JE HAYA NI MAPENZI!! 52: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 18, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 52:





Deo akafurahi, ila kabla hajasema jambo lolote
wakamuona Jeff na Sakina wakiwa pamoja pale
nyumbani kwa wakina Sabrina, ambapo Jeff
akasema,
"Siwezi kabisa kukubaliana na jambo hili"
Wote waligeuka na kumuangalia.
Sabrina akaona wazi kuwa ule ndio muda wa kufanya jambo fulani, akakumbuka na ule msemo kuwa ukicheka na nyani utavuna mabua.
Alijua wazi kuwa akijifanya kuzimia, Jeff ndio atajifanya muongeaji mzuri kwahiyo jambo jema ni kucheza na akili yake kwa haraka iwezekanavyo.
Sabrina alijivika ujasiri na kuinuka, akamfata Jeff na kumshika mkono huku akimvutia kwa nje.
Wote pale ndani walibaki kuduwaa kwani hawakuelewa kwanini Jeff alisema vile na kwanini Sabrina ameona ni vyema kumvutia nje ya nyumba.

Sabrina alimvuta Jeff nje kabisa ili hata akizungumza asiweze kusikiwa na mtu yeyote, Sabrina akajikuta akimuuliza Jeff kwa hasira,
"Hivi una akili wewe?"
Kisha akamnasa kibao, Jeff nae alikuwa ametulia tu ingawa Sabrina alimnasa vibao vitatu mfululizo,
"Unakaa kimya unaniletea kiburi eeh!"
"Tafadhari nisamehe, ila mimi sikuwa na lengo ambalo wewe unalifikilia kuwa ninalo. Siwezi kufanya lolote baya la kukukera wewe Sabrina. Sababu nakupenda"
Jeff alijikuta akimkumbatia kwa nguvu Sabrina.
Muda huo Sakina nae alikuwa ameshatoka nje akiwa ameelekezea macho yake kule alipo Jeff na Sabrina kwahiyo lile tukio la Jeff kumkumbatia sana Sabrina mama yake alikuwa ameliona na kuendelea kuwaangalia pale.

Sabrina akajitahidi kumtoa Jeff kwenye mwili wake, ila Jeff hakutaka kutoka na kumwambia Sabrina,
"Nakuomba jambo moja tu"
"Jambo lipi hilo?"
"Naomba kulala karibu yako kwa usiku mmoja tu, halafu mimi sitakusumbua tena"
"Ila wewe Jeff wewe kwanini unakosa akili kiasi hicho?"
Jeff alizidi kumkumbatia Sabrina bila ya kutaka kutoka kwenye mwili wa Sabrina, ikabidi Sabrina amkubalie ombi lake ili aweze kuganduka kwenye mwili wake.
Kisha Jeff akamuachia Sabrina, muda huo Sakina nae alianza kusogea pale walipo kisha Sabrina akamwambia Jeff
"Tafadhari ondoka, tena ikiwezekana nenda hata ukapumzike  nyumbani kwangu ila usithubutu kumwambia chochote mama yako kuhusu yale mambo kabisa"
Jeff akaanza kuondoka, na Sakina alikuwa tayari amefika eneo lile,
"Imekuwaje tena? Mbona ananiona mimi ndio anakimbia?"
"Huyu mwanao huyu Sakina, itabidi siku tutulie na kuelezana vizuri kwavile anajielewa yeye mwenyewe kwakweli"
"Hadi nimechoka hapa mdogo wangu, ndio shida ya kuzaa katoto kamoja hii yani saivi najuta na kutamani nipate angalau mtoto mwingine wa ziada"
"Basi dada, wee kapumzike tu nyumbani, mi nikipata muda nitakuja tuongee vizuri ili tujue jinsi ya kumsaidia huyu Jeff"
Sakina akamuaga Sabrina pale na kuondoka, kisha Sabrina akaelekea ndani kwao ambapo kila mmoja alitaka kujua sababu ya Jeff kuja na kuwaongelea kiasi kile.
Wakawa wanasubiria jibu kutoka kwa Sabrina, ambapo Sabrina kama kawaida yake akaanza kuwachanganyia mada pale,
"Unajua yule Jeff akili yake sio nzuri, na kiukweli ni mimi tu ninayewe za kuisoma akili yake na kujua jinsi gani namtuliza ile akili"
Sam akaingilia kati na kuuliza,
"Ndio utuambie sasa, alikuwa na shida gani?"
"Jamani hayo mambo tuachane nayo na tuendelee kujadili mambo yetu, wale nishaongea nao na kama lingekuwa jambo la maana basi ningewaambia, ilimradi sijasema chochote basi mjue kwamba hapakuwa na lolote lile la maana. Naomba tuendelee na mambo yetu mengine"
Wakakubaliana na Sabrina ila bado Sam alikuwa na mashaka juu ya maneno ya Sabrina ingawa alikubaliana nae ili kuepusha mzozo tu.

Mipango ilipoisha, Sam alimuomba Sabrina kuwa waende nyumbani, kisha Sabrina akamuuliza Sam,
"Eeh tunaenda nyumbani kwangu au kwako?"
"Nataka twende kwako Sabrina, tena leo nataka nikalale huko huko"
Sabrina hakutaka kumpinga Sam kwani al ijua wazi kama akimpinga basi Sam anaweza kumuhisi vingine.
Alichokifanya Sabrina ni kumuandikia Jeff ujumbe mfupi kuwa aondoke kwahiyo akamuelezea hali halisi ilivyo ili Jeff apate kumuelewa.

Sabrina aliondoka na Sam mpaka nyumbani kwake, ambapo Sam alianza kuikagua nyumba ya Sabrina kila mahali utafikiri yeye ni mkaguzi mkuu wa nyumba za watu.
Sabrina alikuwa akimuangalia tu kwani alijua wazi kuwa hawezi kukutana na kitu chochote.
Sam alipojiridhisha sasa, akarudi na kukaa na Sabrina kisha akamwambia Sabrina,
"Leo tutaenda kula hotelini kisha tutarudi kulala"
"Hoteli gani leo?"
"Kuna hoteli nitakupeleka, huko bado sijawahi kwenda na wewe"
Kwahiyo Sam akamuomba Sabrina ajiandae sasa kwaajili ya kwenda huko hotelini, na alipomaliza kujiandaa Sabrina akatoka na kumfanya Sam acheke wakati wanaondoka,
"Unacheka nini sasa?"
"Khee tumbo lako linaonekana sana siku hizi"
Sabrina akajitazama na kuona kweli tumbo limesonga mbele, naye akajicheka na kuendelea na safari yao.

Walifika hapo hotelini na kuagiza chakula na vinywaji, baada ya muda kidogo Sam akamuaga Sabrina kuwa anaenda maliwatoni kidogo kwahiyo Sabrina alitulia pale alimsubiria.
Zilipita sekunde chache, akasogea muhudumu hadi pale alipo Sabrina na kumwambia,
"Naona siku hizi jamaa anajiweza, hadi kakupa mimba duh!"
Sabrina alimshangaa huyu muhudumu na kumuuliza,
"Unamaana gani wewe?"
"Sina maana mbaya, ila nampongeza tu kwa kumpa daktari wa magonjwa yote"
Sabrina bado hakumuelewa huyu dada, na wala hakujua kuwa alikuwa na maana gani na kujikuta akikazana kumuuliza,
"Unamuongelea nani wewe?"
Sam nae alikuwa amerudi na kumfanya yule dada aondoke, ikabidi Sam amuulize Sabrina,
"Kwani huyo dada alikuwa anataka nini?"
"Hata sijamuelewa, eti ananishangaa mimi kuwa mjamzito"
Hapo hapo Sam akaelewa mushtakabali wa mazungumzo ya yule dada, tena hakutaka kujua kama Sabrina ameelewa au hajaelewa kwani tayari alishakuwa na hasira.
Sam akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Nisubiri kidogo tu"
"Unaenda wa pi tena jamani?"
"Wee nisubiri tu hata sikawii"
Sabrina hakujua ni kitu gani Sam anaenda kufanya huko.

Sabrina alibaki kuduwaa tu, baada ya muda mfupi Sam akarudi pale na kukaa.
Dakika mbili kupita, yule dada nae alifika pale huku akikazana kumuomba Sam msamaha, na baada ya muda kidogo wakaja walinzi kumvuta na kumwambia,
"Umeambiwa hutakiwi kuonekana katika hoteli hii kuanzia sasa"
Wakamvuta na kumfanya hata asiweze kushkia jibu la Sam.
Sabrina akamuuliza Sam,
"Vipi Sam? Inamaana umeenda kumshtaki?"
"Huwa sipendi ujinga kabisa mimi, yeye maisha ya watu yanamuhusu nini? Kama anataka kazi ya kutangaza maisha ya watu basi atoke hapa akayatangaze huko mbele ya safari. Anajua mimi ni nani kwenye hii hoteli au alikuwa anajiongelesha tu bila kujua! Ngoja akatangetange mtaani ndio ajue maisha, wambea huwa hawafanyi kazi kwahiyo asipokuwa na kazi ndio akasambaze vizuri umbea wake"
Sam aliongea kwa jazba kabisa na kumfanya Sabrina atambue wazi kuwa Sam amechukizwa sana na kitendo kile, ikabidi atulie tu ili kuepusha matatizo mengine huku akijilaumu yeye mwenyewe kwa kumueleza Sam.
Chakula kilifika pale, wakala kiasi kisha wakaanza safari ya kurudi nyumbani kwao.

Usiku ulikuwa tayari umeingia, na muda wa kulala ulikuwa tayari umefika.
Sabrina alienda moja kwa moja chumbani kwake na kumvuta mkono Sam ili waweze kulala pamoja, ila Sam alikataa na kumwambia Sabrina kuwa muda wa wao kulala pamoja bado haujafika,
"Muda gani unaouzungumzia Sam? Harusi yetu ni wiki ijayo tu hapo, sasa kuna ubaya gani kama tukiamua kulala wote leo?"
"Sabrina, nakupenda sana. Hebu jaribu tufate sheria za dini, najua hata wewe hukufurahia kupata hiyo mimba kwa kubakwa. Nimeamua kuchukua hayo majukumu na kusema kuwa mimba ni yangu ila bado sitaweza kuivunja ile sheria ya tendo la ndoa"
Sabrina akamuangalia tena Sam na kumuuliza,
"Kwahiyo  na leo utalala hapo sebleni?"
"Hapana, naenda nyumbani kwangu ila yote haya ni katika kukuonyesha tu kuwa jinsi gani nakupenda"
Sam akamsogelea Sabrina na kumbusu kwenye paji la uso kisha akamuaga na kuondoka zake.
Sabrina aliingia chumbani kwake na kukaa kitandani huku akimtafakari Sam,
"Hivi huyu mwanaume ni wa aina gani? Inamaana kweli anangoja ndoa? Yani hakuna chochote alichoshawishika kwangu? Mmh sijapata kuona mambo haya jamani. Huyu mwanaume mzima kweli huyu?"
Sabrina alijidadisi bila ya kupata jibu lolote la maana na kuamua kulala tu.

Asubuhi na mapema, mlango wa chumbani kwa Sabrina ulikuwa ukigongwa, moja kwa moja Sabrina akajua kwamba mgongaji ni Sam ila akajiuliza kuwa Sam amepata wapi funguo wa mbele wa ile nyumba? Jibu likamjia kuwa huenda Sam akawa na funguo hizo.
Akainuka pale kitandani na kwenda kumfungulia, mgongaji alikuwa ni Jeff ambaye alienda moja kwa moja na kumkumbatia kwanguvu Sabrina huku akimwambia,
"Nimekumiss sana mamy"
Sabrina alisimama tu akimshangaa Jeff kisha akamuuliza,
"Umelala wapi wewe?"
"Sikulala, mawazo yote yalikuwa juu yako"
"Kheee makubwa haya, ulikuwa unaniwaza mimi? Kuwa nimekufa au nimekuwaje?"
Jeff akazidi kumkumbatia Sabrina na kumwambia,
"Nakupenda sana, nakupenda sana, nakupenda sana"
Akawa kama mtu anayetaka kulia, Sabrina akamuhurumia na kumkumbatia pia kisha akamuomba airudishe akili yake kwani alimuona kamavile mtu aliyechanganyikiwa.
"Jeff, tulia na unisikilize nitakachokwambia"
"Tafadhari mamy, usiniambie neno lolote zaidi ya nakupenda. Nakuomba sana"
"Haya basi niambie unachotaka cha zaidi toka kwangu ni nini?"
"Nahitaji pendo lako, mapenzi yako. Nakuhitaji mamy, nakupenda sana labda uniue ndio itakuwa njia pekee ya kukuepusha na usumbufu wangu. Kwasasa nahitaji kuwa karibu na wewe kabla ya ndoa yako, tafadhari nikubalie nateseka sana mimi. Na kama kulaumu basi usinilaumu mimi, bali ulaumu moyo wangu ambao umekupenda wewe"
"Sawa, ila niahidi jambo moja tu. Baada ya ukaribu huo na mimi hautanisumbua tena kwenye ndoa yangu, niahidi hilo sasa"
"Nakuahidi sitakusumbua kabisa ingawa moyo wangu utaumia sana"
Sabrina akajaribu kuichekecha akili yake kwa maamuzi ambayo anataka kuyafanya ila hakupata jibu la haraka, na kuamua kutoa jibu la papo kwa hapo.
"Basi tutashinda wote siku nzima ya leo, ila kesho nitakuwa na majukumu yangu mengine"
"Asante mamy"
Jeff akamkumbatia tena Sabrina, kisha Sabrina akamuaga pale na kurudi kumalizia usingizi wake hadi pakuche kabisa.

Sam alikuwa akitafakari kama Sabrina ametilia maanani hayo maneno aliyoambiwa na yule muhudumu na kuanza kujiuliza kuwa huenda Sabrina ameanza kumuhisi kutokukamilika.
"Leo nitaenda usiku, bila ya kumwambia. Napenda nimfanyie surprise"
Akajipanga kwenye akili yake kitu cha kumfanyia  Sabrina ili afurahi.
Kisha akainuka na kwenda kutembelea ofisi yake kwanza.

Sabrina alipoamka rasmi sasa akaenda kuoga na kutoka sebleni, akakuta Jeff ameshamuandalia chai ili anywe, kisha akamuuliza kwa masikhara tu,
"Hujaniwekea madude yako humu kweli na leo? Maana wewe mambo yako unayajua mwenyewe"
"Hapana mamy sijaweka chochote, siwezi kurudia tena makosa. Nimekuwa kijana mzuri sasa, na ningependa nikunyweshe hiyo chai"
"Khee, nitolee balaa mie. Umekuwa na maneno mengi kama muimba mashairi"
Sabrina akainywa ile chai.
Na alipomaliza, alikaa pamoja na Jeff, mara nyingi Jeff alionekana kumfanyia vituko vituko Sabrina ili kumfanya acheke na kufurahia uwepo wake.
Mara simu ya Sabrina ikaita, na mpigaji alikuwa Sakina ila kabla Sabrina hajaipokea Jeff akamwambia,
"Akiniulizia mimi mwambie sipo"
Na Sabrina alipoipokea ile simu, swali kutoka kwa Sakina lilikuwa ni hilo hilo la kumuulizia Jeff, naye Sabrina  akamjibu kuwa Jeff hayupo, na simu ilipokatika wakajikuta wote wakicheka kwa pamoja.

Usiku ulipofika, Jeff akamuomba Sabrina,
"Nina ombi moja"
"Ombi gani hilo"
"Tafadhari nikubalie"
"Ndio nitakukubalia ila mpaka uliseme"
"Naomba usiku wa leo tu nikalale pembeni yako, tafadhari nakuomba"
Jeff alionyesha kama kulengwa na machozi na kumfanya Sabrina akubali kwavile amesema kuwa ataenda kulala pembeni yake.
Kisha wakainuka na kwenda kulala.

Sam alifika kwenye nyumba ya Sabrina kwenye mida ya saa tano usiku, kwavile alikuwa na funguo za geti akafungua bila ya kugonga.
Alipoingia, moyo wake ukamtuma kuwa akachungulie kwanza dirishani kwenye chumba cha Sabrina.
Ila aliposogea madirisha yote yalikuwa yamefungwa vizuri, ila aliposogeza sikio akasikia kuna miguno ya kimahaba kutoka kwenye kile chumba.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa