JE HAYA NI MAPENZI!! 58: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 18, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 58:





Walipokuwa wamesimama, moja kwa moja Sabrina
alifatwa na Jeff kisha yule Jeff akamkumbatia
Sabrina kwa nguvu na kumfanya Sabrina
amshangae kwani hakuonekana tangia harusi ile
ianze ndio anaonekana muda huo.
Jeff akiwa kamkumbatia Sabrina, akaanza
kumwambia,
"Kuwa makini Sabrina, Sam anaujua ukweli wote"
Muda huo huo Sabrina akaanguka chini na kuanza
kutokwa na damu.
Wote wakamkimbilia Sabrina pale chini bila kujali kuwa Jeff alikuwa akizungumza naye kitu gani.
Sam alimnyanyua Sabrina na kumkimbizia kwenye gari, tena bila hata ya kuwangoja wazazi wa Sabrina, alipanda kwenye gari na kuliendesha kwa kasi sana akimkimbizia Sabrina hospitali.
Wazazi wa Sabrina nao na baadhi ya ndugu walipanda kwenye gari jingine na kuanza kulifata gari la Sam.

Walipofika hospitali, Sabrina alipokelewa na kuanza kuhudumiwa kwa haraka sana kutokana na mumewe kujulikana sana katika hospitali hiyo.
Walimpeleka kwenye chumba cha huduma kisha, Sam alibaki nje kumngoja Sabrina.
Baada ya robo saa, daktari alitoka na kumfata Sam,
"Niambie docta nini tatizo?"
"Itabidi tumfanyie operesheni maana hali ni mbaya."
"Operesheni docta wakati mke wangu ni mjamzito?"
"Ndio, inabidi tumtoe kile kiumbe"
"Mungu wangu, kwahiyo mwanangu itakuwaje? Atapona kweli?"
"Tutajitahidi    kuokoa maisha yao. Inabidi tu ukubali tuanze hiyo operesheni kwa haraka"
Sam hakuna na jinsi zaidi ya kukubali na kusaini karatasi kwaajili ya mkewe kufanyiwa operesheni.

Ndugu wa Sabrina walipotewa na Sam njiani kutokana na mwendo ambao Sam alikuwa akiuendesha, kwahiyo wakakosa uelekeo na kushindwa kuelewa pa kuelekea.
Waliamua kumpigia Sam simu ila iliita tu bila ya kupokelewa na kufanya wachanganyikiwe zaidi haswa mama wa Sabrina kwani alijihisi kamavile anaonewa kwa kutokujua hali ya mwanae wala kujua mahali alipo.
Ilibidi tu warudi nyumbani ili kusikilizia kama Sam atawapigia simu kwani walijaribu kuulizia kwa baadhi ya mahospitali ya karibu bila ya mafanikio yoyote.

Sam bado alikuwa na mawazo juu ya Sabrina, na kwavile alikuwa mwenyewe ndio akahisi kuchanganyikiwa zaidi.
Baada ya masaa mawili kupita, daktari alitoka kwenye chumba cha operesheni na kumkuta bado Sam akionekana kuwa na mawazo  sana,
"Bwana Sam, punguza mawazo. Mkeo tunamshughulikia vizuri tu. Punguza mawazo"
"Niambie anaendeleaje mke wangu?"
"Bado amelala, ila anaendelea vizuri tu"
"Na mtoto je?"
"Usijali Bwana Sam, yote hayo tutakueleza vizuri tu ngoja mambo yakae sawa"
Sam alifarijika kidogo ila bado alikuwa na mawazo kwani furaha yake ni kusikia kuwa Sabrina amepona kabisa.

Kulipokucha, Sam alimfata tena daktari ili kupata majibu yake.
"Pole sana Mr.Sam"
Sam akashtuka na kuuliza,
"Pole ya nini tena?"
"Pole ya kumsubiria mkeo usiku wote, ila napenda kukupa na hongera pia"
Hapo Sam akatabasamu kwani alijua lazima ni khabari njema,
"Niambie daktari"
"Operesheni ilienda vizuri, ila sikutaka kukwambia usiku ule kwani nilijua wazi kuwa kwa vyovyote vile ningekuchanganya tu"
"Basi niambie daktari"
"Mkeo tulimfanyia ule operesheni na kumtoa yule mtoto akiwa hai kabisa, kwahiyo napenda kukutaarifu kuwa mkeo kajifungua mtoto wa kike ila tumemuweka kwenye uangalizi maalumu kwakuwa yule mtoto ni njiti"
Mwanzoni Sam alitabasamu ila aliposikia kuwa mtoto ni njiti akanywea gafla na kuuli za kwa upole,
"Njiti kivipi?"
"Njiti kwamaana kwamba amezaliwa kabla ya miezi na hata uzito wake upo chini sana kwahiyo anatakiwa akae katika uangalizi maalumu hadi pale afya yake itakapotengemaa"  Sam akaridhika kiasi na kutaka kwenda kumuona mtoto wake ila daktari akamwambia kuwa itakuwa vyema kama ataenda kumwangalia badae kwa usalama wa mtoto huyo.
Sam alikubali kwani roho yake iliridhika sasa baada ya kusikia kuwa familia yake iko salama.
Kisha akaenda kwenye gari yake ili kuchukua simu kwaajili ya kuwataarifu ndugu zake hospitali aliyokuwepo.
Ila alipoichukua simu yake alikuta kuwa walimpigia sana simu bila kupokelewa.
Sasa alimua kumpigia kwanza mama wa Sabrina ambaye aliipokea kwa haraka sana kupita kawaida, tena hakutaka hata salamu zaidi  ya kujua mwanae alipo.
Ikabidi Sam awaombe radhi kisha akawaelekeza hospitali ambayo yupo na Sabrina na kuwaambia kuwa Sabrina amejifungua.

Joy alikuwa nyumbani kwake pamoja na Sakina muda ambao Sam alikuwa akimpigia simu.
Muda anamaliza kuongea na simu hiyo, Jeff naye alikuwa mahali pale na kumsikia mama wa Sabrina akimwambia mama yake,
"Eti Sabrina kajifungua"
Jeff naye alishtuka na kufanya wamshangae pale,
"Sabrina kajifungua?"
Mama yake akamuuliza,
"Unachoshangaa ni kitu gani?"
"Mbona mimba yake ilikuwa bado ndogo?"
"Wee unajuaje kama ilikuwa ndogo? Mwingine tumbo dogo lakini mimba ishafikia wakati wake"
Jeff ikabidi anyamaza kwani alijua wazi akiongea zaidi anaweza kumwaga mchele kwenye kuku wengi.
Basi akawaacha pale mama yake na mama Sabrina wakiondoka kwenda hospitali kumuangalia Sabrina, alichofanya Jeff ni kuwauliza hospitali yenyewe kisha yeye akaanza kurudi kwao na kumfanya mama yake amuulize,
"Vipi, wewe huendi kumuona Sabrina?"
"Nitaenda wakati mwingine, nyie tangulieni tu"
Hawakutaka kumuhoji zaidi kwahiyo wakamuacha akiondoka nao kuondoka huku Joy akikazana kumpigia simu na mumewe ajue kwavile aliamkia mahospitalini kutafuta hospitali waliyoenda.

Jeff alirudi kwao na kumtafakari Sabrina,
"Kajifungua vipi wakati miezi tisa bado? Au tayari! Inamaana kama tayari basi ile mimba sio yangu mmh!! Na kama sio yangu mbona nilimkuta bado bikira? Haiwezekani, hata sielewi jamani"
Alitamani sana kwenda hospitali kumuona Sabrina ila bado mawazo yake yakamkwamisha kufanya hivyo kwani alijihisi vibaya kama itagundulika kuwa mimba ilifikisha miezi tisa wakati yeye tangia ambake Sabrina na kumpa hiyo mimba miezi tisa ilikuwa bado haijatimia.
Alikuwa na mawazo sana kwa muda huo.

Sam akaitwa na daktari ili aweze jambo kumtazama Sabrina ingawa bado alikuwa amelala.
Sam alishukuru na kwenda chumba walichomlaza Sabrina kumuangalia.
Na alipofika karibu alimuona kama Sabrina akijigeuza hivi na kujua wazi kuwa muda wowote anaweza kuzinduka.
Sam akawa karibu zaidi na Sabrina pale, ila Sabrina aliposhtuka akaita,
"Jeff"
Na kumfanya Sam ajisikie vibaya kwavile yeye ndio yupo nae karibu halafu anashtuka na kumtaja Jeff.
Alimshangaa kuwa anamaana gani, kwavile daktari alikuwa karibu akamsaidia kumuelewesha,
"Usichukie kwa mgonjwa hivyo, mwache akizinduka vizuri atatambua anachotaka kusema ila kwasasa ni kazi bure."
"Hata kama docta, kwanini amtaje Jeff?"
Daktari akamvuta Sam pembeni kidogo ili wasiweze kumsumbua mgonjwa, kisha akamuuliza,
"Kwani Jeff ndio nani?"
"Ni dogo mmoja hivi, tena yeye ndiye aliyesababisha mpaka mke wangu akaanguka"
"Basi hilo sio tatizo, kwanza kabisa ujue kuwa mkeo alianguka na kupoteza fahamu kwahiyo anapotaka kuzinduka picha inayomjia kichwani ni tukio lililompata kabla ya kuang uka na ndiomana akamtaja huyo Jeff"
Sam akamuelewa kidogo daktari na kurudi tena kumtazama Sabrina ambaye alikuwa amesharudi katika usingizi wake.
Kisha Sam akatoka nje kwaajili ya kuwaangalia ndugu wa Sabrina ambao watafika pale hospitali.

Joy na Sakina walifika pale hospitali na kumkuta Sam aliyewapa khabari zote juu ya maendeleo ya Sabrina.
Na wote wakatamani kwenda kumuona mtoto huyo aliyezaliwa kabla ya wakati ila daktari hakuweza kuwaruhusu kwa muda ule.

Jioni ya siku hiyo Sabrina aliweza kuzinduka na ndugu zake waliweza kumsalimia.
Na yeye pia aliweza kupewa taarifa kuhusu mtoto aliyejifungua.
Akamuuliza Sakina,
"Mbona Jeff hajaja kuniona?"
"Yule mtoto ni mwehu eti anashangaa umejifunguaje wakati mimba ilikuwa ndogo. Mi nikamshushua pale hadi akarudi nyumbani mwenyewe, ila atakuja tu yule"
Mama wa Sabrina naye akamsapoti Sakina,
"Ndio lazima aje yule, na anavyompenda Sabrina tena! Sie anafanya kutuchora tu kuwa tuondoke"
Sabrina akawasikiliza pale huku akijisifu kuwa hawajui vya moyoni mwake.
Ila walipoondoka, Sabrina nae alijikuta akitafakari kuwa kwanini Jeff asiende kumuona?
"Huwa Jeff hata wamseme vipi lazima aje, imekuwaje leo?"
Sabrina hakupata jibu ila bado alikuwa na matumaini kuwa Jeff ataenda tu kumuona kwa muda wowote ule.

Jeff akiwa nyumbani kwao, mama yake naye aliwasili kutoka hospitali ambapo moja kwa Jeff aliulizia kuhusu mtoto wa Sabrina,
"Eeh na vipi mtoto wake?"
!Mtoto hatujabahatika kumuona kwavile kazaliwa njiti kwahiyo hairuhusiwi watu kwenda kumuona ona hovyo"
Jeff naye alikuwa hajaelewa maana ya mtoto njiti na kumfanya mama yake apate kazi ya kumuelezea.

Kesho yake asubuhi na mapema, Jeff aliamka na kufunga safari ya kwenda kumuona Sabrina katika hospitali aliyoambiwa jana.
Na alipofika alimkuta Sam kwani Sam alikuwa anaenda nyumbani kidogo kwaajili ya kubadilisha nguo kisha kurudi tena hospitali.
Kwahiyo Sam alipomuona Jeff akamwambia akae hapo hospitali na Sabrina kwa muda huo wakati yeye anaenda kubadilisha nguo.

Jeff moja kwa moja alimfata Sabrina pale kitandani,
"Yani wewe mtoto ni mbaya sana, loh umeshindwa hata kuja jana?"
"Nisamehe bure mamy, kuna mambo nilikuwa nayaweka sawa kwanza halafu kuna kitu unatakiwa utambue"
"Kitu gani hicho?"
"Sam kashajua kuhusu mimi na wewe, kwahiyo anachofanya sasa ni kutafuta usahidi tu kwahiyo tunatakiwa kuwa makini kupita maelezo"
"Kwahiyo wewe ndio usipokuja kuniona Sam ndio hatojua?"
"Hapana sio kiivyo, ila natakiwa kupunguza ile kuja kukuona mara kwa mara ili asitugundue"
"Wewe umejuaje kama Sam ameshajua kila kitu?"
"Siku kabla ya harusi yenu Sam aliniita na nikaongea nae mambo mengi sana ila alinikatalia kuondoka na kunifanya nirudi nyumbani kesho yake. Ila kubwa zaidi ni kuwa aliniambia hivi..."
Kabla Jeff hajasema  chochote tayari Sam alisharudi na tayari alishaingia mule wodini.
Ikabidi Jeff ajigeleshe na kuaga pale na kumfanya Sam amuulize,
"Mbona mapema sana?"
"Aah kuna vitu naenda kuvimalizia, naweza nikarudi badae kumuona"
Sam hakumbishia na kumuacha aende kisha yeye akaanza kumpa mazoezi Sabrina kama ya kumsaidia kukaa na hata kusimama ili waweze kwenda kumuona huyo mtoto wao.
Sam akamwambia Sabrina,
"Nampa jina mtoto"
"Khee hata kama bado njiti?"
"Ndio, nataka awe na jina lake kabisa mtoto wangu"
"Haya niambie, utamuita nani?"
"Nitamuita Cherry"
"Khee Cherry ndio jina gani?"
"Nina maana yangu kumpa jina hilo, hilo jina lina maana kubwa sana kwangu"
"Maana yake ni nini?"
"Muda ukifika nitakwambia maana yake, ila kuanzia sasa mtoto wetu ataitwa Cherry"
Sabrina hakuweza kubisha kwani ni yeye mwenyewe aliyempa Sam sifa ya ubaba kwa mtoto ambaye sio wake kwahiyo hakuwa na uwezo wa kukataa ukizingatia Sam tayari alishakuwa mume wake.
Ila akamuuliza,
"Kwa mfano angekuwa mtoto wa kiume ungemuitaje?"
"Ningempa hilo hilo jina la Cherry"
"Kwanini sasa?"
"Nimekwambia kuwa hilo jina lina maana sana kwangu, na ipo siku nitakwambia maana yake iwapo tu mtoto ataendana na jina lake"
Wakati wanazungumza hayo, daktari aliwafata na kuwapa taarifa kuwa mtoto anatakiwa kuongezewa damu.
"Sasa inakuwaje hapo docta?"
"Na sitaweza kuruhusu damu hiyo itoke kwa mama sababu huyo mama kashapoteza damu nyingi sana, kwahiyo itabidi tuchukue yako baba"
"Hakuna tatizo docta"
Moja kwa moja daktari akaenda maabara na Sam kwaajili ya vipimo vya damu.

Baada ya muda kidogo daktari akarudi na kumwambia kuwa damu yake na ya mtoto haviendani, daktari hakutaka kudadisi zaidi mambo ya kifamilia na kumuomba Sam atafute mtu wa kutoa damu itakayoendana na ya mtoto wao.
Sabrina alitamani ajitolee yeye ila daktari alikataa kutokana na usalama wake.
Sam akafikiria sana na kuamua kumpigia simu Jeff, na alipomwambia Jeff hakusita na kumfanya akubali kwenda hospitali kujitolea damu.
Wakati huo Sam akajiambia,
"Na leo, ndio nitajua ukweli wa mambo"
Jeff alifika hospitali na kupelekwa maabara, akapimwa damu ikaonekana inaendana kabisa na mtoto hivyo wakamtoa damu kwaajili ya kwenda kumuongezea mtoto.
Jeff alipotoka maabara akafatwa na Sam, kisha akamwambia
"Sikukuuliza wewe ukakataa?"
Jeff akashikwa na kigugumizi cha kujibu.

JE HAYA NI MAPENZI!! 59:

Jeff alifika hospitali na kupelekwa maabara,
akapimwa damu ikaonekana inaendana kabisa na
mtoto hivyo wakamtoa damu kwaajili ya kwenda
kumuongezea mtoto.
Jeff alipotoka maabara akafatwa na Sam, kisha
akamwambia
"Sikukuuliza wewe ukakataa?"
Jeff akashikwa na kigugumizi cha kujibu.
Sam akamuangalia Jeff kwa makini huku akingoja jibu ila bado Jeff hakuweza kutoa jibu kwani alikuwa akijiuma uma tu.
Wakati Sam akingoja jibu kutoka kwa Jeff, walifatwa na daktari pale walipokuwa wamesimama, kisha daktari akamwambia Sam,
"Samahani, mkeo anakuhitaji mara moja"
Sam hakupuuzia wito wa mkewe na kuamua kumuacha Jeff mahali pale kisha kwenda mahali alipo mkewe.

Alimkuta Sabrina akiwa amejitahidi na kukaa kitandani mwenyewe bila ya kusaidia na mtu.
"Kheee natumaini sasa umeanza kupata unafuu hadi unaweza kukaa mwenyewe!"
"Ndio, kwanza nina hamu na mwanangu, nimuone, nimnyonyeshe na kila kitu"
"Haya, imekuwa vyema damu ya kumuongezea mtoto imepatikana"
Sabrina akajifanya kushangaa,
"Khee jamani, nani kapatikana kujitolea hiyo damu!"
"Ni baba yake"
Sabrina akashtuka,
"Baba yake! Kivipi?"
"Ni Jeff ndio kajitolea, sasa Jeff nae si kama baba tu!"
"Hapana, Jeff hawezi   kuwa na sifa ya ubaba kwa mtoto wetu, ila anaweza kuwa mjomba. Au kiswahili kinakupiga chenga mume wangu?"
Huku akijichekelesha na kumfanya Sam amuangalie tu, kisha na yeye akajiwa na hoja kwenye akili yake na kumuuliza Sabrina,
"Sawa, mimi sijui kiswahili ila vipi wewe unakijua? Jeff anakuita wewe mama mdogo, iweje sasa mwanao amuite Jeff mjomba? Kwani mjoba si kaka wa mama! Je wewe Jeff ni kaka yako?"
Sabrina akajiona wazi kuwa kachanganya mada, na ili kupotezea malengo ya Sam akajifanya ameanza kujisikia vibaya.
Akajishika kiuno na kujifanya kama anataka kujilaza huku akilalamika kwa Sam,
"Sam, nisaidie baba kiuno kinaniuma sana. Nisaidie, oooh kiuno mimi, kinaniuma jamani"
Ikabidi Sam aanze kumsaidia Sabrina, mpaka akaweza kumlaza kisha akamwambia,
"Ngoja nikamuite daktari"
"Hapana, usiende kumuita kwanza. Ngoja nijiangalie kwa muda kidogo"
"Pole sana mke wangu"
Kisha Sabrina alidai kuwa anataka kupumzika kidogo, hivyo Sam akaamua kumuacha ili angalau apate muda wa kupumzika.

Sam alikuwa na harakati sana ili kuhakikisha kuwa Sabrina na mtoto wao Cherry wanakuwa salama kabisa.
Alipotoka pale hospitali moja kwa moja alienda kwa mtaalamu wa kisaikolojia ili angalau ampe ushauri kidogo kwani hata akili yake ilikuwa ikifanya kazi ndivyo sivyo.
Alimkuta yule mtaalamu kama kawaida na kuanza kumueleza kinagaubaga tatizo lake ili ampe ushauri.
Mtaalamu huyo alijulikana kwa jina la Ayubu.
"Kwakweli naomba tu ushauri wako dokta"
"Bwana Sam, ngoja leo niongee jambo hili. Tangu nimekufahamu, kipindi hiki umekuwa ukija mara kwa mara kuomba ushauri ila tatizo ni moja, kwanini maelezo yako huwa yanapinda pinda?"
"Unamaana gani mtaalamu?"
"Hakuna siku uliyowahi kunieleza matatizo yako moja kwa moja nikakuelewa. Kiukweli Bwana Sam huwa unaniacha kwenye maswali pia, kwanini huwezi kuwa wazi katika kuelezea   tatizo lako?"
Sam akainuka na kuondoka kwani aliona kuwa huyu mtaalamu anataka kuyapekenyua na matatizo yake ya ndani.
Tena aliondoka bila kuaga huku akijiambia,
"Nitakuwa najishauri mwenyewe, sio lazima wanishauri wao"
Alipanda gari yake na kuondoka.
Njiani alimuona Francis, kijana ambae alikutana nae kabla ya ndoa yake na kumpongeza sana kwa kumpata Sabrina.
Sam akasimamisha gari yake mbele ya Francis ili apate kumsalimia, ambapo alishuka na kumsalimia vizuri sana.
"Hongera kaka, nasikia mke wako kajifungua"
"Ndio, ila mtoto bado ni njiti"
"Aah, Mungu atamsaidia tu. Ila natumaini mwanao atakuwa mrembo kama mama yake"
Sam akatabasamu tu, na kumfanya Francis aendelee kuongea,
"Tena hongera kwa kuitimiza ndoto ya Sabrina. Natumaini wewe ni mwanaume wa pekee kwake, na tena umepata mwanamke wa pekee na muaminifu"
Sam akaitikia ila aliamua kuagana pale na Francis ili kuondoka na kuepusha kusongwa na mawazo zaidi juu ya Sabrina.
Ila hata alipokuwa anaendelea na safari yake bado sauti ya Francis ikimsifia Sabrina ilirudi katika akili yake na kumfanya ajiulize maswali na kujijibu mwenyewe,
"Sabrina ni mwanamke aliyetulia, mbona kabeba mimba nje ya ndoa tena kwa mwanaume asiye mumewe? Eti alibakwa, mbona kama anamfahamu mbakaji na kupatana nae? Inawezekana ndiye ampendaye? Ila kwanini asiwe naye? Na kwanini aseme alimbaka? Nadhani alitaka mwenyenye. Aaaaah!!!"
Alijikuta akipiga kelele na kufunga breki mbele ya mtu ambaye ilibaki kidogo tu amgonge.
Sam akashuka kumuomba msamaha, ambapo mtu mwenyewe alikuwa ni mdada.
"Samahani sana dada yangu, akili yangu haipo sawa"
"Nimekusamehe ila uwe makini maana ungenigonga hata sijui ningekuwa wapi muda huu"
Sam akaomba kumpa lifti yule dada na kumpeleka anapoelekea.
Ambapo alimpeleka hadi eneo husika kisha kumpa mawasiliano yake na kumuaga.
Ila kabla hajaondoka, yule  dada akamuita tena Sam,
"Samahani kaka, hujanitajia jina lako na wala langu hulijui. Tumetembea kwenye gari kama mabubu, mimi naitwa Neema. Nani wewe mwenzangu?"
"Mimi naitwa Sam"
"Sawa Sam, tutazidi kuwasiliana"
Sam akamuaga yule dada tena na kuondoka ambapo yule dada alijikuta akimuangalia tu Sam hadi alipotokomea na gari yake.

Sabrina akiwa pale hospitali, ndugu zake walienda tena kumuona na kuondoka ila alishangaa kwa kutokumuona Sam na bila ya kupata simu yake.
"Mmh! Huyu Sam ananipa mashaka usiku na mchana. Kwanini asinipigie simu? Au bado anaendelea na kisirani chake?"
Ila hakupata jibu, hadi usiku sana unaingia Sam hakutokea pale hospitali na kumfanya Sabrina alale huku kichwani mawazo yamemtawala na kuumiza kichwa chake.

Asubuhi na mapema, alifika pale mama wa Sabrina ili kumpelekea mwanae uji.
"Nadhani leo nitatoka mama"
"Na mtoto je?"
"Mtoto hawezi kutoka, docta kasema eti afadhari afikishe hata mwezi kwenye kale kachumba ndio turudi nae nyumbani"
"Basi na wewe itakuwa ngumu, yani upo tayari wewe ukalale nyumbani halafu mwanao alale hospitali? Unaweza hayo Sabrina?"
"Mama, nimechoka kukaa hospitali. Naona watu wamenichoka"
Sabrina akainama na machozi yakamtoka na kumfanya mama yake amuulize,
"Nani amekuchoka mwanangu? Mimi nikuchoke? Hata dunia nzima ikukimbie mimi siwezi kukuacha mwanangu. Kuwa na roho ya umama, usimuache mwanao hapa. Natumaini baada ya wiki tu atakuwa anaendelea vizuri na tutaenda nae nyumbani. Hakuna wa kukuchoka mwanangu"
"Sam kanichoka mama, jana kaondoka hajaniaga na hadi leo hajaja"
"Usimlaumu mwanangu, Sam anakupenda sana. Na hata hivyo mimi ninakupenda mwanangu"
Ikamlazimu Joy siku hiyo ashinde hapo hospitali kumfariji mwanae.

Kwenye mida ya saa saba mchana, Sam alishtuka kutoka usingizini na kujishangaa.
Alipoangalia mida na kuona kuwa ni saa saba mchana ndio akajishangaa zaidi,
"Yani nimelala mpaka muda huu? Kwanini lakini?"
Akajaribu kuvuta kumbukumbu, akagundua wazi kuwa ni uchovu ndio uliomfanya alale mpaka muda huo.
Alikumbuka kuwa, alikesha sana hospitalini kama kwa siku tatu mfululizo bila ya kupata muda kamili wa kulala. Na vilevile jana yake baada ya matukio yote alijikuta akipita baa na kunywa pombe ili kupunguza mawazo na hiyo ndio imemfanya aamke kesho yake saa saba mchana.
Akakumbuka kuwa Sabrina yupo hospitali na anahitaji sana uwepo wake, hivyo akainuka na kwenda kuoga haraka haraka ili akamuwahi Sabrina hospitali.

Muda ulizidi kwenda na kumfanya Sabrina azidi kukosa raha huku akijiuliza maswali mengi mengi kuwa amemkosea nini Sam mpaka kutokwenda kumuona tena.
Ingawa mama yake alikuwa pale kumuangalia na kujaribu kumpotezea mawazo ila yeye alikuwa akifikiria tu kuhusu Sam ukizingatia hata Jeff alikuwa akienda hospitali hapo kwa machale kwani  naye alikuwa akihofia uwepo wa Sam mahali pale.
Baada ya muda kidogo, Sam aliwasili kwenye ile wote aliyolazwa Sabrina.
Ila Sabrina alimuangalia tu bila ya kumfurahia kwani alishawaza hadi kuchoka.
"Samahani mke wangu, kuna mambo yaliingiliana kidogo"
Sabrina bado alimuangalia tu Sam bila ya kusema kitu,
"Tena ngoja nikamuangalie na mtoto kidogo"
Sam akainuka na kwenda kwa daktari ili ampeleke chumba alichowekwa mtoto wao akamuone.

Sabrina bado hakuwa na raha kwani hofu ilimzidia.
Muda kidogo Sam akarejea,
"Daktari kasema, kwa hali inayoendelea kwa mtoto wetu anaweza kuturuhusu wiki ijayo turudi naye nyumbani"
Sabrina akaitikia kwa kutikisa kichwa na kumfanya Sam amuulize,
"Vipi mbona hivyo, umechukia?"
"Hapana nimefurahia"
"Mbona unaongea kwa unyongea hivyo? Nakupenda Sabrina, nakupenda mke wangu. Kama kuna mahali nimekosea tafadhari nisamehe"
Sabrina akatabasamu kidogo baada ya kusikia kuwa anapendwa na kumfanya sasa aweze kupata nguvu ya ziada ya kuweza kuzungumza na Sam.
"Ila muda mwingine ukiondoka uwe unaniaga."
"Kama ni hilo hata usijari, nitakuwa nakuaga jana hata sijui nilipitiwa na kitu gani"
Mama wa Sabrina alipofika na kuwakuta wakitabasamu naye akafurahia hali ile.

Baada ya wiki kuisha, hali ya mtoto wao ilikuwa nzuri na wakaruhusiwa kurudi nae nyumbani na kupewa masharti ya namna ya kuishi naye ili wasiweze kumuathiri kwa chochote.
Sabrina alifurahi kwavile alishachoka kukaa pale hospitali.
Safari ilikuwa ni moja kwa moja hadi nyumbani kwakina Sabrina ili akaweze kupata uangalizi wa karibu zaidi kutoka kwa mama yake.

Walipofika nyumbani, shangazi wa Sabrina naye alikuwepo pale akingoja ujio wao na kumpokea mtoto wao na kwenda kumuweka ndani mahali walipo shauriwa na daktari.
Shangazi wa Sabrina alianza kumsifia mtoto yule,
"Aah umejifungua mtoto mzuri sana, mmempa jina gani?"
"Anaitwa   Cherry"
"Nani kampa jina hilo?"
Akadakia mama wa Sabrina,
"Baba wa mtoto ndio kampa hilo jina"
"Mmh! Nikiwatajia jina ambalo baba wa mtoto alitaka kumpa huyu mtoto mtakaa nyie hapa? Ngoja ninyamaze tu"
Sabrina alikuwa kimya sasa huku akiwaza kimoyo moyo jinsi anavyochukizwa na maneno ya shangazi yake kwani mara zote anahisi kuwa anataka kumuharibia tu.

Sabrina aliendelea kumuhudumia mtoto wake huku akiwaza maisha yake pia yatakavyokuwa na huyo Sam kwani amejikuta mara nyingi akishindwa kumuelewa Sam na zaidi ni kuwa akishindwa kumuelewa kuwa anajua nini na anataka nini kutoka kwake.
Sam alipeleka vitu vingi sana vya mtoto ikionyesha wazi ni jinsi gani anavutiwa na mtoto huyo pia ni jinsi gani anampenda.
Muda mwingi kwa kipindi hiko Sam alikuwa akishinda pale nyumbani kwakina Sabrina kwa lengo la kuwa karibu na familia yake.

Sam siku hiyo kama kawaida, alitoka nyumbani kwake na kufunga safari hadi kwenye duka la vitu vya watoto ili amnunulie mtoto wao baadhi ya vitu na kumpeleke.
Wakati yupo nje ya duka akitaka kuingia akasikia mtu akimuita,
"Sam"
Sam akageuka, akamuona mdada kwenye daladala akiwa amekaa kwenye kitu cha mbele.
Yule mdada akatabasamu na kumpungia mkono Sam wakati ile gari ikiondoka.
Sam alijaribu kuvuta kumbukumbu ya sura ya yule mdada kuwa alimuona wapi ila kumbukumbu hakuipata kabisa na kumfanya aingie mule dukani na kuendelea na mambo mengine.

Alichagua vitu vya kumchukulia mwanae kisha akavilipia na kuanza kuondoka navyo.
Wakati anatoka, akakutana na mtu ambaye hakumfahamu kwa wakati huo ila huyo mtu alionekana kumfahamu Sam na kumsalimia,
"Hebu nikumbushe, tumewahi kuonana wapi?"
"Hata nikikukumbusha huwezi kunikumbuka Mr. Sam ila kwa kifupi ni kuwa hunifahamu ila mimi nakufahamu"
Sam akamshangaa na kumuuliza tena,
"Unanifahamu kivipi?"
"Nitakwambia tu siku nikipata muda wa kutosha. Ila tunza jina langu kwenye akili yako, naitwa Musa"
Kisha yule mtu akaingia mule dukani na kumuacha Sam aende.

Sam alifika na kumfata Sabrina na kumkabidhi vile vitu vya mtoto, ila muda huo huo akapigiwa simu kuwa anahitajika ofisini.
Sam akamuaga Sabrina pale na kuisahau simu yake pale pale kwenye vitu vya mtoto, kisha akaondoka.
Sabrina akaisikia ile simu ya Sam ikiita, akaichukua na kuangalia, namba ilikuwa ni mpya na kumfanya Sabrina ashindwe kuipokea.
Ile simu iliita hadi kukatika, mara ukaingia ujumbe mfupi wa maneno.
Sabrina akafungua na kusoma.
Alipomaliza kusoma alihisi kubanwa na tumbo kwani ujumbe ulimtisha.

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!! 60:

Ile simu iliita hadi kukatika, mara ukaingia ujumbe
mfupi wa maneno.
Sabrina akafungua na kusoma.
Alipomaliza kusoma alihisi kubanwa na tumbo
kwani ujumbe ulimtisha.
Sabrina akainuka na kwenda kujisaidia, kisha akarudi tena chumbani kwake na kushika ile simu, huku akirudia rudia ule ujumbe uliosema,
"Mpenzi Sam, nimefurahi sana kukuona leo. Mwaah"
Alikuwa akijiuliza mara mbili mbili,
"Inamaana Sam anamwanamke mwingine? Inamaana mimi hanipendi hadi anaenda kuonana na huyo mwanamke?"
Alijikuta wivu ukimjaa hadi kupitiliza na kuona kamavile amejiingiza kwenye shimo na kuanza kuwaza mambo mbali mbali,
"Ama kweli, aliyesema hakuna mwanaume wa peke yako duniani hakukosea"
Roho yake ilimuuma sana na kumfanya akose raha kabisa.
Muda kidogo, alifika Sakina kwa lengo la kumsalimia Sabrina,
"Mbona leo huna raha mdogo wangu?"
"Hamna dada, sijisikii vizuri tu"
"Acha kuwa na mawazo mdogo wangu, mume unae tena mzuri tu, anakupenda, anakujali na kila kitu. Angalia wenzio, mfano mimi, mume alishanikimbia tena bila hata sababu. Najitahidi kumuweka kwenye njia salama mwanangu Jeff ili asifate tabia za baba yake lakini naona kama juhudi zangu zinagonga mwamba"
"Kwanini dada?"
"Tabia ya Jeff haieleweki kabisa, sijui hata anataka mwanamke wa aina gani ili atulie nae. Nimeshaongea hadi mdomo kukauka ila huyu mtoto hanisikii kabisa"
Sabrina akategesha sikio vizuri ili kujua kama tabia ya Jeff imebadilika kutoka ile anayoijua yeye.
"Hebu niambie vizuri dada, kwani kafanyaje?"
"Leo alikuja yule binti wa kuitwa Dorry, yani mwanangu alivyomuacha pale nyumbani hadi huruma. Sijui hata ameenda wapi"
"Usijali dada, Jeff anasumbuliwa na ukuaji"
Kisha akambadilishia mada ili asije kuongea na mengineyo bure.

Sam alipokuwa ofisini, akagundua kuwa simu yake hakuwa nayo na kuanza kujiuliza kuwa ameiacha wapi,
"Au nimeiacha pamoja na vile vitu vya mtoto nilivyompa Sabrina?"
Aliamua kutumia simu yake ya mezani pale ofisini na kumpigia simu Sabrina  ili kujua kama simu yake ipo kwa Sabrina, ila alipiga bila ya kupokelewa na kuamua kupiga simu yake mwenyewe ambayo nayo ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.
Akazidi kujipa jibu kuwa lazima itakuwa ameisahau kule kwa kina Sabrina.
Akaweka vitu sawa na kuamua kuondoka ofisini pale kwa lengo la kwenda kuifata simu yake.
Wakati ameondoka, njiani akagundua kuwa gari yake inakaribia kuisha mafuta na kuamua kwenda kwenye kituo cha mafuta cha karibu na pale kujaza kwanza gari lake.
Wakati yupo pale kwenye kituo cha mafuta, kuna mtu alimuita,
"Sam"
Na Kumfanya Sam ashuke kwenye gari yake na kumfata yule mtu,
"Mambo Sam"
"Salama tu"
"Mbona unaniangalia kama vile hunijui?"
"Samahani kwakweli, hebu nikumbushe nilipokuona"
"Mimi naitwa Neema, kuna siku ulitaka kunigonga na gari yako"
Sam akavuta kumbukumbu na kumkumbuka Neema,
"Aaah, nishakukumbuka tayari. Na si ndio wewe ulinipungia mkono ukiwa kwenye gari?"
"Ndio ni mimi Sam, nimefurahi sana kukuona."
"Basi vizuri Neema, tutazidi kuwasiliana"
Sam akaanza kuondoka akifata gari yake, naye Neema akamfata nyuma na kumwambia,
"Sam, tafadhari naomba unipe lifti na leo"
"Hilo halina tatizo, panda tu kwenye gari twende"
Neema alipanda kwenye gari ya Sam na safari ikaendelea.

Walipokuwa ndani ya gari Neema aliamua kuanzisha maongezi baada ya kuona kuwa Sam yupo kimya sana,
"Hivi Sam unaonaje tukapanga siku tukae pamoja na kubadilishana mawazo?"
"Hilo ni wazo jema, ila muda nao unabana sana"
"Basi hakuna tatizo, siku ukiwa na muda tu niambie halafu mimi nitakuja ulipo"
"Sawa nitakujuza, usihofu juu ya hilo"
"Asante Sam, unaonekana kuwa mkarimu sana. Hongera kwa hilo."
Sam akamfikisha Neema mahali alipokuwa anaenda kisha na yeye akaendelea na safari yake.

Sabrina alipomaliza maongezi na Sakina aliamua kurudi tena chumbani kwake, ambapo alikuta simu yake ikionyesha kuwa ilipigwa bila ya kupokelew a. Alipoiangalia ile namba ilikuwa ni namba ya ofisini kwa Sam ambapo aliamua kuipiga na yeye ila haikupokelewa pia.
Akaachana nayo huku kichwani akiwaza kuwa lazima Sam atakuwa na mwanamke na ndiomana hayupo ofisini.
Akaiweka ile simu pembeni, baada ya muda mfupi akasikia ujumbe mfupi ukiingia kwenye simu ya Sam.
Akaichukua na kuufungua ule ujumbe,
"Mpenzi Sam, asante kwa ukarimu wako. Nashukuru kwa kunifikisha nyumbani"
Roho ya Sabrina ikamuuma zaidi ya mara ya kwanza kwani ule ujumbe ndio ulimthibitishia wazi kuwa Sam alikuwa na mwanamke ambaye ndio huyo alikuwa akimshukuru kwa maneno matamu.
Sabrina akakosa raha zaidi na kumfanya azidi kuumwa na kichwa.

Sam alipokuwa anaendelea na safari yake, akaona eneo watu wamejaa sana na kuamua kusimamisha gari yake.
Na alipoangalia vizuri akagundua kuwa eneo lile kuna ajali imetokea.
Sam akashuka na kusogea eneo la tukio, alipomuangalia mtu yule aliyepata ajali aliona wazi kuwa ni mtu anayemfahamu kabisa, ikabidi asogee pale na kuamua kumsaidia.
Wakasaidiana na baadhi ya watu kumpakia yule mtu kwenye gari yake na kumuwaisha hospitali.
Walifika hospitali na moja kwa moja akapelekwa kwenye huduma.
Ikabidi Sam ajaribu kutafuta simu ya yule mtu kisha akamuomba daktari simu na kuanza kuangalia namba kwenye simu ya yule mgonjwa na kuwapigia ndugu wa mtu yule kwenye simu ya daktari.
Alipomaliza ikabidi akae sasa akingoja ndugu wa yule mtu wawasili.
Muda huo akaamua kumpigia simu Sabrina pia kwa kupitia ile simu ya daktari ili kumjulisha kuwa yupo hospitali,
"Sabrina, Sam anaongea hapa. Kuna tatizo limetokea na sasa nipo hospitali na sijui kama nitaweza kuja huko leo."
Sabrina akasonya na kukata ile simu, na kumfanya Sam atikise kichwa kama ishara ya kusikitika,
"Yani hawa wanawake bhana, basi hapo kashaniwazia mabaya wakati niliyemsaidia ni rafiki yake mwenyewe, ila upo muda ataelewa tu."
Sam alijisemea bila ya kujua kinachoendelea.

Kabla Sabrina hajapokea simu kutoka kwa Sam, alikuwa akiwaza sana na moyo kumuuma sana juu ya jumbe ambazo aliziona zikiingia kwenye simu ya Sam.
Hata hivyo aliona usiku ukijongea na kuona kuwa kuna uwezekano wa Sam kutokufika hapo kwa siku hiyo hadi kesho.
Wakati akitafakari hayo, kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Sam kwa namba ile ile,
"Mpenzi ni baridi sana leo, natamani uje ili uwe karibu yangu nipate joto lako"
Na baada ya muda mfupi ndio akapata ile simu kutoka kwa Sam kuwa hatoweza kwenda siku hiyo.
Sabrina akaoanisha matukio na kuweka kuwa tukio moja huku akiamini kuwa Sam lazima ameenda kulala na huyo mwanamke.
"Huyu Sam, ameishi na mimi siku zote, hajawahi kulala na mimi. Sijui huwa ananionaje? Leo hii ananidanganya mimi kuwa yupo hospitali kumbe yupo na mwanamke!!"
Sabrina akajikuta akitokwa na machozi ambayo hakuyatarajia ila yote ni kutokana na wivu ambao ulikuwa umeikamata roho yake kwa wakati huo.
Alijaribu kulala ila usingizi haukumjia, alikuwa akimtazama tu mtoto wake huku akiwaza maisha yake.

Ndugu wa yule aliyepata ajali walifika, wa kwanza kabisa alikuwa ni Francis ambaye alimshukuru Sam kwa kumsaidia ndugu yake,
"Kumbe huyu ni ndugu yako?"
"Ndio ni ndugu yangu, anaitwa Fredy"
"Niliwahi kumuona mara kadhaa akimleta Sabrina pale ofisini na ndiomana nikamkumbuka ila sikujua kama ni ndugu yako kwakweli"
"Sasa namba yangu ukaipata vipi na kuanza kunipigia?"
"Niliangalia simu yake nikaona jina kaka, ndiomana nikapiga na hata sikujua kama naongea na wewe"
Francis akamshukuru pale Sam kwani Fredy angeendelea kushangaliwa pale alipopata ajali basi angeweza kupoteza hata maisha.
Sam hakuweza kuondoka na kwenda kwakina Sabrina kwavile muda ulikuwa umeenda sana, hivyo akangoja pakuche ili aweze kwenda.
Na hakutaka kupoteza muda kwani kulipokucha tu akaamua kuianza safari ya kwenda kwakina Sabrina, hakutaka kupitia mahali popote zaidi ya kufika hapo.

Sabrina nae alikuwa akilala kidogo na kuamka hadi panakucha kwani mawazo yalimjaa sana kwenye akili yake.
Na muda kidogo akasikia mtu akigonga mlango.
Sabrina aliinuka na kwenda kufungua, mgongaji alikuwa ni Sam.
Sabrina alimuangalia kutoka juu hadi chini kisha akamuuliza,
"Umefata nini asubuhi yote hii?"
"Nimekuja kuwaona"
"Kuwaona wakina nani?"
"Wewe na mwanangu"
"Ili iweje?"
"Ndio maswali gani hayo Sabrina jamani?"
"Sio maswali gani, nisubiri hapo hapo"
Sabrina akafunga mlango na kumuacha Sam pale nje, baada ya muda kidogo akarudi kisha akamkabidhi Sam simu yake na kumwambia,
"Nenda kwako ukaoge kwanza ndio uje uongee na mimi, huwezi kuja kumshika mwanangu na mauchafu yako kutoka kwa mwanamke wako. Usije ukambemenda bure mwanangu. Kwaheri"
"Kivipi Sabrina?"
Sabrina aliingia ndani na kubamiza mlango na kumuacha Sam akiwa ameduwaa pale nje.

Sam akaamua kupanda gari lake na kuelekea nyumbani kwake huku akijiuliza kuwa kosa lake ni kitu gani hadi kufikia hatua ya kufungiwa mlango vile na Sabrina,
"Kwani nimemkosea nini huyu mwanamke jamani? Yani kutokwenda jana usiku tu? Si nilimwambia kama kuna matatizo na nipo hospitali, yani kashindwa hata kuniuliza ilikuwaje mmmh hapa mwanamke sina kwakweli."
Sam alijiwazia hadi anafika nyumbani kwake.
Akaamua kwenda kuoga ili akirudi tena kwakina Sabrina awe msafi ili asimkere tena.

Sabrina alitafakari na kuoanisha matukio vizuri sasa,
"Amekuja alfajiri na nguo zile zile za jana, inaonyesha wazi alilala kwa yule mwanamke kweli. Kwanini Sam ananifanyia hivi lakini, kama hanitaki si bora aniambie tu kuliko kunifanyia vituko namna hii"
Akaamua kumpigia simu Sakina ili aweze kuongea na Jeff,
"Hivi Jeff yupo?"
"Yupo ndio, ila jana karudi amechoka sana sijui hata alikuwa wapi. Yani huwezi amini hadi muda huu bado kalala"
"Sawa, akiamka basi mwambie aje maana nina shida naye sana"
Sakina alikubaliana na Sabrina lakini Sabrina alimuita Jeff si kwasababu alikuwa na shida naye kweli ila ni kwavile alitaka kumuona tu ili apunguze maumivu ya moyo wake kwa siku hiyo.

Jeff alipoamka, mama yake akampa ujumbe aliopewa na Sabrina na kumfanya Jeff atabasamu kwa kukumbukwa na Sabrina.
Kisha akaamka na kwenda kuoga ili aweze kwenda kumuona huyo Sabrina.

Sam naye alipomaliza tu kijiandaa akaianza safari ya kwenda kwa wakina Sabrina.
Njiani akamuona shangazi mkubwa wa Sabrina na kuamua kusimamisha gari,
"khee shangazi za siku"
Wakafurahiana pale na ikaonyesha wazi kuwa shangazi naye alikuwa akienda kumuona Sabrina na kumfanya Sam afurahie kuongozana nae kwani safari yao ilionekana kuwa ni moja tu.

Jeff alienda kwakina Sabrina na kumkuta Sabrina akiwa chumbani kwake na mtoto.
Naye Jeff akaingia huko kumsalimia,
"Nimeambiwa kuwa una shida na mimi sana"
Sabrina akatabasamu, na kabla hajaongea kitu akasikia mama yake akiwakaribisha watu na kumfanya asikilizie vizuri.
Wale watu waliingia mpaka chumbani kwa Sabrina na kumfanya Sabrina afurahi kwavile aliyeingia alikuwa ni shangazi yake mkubwa.
"Jamani shangazi Penina, karibu sana"
Wakafurahi na kusalimiana, kisha Penina akakaa na kupewa mtoto ili amshike kidogo.
Penina alipomshika yule mtoto, alimuangalia kisha akamuangalia Jeff na kusema,
"Jamani huyu mtoto kafanana na huyo kijana kama mwanae vile"
Wote walimuangalia Jeff ili waone ufanano wake na mtoto.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa