JE HAYA NI MAPENZI!! 55: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 18, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 55:






Shangazi wa Sabrina, akamwangalia Sabrina na
kumwambia,
"Umeona, mficha maradhi kifo humuumbua"
"Una maana gani shangazi?"
"Mama yako hapo ameshachanganyikiwa"
Sabrina akageuka na kumuangalia mama yake, mara
gafla mama yake akaanguka chini.
Ikabidi Sabrina amkimbilie mama yake pale chini alipoanguka.
"Vipi mama?"
Huku akimsaidia kuinuka,
"Hata sielewi, yani nimepatwa na kizunguzungu cha gafla tu"
"Pole sana"
Na wengine wakasogea huku wakimpa pole na kumwambia kuwa huenda ikawa malaria.
Baada ya muda mfupi, baba wa Joyce aliwaaga kidogo pale ndani kuwa kuna mtu anamfata kwenye kituo cha daladala, Deo akamuuliza,
"Kwanini usiagize vijana?"
"Huyo mtu ni muhimu sana anione mimi"
Ikabidi tu wamruhusu aende ambapo walikaa na kumsubiri kwa muda mrefu bila ya kupatikana hadi mkewe akapatwa na wasiwasi,
"Hata sielewi amepatwa na kitu gani jamani, simu yake haipatikani, mambo ya hapa hatujayamaliza. Hata sielewi"
Deo akaamua kutoa maamuzi kuwa watarudi siku nyingine kwavile kisingefanyika kitu wakati baba mzazi wa binti wanaetaka kumchumbia hayupo.
Ikabidi waage na kuruhusiwa tu kuondoka kwa muda huo ili kuendelea na mambo yao mengine ingawa muda tayari ulikuwa umeenda sana.

Walipofika nyumbani, James akaamua kuondoka kwani alifadhaika kwa kitendo cha baba mkwe wake kuwaacha njiapanda.
Sabrina nae hakuwa na usemi zaidi ya yeye kubakia pale kwao kwa lengo la kumuangalia mama yake kwani alihisi kuwa huenda akawa na malaria.
Muda huo shangazi yao alikuwa naye ameshaondoka.
Sabrina alikaa na kuzungumza na mama yake kidogo,
"Kwani mama, shangazi anajua nini kuhusu wewe?"
"Tena mwanangu, ngoja nikwambie kitu. Huyo shangazi yako achana na maneno yake yatakuchanganya tu. Kwanza tambua hili, huyo shangazi yako aliugua sana kipindi cha ujana wake. Baba yako hupenda kumtumia kwenye mambo kama haya sababu anampenda tu ila akili za huyo shangazi yako si njema"
Sabrina alijidadisi na akili yake na kupata jibu kuwa huenda maneno ya mama yake yana ukweli ndani yake kwani hata yeye binafsi inakuwa ngumu sana kumuelewa shangazi yake huyo.

James alipokuwa ameenda kwa mtu aliyemuita, akaanza kuambiwa maneno ambayo yalimpa mashaka na kumfanya ashindwe kurudi nyumbani kwake,
"Hivi wewe hujiulizi kwanini unafanana na yule kijana kiasi kile? Au bado unajidanganya na ile kauli kuwa duniani wawili wawili? Hujiulizi kwanini yule kijana kapewa jina linalofanana na la kwako? Mi ukweli siujui ila kuna matukio ambayo nimeyafatilia na yakafanya nigundue kitu"
James ambaye ni baba wa Joyce alitafakari bila ya majibu ya haraka, ingawa huyu mtu aliyemuita alimruhusu kuondoka ila bado James hakuondoka kwavile moyo wake ulikuwa na maswali mengi bila ya majibu.

Mama wa Sabrina alipokuwa nyumbani na mumewe, aliamua kumueleza hali halisi kiunaga ubaga ili ajue jinsi gani watasaidiana,
"Ila Joyce, si tulikubaliana kuwa kuwa James ni mtoto wangu?"
"Ndio natambua hilo Deo"
"Sasa tatizo liko wapi?"
"Hatuja mtendea haki James, hebu jaribu wewe kufikiria kuwa leo  hii watoto wako wanaoana, je utajisikiaje?"
"Ila huyo James hajui kama huyu ni mtoto wake"
"Ndio hilo kosa tulilolifanya Deo"
"Sidhani kama ni kosa, hebu tuangalie maisha yetu. Watoto wafunge ndoa mambo yaendelee"
"Ila dunia haina siri Deo"
"Ungetambua hilo basi toka mwanzoni usingetaka kunificha, ila ulinificha hadi pale ulipoumbuliwa na mdogo wangu"
Joy akaona sasa maneno yatakuwa makubwa na yatavuka mipaka hivyobasi akaamua kukaa kimya ili kuepusha mumewe kukumbushia yaliyopita.

Sabrina alienda nyumbani kwa Sam na kutulia ndani huku akimsubiria, na Sam aliporudi alimkuta Sabrina akiwa ndani,
"Nasikia eti imeshindikana kumtolea mahari dada yangu"
"Ndio imeshindikana sababu ya mjomba wako. Kaondoka na kutokomea halafu hajarudi tena, sijui na yeye vipi. Au hataki kaka yangu amuoe mwanae? Hata sijamuelewa kwakweli"
"Haya sasa, na wewe ulipotoka pale ndio ukaamua kuja hapa?"
"Nilivyotoka nikarudi nyumbani ila kuna mambo ambayo nimeyafikiria na ndio yamenileta hapa"
Sam akajiuliza kwa haraka haraka kuwa ni mambo gani ila hakupata jibu, na alipojaribu kumuuliza Sabrina naye hukumjibu zaidi ya kumwambia kuwa hayo mambo atayaona tu bila papara.
"Una maana gani Sabrina?"
"Usiwe na mashaka Sam, utaona tu"
Usiku ukaingia kabisa huku Sabrina akiwa hapo hapo nyumbani kwa Sam ambapo kila Sam alipombembeleza kuwa amrudishe nyumbani kwao, bado Sabrina aligoma kuondoka na kuendelea kuwepo mahali hapo.

James ambaye ni baba wa Joyce, alishindwa kuelewa kwani alitafakari sana bila ya kupata majibu ila upande mwingine wa moyo wake ulikuwa unamwambia kuwa ukweli wote ataupata kwa mama mzazi wa mtoto huyo, hivyobasi akapendekeza kuwa aweze kuonana nae na waweze kuzungumza juu ya hali halisi.

Usiku uliingia vizuri, na moja kwa moja Sabrina alienda kulala chumbani kwa Sam ambapo Sam akataka kulala sebleni ili kumpisha  Sabrina kitandani.
Ila kabla hajaenda Sabrina akamshika mkono na kumzuia kisha akamuuliza,
"Utanikimbia hadi lini Sam?"
"Sikukimbii Sabrina kama unavyofikiria, ila napenda kutunza kiapo changu"
"Sawa, hata kama unatunza kiapo iweje ushindwe kulala na mimi kitanda kimoja? Kwani tukilala tu nini kinaharibika?"
Sabrina akajaribu pale kumshawishi Sam, na mwisho wa siku Sam akakubali na wakalala kitandani pamoja.

Usiku ulipofika, Sabrina akashtuka na kuamka ila alipomtazama Sam pembeni hakuwepo na kumfanya Sabrina apatwe na hasira sasa kuwa kwanini Sam anamkimbia kiasi hicho?
Akaamua kuinuka na kwenda kumchungulia sebleni, akamkuta amelala kwenye kochi na kumfanya Sabrina asikitike sana huku akizidi kujiuliza na kujiambia kuwa huenda anataka kuolewa na mwanaume ambaye si mzima ndiomana anamfanyia mambo hayo.
Hakutaka kumkurupusha pale zaidi ya kurudi chumbani na kulala.

Asubuhi kulipokucha, Sabrina  alipoamka, alimkuta Sam akiwa amelala pale pembeni kisha na yeye akamkurupusha,
"Hivi wewe, kunikimbia usiku na kwenda kulala sebleni ndio nini?"
"Jamani Sabrina, sijakukimbia wala nini. Tena leo ndio hata kutoka hapa kitandani sijatoka"
"Sam, wakati nimekuona kwa macho yangu mwenyewe!"
"Labda uliota Sabrina ila kiukweli leo sijachomoka hapa kitandani"
"Haya bhana nikatalie, ila siandikii mate wakati wino upo"
"Una maana gani?"
"Najua nitakapo kukamata, tulia tu"
Sam akacheka, kisha akainuka na kwenda kuoga kwaajili ya kujiandaa na majukumu ya siku hiyo.
Sam alipomaliza kujiandaa, ikabidi amuage Sabrina kwavile Sabrina alisema hataki kutoka siku hiyo na anataka kushinda hapo hapo nyumbani kwa Sam.

James ambaye ni baba wa Joyce, siku hiyo aliamua kufunga safari na kwenda nyumbani kwakina Sabrina kwa lengo la kuwaomba msamaha kwa kitendo chake cha kuondoka na bila ya kurudi tena ila lengo lake kuu lilikuwa ni kumuuliza mama wa Sabrina kuhusu maneno ambayo ameyasikia kwa siku ile.
Na alifika na kupokelewa vizuri tu na kijana mmoja aliyekuwa kaka wa Sabrina hadi ndani.
Alimkuta mama wa Sabrina akiwa sebleni huku akiendelea na mambo mbalimbali, ila alishtuka kumuona James mahali pale ingawa alimkaribisha,
"Karibu James, naona unamshangaa huyo ni mwanangu anaitwa Sam"
James akacheka na kumwambia,
"Watoto wako wote nilikuwa nawajua kwa sura na kwa majina. Ila mwanao mmoja tu ambaye nilikuwa namjua kwa jina tu, huyo mkubwa James. Sikuwahi kubahatika kukutana nae ingawa nilitamani sana kumuona, na kumbe ndio huyo mkwe wangu"
Mama Sabrina akaamua kujichekelesha hapo ili kuendelea kuukata mzizi wa mawazo kwa James, kisha yule Sam ambaye ni kaka wa Sabrina akainuka na kuwaacha waongee vizuri kwani aliona wazi kuwa wanafahamiana na itakuwa vyema kwao kama watakumbuka ya zamani kwani aliwasikia hata wakitaja khabari za kwaya.
"Kuna mambo mawili yaliyonileta hapa ila hili moja naomba kama utapata nafasi basi tupange siku tuonane na kuweza kuzungumza"
Mama Sabrina aliweza kuhisi kuwa ni jambo gani ila hakutaka Deo akirudi hapo amkute mtu huyo, hivyobasi akamuaga na kukubali kupanda siku ya kuzungumza.
James alipoondoka, akampa nafasi mama Sabrina kufikiria uongo wa kumwambia James ili akubali na aamini,
"Hata hivyo kuna mwingine wa ziada anayejua ukweli huu? Hata kama yupo basi atakuwa anakisia tu. Akisema kuhusu kufanana na mwanangu, nami nitamjibu kuwa duniani wawili wawili, nisipofanya kuongopa zaidi basi lazima nitaharibu tu"
Kwahiyo mama Sabrina akajipanga kwa mambo ya kuongea na James siku atakayo kutana naye.

Jeff alikuwa mpweke sana siku hiyo hadi mama yake alitambua hali ya mwanae,
"Mbona upo hivyo?"
"Nimemkumbuka sana Sabrina"
Sakina akamshangaa na kumuuliza kwa mshangao,
"Umemkumbuka Sabrina!! Kivipi?"
Hapo akamfanya Jeff naye ashtuke na kugundua kuwa ameropoka bila ya kutarajia.
Sasa akatafuta njia ya kumgelesha mama yake ili asielewe chochote na kujifanya akicheka,
"Unacheka nini sasa? Hebu niambie huyo Sabrina umemkumbuka kivipi? Unajua kama umenishangaza hapa, yani kumkumbuka Sabrina ndio mpaka uwe mpweke? Au una mengineyo wewe mtoto!"
"Mengineyo? Yapi hayo mama?"
Jeff alimuukiza mama yake kwa mshangao ili kujaribu kuona kwamba kama kuna chochote anachohisi,
"Una mengineyo huko kwa Sabrina wewe sio bure, maana ninavyohisi mtaa anaokaa Sabrina ndio huko kuna huyo mtu mzima anayekutoa akili wewe"
Jeff akagundua kuwa mama yake hajui chochote, hivyobasi na yeye akatumia nafasi hiyo kumuuliza mama yake maswali,
"Kwani mama mapenzi ni nini? Na je mapenzi yanachagua umri?"
"Halafu wewe Jeff usichefue, tena usinitibue kabisa na hayo maswali yako ya kijinga. Nilikutafutia binti mzuri hapa ila bado unang'ang' ania watu wazima. Kwakweli ipo siku yako utakayokumbuka maneno yangu yote wewe"
Jeff hakutaka kubishana na mama yake kwahiyo akaamua kuinuka na kwenda chumbani kwake ambapo moja kwa moja alimpigia simu Sabrina na kuanza kuongea nae,
"Wee mtoto, niache nipumue wewe. Huwa sipendi matatizo Jeff jamani"
"Ila mi natamani kukuona tu, yani hizi siku mbili kwangu imekuwa kama mwaka. Tafadhari nakuomba, yani nikuone tu"
"Sitaki, tena usithubutu kuja huku. Utaniona siku ya harusi yangu tu, nishafunga mkataba na wewe. Sitaki kumkera mume wangu"
Kisha akaikata ile simu na kumfanya Jeff apatwe na hasira, na kutaka kwenda nyumbani kwa Sam kumuona Sabrina kinguvu hata kama mwenyewe hataki ila akukumbuka kuwa Sam ana bastora, ikabidi awe mpole na kutafuta njia nyingine ya kumuona Sabrina kwa amani tu.

Sabrina alikuwa ameshachukizwa na simu ya Jeff,
"Haka katoto haka, katanipanda kichwani sasa. Natakiwa kuwa na msimamo wangu kwani mwisho wa siku nitaonekana malaya, sifai na majina yote mabaya nitapewa. Saivi nakuwa mkari tu ili niikomeshe tabia ya Jeff hata kama nina mimba yake. Kwanza nafuta kauli, sio mimba yake bali ni yangu"
Sabrina aliongea kwa hasira huku akimngoja Sam arudi nyumbani.
Kabla Sam hajarudi, kuna kijana aliyefika pale huku amebeba chakula kilichofungwa na kumkabidhi Sabrina kwa madai kuwa amepewa na Sam. Kisha naye Sam akampigia simu Sabrina katika kuthibitisha hilo.

Sam aliporudi, usiku nao ulikuwa umeingia na alionekana kama mtu aliyekunywa pombe.
"Kheee Sam! Ndio siku nyingine unakuwaga hivyo?"
"Jamani mama, unashangaa nini? Wewe si unataka tulale wote! Basi, mumeo nimesharudi na tayari kwa kwenda kulala sasa"
Sabrina alisikitika kiasi, kisha wakaenda chumbani na kujiandaa kulala ambapo Sam alijitupia tu kitandani na kulala fofofo, na kumfanya Sabrina naye alale tu.

Usiku sana Sabrina akashtuka, ila pale pembeni yake Sam hakuwepo na kujua wazi amefanya mchezo kama wa jana.
Sabrina akainuka na kwenda kumchungulia sebleni, akamuona mtu kwenye kochi akiwa amelala huku kajifunika shuka gubigubi, moja kwa moja Sabrina akajua ni Sam tu.
"Na leo lazima nimkomeshe, naenda kuchukua simu na kumpiga picha"
Kisha Sabrina akarudi tena chumbani.
Alipotazama kitandani, akamuona tena amelala akiwa amejifunika gubigubi kama sebleni.
Sabrina akajikuta akipiga kelele na kuanguka.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa