alijikuta akiwa na mawazo mengi sana.

Kulipokucha, kama kawaida Sam aliamka na kujiandaa kisha akamuaga Sabrina kuwa atarudi kwenye mida ya saa sita kumchukua kwaajili ya kwenda kanisani kwa mazoezi ya awali ya ndoa yao.
Sabrina alibaki mwenyewe sasa na kutoka tena sebleni, bado alimkuta Jeff akiwa amelala na wala hana habari.
Kwavile Sabrina alitamani sana kujua kuhusu Jeff kuwa hapo akaona ni vyema amuamshe tu.
"Wee Jeff, wewe, wewe hebu amka"
Huku akimtikisa tikisa ila bado Jeff alionekana kuwa na usingizi mzito sana na kumfanya Sabrina hata achukie kwavile lengo lake lilikuwa ni kujua kuwa imekuwaje hadi Jeff yupo pale nyumbani kwa Sam.

Baada ya muda kidogo, Jeff alimka akiwa na uchovu sana huku akijinyoosha na kukaa pale kwenye kochi, kisha akainama na kushika tama kamavile mtu mwenye mawazo mengi.
Muda wote Sabrina alikuwa akimuangalia tu, kisha akamshtua kwa kumuita,
"Wee Jeff"
Jeff naye akashtuka na kumuangalia Sabrina, kisha akainuka na kwenda kumkumbatia na kumfanya Sabrina amshangae,
"Kwani wewe Jeff una matatizo gani wewe?"
Jeff alizidi kumkumbatia Sabrina huku machozi yakimtoka, ikabidi Sabrina amwambie kwa ukali sasa,
"Wee Jeff nini?"
"Nakupenda Sabrina, nakupenda sana. Kwanini uninyanyase? Au umri wangu, au umbo langu? Nakupenda jamani"
Sabrina alimuangalia Jeff huku akitikisa kichwa kama ishara ya kumsikitikia,
"Yani wewe mtoto wewe, aliyekuroga alishakufa maana angekuwa hai angekuonea huruma kwa huu upuuzi wako unaouwaza kichwani mwako"
"Sio upuuzi Sabrina, jaribu kusoma hisia zangu. Bila wewe siwezi mimi, wewe ndio mwanamke wa maisha yangu.  Nakuhitaji wewe, nataka kuwa na wewe, simtaki mwinginewe"
Sabrina akaona kama akiendekeza kumsikiliza Jeff basi atazidi kujiweka pabaya ukizingatia pale walipo ni nyumbani kwa Sam.
"Sasa Jeff sikia, hayo maneno yako si ya kuzungumza mahali hapa. Hebu jaribu kuelewa hapa upo kwa nani na anamahusiano gani na mimi. Tafadhari sana Jeff usiniharibie"
Jeff hakuongea muda huu ila alijiinamia tena kanakwamba anaendelea kuwaza alichokuwa anawaza.
Sabrina naye aliinuka na kwenda jikoni ili kuandaa chai.

Wakati Sabrina yupo jikoni, Jeff naye akaenda jikoni kumfata Sabrina ambapo alimfata kwa nyuma na kumkumbatia,
"Hivi wewe Jeff una matatizo gani? Na hii nyumba itakushinda muda sio mrefu nakwambia. Haya niachie"
"Sawa nakuachia, ila naomba nikubusu tu"
Sabrina aliona ni kero kwa uwepo wa Jeff pale, kisha akamuacha ambusu ili amuachie.
Naye Jeff akafanya hivyo, kisha akarudi sebleni na kumfanya Sabrina aongee   peke yake pale jikoni,
"Yani huyu mtoto huyu, hata sijui nifanyeje mimi"
Sabrina alinung'unika sana kisha akaenda kuandaa chai yake na kuanza kunywa.
Muda sio mrefu Sam akawa amerudi, kisha akamwambia Sabrina ajiandae ili waende,
"Si ulisema saa sita wewe? Mbona muda bado?"
"Nimepigiwa simu kuwa tuwahi ndiomana nimekufata muda huu"
Sabrina akaenda kujiandaa na baada ya muda mfupi akawa amemaliza tayari kwa kuondoka.
"Vipi, huyu Jeff anabaki hapa ndani?"
Sabrina alimuuliza Sam, naye Sam akamjibu
"Muache tu, muda akijisikia kuondoka basi ataondoka mwenyewe"
Kisha Sam akamshika mkono Sabrina na kuondoka naye.

Wakiwa ndani ya gari, Sabrina akawaza sana kuwa ni kitu gani kimepelekea Sam kumkubali Jeff kiasi kile, akawa anawaza tu moyoni,
"Lazima kuna kitu hapa ambacho mimi sikijui. Kwani sio rahisi hivi kwa Sam kupatana na Jeff"
Muda wote mawazo yakamjaa huku akijaribu kutafakari kuwa ni kitu gani kimewapat anisha kiasi kile Sam na Jeff.
Kisha Sabrina akagundua kitu kuwa Sam amepanda gari ambayo huwa hata hatembei nayo mara kwa mara, kisha akamuuliza
"Vipi leo gari hii?"
"Aaah! Nimeikumbuka tu, nikaona ni vyema leo nayo ione mji"
"Sawa"
"Hii gari nitakupa wewe ukishajifungua"
Sabrina akatabasamu kwani kauli hiyo ilimfurahisha.

Walipokaribia kanisani, Sabrina akamuona mtu karibia na mlango wa kanisa na kuhisi wazi anamtambua mtu huyo tena si kumtambua kwa mema bali kwa mabaya,
"Sam tafadhari, pinda hii gari tukaingilie mlango ule mwingine"
"Ila mbona itakuwa kama tunazunguka sana?"
"Hapana, twende tukaingilie kule. Nina maana yangu"
Sam hakupinga zaidi ya kugeuza gari na kuelekea upande mwingine ambapo walienda kuingia kwenye geti la nyuma la kanisa hilo.
Moja kwa moja Sam na Sabrina wakaenda kwa mchungaji ili kupata muongozo.
Ambapo mchungaji alisalimiana nao na kuwauliza,
"Mbona mmewahi sana?"
"Nimepigiwa simu kuwa eti tunatakiwa kuwahi"
"Nani kakupigia simu? Maana hakuna mtu aliyepigiwa simu kuwa awahi kuja"
Sabrina akamwangalia Sam na kumwambia,
"Unaona Sam, yule mtu aliyesimama pale sio mtu mzuri pengine ndio wao wamekupigia simu. Hata sijui wana lengo gani na sisi"
"Kwani yule unamjua?"
"Mi simjui ila namkumbuka kuwa ni kati ya wale vijana wawili walionivamia pale kwangu siku ile"
Sam akashtuka, na kuamua kutoka ili akawafatilie ila Sabrina akamzuia,
"Niache Sabrina, nikashughulike nao"
Mchungaji akamuangalia Sam na kumwambia,
"Waache, Mungu ndiye atakaye shughulika nao"
Ingawa Sam alitulia kwa kufata maneno ya mchungaji ila moyoni mwake alimponda,
"Ndio shida ya walokole hii"
Ikabidi tu mchungaji awape muongozo kwavile wamewahi sana kwenda eneo la tukio kabla ya muda muafaka.
Akawaelekeza ya kufanya, kisha akawaruhusu kwaajili ya kuondoka.
Sam na Sabrina walitoka nje na kuingia kwenye gari yao kisha  wakaianza safari ya kuondoka zao.
Walipofika nje, Sam bado akataka kupeleka gari eneo lile ambalo Sabrina alimuona yule mtu,
"Tafadhari Sam, twende nyumbani. Mi nakuomba, nihurumie mimi na mtoto wetu aliyetumboni, turudi nyumbani"
Sam kama kawaida yake huwa hapendi kumkwaza Sabrina, hivyobasi akafanya safari ya wao kurudi tu nyumbani.
Walitembea kimya njia nzima hadi walipofika nyumbani na kuingia ndani ambapo bado walimkuta Jeff akiwa pale pale ndani kwao.
Sabrina akamuuliza Jeff,
"Khee hujaondoka?"
Jeff akamuangalia Sabrina na kutabasamu na kumfanya Sabrina amuulize tena,
"Kinachokuchekesha sasa?"
Sam akaingilia kati,
"Sabrina acha kumfokea mtoto, muda wake wa kuondoka ukifika ataondoka tu"
Na kumfanya Sabrina azidi kupatwa na mashaka zaidi kuwa kwanini Sam anafikia hatua hadi ya kumtetea Jeff.
Baada ya muda kidogo, Sam akamuaga tena Sabrina kuwa anatoka kidogo ila muda huu alitoka na Jeff na kumfanya Sabrina afurahi kiasi kwani uwepo wa Jeff huwa unamkosesha amani kabisa.

Nyumbani kwa wakina Sabrina hali haikuwa shwari sana kwani mama yake bado alikuwa na mawazo ya namna ya kuokoa jahazi la mtoto wake James, kwani ikiwa ukweli utakuwa wazi basi atamuharibu kisaikolojia mtoto wake huyo.
Kwahiyo aliona kuwa ni vyema ukweli usijulikane ili kuendelea kulinda heshima yake na heshima ya watoto wake wote watatu.
Wakati akifikiria mambo hayo, akapigiwa simu na wifi yake ambaye ni yeye anayeujua ukweli wa mambo kwa undani zaidi,
"Eeh wifi unaamuaje kuhusu kusema ukweli?"
"Tafadhari nakuomba hili swala niachie mwenyewe"
"Nakuachia ndio, uzuri ni kuwa nawajua fika wewe na mwanao kuwa mabingwa wa kudanganya. Mko radhi wenzenu waumie ili nyie mtunze siri"
Mama Sabrina akaona huyu wifi yake anamletea khabari za kumchanganya tu wakati kashamwambia kuwa amuachie yeye mwenyewe amalizane nao.
Kwahiyo akaamua kuikata ile simu bila ya kujua kuwa amemchukiza mpigaji.

Sabrina hakuwa na wasiwasi na pale nyumbani kwa Sam kwavile nyumba ile ilikuwa na ulinzi wa kutosha, kwahiyo Sabrina akakaa kwa uhuru zaidi, na kuendelea kufanya mambo yake mbali mbali.
Simu yake ya mkononi ikaita, na mpigaji alikuwa Sakina,
"Umewasiliana na Jeff kwa siku ya leo maana hata sielewi alipo"
"Nimetoka kuwasiliana nae muda sio mrefu, hebu kwanza nimpigie simu tena nimwambie awasiliane na wewe"
Sabrina hakutaka kumwambia Sakina moja kwa moja kama mtoto wake jana alilala hapo nyumbani kwa Sam.
Kwahiyo simu ilipokatika, Sabrina akajaribu kumpigia simu Jeff lakini hakupatikana na kuamua kumpigia simu Sam,
"Upo na Jeff hapo?"
"Ndio nipo nae"
"Naomba niongee nae"
Sam akampa simu Jeff kisha akaongea na Sabrina, na muda huo huo Jeff akamuaga Sam kuwa Sabrina kamuita kidogo kwahiyo anarudi nyumbani kumsikiliza.
Sam hakuwa na pingamizi lolote na kumruh usu kuwa aende tu.

Jeff alirudi nyumbani kwa Sam na kumkuta Sabrina,
"Kwani nimekwambia uje huku au uende kwa mama yako?"
"Huku nimekuja kukuaga tu, wala sikuja kwa ubaya"
Sabrina akamuangalia Jeff na kumwambia,
"Haya kwaheri"
Jeff akamsogelea Sabrina na kumkumbatia huku akimwambia kuwa anampenda,
"Wee Jeff nenda zako wewe usiniletee balaa mie"
"Hapana sina balaa, ila naomba unibusu"
Kisha Jeff akasogeza midomo yake karibu na midomo ya Sabrina.
Wakashtuliwa na mlio wa mlango ambapo aliyeingia alikuwa ni Sam.
Kisha Sam akawaambia,
"Msishtuke endeleeni tu nimeshajua kila kitu"
Wakajikuta wakitazamana kwa aibu.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa